UWATAKASE KWA ILE KWELI NENO LAKO NDIYO KWELI.

[ad_1]

Sawa sawa na neno la MUNGU katika kitabu cha Yohana 17:17, inaelezea kuhusu neno la MUNGU la kweli ndilo litakalo. Mamilioni ya watu katika ulimwengu wote wamepotea na kupigwa upofu wasijue kweli ya neno la MUNGU na ndiyo maana wanakubali maneno yasiyotokana na biblia na kuyapokea na kama ukiyapokea ina maana hayo siyo maneno ya MUNGU ya kweli ni ya uongo na kama uliyakubali tayari udhihirisho wa kutakaswa na neno la MUNGU haitokei milele sababu tayari inakuwa ni kinyume na hao watendao maneno tofauti na biblia hawa ni adui wa YESU 100% na ndio mpinga kristo, sababu ya kuitwa ni wapinga kristo ni kuwashirikisha wanadamu mafundisho ya uongo wakichanganya na biblia.
Sasa mfunguke mataifa yote, YESU ni mzuri na yeye ni mkweli milele na ahadi zake ni kweli tupu, akiwa pamoja na BABA yake na ROHO MTAKATIFU wao wote wanasema kweli, na mpaka sasa wapo na umoja na hawajagombana na hawatagombana milele au kutengana. Hivyo na watu wote wanatakiwa wafuate umoja wao na kweli yao ndipo watafika mbinguni. Amenituma niwafungue macho yenu na akili zenu wale mliofungwa na hamjijui; mmebakia kujitia moyo na kusimama na mstari huu wa Yohana 17:17 wakati nyie ni waongo na siyo wa kweli, kivipi?
Ø Kila anayeshiriki au kubatiza ubatizo wa maji ya kikombe au kubatizwa kwa jina la mchungaji au katika kisima, usitegemee kuwa neno la MUNGU litawatakasa, sababu nyie mmeshiriki uongo, tafuta hakuna katika neno la MUNGU haya yameruhusiwa.
Ø Mnaoabudu sanamu, kufanya ibada za wafu, kuabudu kina Mathayo, Musa, Eliya na Maria na wengineo. Mjue mmejichafua na mnaharufu mbaya mbele za MUNGU na mnajipachika harufu ya dhambi Isaya 45:20, Isaya 44:6-9. Msitegemee maombi yenu yatasikiwa na MUNGU aliye hai wala damu ya YESU iwatakase, wala neno la MUNGU liwatakase, hata mnavyokariri na kusoma biblia na ungali hayo unayatenda ujielewe umekuwa adui wa MUNGU hivyo utarajie mapigo kutoka kwake na hukumu ile siku ya mwisho, au ukitaka kupona uokoke sasa na usishiriki hayo yasiyopo katika neno la MUNGU na kweli yake ikutakase uwe na akili timamu.
Ø Kanisa likichangisha pesa au harambee msitegemee kubarikiwa sababu neno la MUNGU lililokweli haliruhusu kuchangisha au kuomba omba na kumfanye YESU ni masikini, hata kama mnaelezwa mnamjengea MUNGU kanisa, fuatilia neno lake. Usijisumbue kwa kila jambo bali ombeni na yeye atafanya. Sasa mmeacha kuomba ili MUNGU ajitukuze peke yake mnageuka kumuaibisha. Hii ni dhambi na siyo neno la MUNGU, habari za michango makanisani (hayo ni maneno ya shetani).
Ø Ukipewa huduma yeyote ya kiroho ukalipia pesa kama vile hospitali ya kibinadamu. Na hata anayekudai pesa hizo ndio akuombee, elewa hilo silo neno la kweli kutoka kwa MUNGU hivyo hautakaswi na MUNGU bali unanajisiwa na maneno ya uongo. Sasa funguka maana wengi wanafarijika na neno hili, lakini wapo katika kambi ya kanisa au watumishi wanaosema au kutenda maneno ya uongo.
Nawaeleza hautakaa utakasike sababu hayo myatendayo siyo neno la kweli bali mnaposhiriki unajijengea njia ya jehanamu. Fuata neno kama lilivyo usibadilishe lolote na hata kanisa ambalo linabadilisha neno la MUNGU uelewe hilo ni pando la shetani lipo hapa ulimwenguni kwa lengo la shetani au mpinga kristo na ndiyo maana lipo kinyume. Ingekuwa lipo na limeletwa na YESU lingefuata kweli yake na kuitenda peke yake.
Na wengine wanasema shika neno au tenda neno, hili ni neno zuri, ila uchunguze pia isiwe ni shika neno kwa mdomo halafu kimatendo ni unafiki kivipi? Mfano unabatizwa kwa jina la kiongozi huyo badala ya jina la YESU, je nikuulize huku ndiko kushiriki neno? Au ni kulitupa neno na kupokea uongo? Wakristo mfunguke ufahamu zenu, sasa hivi bwana mchunguze iwe ni Nabii, Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti, mwalimu wapo wenye neno la kweli ila 95% wamechanganya maneno ya uongo, na hadi iwe hivi ina maana wametekwa na shetani full sababu ya kukataa kumsikiliza YESU atakavyo. Haiwezekani hivi hivi mtu kwa akili zake kama hajatekwa na shetani aibadilishe biblia na kutenda tofauti, hiyo ni dalili kuwa ndani yake hata ROHO MTAKATIFU hayupo na ndiyo maana kazi yao ni kusaliti neno la MUNGU na kusema kinyume. Na waumini mnatengenezewa na njia ya jehanamu pasipokujua, toka utengwe na huko uokoke leo hii ili akusafishe na kuyaondoa mapando ya uongo.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU UNITAKASE MOYO WANGU NA UUONDOE UONGO WA MANENO YA UONGO NILIYOINGIZIWA KWA KUFUNDISHWA MAKANISANI, BILA KUJUA. UZITEKE NA AKILI ZANGU ILI NISITEKWE TENA, UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE UNIONGOZE SASA MAHALI SALAMA ULIPO WEWE.
NABII HEBRON.

[ad_2]