WATU WOTE AMBAO HAWAJABATIZWA UBATIZO WA MAJI MENGI YESU WA NAZARETI AMENIAMBIA HAO WOTE SIYO WAKRISTO.

[ad_1]


Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron au unaweza kuiita makala ya YESU WA NAZARETI, aliye kufa na kufufuka na sasa yupo mbinguni kwa BABA yake. Mimi jina langu linatumika tuu kwa sababu ni mimi ndiye ninayekufikishia ujumbe huu. Ila yaliyomo ndani ya makala ni jinsi anavyonieleza na mimi ndipo hukufikishia ujumbe wake kwa mataifa yote na watu wake ili wapone na wajue ukweli wa MUNGU na siyo uongo wa shetani aliouingiza katika wanadamu ili wasiwe wakristo halisi, bali ni wakristo wa uongo. Na ujanja aliyotumia shetani, anajua watu wengi wanampenda YESU na hawampendi yeye. Hii ni sababu jina la YESU linalothamani, lingekuwa halina uthamani watu wasingeukimbilia ukristo.
                                
Sasa alichokifanya hapa ili awateke wanadamu na hata wakijiona wao ni wakristo halali na kumbe ni wakristo feki. Shetani alianzisha ubatizo wake wa kikombe (maji ya kumwagiwa kichwani tuu na siyo kuzama kwenye maji kama yeye alivyotii akabatizwa na Yohana mbatizaji. Soma (Yohana 3: 13- 16), ni ubatizo uliotoka kwa MUNGU aliye hai ndiyo maana unabatizwa kwa jina la BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU. Sasa tendo hili likiwa tofauti na lile la MUNGU alilomtuma Yohana aje afanye kwa njia ya maji mengi tayari hapo ni kumuasi MUNGU na kuvunja sheria zake alizozihakikisha akipiga muhuri ya kuwa (NDIZO TU).

Nitatoa mfano katika ulimwengu huu umeshajiuliza swali Je? Ni kwa nini bunge likitunga sheria hata kama wamezipitisha muda huo hazianzi kutumika mpaka Rais wa nchi azikubali na kusaini na kupiga muhuri. Na endapo hatazisaini sheria hizo hakika hazitatumika na serikali hiyo. Je? Unaelewa mpaka sasa? Sasa nakurudisha katika biblia ambayo ndiyo katiba ya mkristo ambayo maneno yake ameyahakikisha MFALME WA WAFALME yaani MUNGU ili watu wote waifuate na akasema kisiongezwe neno lolote wala kupunguzwa akasema na OLE WAKE yule atakaye vuruga au kufanya tofauti (Ufunuo Wa Yohana 22: 18-19).

Sasa katiba ya MUNGU imevunjwa na baadhi ya wanadamu wenye kiburi cha kumdharau MUNGU. Na wengine wamevunja au kushiriki bila kujua; sababu hawaijui kweli, ila leo utaijua kweli nayo itakuweka huru. Na ujumbe huu ni kwa ajili ya ulimwengu wote na mataifa yote.

Tarehe 15.11.2013 muda wa saa tisa mchana kwa saa za Afrika mashariki, nilikuwa katika ibada katika kanisa langu. Kabla sijaanza kuhubiri akaja mbele yangu, akaniambia, Hebron wafundishe watu wote wanijue mimi na wasiangamie. Kazi ya kanisa imeharibika, kanisa limenikataa ndani ya mioyo yao ila kwa midomo yao hunitaja tuu wala mimi sipo nao, sababu mimi na BABA yangu na ROHO MTAKATIFU tunaliangalia Neno La MUNGU tuu kama lilivyo, likiwa tofauti tayari hilo silo Neno La MUNGU aliye hai. Neno lake halibadilishwi ameshalihakikisha na vifungu vyote. Niliogopa! Akaniangalia machoni akaniambia USIOGOPE. Haya niliyokueleza waeleze watu wote nawataka wawe watoto wangu yaani wafuasi halisi wa mimi YESU WA NAZARETI na niliye pia BABA yako.

