[vc_row][/vc_row][vc_column width=”1/2″][/vc_column][vc_column width=”1/2″][/vc_column][trx_section][vc_empty_space][/trx_section][vc_column_text]Ndugu nakusalimu kwa jina la YESU KRISTO, ambaye ndiye Bwana na Mwokozi wa Mataifa yote, pia ndiye Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana na hapana Mfalme mwingine zaidi yake. Mimi jina langu naitwa Hebron Wilson Kisamo, YESU amenichagua nimtumikie yeye kwa jinsi anavyotaka yeye ili kukomboa ulimwengu huu ambao umepotea na shetani ameumiliki kwa asilimia 98% sawa sawa na YESU alivyoniambia mwenyewe. Amenituma ulimwengu wote ikiwa inamaana nchi zote, mabara yote. Ujumbe huu aliniagiza rasmi na kunipa mamlaka yake tarehe 14.06.2010. Na akanipa jina la Kanisa lake niliite YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRY. Akaniambia mwanangu nitautumia huu mwili wako kuukomboa ulimwengu wote, utachukiwa sana,utafanyiwa na kuitwa majina mabaya lakini usiogope tena ufurahi zaidi, kwani mimi YESU walinifanyia mabaya zaidi na ya uongo yakitokea kwa baba yao wa uongo ambae ni lusifa, nilifurahi daima.Hakuna jambo lolote litakalofanikiwa juu yako au silaha yoyote juu yako, nipo na wewe milele. Nitakutumia kwa namna ya tofauti na kwa kiwango kikubwa sana ambacho hakijaonekana tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Adui yako ni adui yangu, akasema YESU kwa sauti ya uchungu sana, watumishi wamenisaliti maagizo niliyowapa hawayafanyi na wamegeuza NENO langu kuwa maandiko badala ya Neno, maandiko yanatoka kwa shetani maana lusifa anaijua Biblia yote, na maandiko hayana uthibitisho wa nguvu zake YESU. Neno linatoka kwa YESU na lina udhihirisho wa nguvu za MUNGU. Napia wana wa adamu wanateseka wanalia na kuomba hawapati majibu, na zaidi wanazidi kupotoshwa na viongozi wa kanisa, maagizo niliyoyaacha nilivyokuwa ulimwenguni kabla ya kurudi kwa BABA yangu ili kuniandalia maandalizi ya ujio wangu ili nipate kuwaponya wengi waende mbinguni, imekuwa kinyume idadi kubwa ni ya watu wa shetani. Waliokuwa watumishi wangu wamenisaliti 98% sipo nao. Wameamua kwenda kuzimu, na shetani anawatumia na jinsi anavyowatumia, ni kubadili au kwenda kinyume na agizo la MUNGU, mfanowatumishi kwa sasa wamefanya kanisa ni mahali pa biashara, kunyanganya watu vitu vyao na wakijua wamenitolea mimi, na kunifanya mimi YESU ndiye mnyanganyi,kwa midomo yao hunitaja kama wananipenda ila mioyoni mwao hawapo na mimi, wamekuwa watumishi wa pesa na sio mimi, wamekuwa wakitenda miujiza lakini siyo yangu ni miujiza ya shetani, na hao ni kati ya wale ambao siku ya mwisho nitawakataa na kuwaambia sikujui. Kanisa limeniacha kunitegemea mimi, imebaki 2 % tu ulimwengu mwote. Sasa mimi YESU ninalikomboa kanisa mwenyewe na ndipo unabii na utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza unatimia sasa.[/vc_column_text]