Close

UPENDO WA SHETANI


Upendo wa shetani ni ile hali ambayo inakuwa ndani ya mtu kwa nje anaonyesha anakupenda  ila ndani ya moyo wake anakuwazia mabaya matupu hata kukuua, ila kwa nje akiongea na wewe anajifanya yupo yupo na wewe na mda mwingine hujiweka  rafiki wa karibu sana  na hata usimjue ila anakuwa analo jambo lake analolijua  kwa hiyo hii inaitwa chuki na siyo upendo.
Mtu huwa anakupenda sababu anapata vitu kwako, mfano unampa pesa, au msaada na ukiacha tu, huanza kukuchukia au hata kukusema vibaya. (Inaonyesha ni vitu vyako ndiyo alivyovitamani).
Mtu asiyekuheshimu kama upo na hali yako hiyo na kisha anaongea na wewe hata kukupa salamu  huyo anayo chuki.
Mtu anayejifanya yupo upande wako na pia yupo upande wa maadui wako, huyo ni msaliti wa mtu kama vilea YUDA alikuwa pande mbili/
Upendo wa shetani ni matunda yote au tabia zote za kinafiki juu ya mtu na mtu au pia mtu anajiita mkristo yani anampenda MUNGU lakini matendo yake ni udhalimu mtupu. Huyo anayo roho ya shetani na ni mnafiki wa MUNGU na ni rafiki wa shetani.
Upendo wa shetani  – ni kukosa na kutenda kinyume kama kubadilisha Neno la MUNGU kama alivyoagiza yeye ( mfano WAGALATIA 1:5-6)
Mtu mbinafsi hajali wenzake , kudharau, siyo msikivu, siyo mtiifu, kwa upande wa kanisa ukiona kanisa linawapenda  wale wenye pesa na kuwajali tu! Na hao wasio na kitu hapo ujue ni upendo wa shetani.
Ukikuta watu wanaabudu miungu mingine tofauti na MUNGU aliyeumba vitu vyote hapo ujue kuwa hawampendi MUNGU aliye hai wanampenda shetani , haijalishi wanamtaja YESU hata kusoma BIBLIA, huo ni unafiki na  imeandikwa  MUNGU huwachukia waovu; hawa ni waovu.
Ukikuta mtumishi anakudai pesa ndiyo akuombee huyo anao upendo wa shetani, ndio wenye tamaa, na imeandikwa nimekupa bure toa bure, hapa tayari hakuna utii ni utovu wa nidhamu kwa MUNGU na wizi. Upendo wa MUNGU wa kweli hauangalii vitu, hebu ona  hapa sasa unaangalia pesa  (vitu) hii ndiyo upendo wa shetani.
Na zaidi unadaiwa utoe pesa na kama  hauna unaambiwa leta hata mifugo yako na kiasi kikubwa cha pesa na hata ukitoa bado shida haiishi ipo palepale au inazidi . Hii inaonyesha kama tayari huu upendo hauna neno la MUNGU  bali una uwongo wa shetani na hamna ukweli.
Upendo wa shetani  (chuki) hukaa ndani ya watumishi wote na watu wote  walio wanachama wa freemason, zaidi  wapo majina yao katika mtandao, hawa wote tayari ni mfano halisi yakuwa  wanamchukia MUNGU na ndani yao ni udhalimu, na wauaji wa roho za watoto aliowaumba  MUNGU kwa upendo wake na shetani huwatumia  kama roho yake ya chuki kuangamiza. Au kwa maana nyingine yeyote ametengwa tayari na MUNGU, hao ni wafanyakazi au vibarua wa shetani, ni wakati wa wanadamu wote katika ulimwengu kujitenga nao na kumtafuta  MUNGU wa kweli na siye  MUNGU wa unyang’anyi. YESU anarudi utakuwa wapi wewe? Jiulize na roho  yako ifunguke.
Upendo wa shetani  (unatamani uzinzi). Japo  imaeandikwa usizini, ukikuta  mtumishi anazini  – ujue ndani yake amesha mchukia MUNGU na sheria zake na ndani yake ni roho wa shetani.
