Close

YESU NDIYE MZABIBU WA KWELI


YESU NDIYE MZABIBU WA KWELI
Je, wewe upo kwa mzabibu wa kweli au mzabibu pori?
Ndugu msomaji na uliyeumbwa kwa mfano wa sura ya MUNGU, wa nchi yoyote au rangi yoyote au jinsia yoyote na dini yoyote, ujumbe huu ni kwa watu wote, iwe unampenda MUNGU au humpendi, au yawezekana umeshindwa kumuelewa YESU wa Nazarethi jinsi alivyopanga sheria zake zifuatwe ili kila mtu apone na aurithi ufalme wa MUNGU.
NENO la MUNGU linasema YESU ndiye mzabibu wa kweli na pia YESU ndiye njia ya uzima na hakuna yeyote atakayemuona MUNGU pasipo kupitia kwake. Hii ni fomula aliyoipanga MUNGU peke yake kwa ajili ya ulimwengu mzima, maana sisi sote ni mali yake na anataka tupone sababu injili yake imebadilishwa, watu wanamfuata YESU kwa njia ya mapokeo ya wanadamu badala ya mapokeo ya MUNGU, na kama watu wanaishi kwa mapokeo ya wanadamu, hakika hawatamuona MUNGU. Haya yote kaniambia YESU, niueleze ulimwengu wote, na hakuna atakayeweza kunizuia kusema kweli yake. Usifikiri ni mwanadamu ndiye aliyenituma. Ukitumwa na mwanadamu, utafanya hayo hayo wanayoyataka wao kwa faida zao, na hawana MUNGU. Sasa ndio wakati wa kujua ukweli kuhusi YESU, na itafanyika mpaka yeye arudi kimwili. Wana wa MUNGU wanateseka sana 98% umwenguni mwote kwa sababu hawaujui ukweli. Injili imefanyika kama mapokeo ya mwanadamu na kuacha yale yaliyoamriwa na MUNGU yafuatwe, na katika NENO Yohana 15:1-7 kwa siku ya leo nitafundisha na hakika utafunguka ufahamu wako, na utajijua upo wapi. Je, ni wa MUNGU anu ni wa shetani, ila sikulaumu wewe. Hii ni kwa sababu 98% viongozi ulimwenguni mwote wamemsaliti YESU, wanamtaja jina lake kwa midomo tu, ila ndani ya mioyo yao ni mbwa mwitu. 45% ni wachawi kupita hata waganga wa kienyeji. Wamefanya kanisa ni dili la kutafutia pesa na kuwaibia nyota. Hao ndio mmanabii wa uongo, ila usiogope, leo YESU atakutoa, na hao wataabishaji wa wana wa MUNGU mwenye kanisa anawashughulikia  yeye peke yake na yupo kazini, kwa wale wanao tumia nguvu za giza, freemason, wanalitambua vizuri, na ni mwisho.
NENO la MUNGU katika injili linasema, YESU ndiye mzabibu wa kweli, na BABA yake ndiye mkulima. Mkulima huyu ni MUNGU aliyempanda YESU, na YESU ndiye mzabibu na wanaomwamini yeye na kumfuata yeye 100%, ndio matawi ya YESU wa Nazarethi.
Ndugu msomaji, soma kwa makini. Ipo siri kubwa sana hapa, ambayo umeshindwa kuitambua maisha yako yote, ila leo YESU anakufunulia huu ufunuo, ili ufunguke. Siku hizi kanisa ulimwenguni mwote 98% siyo mzabibu wa YESU, ni mzabibu pori (au ni mzabibu wa shetani), na 2% ndio mzabibu wa kweli wa YESU kristo wa Nazarethi
NITAANZA KUELEZA KUHUSU MZABIBU WA KWELI.
YESU anaposema yeye ndiye mzabibu wa kweli na MUNGU ndiye mkulima, na wale wanaoyafuata yale yote yaliyoandikwa katika kitabu kitakatifu yaani Bilblia na kuyatenda, hayo ndiyo matawi ya YESU.
Nitatoa mfano kidogo: Tunajua YESU ndiye njia ya uzima na kweli, na haya yote anayotufundisha YESU, haya yanatoka kwa BABA yake na ametuletea habari hii njema, ili na sisi tufike mahali alipo yeye, kama ilivyo na akatupa mwongozo kabisa, wewe ukikaa ndani yake, omba lolote utatendewa. Ina maana na yeye anatenda na usipokuwa ndani yake, utatupwa nje. Ndani ya YESU, ndipo palipo na uzima, ila nje ya YESU, ndipo palipo na mauti ya milele na jehanam na mateso. Siku hizi katika ulimwengu huu, shetani ameliteka kanisa kupitia ufunuo huu, na shetani kulifanya kanisa liwe mzabibu pori na ndio maana majibu hamna kanisani, watu wamebakia kupunga upepo tu, muda wa ibada ukiisha hutawanyika bila baraka wala majibu. Shida ndiyo fomula ya kanisa 98% ulimwenguni mwote, tunajua kwamba baraka za shetani ni nuksi, magonjwa na vifungo; sasa iweje wewe uliye Mkristo ambaye ni tawi la YESU hayo yakupate, na hata ukiomba haupati majibu? Umebakia ni kufunga miaka na miaka, hamna kitu na umeokaka? Ufunguke, hii ina maana wewe haujaunganishwa katika mzabibu wa kweli ambao ni YESU, haijalishi upo kanisani. Chunguza, je, hilo kanisa ni mzabibu wa kweli au ni mzabibu pori?
