VITUKO VYA WATUMISHI (ALL OVER THE WORLD)

[ad_1]

(KUWADHALILISHA WANAWAKE)

Makala hii nimeiandika nikiwa na uchungu na hasira kama YESU WA NAZARETI alivyo na hasira kuhusu watoto wake na jinsi ya kike baadhi yao wanafanyiwa matendo ya kudhalilishwa bila kujua na kupenda wanapoenda katika makanisa kwa watumishi baadhi yao wanawadanganya eti MUNGU amesema uvue nguo zote uwe uchi ndio tufanye maombi, na wenyewe wakiwa wanaamini huyo mtumishi hutumia jina la YESU hutii, na mwishowe huanguka katika uzinzi.
Na wengi pia wameniletea mashtaka ya jinsi walivyojeruliwa na watumishi tena wenye majina makubwa wengi wakati wa private prayer, wanaingiziwa vidole katika viungo vyao vya siri na watumishi, na pia siyo siri hata mnaosoma mmeshayasikia na wengine mmetendewa hayo.
Ninachowaambia hao ni wazinzi na hawana MUNGU kabisa wala siyo watumishi wake hao ni wazinzi haijalishi anacheo gani katika kanisa. YESU hana tabia mbaya kabisa na yeye haruhusu mtu avue nguo ndio amuombee, namtetea YESU WA NAZARETI. Mliofanyiwa hayo halafu mkaambiwa MUNGU ameagiza hivyo ni uongo, huo ni uzinzi. Na wengine viungo vyao wamevinyonya kwa midomo yao hao watumishi. Ukiona umefanyiwa hivyo na mtumishi kupitia mdomo wake ujue amekuibia uthamani wako na Baraka zako za mwanamke.
NOTE:
Epuka kwenda kwenye maombi peke yako nenda na mtu wa pili, na pia kama ni mke wa mtu nenda na mume wako (maana nyie ni mwili mmoja). Mkijua mtumishi amezini yeyote yule hata na ile madhabahu ujue imeshalaaniwa milele. Nawaeleza wanawake, YESU anawapenda sana ameliona kilio chenu ila amesema yeye amekaa ndani ya mtumishi mtakatifu ila anayefanya uzinzi siyo mtumishi wake. Na msiwaamini kabisa, ila OLE wao waliyowafanyia uovu huo, tena wanatumia jina la mwana wa MUNGU kufanyia uzinzi.
Swali?
1.     Hivi ni halali watumishi kuzini?
2.     Hivi ni haki watumishi baadhi kuwaingizia vidole sehemu za siri?
3.     Je? Hii ndiyo injili aliyoituma YESU ifanywe (jibu siyo).
4.     Sasa watu wataponea wapi roho zao?
5.     Je hizi ndizo sifa za watumishi wa YESU? Jibu siyo, na hao siyo ni wahuni (waovu).
6.     Hivi hizi serikali zote katika ulimwengu huu na mataifa yote, ina maana hawajui haya mateso wanayofanyiwa raia wao kupitia wanaojiita watumishi wa kanisa katika nchi zao? Jibu wanajua, viongozi wa nchi zote, mtaulizwa ile siku ya mwisho ya kuwa hamkusimamia haki na kuwalinda raia wasipotezwe roho zao, hasa kutumia jina la MUNGU raia wanafanyishwa uzinzi, na nyie ndiye mmewapa kibali wafanye ya MUNGU mema ila wamevunja hata katiba za nchi zenu.
7.     Ndiyo maana serikali nyingi zina laana ni sababu watumishi wanakula kondoo na wao ndio viongozi wa ufisadi, yaani matendo mabaya.
8.     Chunguzeni makanisa na mienendo ya watumishi. Jinsi wanavyolitumia jina la YESU vibaya na mwenyezi MUNGU na mkijua ni watumishi safi, kumbe ni shetani ndiyo amejaa kwenye mioyo yao.
9.     MUNGU uwafungue watoto wako wanaotumikishwa na wahuni wanaojiita watumishi wa MUNGU. Hao siyo, huo ndiyo ukweli. watumishi wa MUNGU hawazini kabisa.
10.                       Wazazi muwe makini na watoto wa kike wanaharibiwa na watumishi wanawafanyisha uzinzi na kuwaambukiza ukimwi. Na pia kwa sasa hivi jinsi alivyonieleza YESU, wanaojiita watumishi 47% wanao ukimwi hii ni kwa dunia nzima. Na wengi wao ni hao wenye majina makubwa katika nchi zao, kama mnabisha wapimeni afya zao mtaujua ukweli huu 100%.

NABII HEBRON.

[ad_2]