Close

UNYAKUO NI LINI? MUDA WOWOTE KUANZIA SASA, YESU WA NAZARETI ANARUDI.


Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na yupo mbinguni anasubiri tu siku na muda aruhusiwe kuja kuwanyakua wale walio wake awapeleke wakakae mahali alipo yeye kwa muda wa miaka saba ndipo arudi atawale kimwili na wale waliookoka na kuishi katika utakatifu au kwa lugha nyingine wameushinda ulimwengu.
Mara nyingi YESU amekuwa akinieleza waandae watu ili niwapate mimi na shetani awakose, sababu wanadamu wengi zaidi wanaona wapo sawa kabisa na wanafikiri kuwa katika siku ya unyakuo na wao watanyakuliwa waeleze wanirejee mimi wengi zaidi wapo katika njia pana kwa sasa (barabara ya jehanamu) na sababu kubwa Hebron watu wananipenda ila wameletwa watumishi wapinga kristo wanawafundisha kinyume na biblia au elimu ya wanadamu au mapokeo ya watumishi ambao wameniasi mimi YESU, na wengine ni wa mishahara na wachawi, wafanya biashara na wengine ni wanyang’anyi. Ukisoma katika kitabu cha Yohana 14: 1-3 na Mathayo 24: 29-37, siku hiyo itakuwa ni ya kutisha, mwezi utakuwa giza na jua pia, kisha nyota zitaanguka kutoka mbinguni zitue katika ardhi hii watu wanayoishi, na mbingu zitatetemesha na ndipo mwana wa pekee YESU WA NAZARETI ataonekana akishuka kuwanyakua wale tu waliookoka na kuishi maisha matakatifu.
Leo nitaelezea kidogo kuhusu miaka (1000) elfu moja ya utawala wake. Umeanza lini na utaisha lini. Sababu katika vitu ambavyo watu walipigwa upofu na shetani ni kuhusu habari za unyakuo na milioni ya watu hawaelewi itakavyokuwa na ni kipindi gani? Japo tokea miaka yote iliandikwa katika biblia unyakuo ni wakati wowote tokea enzi za kina Petro pia nao walitazamia ingekuwa kipindi kile walichokuwepo wangemsubiri  na milioni ya watu hawaelewi itakavyokuwa na ni kipindi gani? Japo tokea miaka yote iliandikwa katika biblia unyakuo ni wakati wowote tokea enzi za kina Petro pia nao walitazamia ingekuwa kipindi kile walichokuwepo wangemsubiri YESU awachukue katika unyakuo, kumbe hata wao walifichwa, mimi pia nilikuwa nafikiri hivyo hivyo mpaka YESU peke yake aliponifundisha kwa ajili ya utukufu wake MUNGU kwa sababu hizi ndizo nyakati za yeye kurejea ila siku na saa, mwaka, hizo sizijui, ameniambia kuanzia tarehe 5.11.2012 saa sita ya usiku nilipokuwa katika maombi akaletwa joka kuu akiwa amefungwa minyororo na malaika Mikaeli na kumnyang’anya kila kitu alicho nacho na kumfunga (Ufunuo 20: 1-3) ufunuo huu ulitimia  tarehe 5.11.2012, na ndipo miaka 1000 ya utawala wa YESU WA NAZARETI ulianza rasmi katika ulimwengu wa roho, kwa wachawi wanaelewa, watumishi freemason wanajua kabisa kuwa pale walipokuwa wanapata nguvu hapapo tena, hizi nguvu zilizobakia hayo ni masalia tu na yataendelea kuporomoka na mtaona katika sehemu mbali mbali makanisa yaliyoongozwa na mpinga kristo au makanisa ambayo walitumia nguvu za giza na hata nchi na marais mbali mbali waliokuwa wakitegemea uchawi ili kuongoza nchi hawatafankiwa tena sababu aliyekuwa anawasaidia kafungwa sasa. Na joka kuu huyu ndiye baba yake shetani, shetani ni mdogo sana ila watu tulifundishwa kuwa shetani ndiye mkubwa, jibu ni hapana shetani ni mtoto wa joka kuu. Sasa hata shetani hana nguvu tena zimebakia roho zake tu ila hazina nguvu, hii ndio kupindua ufalme wa Ibilisi.
Sasa nawaeleza kwa ufupi ili mkae sawa sawa na muokoke leo hii sababu usipookoka usijidanganywe utaenda mbinguni, wasiookoka mahali pao ni jehanamu, ila na unaweza ukaokoka na mbinguni usiende, hii ni sababu ya matendo yako je yalikuwa matakatifu? Wengi wameokoka wanajihesabia kuwa wataenda mbinguni, leo nakufundisha majibu ya wewe kwenda mbinguni au jehanamu, jitazame njia zako na uhusiano wako na YESU WA NAZARETI na neno lake. Hivyo mpaka sasa umepata picha at least ila endelea kusoma makala ya Nabii Hebron katika blog ya www.prophethebron.blogspot.com  moja baada ya moja hakika ukisoma hata zaidi ya makala kumi utakuwa umepata picha ya maisha yako na je upo salama au umepotezwa umepelekwa katika njia pana pasipokujua wala kupenda.