Mfano siku hizi unakuta mtumishi amekufa na na ukimwi au anao ukimwi,  Je aliupata akiwa na MUNGU wa kweli au shetani ambaye ndie mungu wa uongo? Je angekuwa anampenda MUNGU  kiukweli angeupata ukimwi? Jibu hampendi MUNGU, mshahara wa dhambi ni mauti. Na zaidi hata akifa na ukimwi kanisa linaficha na kusema uongo katika taarifa ya sababu ya kifo, je, MUNGU wa kweli ni muongo? Jibu  husema kweli. Hii ni dalili tosha kuwa hamna MUNGU wa kweli, utawajua  watu kwa matendo yao. Ni aibu! na kama viongozi wanakufa  kwa ukimwi sasa hilo kanisa linaenda wapi? Mbinguni au jehanamu? Jibu linaenda jehanamu, na mahali pa namna hiyo ni chukizo kwa MUNGU na ndiyo maana  adui anawauliza watumishi wake.
Ukikuta  mtumishi anazini na muumini au hata mwanadamu yeyote yule iwe ni mtumishi wa kike au wakiume, hao wote  siyo rafiki wa  MUNGU ni rafiki wa shetani na anayo roho  ya namna ya shetani.  Huyo siyo mtumishi anayetumiwa na MUNGU mtakatifu je  MUNGU anashiriki na  uzinzi? Jibu hapana. Hivyo ni namna ya kuelewa kuhusu MUNGU wa kweli na watu wapone roho zao.
Ukiona michango makanisani, ujue hapo tayari  MUNGU hayupo ni roho ya tamaa ya kwenda kinyume na upendo wa MUNGU . soma  1WAKORINTHO 13 yote. Halafu uangalie na uchunguze utaona ni matamaa tu,  na kukosa utiifu kwa MUNGU aliyekataa.  Nyumba yake ni nyumba ya Ibada  (yani sala tu) soma MARKO 11: 15 -18 YESU alikataa, ila kwa ajili ya watumishi kumpenda shetani na tama zake wameamua kuwa wanyang’anyi, kama majina yao wakitumia jina la YESU. Watumishi wa namna hii wameshikiliwa na upendo wa shetani ndiyo maana wanafanya ya shetani.  Na ibada hizo na kila kifanywacho ni unafiki mbele za MUNGU na MUNGU hawasikilizi wanafiki au wasaliti wa amri zake. Mwisho ni hukumu na jehanamu ipo tayari, na MUNGU amaeniambia
    hukumu ipo tayari inawasubiri. Amua  mwenyewe Jehanamu     
    au  Paradiso.
UPENDO WA MUNGU NDANI YA MWANADAMU.
Upendo  huu ni roho ile ya upendo ndiyo inayofanya kazi ndani ya mwanadamu kwa kusudi la kuujenga mwili wa Kristo. Bila upendo wa MUNGU  ndani ya mwanadamu kanisa la YESU halijengeki, ikiwa ina maana Utiifu hautakuwepo na roho ya kumpenda MUNGU kiukweli, mfano wanaoabudu sanamu huo sio mwili wa Kristo ni mwili wa shetani au yasiyofuata BIBLIA na sheria zake tayari huo siyo mwili wa  Kristo maana ndani yake haipo kweli yake na upendo ni kweli tupu ya MUNGU na kama  kweli tupu ya MUNGU imeondolewa na yeye  hayupo siyo anayeaujenga huo mwili. Na hata ule mkate wa kimwili unaoliwa kanisani na ile damu kama kanisa limeacha sheria za MUNGU  mkate ule unakuwa ni mwili wa shetani na damu ya shetani  na waumini wanakuwa  na afya ya kiroho ya shetani, wanaumizwa tu. Hebu jiulize itawezekanaje ulishwe  mwili wa YESU na huyo ambaye yeye anaabudu  YESU 100% waabudu sanamu, au Miungu  mingine, na hata ukikataa ubatizo wa  maji mengi  ambao ndio wa MUNGU, eti akuunganishe  na mwili wa YESU. Hii ni uongo  ni mkate ambao ni  yesu wa uongo  na mkate wake ambaye yupo kuzimu  (Kristo wa uwongo) utaona  jinsi watu wanavyolishwa  mwili wa Yesu wa kuzimu.  Na zaidi hata mgonjwa  akikata roho  hupelekwa mwili huo ikiwa ni chakula cha shetani anaangamia zaidi . Mwili wa Yesu hautokei au kutumika  katika watu  wasiofuata sheria za MUNGU. Huo ni feki  tupu!  Swali ! Je,  mwili wa YESU na damu yake inatumiwa na sanamu au na dini zisizofuata ubatizo wa kweli wa maji mengi?
Huo ni mwili feki kabisa ndiyo maana mtu anakula  huo mkate miaka 40, karibu anafikisha hata debe hamna matokeo zaidi ni mapepo yamejaa ndani ya mwanadamu na matatizo badala ya kuwa na uzima tele ni mauti tele.
 – Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo