JE UNAFAHAMU
CHAMA CHA JOKA KUU KILICHOPO HAPA DUNIANI?
YESU WA NAZARETI wakati akiniandaa na kunifundisha kuhusu
kazi yake na jinsi ya kuifanya au mwongozo wake yeye, akinifundisha mambo mengi
sana mengine hayo yatabakia kama ni yangu binafsi kwa utukufu wa MUNGU. Alinionyesha
chama cha joka kuu alichokianzisha yeye na kikaja duniani na akapata wanadamu,
wao wakawa katika hicho chama na lengo la joka kuu kukianzisha hicho chama ni
kuipindua ulimwengu ambao MUNGU aliiumba na akaweka viumbe na vitu vyake ili
vimtukuze yeye tu. Alichokifanya joka kuu yeye alileta roho zake na akawatumia
wanadamu na hata sasa hizo roho zimejaa katika nchi mbali mbali, chama cha joka
kuu ambacho ndicho chama kikubwa na anakimiliki yeye peke yake, chama hicho
kinaitwa illuminati party.
Sasa muelewe watu wote wa mataifa yote chama hiki kina kila
kitengo ikiwemo hata kitengo cha makanisa na hata sasa wapo wahubiri maarufu
katika ulimwengu huu ambao watu wanafikiri ni wahubiri maarufu kutoka kwa MUNGU
na kumbe ni wahubiri maarufu wa kutoka kwa joka kuu. Na hawa wahubiri walipewa
uwezo mkubwa wa pesa, miujiza na mengineyo ili watumike kuwaangamiza wanadamu,
mfano ingia google search illuminati pastors member, iwe ni kwa bara mfano bara
la Afrika, America, Europe, Asia na kwingineko utaona majina yao. Sasa hawa
mimi nilishaelezwa na YESU akaniambia hao ni adui zake, sasa na wewe msomaji
ufunguke ufahamu kama YESU anasema ni adui zake na ni adui wa MUNGU, je hauoni
na wao wanawatengenezea watoto wa MUNGU mazingira ili wawe nao ni adui wa YESU
pasipo watu kujijua.
Umshukuru YESU aliyenijulisha mimi Nabii Hebron na sasa
ninawajulisha watu wote ili mpone na mkajitenge nao. Hata kama katika kanisa
unalo Sali pastor wako hayupo katika list hiyo ila dhehebu lipo katika chama
hicho au Askofu, Nabii, Mtume, Mwalimu, Mwinjilisti uelewe yeye
ameshaliunganisha kanisa na chama cha joka kuu. Chunguza madhehebu, ukiyakuta
katika list ya illuminati wewe usipoteze muda. Kimbia ili upone roho yako n
usiwe mwana chama wa joka kuu. Najua watoto wa MUNGU hawampendi joka kuu ila
wale waasisi na viongozi wanampenda joka kuu na sasa wapo kuiendeleza hiyo kazi
ya joka kuu. Na kama umeshajua hivyo je nikuulize ni ibada ngapi umeshiriki na
joka kuu? Au ni miaka mingapi? Ila sasa umshukuru MUNGU. Ulimwengu ulimgeuka
MUNGU 98%, amenituma YESU niupindue ufalme wa shetani na baba yake ambaye ni
joka kuu na kazi inaendelea vizuri sana. Ni lazima ufalme wa shetani uangamie
katika jina la YESU WA NAZARETI.
Pia hata wanachama wake na wao watengane na baba yao joka
kuu katika kuangamizwa na MUNGU, huo ndio uhalali na mtayaona na myaonapo
msishangae, ni YESU WA NAZARETI yupo kazini. Chama hiki kimeyashikilia makanisa
mengi na kama kimeyashikilia hayo makanisa basi ni dhahiri kabisa hayo ni
makanisa ya joka kuu, na yesu wa kuzimu na mpinga kristo. Mpaka hapo unazidi
kupata picha wewe chunguza madhehebu zote katika ulimwengu huu ya kila dini,
yale utakayoyakuta utakuwa unapata jibu je upo katika kanisa alilolijenga YESU
au alilolijenga joka kuu, na unaposali katika kanisa ambalo lipo katika chama
cha illuminati uelewe umemezwa, upo katika tumbo la joka kuu katika ulimwengu
wa roho. Na ndiyo sababu ili umezwe na joka kuu ni lazima usiokoke, ubatizwe
ubatizo wa maji ya kikombe, ubarikiwe ukiwa mtu mzima, ubatizwe kwa jina la
mchungaji na ubatizwe katika kisima, kanisa lazima lifanye biashara na kuwa na
mabenki na kuchagua partners wawe wanasupport hiyo huduma. Lengo la chama hicho
ni kuwakusanya wanadamu na kuwaingiza katika ufalme wa joka kuu wasiende
mbinguni ili wakachomwe na yeye katika ule mwisho wa ulimwengu katika moto wa
milele wa jehanamu.
Sasa enyi mataifa yote je niwaulize mnapenda kwenda katika
ziwa la moto? Jibu ni uamuzi unao wewe, na wengine ni viongozi mbali mbali
lakini nao wapo katika chama cha joka kuu, na kama wapo katika chama hicho sasa
haupati picha 98% kila kitu shetani alishatawala? Ikabakia 2% ya YESU, sasa
YESU anaukomboa ulimwengu wake yeye peke yake na watu waliomsaliti anasema
atapambana nao yeye mwenyewe ajuavyo yeye. MUNGU amekasirika sana, watu
wameamua kuwa wana chama wa shetani, wamemkataa MUNGU, basi kama ilivyo
aliyopanga MUNGU kwa ajili ya shetani yatawahusu na hao waliopo chini yake. Najua
wengi hamjui sasa tubu wewe unayeabudu katika madhehebu yaliyo kaatika chama
cha shetani na haukujua, utubu na ujitoe huko kabisa.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote,
uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele, najitenga na chama cha joka
kuu katika jina la YESU. Naja kwako YESU WA NAZARETI unishike mkono, uniongoze
wewe nisipotee tena. Hata nikikosa
kanisa la kweli nilinde huku nilipo na uniongoze kwa roho wako mtakatifu
milele, Amen.
NOTE:
1.
Chunguza dhehebu lako.
2.
Chunguza kiongozi wako, iwe ni katika kanisa au
nchi.
3.
Chunguza matajiri katika ulimwengu huu wale
maarufu.
4.
Chunguza kila sekta utaona ni chama cha joka kuu
linashikilia na hata katika miziki.
Usiogope hiki ni chama cha siri sana na kimejificha mambo
yake hayajulikani na watu sababu yangejulikana watu wangewakimbia, wakabakia
viongozi wa dini ambazo wamejiunga huko, msidanganyike ulimwengu wote. YESU hashirikiani
na chama cha illuminati wala chama chochote katika ulimwengu huu. Sasa mpone. Zaidi
karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOI WA MATAIFA YOTE Arusha,
Tanzania. Na usome vitabu vya Nabii Hebron, toleo la kwanza na toleo la 16 na
vinginevyo vipo katika blog www.prophethebron.blogspot.com
au ingia katika website www.prophethebron.org.
Nawafunika kwa damu ya YESU ila wachawi nawachoma kwa damu
ya YESU WA NAZARETI.
NABII HEBRON.