Akaniambia nipo na wewe katika ibada na Malaika na Serikali yote ya mbinguni tumekuja kushiriki pamoja na wewe na kanisa lako ulilokabiziwa na BABA, uliongoze mpaka ule mwisho wa ulimwengu huu au maana nyingine mpaka ujio wangu mimi mara ya pili kuja kimwili; akamaliza, akaniacha, nikatafakari nikiwa nimekaa kwenye kiti japo muda huo kanisa walikuwa wanaimba na kumsifu MUNGU, ila wao hakujifunua kwao ili wamwone. Na mengi aliniambia ila sitayaandika hapa.

Ndugu msomaji au wasomaji wanaopenda ukristo Je? Kwa nini unabatizwa ubatizo wa maji ya kichwani halafu unajiita wewe ni mkristo halali? Nimekueleza ukweli, YESU ameniambia watu wote na watakaoendelea na ubatizo huo, WAJIJUE WAO SIYO WAKRISTO WA KWELI AU WAFUASI WANGU WALA SIYO TAWI LANGU, wala MUNGU siye mkulima au mwanzilishi wa ubatizo huo wala Serikali ya Mbinguni. Na hata katika biblia aliyoichagua yeye na akasema tuifuate hapo. Na kama haupo ina maana wote waliobatizwa ubatizo huo wa kikombe wamewekewa pando lisilojulikana, na kama halijulikani asili yake na wote walioshiriki pando hilo la shetani na wao ni pando la shetani.

YESU anarudi muda wowote ameniambia, waambie wanadamu wanirudie mimi na ile siku wengi watalia na kusaga meno wakisema wao ni wakristo halafu nitawaambia siwajui nyie, wote wanaojiita wakristo na wamebatizwa ubatizo wa maji ya kikombe, hamtaenda mbinguni, huo ndio ukweli, na kama huamini  ile siku ya mwisho utakumbuka maneno haya. Nimekupa siri ili upone hata wanaobatiza ubatizo wa kikombe ameniambia hao siyo watumishi wake 100%.

Yeye hakufundisha wanafunzi wake ubatizo huo na aliwafundisha ili sisi tuige tufuate mfano huo huo. Sasa, nikuulize swali, hivi hata kibinadamu Mwalimu anavyokufundisha darasani kitu fulani si iliukijue na ukifanye hicho? Sasa, anapotunga mtihani akakuuliza swali alilokufundisha ukajibu lingine tofauti je? Atakupa vyema au tiki (√) au atakukata (X). Sababu ya kukupa X ni umekosea. Turudi katika somo la ubatizo aliouamrisha na kufundisha hapa Mwalimu ni MUNGU aliye hai na wanafunzi ni wanadamu. Je? MUNGU alifundisha ubatizo upi ufuatwe?
  1. Ubatizo wa maji ya kikombe? Jibu siyo hivyo X
  2. Alifundisha ubatizo wa maji mengi kwa watu wote kijito cha utakaso na alimtumia Yohana Mbatizaji kufundisha.

Ubatizo ni kadi ya mwanachama au mfuasi wa YESU wa kweli na kadi original ni ubatizo wa maji mengi yanayotembea katika kijito cha utakaso. Ila kadi feki ya fojari ya wanachama au mfuasi wa YESU wa uongo (kuzimu) ni ubatizo wa kikombe. Mpaka hapo unazidi kuelewa, sasa tupa hizo kadi feki za ukristo yaani ubatizo usiopo katika biblia. Ukibatizwa na kuokoka kikweli kwa ubatizo wa maji mengi na uhame kabisa hiyo kambi ya wakristo feki na uwafundishe na wengine ili wasiwe feki, maana najua wengi hawapendi kuwa mkristo feki au siyo? Sasa umejijua vizuri na usiwe mchoyo kumweleza na mwingine hata ikibidi mwambie aingie katika website ya www.prophethebron.org na aingie katika blog yangu atapona na wewe utabarikiwa sababu YESU atazidi kuwapata wanachama hai na sio wafu.

Cha ajabu baada ya kutafakari ujumbe huu kwa muda ya siku mbili zaidi na nikiendelea kuomba. Nikapiga picha katika ulimwengu wote, nikaangalia jinsi wakristo wanaojiita kwa jina lake wanaempenda wanapigwa upofu na kupewa kadi feki pasipo wao kujijua. Na hii yote ilisababishwa na wamisionary walioleta injili Afrika na katika mabara mengine hawakuleta injili ya kweli kama ilivvyopangwa na MUNGU. Wakabadilisha, hii ndio injili ya mapokeo ya wanadamu!

