Close

WAJUE WATU WALIOPO KUZIMU WANATESEKA NIMEWAONA KWA MACHO YANGU!!!

Enyi mataifa nawasihi mrejeeni MUNGU wa kweli na muokoke na kuishi maisha matakatifu ambayo ndilo kusudi la MUNGU, na ukitenda wema na kuokoka kikweli hakika hautaenda kuzimu baada ya wewe kufariki. Wakati wako ndio huu sasa, ukishakufa basi hauna nafasi tena ya kutubu sababu roho yako itapokelewa kuzimu, maana mtu apandacho ndicho avunacho. Usidanganyike utaombewa ukifa, mabilioni ya watu mbali mbali waliokufa tayari wapo kuzimu yamkini hata ndugu zako.
Nilichoonyeshwa na YESU WA NAZARETI na nikapiga hesabu ya kibinadamu nikakuta kila familia katika watu waliokufa katika kila familia 97% wapo kuzimu. Nilianza kwa kuangalia katika familia yangu, wengi waliokufa nimewaona kuzimu na walikuwa ni wakristo. Nikaangalia baadhi sehemu mbali mbali mambo ni hayo hayo tu. Niliogopa sana, akaniambia YESU nilitaka uyaone haya halafu ujue jinsi watu wanavyovunwa na shetani. Akaniambia MUNGU ni wa haki haangalii umaarufu wako, yeye anaangalia wokovu tu na utakatifu maana hivyo ndivyo alivyowaamrisha na alinituma mimi na nikaja hapa ulimwenguni nikaulete wokovu ambao ndiyo njia ya uzima. Akaniambia MUNGU hana dini yeyote, dini zote siyo yeye amezianzisha ni wanadamu kwa akili zao. Akanionyesha mbinguni sikuona majina ya madhehebu yeyote ambayo yapo hapa ulimwenguni, niliona wokovu na utakatifu peke yake.
Akanionyesha viongozi wote waasisi wa madhehebu yote sura zao na kwa majina yao wamefungwa minyororo wanasubiri ule mwisho wa dunia wachomwe moto, niliogopa. Akaniambia Hebron, usiogope hawa wote sijawatuma mimi kuanzisha haya madhehebu, kumbuka hata mimi nilivyokuja hapa ulimwenguni niliyakuta, angekuwa ni BABA yangu kayaamrisha yeye asingenituma mimi nije katika ulimwengu huu tena. Akaniambia hawa ndio wamefanyika kuanzisha matawi ya shetani wakitumia jina langu na kulibadilisha Neno la MUNGU na watu wakawaamini nakuwafuata na kushiriki uongo. Nilizidi kuogopa sana, maana sikuyajua hayo, na katika dhehebu nililokuwa mshirika tokea kuzaliwa kwangu, nikamuona huyo muasisi na cha ajabu hapa duniani watu wanamsifu na wanasema tufuate nyayo zake, kumbe wanafuata alipo na yeye. Akaniambia madhehebu na dini zilianzishwa na shetani.
MUNGU hana dini yeye aliamrisha wokovu na utakatifu peke yake kupitia mimi YESU ambaye ndiye njia ya uzima ili kila atakayenifuata atafika nilipo mimi, na hao wasionifuata mahali pao ni hapo ulipopaona. Akaniambia nenda uwakomboe watu na mataifa yote na uwaeleze ukweli na mimi nipo na wewe, muda wangu umekaribia kuja nahitaji uwalete watu wengi Kaanani katika nchi ya Ahadi. Nitaeleza kwa ufupi maana ni mambo ya kutisha na jinsi watu wanavyoteseka kuzimu wanatumikishwa mateso ambayo hapa ulimwenguni hakuna. Na vyakula wanavyokula kuzimu ni nyama za watu waliokufa ambao hawajaokoka kikweli na ambao hawajaokoka kabisa, ndiyo chakula chao. Na hutumia mafuvu ya vichwa vya watu kama sahani za kuwekea chakula.
WALIOPO KUZIMU
1.     Wanajimu wote waliokufa na waganga wa kienyeji, washirikina.
2.     Viongozi wote waasisi wa dini zote na madhehebu.
