Close

WANADAMU WALIO/WANAOSULUBISHWA KWA NIABA YA YESU WANAMKUFURU MUNGU

[ad_1]

Kila mtu anajua kuwa YESU WA NAZARETI ni mwana wa MUNGU wa pekee na hakuna mwana mwingine wa pekee kutoka kwa MUNGU katika ulimwengu huu na yeye ndiye mkombozi wa pekee zaidi yake hakuna wote ni waongo na zaidi alitabiriwa atazaliwa na atakufa na kufufuka na kupaa na ikatokea. Na sasa tunasubiri Neno la MUNGU litimie kwa kurudi mara ya pili ambao ndiyo mwisho. Katika ulimwengu huu wapo watu wanaosulubishwa msalabani eti wanajitolea kila mwaka wasulubishwe badala ya YESU, na wanaokubali kusulubishwa wanaona wanatenda vyema kabisa ila nawaeleza watu mnaojisulubisha badala ya YESU wote mmemkufuru MUNGU. Kwa kufanya hivyo ina maana unalipinga Neno la MUNGU, aliposema kwa kupigwa kwake sisi sote tumepona.

Pili haijaruhusiwa katika Neno la MUNGU eti wanadamu wasulubishwe badala ya YESU, wakati MUNGU alimtoa mwanae aliyempenda aje atufie sisi msalabani ili tupone. Sasa jiulize huyu mwanadamu anayesulubishwa msalabani yeye anasulubishwa kwa ajili ya nani tena? Jibu hakuna, anajitesa bure na zaidi amezidi kumkosea MUNGU na kupinga Neno La MUNGU au kulibadilisha Neno la MUNGU. Na zaidi YESU kusulubiwa ilikuwa ni ahadi ya MUNGU. Je hawa wanadamu wanaosulubiwa wakati wa Pasaka kwa niaba ya YESU je, ni ahadi ya MUNGU? Jibu siyo. Na kama siyo ahadi ya MUNGU ya nini kumkufuru MUNGU? Kama ulikuwa hauelewi tubu sasa na uache.

NABII HEBRON.

[ad_2]