Close

WANAOABUDU SANAMU BABA YAO SIYO MUNGU (2WAKORINTHO 6:14-18)


Neno la MUNGU linasema: Msifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa; Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na shetani? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, ya kwamba, mtakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana. Msiguse kilicho kichafu, Nami nitawakaribisheni. Nitakuwa BABA kwenu nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.
Ndugu msomaji, huu ni wakati wa kuijua kweli mpaka YESU wa Nazareti atakaporudi kuja kuchukua wale wake. Ila wengi katika ulimwengu huu wamepotea japo wanajiita wakristo, na mimi siku ya leo nakufungua ufahamu wako ufunguke na zaidi uendelee kusoma makala ya nabii Hebron utajifunza mengi ili uwe salama. Katika ujumbe huu wa MUNGU, ni kwa ajili ya watu wake wa dunia hii bila ubaguzi wa rangi au jinsia yoyote kwa anayetaka kupona, na ili MUNGU awe baba yake. Badala ya wanadamu kuwa watoto wa shetani bila kujua kwa sababu ya kutokufundishwa ukweli wa Neno la MUNGU kama alivyotaka, na badala yake ikachanganywa maneno ya dini au taasisi na kusudi la MUNGU. Tambua taasisi zote na dini zote na madhehebu hayajatokea kwa MUNGU dini iliyo safi ni wokovu tu ulioletwa na YESU bila kuchanganywa na na lolote tofauti na MUNGU, ila dini na taasisi zina sheria zake au kanuni zake halafu wakachanganya na Neno la MUNGU. Hapo ndipo uharibifu ulianzia na wanadamu wakaanza kulishwa Neno lisilo sahihi ndani ya mioyo yao ili kuziua roho za wana wa MUNGU na kufarakanishwa na MUNGU na MUNGU kuwakataa wanaoabudu sanamu na kuwakana sawa sawa na neno la 2Wakorintho 6:14-18) MUNGU anasema wote wanaoabudu sanamu yeye siyo BABA yao, na hata katika mstari wa (16) anasema pana patano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? MUNGU huyu huyu anasema katika nyumba yake haitakiwi sanamu yoyote ile yeye hana shirika nazo. Hebu ona sasa jinsi kanisa limekuwa (pango) na siyo kanisa tena maana vitu hivyo havitakiwi hata vikae katika hekalu. Je, Unaona jinsi watu walivyopotea na kumgeukia shetan? Na waumini walijua BABA yao ni MUNGU aliyeiumba dunia, kumbe matokeo yao baba wao wa sasa ni mungu mfu (ewe muumini ukiona hayo yanafanyika katika nyumba yoyote ya ibada tambua hayo ni kwa mungu mfu 100%). Na MUNGU amesema tokeni hapo, usiguse uchafu kimbieni na utakapotoka au kujitenga na madhabahu hiyo hapo ndipo MUNGU atakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na kike.
NOTE:
  1. Ili uwe au MUNGU awe ndiye Baba yako usishiriki ibada hizi hata kama ndani ya hekalu kuna sanamu. Haijalishi jina la YESU linatajwa. Kataa elimu potofu ya mapokeo tofauti na yaliyoandikwa katika Biblia takatifu na kupindisha au kulibadilisha Neno la MUNGU. Wanaofanya hivyo ndani yao ni roho wa shetani ndiye anayewaongoza na ndiye baba yao 100%. Funguka akili yako, tupa masanamu na uyachome. Kumbuka hata Musa alichoma na kuzipasua alivyokuwa jangwani na ndipo wale wana wa Israeli wakapona na MUNGU akawa ndiye Baba yao akawaongoza. Huu ni mfano halisi 100% ukiabudu sanamu au hata zikikaa tu kanisani, tayari mnaoshiriki hapo siyo watoto wa MUNGU, hata anayeongoza au kusimamia ibada hizo huyo pia siyo mtoto wa MUNGU, ni wa shetani 100%. Huu ni ufisadi.
  2. Leo hii amua mwenyewe kama unataka MUNGU ndiye awe Baba yako kwa kuacha kushiriki ibada hizo na hata kufika nyumba za ibada zilizowekwa hata kama ni sanamu ya YESU, au chochote kile. Ni uchafu (Beliari) ufisadi. Kwanza YESU siyo sanamu, hata mwanadamu siyo sanamu. Ili kupona jitoe huko kabisa na wewe utapona ila kama bado upo huko ujijue wewe ni mgonjwa wa kiroho na umeshakufa kiroho, na waliokufa kiroho baba yao ni mungu mfu (ibilisi) na ibilisi anazo kanuni zake za kuabudiwa katika mahekalu ni kuweka masanamu. Na yeyote anayeshiriki siyo mwana wa MUNGU, nukuu katika neno nilivyokufafanulia.
  3. Nimekufundisha natumaini umeelewa kabisa. Chagua mwenyewe. Ni chaguo lako leo utamtumikia MUNGU aliye hai au mungu mfu wa masanamu na katika mahekalu yake?
  4. Na kiongozi wa ibada hizo huyo ni mjumbe wa shetani 100% anatumiwa kuwafarakanisha wanadamu wasijue kama MUNGU ndiye Baba yao na kuhamishiwa upande wa shetani (makristo wa uwongo). Zaidi soma kitabu cha Nabii Hebron MPINGA KRISTO NI NANI?

Ubarikiwe

Nabii Hebron