3.     Maaskofu, Wachungaji, Mapadre, Mashehe, Maimamu, PAPA wote waliofariki, Wainjilisti, Waalimu, Manabii, Mitume maarufu katika ulimwengu huu kwa majina yao waliokufa. Na watu wote wa nchi zote waliokufa bila kuokoka na kuishi maisha matakatifu wote wapo wanateseka.
4.     Wanamziki wote waliokufaga walioimba nyimbo za kidunia hawaendagi mbinguni; mpaka waokoke na waache kuimba hiyo miziki wakiwa hai, haijalishi wanajiita wakristo.
Kila mtu anayeimba miziki ya kidunia au kuicheza au hata ukienda disko, unapoimba hizo nyimbo unakuwa unamtukuza aina ya mungu anayeitwa mziki. Yupo mungu mziki na ndiye anayewapa wanadamu nyimbo ili waziimbe na wanapoziimba wanakuwa wanamtukuza yeye, na hivyo kuwafanya wanadamu wote wanaoimba miziki ya kidunia watu hao wanakuwa wapo chini ya mungu wa kuzimu na anacho kibali kabisa ya kuwachukua kuzimu maana wanamtukuza yeye kama mungu wao, ila wanamziki hawajui haya yamefichika, YESU kanifunulia niwaeleze mpone.
Ukisikia sikia, ukikaza shingo ukifa utawafuata wengine waliokufaga wote. Baadhi ya wanamziki maarufu waliyopo kuzimu na wanateseka mpaka sasa yupo Bob Marley, Lucky Dube, Pepe Kale, Kanumba na wengine wengi maarufu wapo wanateseka mateso yasioelezeka, ni maelfu ya wanamziki, na hata hawa waliopo duniani majina yao yapo kuzimu wanasubiriwa wakifa tu waende mahali yalipo majina yao. Pia waigizaji wa sinema maarufu wapo, wachezaji maarufu wapo na wote waimbaji wa miziki ya injili wanaotumia uchawi au nguvu za giza.
Wapo mawaziri, wabunge, viongozi mbali mbali wa nchi mbali mbali na watu maarufu waliokufa.
AFRIKA
1.     Mawaziri wote wakuu waliokufaga wapo kuzimu wanateseka.
2.     Maraisi tokea 1949-2014, hakuna aliyeenda Paradiso wapo kuzimu wanateseka, wanatumikishwa na wanalia lakini msaada hakuna, wanafanyishwa kazi ngumu, wanachapwa bakora.
AMERICA, EUROPE, ASIA na mengine yote hali ni hivyo hivyo na inavyoonyesha walifikiri starehe walizokuwa nazo hapa ulimwenguni wakifa wataenda nazo wakamsahau Mwenyezi MUNGU na kumrejea yeye. Na wengine hata sijui majina yao ila ni sura zao wapo pamoja katika kundi la mateso. Yupo OSAMA, HITLER, IDDI AMINI, GADAFFI, SADAMU HUSSEIN, SAVIMBI na sababu wengine sijui majina yao niliona nchi zao inatimia 99% ya wote viongozi waliofariki tokea ulimwengu uumbwe wapo kuzimu hata Farao wa Misri yupo kuzimu.
NOTE:
Nawasihi watu wote wa ulimwengu huu mrejeeni YESU WA NAZARETI yeye ndiye tiketi salama, na uhakikishe unampata YESU wa kweli maana hata waliopo kuzimu walikuwa na yesu ambaye ni wa uongo na ndiyo maana wanateseka. Yapo majeneza ya shetani katika ulimwengu wa roho yanawinda wanadamu ili wakupate, na salama yako ni wokovu tu na utakatifu wa ukweli. Ni mabilioni ya watu wanavunwa na shetani kila siku, kila saa, je na wewe upo wapi? Uwe mjanja uokoke, waliopo kuzimu hawakuwa wajanja walipokuwa hapa ulimwenguni, ndiyo maana wamenaswa katika huo mtego. Mpokee YESU usikamatike na uwe makini usimpokee yesu wa uongo anakaa katika watumishi wa pesa, michango, harambee, ubatizo wa maji ya kikombe, masanamu, umchunguze anayekuongoza matendo yake.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE NAJIKABIDHI KWAKO, UNIANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA, MIMI SIMTAKI SHETANI TENA, MIMI NI MALI YAKO. AMEN.

NABII HEBRON.