WAKRISTO HAWAMTII YESU!!!

[ad_1]

Wakristo wengi katika ulimwengu wote hawamtii YESU WA NAZARETI kama ndiyo BWANA na mwokozi wao, bali wameanza kumtii yesu wa uongo na kukataa kumtii YESU WA NAZARETI, ambaye ndiye YESU WA KWELI, wengi mtajiuliza ni kivipi wakristo hawamtii YESU na inawezekana pia wewe ni moja wapo ambaye haumtii YESU, ila kama ulikuwa hauelewi natumaini utapona roho yako  na kumrejea YESU kwa heshima zote na kumtii kiimani na kimatendo.
Chanzo cha YESU kutoheshimiwa ni sababu ya mafundisho ambayo watumishi wanayafundisha ambayo ni ya uongo. Ukisoma Wagalatia 1: 6-9 utaona injili ilivyobadilishwa na sababu ya injili kubadilishwa ni ili ukiifuata tayari na wewe unapotea na inakuwa siyo tena neno lake MUNGU, tayari mwanadamu unakuwa una maneno ya shetani na siyo ya MUNGU tena, japo hautaelezwa, nakueleza mimi Hebron uelewe, ufunguke. Amenituma niseme kweli yake watu wamjue na wamrejee, kumrejea yeye ndiyo kumtii. Haina maana kujidanganya wewe ni mkristo wakati wewe haumtii YESU. Nitaelezea kwa ufupi yamkini utafunguka, mfano yeye aliye njia ya wokovu yaani YESU alikuja ili atuletee wokovu watu wote. Sasa kila ambaye hajaokoka mtu huyo hamtii YESU amedharau ujio wake aliotumwa na MUNGU kuja kuwaokoa watu mpaka sasa, na kama hujaokoka ina maana haumpendi YESU, kama ulikuwa hauelewi sasa elewa na uchukue maamuzi yako kutoka moyoni ili usiunganishwe katika mkumbo wa watu wasiomtii YESU.
Tunajua YESU alibatizwa ubatizo wa maji mengi akasema na sisi tubatizwe hivyo hivyo kama yeye. Sasa wanaojiita wakristo feki wamevuruga ubatizo wake wa maji mengi wakaudharau ubatizo wake wa maji mengi wakaleta wa kwao wa maji ya kikombe na maji ya kisima (huku ndiko kutokumtii YESU, huku ni kumdharau, na watumishi wote wanaotenda kinyume na Neno la MUNGU wote hawamheshimu YESU, hawamtii, wanamdharau na zaidi wanawaambukiza waumini japo wanampenda YESU dhambi ya kutomtii YESU. Na ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron unapaswa uelewe ukweli huu, kuhusu hawa watumishi ambao hawamheshimu YESU, ina maana ndani ya mioyo yao hawaongozwi na YESU aliye hai na wangekuwa kweli ni watumishi ambao wanaongozwa na YESU WA KWELI lazima wangemtii BABA yao, lakini sababu wanamilikiwa na baba yao wa uongo ndio maana kila kitu wanafanya tofauti na YESU.
Mfano mwingine, YESU alituma watumishi kwa watu wote akasema nimewapa bure, toa bure, cha ajabu watumishi hawamtii YESU wanachaji watu pesa na zaidi hawana huruma, ni wanyang’anyi wanaotumia jina lake kunyang’anya watu mali zao, na wengine wakifanya mikutano hawaombei watu bure wanakuwa na kiwango cha mtu wa private ni kiasi kikubwa cha pesa na wale ambao wataombewa wakiwa wengi nao wanalipa kiasi kidogo, na wale wasio na pesa hakuna kuombewa kabisa. (Hawa ni majambazi wa kiroho wanaotumia jina la YESU kutafutia pesa na zaidi siyo nguvu za MUNGU inayofanya kazi ndani yao ni uchawi, ila wanajificha kwa kivuli cha kujiita watumishi wa YESU).
Sasa kimwili pata picha utaona sababu ya watu kutokumtii YESU au kumkubali ni sababu watumishi wao ndio wamewapandia hiyo mbegu katika roho zao katika njia ya mafundisho ya uongo.
NOTE:
Ukiona unafundishwa jambo lolote kinyume na YESU ujue huyo anayefundisha hayupo na YESU WA KWELI na hamheshimu YESU na anakuingiza na wewe katika mtandao wake uangamie roho yako, mfano watumishi wote wanaobatiza watu kwa majina yao, wanawanyoa watu nywele makanisani, wanabatiza ubatizo wa maji ya kikombe, wanaofanya biashara na kuwa na mabenki, wanaoabudu sanamu, kuandika majina katika sadaka, wenye partners na wengineo wanafanya uovu na kwenda kinyume na biblia. Hao wote mahali pao ni jehanamu, na hao ndiyo hawamtii YESU, ndiyo wanafikii wanamtaja ila hawafanyi kama anavyotaka.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, ninarejea kwako, naacha dhambi, uniongoze wewe nikutii wewe, nisimtii shetani tena na yesu wa uongo, Amen.
Zaidi soma makala ya Nabii Hebron ufunguke na kukua kiroho.

NABII HEBRON.

[ad_2]