Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO

ambaye ndiye Bwana na Mwokozi wa Mataifa yote, pia ndiye Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana na hapana Mfalme mwingine zaidi yake. Mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, ...

Soma Zaidi

Mtume na Nabii

Hebron Wilson Kisamo

Mtume na Nabii Hebron Wilson Kisamo

Mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyonambia mwenyewe.

Amenituma ulimwengu wote ikiwa inamaana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.06.2010. Na akanipa jina la Kanisa lake nilite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY.

Huduma ya ukweli

Ndugu msomaji usiogope, huu ndio ukweli halisi alioniambia mwenye kanisa, yaani YESU. Mengi utayakuta kwenye vitabu nilivyoviandika, CD na DVD. Hakika utafunguka ufahamu wako utajua jinsi KANISA lilivyotekwa na shetani. Na zaidi, YESU alipokuwa akinifundisha, alinionyesha na kunifunulia ulimwengu wote, jinsi ulivyo kwa sasa, akasema watumishi ndio wanatumiwa 98% kuliharibu KANISA. Kwa mfano aliniambia, idadi kubwa ya watumishi wakubwa ulimwenguni ni member wa freemason, akaniambia hao sio watumishi wake.


Haijalishi wanalitumia jina lake, hao ni manabii wa uwongo, na asili yao ni manabii wa uwongo, na mengine mengi utayakuta huku kwenye website na kwnye blog; YESU ameshuka Tanzania kupitia watu wake ila wale waovu wataangamia tu, shimo la moto linawasubiri. Kuzimu nimeshafunga milango ambayo watumishi na wachawi waliyokuwa wanapitia kwenda kuchukua nguvu hamna tena na hawana msaada tena. Mwisho wao umefika. Na sasa utukufu wa KANISA la mwisho umetimia, kuzimu haina nguvu na hawaliwezi KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. YESU aliponipa ujumbe huu, nilikuwa kazini Serengeti katika kazi niliyokuwa nafanya ya utalii (Professional Driver Guide), niliogopa sana maana sikuwahi kumuona YESU “live live”. Siyo kitu cha kawaida, ukuu wake unatisha. Mengi utayakuta ndani ya website hii na nitaendelea na kila ujumbe anaonipa kukufikishia wewe kwa njia hii. Ufunuo wa Yohana 1:8

Siku za ibada

KUMBUKA, HUDUMA YA MAOMBI NA UPONYAJI NI BURE (Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma,toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Mathayo 10:8)

Ibada

Jumanne saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana

Ibada ya ukombozi

Ibada ya ukombozi

Ijumaa saa tisa alasiri hadi saa kumi na mbili jioni

Ibada ya Majibu

Ibada ya majibu

Jumapili saa tatu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana

Ibada ya Siku ya Bwana

Ibada ya jumapili
Upcoming events

Njoo ushuhudie nguvu za Mungu zikifanya kazi.

From The Blog

KITABU: LIJUE KANISA ALILOLIJENGA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI

KITABU: LIJUE KANISA ALILOLIJENGA YESU KRISTO WA NAZARETI ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI

 TOLEO LA SABA ISBN 978 – 9987- 9553-6-7 EMAIL:    [email protected] WEBSITE:  www.prophethebron.org BLOG:      …

READ MORE
KITABU: MJUE YESU KRISTO WA UONGO (Mathayo Mtakatifu 24:4-5)

KITABU: MJUE YESU KRISTO WA UONGO (Mathayo Mtakatifu 24:4-5)

TOLEO LA SITA  ISBN 978 – 9987- 9553-7- 4 MTUME NA NABII- HEBRON WILSON KISAMO KIONGOZI NA MWANZILISHI WA HUDUMA KANISA…

READ MORE
MJUE YESU KRISTO WA KWELI NA YESU KRISTO WA UONGO

MJUE YESU KRISTO WA KWELI NA YESU KRISTO WA UONGO

MJUE YESU KRISTO WA KWELI NA YESU KRISTO WA UONGO Ndugu msomaji na mwanadam yeyote wa taifa lolote kwa rangi yoyote na j…

READ MORE
Ujumbe wa maandalizi ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO

Ujumbe wa maandalizi ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO

Ndugu msomaji wa blog hii, nakusalimu katika jina la YESU KRISTO ambaye ni BWANA na mwokozi wa mataifa yote. Kwanza kabi…

READ MORE