Close

UNYAKUO WA SHETANI NI UPI?


Ufunuo 20:7-15

Maana ya unyakuo wa shetani hii inakuwa ni kinyume chake, badala ya kunyakuliwa ni kudondoshwa kuzimu katika ziwa la moto, katika tendo hili litatokea baada ya vita vya Gogu na magogu kutokea ambayo vitakuwa ni vita ambavyo havijawahi kutokea katika ulimwengu huu hivi vitakuwa ni vita vya mwisho, na ndipo atakapokuja mwana kondoo wa MUNGU akiwa na serikali yake watu 144,000 kuja kutoa hukumu, na hukumu hii itakuwa ni kabla ya miaka hii 1000 haijaisha. Kila aliye kufa hata aliyefia baharini, vitani sehemu yeyote ile wote watainuka na kuwa hai kila mmoja na ndipo kila mtu atapita mbele ya mahakama ya YESU aangaliwe aliyoyatenda na wale waliotenda dhambi wote watahukumiwa na kuunganishwa na shetani katika moto wa milele. Unyakuo huu wa shetani atawanyakua watu wale waliokubali matendo yake na kwenda kinyume na neno la MUNGU na hawakuishi maisha matakatifu.
Siku hiyo itakuwa ni siku ya kutisha haitakuwa siku ya kutubu au kujitetea nafasi yako ni sasa ili upone na wengine siku hizi wanadanganywa ukifa utaombewa nawaeleza ukweli hao ni waongo na ndani yao ni roho huyo huyo wa mpinga kristo anawazubaisha watu wafe na dhambi, wakati ni sasa, ukifa na dhambi utavuna moto wa milele, na ujue wanadamu wametekwa wakamuona MUNGU hana akili eti tenda dhambi halafu utaombewa ukifa utapokelewa, nawaeleza kama ingekuwa ni hivyo watu wanasamehewa makosa yao wakifa na dhambi basi katika siku ile ya hukumu isingekuwepo na sababu watu wote wangeombewa.
Lakini ukija katika biblia utaona kuwa vitaletwa vitabu venye rekodi ya kila mtu, hii ina maana kila utendayo yanarekodiwa, yanakusubiri wewe utasomewa mbele ya kiti cha enzi upate haki yako sawa sawa na matendo yako. Msiamini kabisa hayo mafundisho ya kukubali uombewe ukifa na dhambi, muda wako ndio leo na siyo ukifa uwe maiti. Katika ule mwisho watu watalia na kusaga meno wengine watasema laiti ningelijua, nakueleza amenituma YESU niwaeleze ukweli wapo mabilioni ya watu kuzimu na walikuwa wakristo wamefia katika dhambi wakijua wataombewa huku ulimwenguni na wanayo hasira sana sababu waielezwa uongo na sasa inawagharimu kwenda jehanamu na wameshajua kabisa wanasubiri moto tu, walidanganyika na makanisa ya uongo na watumishi wa uongo, laiti ungeruhusiwa uone watu waliokufaga kuzimu wanavyoteseka na walipokuwa hapa ulimwenguni waliimbiwa parapanda na wakatamkiwa ile siku ya mwisho ufufuke, hayo yote ni theologia ambayo imetoka kuzimu ili ije izae matunda ya kuwaua wanadamu kiroho na waingie jehanamu na wasiende mbinguni bali warudi huko ilipotokea hiyo elimu.
Pia lazima uelewe ni amri ya MUNGU kila mtu atanyanyuka siku ile ya hukumu, apite mbele ya mahakama asomewe mashtaka yake. Hii yote ni kazi ya shetani ili awavune watu pasipokujua. Ila wapo watumishi ambao wametumwa na shetani kabisa kazi yao ni  kuangamiza roho za watu na akiweza kuwapeleka wengi kuzimu shetani anawapa utajiri mkubwa, na wengine mnaona eti utajiri huo wamepewa na YESU, hicho ni kivuli cha kuwapiga watu upofu. Ukiona mtumishi amepata utajiri kwa ajili ya kuchaji watu pesa, michango, harambee, kutumia jina la YESU kutafutia pesa, kuwa na benki na mengineyo. Soma kitabu cha Nabii Hebron JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI utaelewa zaidi.
Na watumishi hawa wanaopeleka watu kuzimu siku zote hawa ni marafiki kiroho na kimwili haijalishi utaona labda mtumishi ametumia nguvu za giza lakini utaona ameshirikiana na wenzake katika mikutano ya semina au umoja wao elewa ipo shida, hao ni watoto wa baba mmoja, lusifa, wanazo agenda zao. Na yamkini utaweza kukuta hapo awali kweli mtumishi alikuwa anatumiwa na MUNGU ila ukiona matendo yake yamebadilika elewa ameshapewa kisogo na MUNGU, shetani ndiye amekaa hapo, wewe mkimbie wala usiage mueleze YESU akuongoze uende wapi, ukikosa kaa nyumbani na uwe unaomba kuliko kujipeleka kwenye mdomo au lango la kuzimu. Unaposhiriki au kuingia katika kanisa ambalo Pastor ni wa kuzimu au amemsaliti YESU uelewe unaingia katika lango la shetani, na ukiingia katika kanisa la kweli ambalo YESU wa kweli yupo ndani ya Pastor au mtumishi ujue umeingia katika lango la mbinguni upo salama. Na siyo kuwa kanisa litaandikwa ni la kuzimu hapana, wewe cha kujua chunguza mafundisho, linganisha na bibia (soma zaidi blog yangu utaelewa yapo masomo mengi sana ya kukufanya wewe unayetaka kupona roho yako na moto wa jehanamu na utii utapona).
Na zaidi dalili nyingine utaona mtumishi anatumia akili kuliendesha kanisa badala ya ROHO MTAKATIFU uelewe tayari hapo ni lango la kuzimu. Na pia ukiona katika kanisa mtumishi ameshawabatiza waumini wake halafu anaamka tu siku nyingine anasema kanisa lote mkabatizwe tena, uelewe huyo ni pepo atendaye kazi ndani yake. Mnapobatizwa tena anawafungia maagano yake msimjue ameachwa na MUNGU na nyie mbakie hapo kama wajinga, na njia nyingi zipo ila soma vitabu na karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ufundishwe ili ujitambue ukaaje usije ukanyakuliwa na shetani. Ile siku ya mwisho ipo karibu sana sababu tayari tumeshaanza kipindi cha miaka 1000 tokea 5.11.2012.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote na uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele, niondolee mafundisho ya uongo katika damu yangu, nyama na mifupa, unioshe kwa damu yako ya thamani, usiniache nitekwe tena.
KARIBU KATIKA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

NABII HEBRON.