Close

WAKENYA, TANZANIA, UGANDA, RWANDA, CONGO, MNAIBIWA PESA ZENU NA MALI ZENU NA BAADHI YA WATUMISHI WANAOTUMIA JINA LA YESU KUTOA HUDUMA ZA KIROHO.

[ad_1]

WAKENYA, TANZANIA, UGANDA, RWANDA, CONGO, MNAIBIWA PESA ZENU NA MALIZENU NA BAADHI YA WATUMISHI WANAOTUMIA JINA LA YESU KUTOA HUDUMA ZA KIROHO.

MATHAYO 10: 8 -9.

Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni  pepo; mmepata bure toeni bure. Msichukue dhahabu,wala fedha, wala mapesa mishipini mwenu.


Ujumbe huu siyo ni kwa watu wa nchi za Afrika Mashariki tu ni pmoja na sehemu nyingine zote za ulimwengu huu. YESU wa Nazareti  amechukia sana kwa ajili ya watumishi ambao wameibadilisha kazi yake na kuwa ni huduma  kama ya hospitali isiyotolewa bure  na zaidi  hata hospitali za kibinadamu baadhi siku hizi zinatoa huduma kwa watu bure.

Ila kwa ujumla YESU anasema msidanganyike na hawa watumishi ambao  ili akuhudumie au akuombee lazima utoe pesa kwanza au ili akupe appointment umueleze shida  zako utapita kwanza kwa cashier unalipa  kiasi fulani na unapewa risiti ndipo umuone akukubali.

Hao sio watumishi wanaoongozwa na MUNGU wa kweli, maana YESU aliwaambia nimewapa bure toeni bure, muwapende watu na msichukue  pesa wala dhahabu za watu. Sasa funguka, sasa hivi watumishi 98% ni matapeli, 45% ni wachawi kiwango cha kutisha na ni wanachama wa chama cha freemason wanatumia nguvu za giza kuendeshea makanisa, na makanisa haya siyo makanisa tena  imebakia kanisa jina tu mwenye kanisa yani YESU wa Nazareti ameshaondoka amebakia yesu wa uongo ambaye nyumba yake ya ibada huitwa pango la unyang’anyi wa kitumia jina la YESU na kumfanya YESU mwana wa MUNGU aitwe mnyang’anyi, wakati yeye siyo mnyang’anyi kabisa.

Ninawaandikia waraka huu mimi  Hebronkwa kila mtu atakaye usoma amshuhudie mwingine  ili watu wasinyang’anywe malizao na shetani. HAO NI WEZI,Soma MARKO(11:15-18). Na zaidi BIBLIA INASEMA NI WATUMISHI WA MATUMBO YAO. WARUMI 16:17-18.

Ndugu zangu  nawasihi waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho uliyojifunza mkajiepushe nao. Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii BWANA WETU KRISTO BALI MATUMBO YAO WENYEWE, NA KWA MANENO LAINI NA YA KUJIPENDEKEZA WAIDANGANYA MIOYO YA WATU WANYOFU.

Mtu mnyofu  ni wewe unayeambiwa toa pesa ndipo YESU atamaliza shida zako, na wana maneno laini mpaka utatoa pesa tu, ukiambiwa eti, huduma hii haina mfadhili yeyote, hapo funguka utambue hajatumwa aifanye hiyo kazi na YESU ndiyo maana, YESU hamfadhili anaangalia kwa watu , zaidi YESU akimtuma Mtumishi humtengenezea njia ili aifanye  hiyo kazi  na njia yenyewe siyo ya kuchangisha watu pesa au  kuomba omba watu pesa kwenye Radio na TV pesa za kuendesha vipindi .

YESU ni tajiri na sio omba omba kama kazi hiyo ni yake ataifanya mwenyewe na siyo kwa njia ya kuomba omba, na YESU ameniambia ole wao watumishi wafanyayo hayo, shoka lake tayarilipo shingoni mwao. Wamekuwa watumishi wa shetani japo wanasimama makanisani, ka nisa limekuwa kama soko, habari inayozungumzwa ni sadaka  tu, ndio wimbo , badala ya rehema.

Kama hauna pesa hauonekani wewe ni mtu katika kanisa , wenye pesa ndio wanaopendwa. Nikuulize swali hilondilo  kanisa alilolijenga YESU? Jibu Siyo.
Soma vitabu vyangu katika Blog yangu;  KANISA ALILO LIJEANGA YESU NA JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI, MPINGA KRISTO NI NANI? NA VINGINEVYO ILI UPONE, NA KAMA NI  MTUMISHI UNAYEFANYA BILA KUJUA UPONE UACHE  KUTOZA WATU PESA  MAANA NI DHAMBI.

Unapotoza watu pesa unapata dhambi, hivyo tambua kuwa mtumishi yeyote anayetoa huduma ya kiroho kwa kutoza au kuchangisha  mtu pesa huyo anayo dhambi na anatenda dhambi.  Ila wale walio wanachama wa freemason  kazi yao ni kuomba omba  tu pesa kwa waumini maana hawana mfadhili na mfadhili wao ni masikini na sababu ni shetani hana kitu hivyo  kazi yao ni kuomba omba tu kila siku kwa Radio na TV, semina na mikutano.

Hivyo ufunguke ujue ukweli matokeo yake utaibiwa baraka zako na nyota yako na ndiyo maana shida haziishi kwa wakristo makanisani wakati YESU ndiye jibu. Shida  ni mafarisayo na masadukayo wamejaa.

Usiogope fanyia kazi  nakuombea hata kama sijakuona, usiteswe tena.  Kama wameitwa na YESU  wamuombe YESU awape pesa, siyo kuwatumikisha watoto wake.

Imeandikwa amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu, amebarikiwa  amtegemeaye MUNGU, ona sasa watumishi wanamtegemea mwanadamu badala ya kumtegemea MUNGU, na zaidi nchi zinabeba laana kwa ajili ya watumishi wanaofanya mabaya tofauti na MUNGU. Mnabakia kulaumu viongozi wa nchi shida  ni wako wapi watumishi wa kweli ambao MUNGU huwasikiliza? 98% ni wa uongo, 2% ndiyo ya kweli na mara nyingine hata 2% haipo katika nchi ni 0%.

NOTE:
Usidanganyike tena, MUNGU amekupa wewe pesa ukipenda mtolee na uangalie mahali pa kutoa ili ubarikiwe, na usilazimishwe kutoa na kupangiwa kiasi cha kutoa. Na utoe ukipenda moyoni mwako. Ila usitoe kwa shetani na kwa mpinga Kristo. Roho akuongoze.

Ujumbe huu ni wa YESU wa Nazareti kwa ulimwengu wote, Ila nchi 4 nilizozitaja watu wanalia hata wamenitafuta niwasaidie walikosa pesa za kulipa ndio wasaidiwe na watumishi hasa KENYA na RWANDA, huu ni wizi umejaa, na TANZANIA.

NABII HEBRON

[ad_2]