WATUMISHI WANAOJIITA WAO NDIYO ELIYA WA MWISHO WA SASA NI WAONGO 100%

[ad_1]

Wote wanaojiita ndiyo Eliya wa mwisho, ndugu msomaji hawa wote ni waongo kabisa, YESU wa Nazareti alipo kuwa anaongea na mimi akaniambia mambo mengi sana ila hayo ni mpaka aniruhusu kwa muda wake nitayasema waziwazi . Akaniambia Hebron, hivi hawa wanadamu wamechanganyikiwa? Mbona wamekuwa waongo na kujipachika au kujiita wao ndiyo Eliya? Nikanyamaza , akaniambia mimi YESU wa Nazareti, sijawaita, wala Baba yangu wala serikali ya mbinguni. Akaniambia tazama katika nchi zote katika ulimwengu huu ,kuanzia Tanzania ni watumishi wengi wanaojiita wao ni Eliya wa mwisho. 

Akaniambia siyo kweli , ole wao wanaomkufuru ROHO MTAKATIFU akaniambia zaidi ya watumishi 3752 katika ulimwengu huu wanajiita wao ndiyo Eliya wa mwisho, akaniambia Eliya wa mwisho katika hao wote hakuna hata mmoja, atawaaibisha kwa jinsi anavyojua yeye mwenyewe, niliogopa sana kusikia hivyo maana ni watumishi wengi katika nchi zote wanajiita Eliya wa mwisho na kumbe wanasema uongo na kama wanasema uongo ndani yao baba wa uongo ndiye anayeishi ndani yao. Ndiyo maana wanasema uongo, hata kumsingia MUNGU aliye hai. 

Ila nanukuu maneno ya YESU wa Nazareti. Hao wote roho ya upotovu ndiyo imewaingilia ipo ndani yao inafanya kazi ila YESU atayadhihirisha sasa kwa ulimwengu wote. Maana MUNGU amekasirika sasa, sawa sawa na enzi zile alipoichoma Sogoma na Gomora, na pia enzi za Gharika. Imefikia mahali hata watu wanajiita wao ni YESU,!! Je, anayejiita hivyo huyo alikufa na kufufuka? Alipaa kwenda mbinguni? Je anaishi mbinguni au duniani ? huyo au hao wanaijiita wao ni YESU ni waongo ni shetani ndiye anakaa ndani yao ili kuupoteza ulimwengu huu. Na wengine wanajiita MUNGU, hao wote ni waongo kabisa. Ndani yao ni roho ya mpinga kristo inayofanya kazi msidanganyike. 

Nyakati hizi ni mbaya sana, shika sana ulicho nacho asije mwizi akakuibia, ukiwaamini tu watumishi waongo kama hawa tayari ujijue umeibiwa imani yako. Hiyo ndiyo maana ya Linda sana ulichonacho, hata ukimuona yeye ndiye MUNGU tayari unaibiwa ulicho nacho, hata akikubatiza kwa jina lake tayari umeibiwa ulichonacho haijalishi ni ubatizo wa maji mengi tayari umefungwa hicho ni kifungo. 

Ili upone, ubatizwe upya ili livunjwe hilo agano la jina lake, kinyume na hapo mbinguni hautaenda. Na wengi wameachwa na YESU sababu ya uovu wa kujifananisha na MUNGU na kubatiza watu kwa majina yao na kumuasi MUNGU , Japo walionywa wakakataa kutenda ya MUNGU. MUNGU akawapa kisogo na hii ni milele wala hawatabadilika. Na ili muamini utayaona ile siku ya mwisho. 

Nabii Hebron .

[ad_2]