Mzabibu wa kweli ili ujijue kama upo sehemu ya huo mti, na wewe ni tawi lake YESU wa Nazarethi, kwanza chunguza injili inayofundishwa mahali hapo, ukikuta ipo kinyume na YESU aliyoyaagiza yafuatwe, hakika ujue na wewe haujaunganishwa kwenye mzabibu wa kweli. Nitaelezea kwa kifupi tu mfano wa YESU alivyokuwa ulimwenguni hapa aliingia kanisani (Marko 11:15-18) uisome. Alikuta kanisa linafanya biashara na minada ndani ya nyumba ya sala. Aliingia akavuruga na kukataa, leo hii, kanisani yamerudishwa, na kama yamerudishwa, ujue hilo ni tawi la shetani. Nikuulize swali, je, YESU ameyaruhusu? Jibu hapana kwa hiyo (Yohana 15:6), hilo tawi siyo la YESU na hunyauka na watu wote waliopo hapo na mwisho ni kutupwa motoni na kuteketea.
Imeandikwa, sadaka ni siri yako na MUNGU – leo andika jina na kiasi
Imeandikwa, mtoe bure huduma – leo toa pesa, hii ni shetani na hata huo uponyaji siyo wa YESU.
Imeandikwa, Mathayo 28:19-20 mkawabatize watu na kuwafanya  kuwa wanafunzi wangu, na kuwafundisha yale yote niliyowaamuru. Sasa hata ubatizo hebu angalia, soma Biblia, hakika hautaona ubatizo wa kikombe 100% tafuta na wewe, huu haujatoka kwa MUNGU, na mliobatizwa hivyo wote siyo tawi la YESU, mbadilike mbatizwe upya asema BWANA YESU. Mtaangamia, huo ndio ukweli. YESU hakufundisha huo ubatizo. Huo ubatizo asili yake ni mzabibu pori ambao umepandwa na joka kuu ambaye ndiye baba yake shetani, na wewe uliyebatizwa hivyo  kabatizwe upya upone, imeandikwa; ole wake atakayeongeza maneno ya unabii wa kitabu kitakatifu; soma kitabu cha Ufunuo wa Yohana 22:18-20 na nyie wote majina yenu yameondolewa katika ule mti wa uzima ambao ndio mzabibu wa kweli yaani YESU wa Nazarethi, lakini usiogope, ufurahi maana unapoujua ukweli ndipo unapona roho yako. Na hata ambao hawajabatizwa kama YESU, hao sio wanafunzi wake, ni wanafunzi wa mzabibu pori. Huu ndio ukweli, na anayebisha asome Biblia vizuri, ataelewa. Na inawezekana wengine hawajui, wapo wapo tu. Uwe una masters degree ya Biblia, tafuta, onyesha ni wapi  huu ubatizo wa kikombe upo, jibu haupo. Unajua jambo lolote linalofanywa na kanisa lolote, ulimwengu mzima kwa kubadilisha mfano katika ubatizo tofauti na YESU. Hilo sio tawi lake.
MZABIBU PORI:
Huu ni mzabibu unaoota porini au msituni, hauna mtu wa kuutunza na kuupalilia, wala kuunyeshea maji au kupewa huduma yoyote, hata ulinzi. Wanyama huweza kuula wote au kuukanyaga, matunda yake hayafai kwa wanadamu na matawi yake hayana mwelekeo. Katika Ufunuo wa Yohana 15:1-7 hapa ndio mahali shetani aliiba ufunuo na kuubadilisha ufunuo huu na kuuingiza kwa njia ya mapokeo ya mwanadamu na wao wakayakubali kupitia viongozi watangulizi, na hawa waliofuatia wakayarithi ya wanadamu badala ya MUNGU.
Mfano;
Imeandikwa usiabudu chochote isipokuwa MUNGU peke yake – leo sanamu inaabudiwa
Msikope wala kulipa riba kanisa – leo baadhi yanakopa
Mbatize ubatizo wa maji mengi – leo ubatizo wa kikombe
Msichangishe pesa, nimewapa bure toeni bure – leo leta pesa uombewe
Rebeka ndoa yake ilibarikiwa tu – leo kanisa linafunga ndoa kwa shida na raha
Sadaka ni siri yako – Leo siyo siri; andika jina na kiasi kwenye bahasha
Sadaka ya mtu ni ibada kamili na MUNGU, mtu akitoa shilingi hamsini au sarafu, mtumishi anachukua za noti tu na hizo za chuma (sarafu) baadhi ya watumishi huzitupa chini, au kwa dharau anasema eti MUNGU hapokei hizi pesa, huyo ni mtumishi wa pesa. Ukisoma katika injili, utaona mama mmoja alitoa ile sarafu, tena YESU akaithamini zaidi. Sasa haya yametoka wapi? Jibu ni mzabibu pori.
Freemason (watumishi):. Hawa wote ni matokeo ya mzabibu pori ambao mkulima ndiye joka kuu na shetani ndiye huo mzabibu na wanadamu wanaoyafanya kinyume na alivyoagiza YESU ndiyo hayo matawi ya mzabibu pori, na hata kibinadamu, mzabibu au tunda pori katika shamba hukatwa na kutupwa au kuchomwa moto na kuteketea.
Katika mkutano au kanisa ulimwenguni mwote, ambalo lipo kinyume na amri za MUNGU, na  mtumishi  analitaja jina la YESU, hata kufanya miujiza, funguka ufahamu, hiyo siyo roho ya MUNGU wa kweli. Imeandikwa, uchunguze kila roho. Iko maana kubwa sana, ila siku ya leo ufahamu unakurudia, na kama ulikuwa chini ya mzabibu pori, leo utapona na wale maajenti wa mzabibu pori, ole ya MUNGU itakuwa tu juu yao. Ndivyo alivyoniambia.