ambaye ndiye Bwana na Mwokozi wa Mataifa yote, pia ndiye Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana na hapana Mfalme mwingine zaidi yake. Mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo,
Publications
Need Prayer? We Would Love To Pray For You.
We have a strong sense of community with parishioners.
Ndugu msomaji usiogope, huu ndio ukweli halisi alioniambia mwenye kanisa, yaani YESU. Mengi utayakuta kwenye vitabu nilivyoviandika, CD na DVD. Hakika utafunguka ufahamu wako utajua jinsi KANISA lilivyotekwa na shetani. Na zaidi, YESU alipokuwa akinifundisha, alinionyesha na kunifunulia ulimwengu wote, jinsi ulivyo kwa sasa, akasema watumishi ndio wanatumiwa 98% kuliharibu KANISA. Kwa mfano aliniambia, idadi kubwa ya watumishi wakubwa ulimwenguni ni member wa freemason, akaniambia hao sio watumishi wake.
Haijalishi wanalitumia jina lake, hao ni manabii wa uwongo, na asili yao ni manabii wa uwongo, na mengine mengi utayakuta huku kwenye website na kwnye blog; YESU ameshuka Tanzania kupitia watu wake ila wale waovu wataangamia tu, shimo la moto linawasubiri. Kuzimu nimeshafunga milango ambayo watumishi na wachawi waliyokuwa wanapitia kwenda kuchukua nguvu hamna tena na hawana msaada tena. Mwisho wao umefika. Na sasa utukufu wa KANISA la mwisho umetimia, kuzimu haina nguvu na hawaliwezi KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. YESU aliponipa ujumbe huu, nilikuwa kazini Serengeti katika kazi niliyokuwa nafanya ya utalii (Professional Driver Guide), niliogopa sana maana sikuwahi kumuona YESU “live live”. Siyo kitu cha kawaida, ukuu wake unatisha. Mengi utayakuta ndani ya website hii na nitaendelea na kila ujumbe anaonipa kukufikishia wewe kwa njia hii. Ufunuo wa Yohana 1:8
Jumanne saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana
Ibada ya ukombozi
Ijumaa saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni
Ibada ya majibu
Jumapili saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana
Ibada ya Jumapili
Upcoming Events
VIPINDI VYA REDIO
Mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwengu wote ikiwa inamaana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.06.2010. Na akanipa jina la Kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.