SIKU ILIPOANZA KUHESABIWA MIAKA 1000
Ni tarehe 5.11.2012, hivyo mpaka sasa tupo tayari katika utawala wa YESU WA NAZARETI katika ulimwengu wa roho na shetani yupo chini na YESU anatawala sasa, na mpinga kristo atachoka na kazi zake mtaona zimeharibika, itakuwa ni mivurugano na wengine watajitoa. Sasa miaka yote ilitabiriwa na watu wakawa wanasubiri hiyo miaka elfu moja itakuwa ni lini, wengine walifikiria ni tayari kama vile hata kipindi cha kina Petro. Sasa kama tayari miaka elfu moja ya utawala wa YESU WA NAZARETI umeshaanza kimwili basi huu ndio wakati wa yeye kuja kuwanyakua wale watakatifu, jinsi itakavyokuwa siyo mpaka 1000 ziishe hapana, ni kuanzia tarehe niliyoambiwa miaka elfu moja imeanza, hii itatokea wakati wowote atashuka kuwanyakua wale walio wake atawachagua na ipo nguvu itakayowashukia watakatifu waliompendeza MUNGU itawanyanyua mawinguni kama alivyopaa YESU, Eliya, Henoko na wale wenye dhambi watabakia hapa ulimwenguni kwa muda wa miaka saba (hii ni miaka ya dhiki kuu, baada ya miaka saba kupita au siku 1260, YESU atarudi kuitawala dunia yote kimwili kama alivyokuwa wakati ule Yerusalemu akitembea, na hao ambao watateseka kipindi hicho mpinga kristo ataachiwa awatese watu na jinsi mateso yatakavyokuwa ni bora uokoke leo hii.
JE NI WAKRISTO WA JINSI GANI WATANYAKULIWA?
·        Awe ameokoka na amebatizwa kwa ubatizo wa maji mengi na yanayotembea, aishi maisha matakatifu ya kumpendeza MUNGU kila siku.
JE NI WAKRISTO WA JINSI GANI WASIYONYAKULIWA?
·        Mkristo ambaye hajaokoka, aliyebatizwa ubatizo wa maji ya kikombe.
·        Mkristo  anayeabudu sanamu, mkristo anayebusu msalaba, anayeshiriki divai (pombe), mkristo aliyebatizwa kwa jina la mchungaji, mkristo anayewaabudu wanadamu mfano Mathayo, Maria, Petro na wengineo biblia imeruhusu (MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU) hawa wengine unaowaabudu hawana tofauti na wewe au mimi Hebron.
·        Wakristo wachawi, walevi, wafisadi, wakristo wanaofuata neno lililobadilishwa.
·        Wakristo wanaoombea wafu (MUNGU yeye siyo MUNGU wa wafu, yeye ni MUNGU wa wenye uhai peke yake.)
·        Na mtu yeyote ambaye hajamkiri YESU kama ni BWANA NA MWOKOZI WAKE.
JE UNAJUA MAKANISA NA WATUMISHI GANI AMBAO HAO HAWATANYAKULIWA NA YESU.
Haya siyo mapando ya MUNGU ni mapando ya shetani yanapandwa kwa wanadamu ili wapelekwe jehanamu.
·        Kila kanisa ambalo linabatiza ubatizo tofauti na ule aliobatizwa YESU wa maji mengi hayo siyo makanisa ya YESU, kubatiza ubatizo tofauti kwa kutumia kikombe na kubatiza mtoto mdogo, hii ni injili ya kuzimu na mpinga kristo.
·        Kuwabariki watu wazima (ubarikio), kubatiza katika kisima.
·        Kuchangisha pesa makanisani, harambee, kuwapa watu divai yenye alcohol.
·        Watumishi wanaofanya mazinga umbwe mfano kufufua misukule, hao ni wachawi.
·        Makanisa yenye huduma sita badala ya huduma tano.
·        Mtumishi freemason, waangalie hata kwenye mtandao wapo wasiwadanganye watu hao tayari washajitoa kwa shetani na mpinga kristo ili kuwateka watu.
·        Makanisa ambayo watumishi wake wakati wa kuapishwa wakalala chini flat badala ya kupiga magoti wapakwe mafuta.
·        Makanisa yanayoosha waumini miguu badala ya watumishi kwa watumishi (soma blog ya Nabii Hebron Maana ya kuoshwa miguu).
·        Watumishi wanyang’anyi wa mali za watu wakitumia jina la YESU.
·        Makanisa yote ukiona yanabendera zake, nakueleza uelewe hapo ni nguvu za ufalme wa shetani.
·        Makanisa yote ambayo utakuta yameandikwa maneno ya freemason au alama zake.
·        Na makanisa yote ambayo yanaongozwa na mpinga kristo na kila makanisa ambayo yameongeza au kupunguza biblia, kubariki dhambi au kuhalalisha pombe.
NOTE:
Yapo mengi ili upone soma vitabu vya Nabii Hebron na ufuatilie mafundisho na vipindi vya redio, tv na blog utapata neno na roho yako itakuwa hai. YESU anarudi na hata ukisoma vitabu vyote hakuna jina la Nabii wala Mtume yeyote ambaye atakuja siku ya KIAMA, utaona YESU mwana wa MUNGU wa pekee na ndio maana MUNGU atamtumia huyo huyo tena na akija atamchukua yule yule  aliyemkubali yeye peke yake na siyo wengine mfano hata ukimkiri Petro au Musa au Eliya au Maria na wenigneo wote, ujue umepotea, njia aliyoiweka MUNGU ni YESU ndiye njia pekee na kama ndiye basi hakuna haja ya kuwaabudu mitume wengine, manabii wote waliopita sababu hata biblia haijaandika hao ndio njia, sasa why uwaabudu hao? hao siyo njia ya kweli, funguka leo. Njoo sasa umpokee YESU ili na wewe akija uwe wake na akunyakue, hao wengine wote siyo njia, ulimwengu fungukeni macho na akili. (Jichunguze ukristo wako je ni msafi au mchafu kiroho? Fanya maamuzi sasa.)
TOBA:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele na siku ukija kulinyakua kanisa lako usiniache. Namkataa shetani kabisa na mafundisho yake ya uongo. Niongoze YESU WA NAZARETI.
NABII HEBRON.