Sasa nikuulize swali, Je? Wewe unataka injili ya wanadamu au injili ya YESU? Jibu ni YESU WA NAZARETI. Sasa kwa nini watu wanapewa injili za wanadamu badala ya injili ya YESU ya kweli? Sababu ni baada ya wale mitume wa kwanza wa YESU kuondoka na wengine kuuwawa na wale wanafunzi wa mitume walipokufa au kuuwawa, ndipo injili ikabadilishwa. Na sababu za hao mitume kuuwawa mfano; Petro, hao waliomuua walimuua kwa sababu ili kuvunja ukristo wa kweli na kuyaharibu au kuyakataa mafundisho ya ubatizo wa maji mengi ile waliokataa. Ndiyo maana wakauwawa, hawa ndiyo majasiri ndiyo maana wapo mbinguni wamekuwa ni moja wapo ya wazee 24 waliopo mbinguni kwa sasa.

Na pia ukiangalia wale waliomuua Petro enzi hizo na wakaweka kaburi lake mpaka leo hii, Je? Kama kweli wangekuwa wanamuenzi mtume Petro kwa yale aliyoyafundisha wangebatizwa ubatizo wa maji mengi. Ila sababu walimuua ni ili wapoteze kumbukumbu za mafundisho ya kweli ya ubatizo wa maji mengi na kuwafanya watu wawe wakristo feki, ambao YESU ameniambia hawajui kabisa. Hata hao wanaotaja majina ya watoto wa YESU yaani wale mitume wa kwanza, ingekuwa kweli wana waheshimu au kuwapenda  wangebatizwa ubatizo wa maji mengi, ile ambayo walitumwa na YESU waineze katika ulimwengu wote.

Nikuulize swali, sasa je? Huu au hii injili ya ubatizo wa maji ya kikombe huku ndiko kueneza injili ya kweli au ndiko kuua ukristo? Jibu, ndipo kuua ukristo. Wanabatiza ubatizo tofauti na alioagiza YESU WA NAZARETI (Mathayo 18: 19-20) “wabatizwe wawe wanafunzi wangu na mkiwafundisha kuyashika yale yaliyoyangu.” Sasa ewe mwanadamu hapo watu wamepigwa chenga na shetani na leo hii ujue kama unabatizwa ubatizo wa kikombe ujue shetani amekuweza na amekupiga chenga na akakufunga goli yeye amekuwa mshindi kwako!

Fanya zoezi upya, ubatizwe ubatizo wa maji mengi, hapo utakuwa MKRISTO HALISI. Kinyume na hivyo jehanamu inakuhusu tokea hapa duniani, hiyo ni ticket ya kuenda jehanamu hata kama unatoa sadaka, unasali sana, unaimba na kumsifu. Mwenye chama siku akija atawachukua wale tu wanachama wenye kadi zake na awape makao. Na hata sasa wote wote wanaokufa wakiwa wamebatizwa na kikombe wanaenda jehanamu na nimewaona LIVE LIVE. Zile ibada za maziko ni imekuwa kama desturi tena.

Na waonye wale wanaosema wewe uliyekufa umetutangulia mbele za haki na sisi tutakufuata. Laiti ungejua ungefuta hayo maneno, haujui kama ameenda mbinguni au kuzimu. Kwa kinywa chako unajipatanisha na usichokijua na hiyo roho inakaa ndani yako. Na mnavyosema mbele za haki, ni kweli, haki kweli kweli inafuatwa. Siyo kama haki za hapa duniani, unaweza onewa, pendelewa, honga upate msaada. Huko hakuna muda ni sasa na leo, maana hata kesho hujui kama utaishi; fanya maamuzi.
(SOMA KITABU CHA UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE CHA NABII HEBRON).

OKOKA
BWANA YESU WA NAZARETI NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU ZOTE UNIANDIKE KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE NIBADILISHE NIWE MKRISTO WAKO WA KWELI, NIONGOZE NIBATIZWE UBATIZO  WA KWELI. AMEN.
NOTE
Fanya maamuzi haraka YESU WA NAZARETI anakuita uwe wake. Ukigoma ubatizo wake na kukaa katika utakatifu hautamuona milele. Ila jehanamu ndiyo imeandaliwa shetani na wanadamu watakao muasi YESU WA NAZARETI.


NABII HEBRON

[ad_2]