MAANA YA KUOSHWA MIGUU. YOHANA 13:1-15

MAANA YA KUOSHWA MIGUU. YOHANA 13:1-15

[ad_1]




NABII HEBRON AKIWA NA BABA YAKE WA KIROHO MOSES KULOLA. 











Basi kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti; Yesu akijua ya kwamba Baba amempa vyote mikononi mwake, na yakuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simon Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, nifanyalo wewe hulijui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, kamanisipokutawadha, huna shirika nami. Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. Yesu akamwambia, yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote mlio safi. Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, si nyote mlio safi.

Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia je! mmeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mwaniita, mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, ninyi mtende vivyo.
Ndugu msomaji jambo hili sio jambo geni la kuoshwa miguu makanisani ila nataka uelewe kusudi la YESU na ni nani wanaopaswa kuoshwa miguu na ni kwa jinsi gani? Hali YESU akijua ya kuwa muda wake umekaribia kuchukuliwa aliwaita wanafunzi wake akawaosha miguu ikiwa ni ishara ya utayari kwa ajili ya kazi yake, akachukuwa kitambaa akajifunga kiunoni wakati akiwanawisha miguu – hii ina maana aliwaachia ujasiri kwa ajili ya kazi yake ili wayaendeleze yale aliyowafundisha kwa wanadamu wote, na ukisoma utaona Petro alikataa asioshwe miguu ila YESU akamwambia usipokubali nikuoshe hautakuwa na shirika na mimi, hii yote ilikuwa ni maandalizi ya kuwaandaa wale mitume wake au wanafunzi wake kwa ajili ya kazi yake. Na akasema ikiwa mimi mwalimu nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi kwa kuwa mimi nimewapa kielelezo ili kama mimi nilivyowatendea nanyi mtende hivyo hivyo.
Ndugu msomaji, natumaini umesoma huu waraka niliokuandikia hapo juu Yohana 13:1-15. Yesu anasema mtawadhane ninyi kwa ninyi na kufuata kielelezo alichowaachia na kwa jinsi ile ile na akasema ni ninyi kwa ninyi inamaana ni watumishi kwa watumishi. Na zaidi nikuulize swali; je, kwa nini Yesu hakuwatawadha miguu watu wengine tofauti na wale mitume?
Hii ni kwa sababu hawa mitume waliandaliwa kwa kazi yake tu, na ni tofauti na wafuasi wa Yesu, ndiyo maana anasema ninyi kwa ninyi na nimeshawapa kielelezo na ukisoma mstari wa 15 inaelezea, na kielelezo hicho ni wale mitume / watumishi sasa swali nakuuliza, ndugu msomaji, je wewe unayeoshwa miguu wewe ni mtumishi? Au ni mfuasi wa Yesu? Soma utaona imeandikwa ni watumishi kwa watumishi ili kuifanya kazi yake, ila siku hizi Neno na maagizo aliyoyaagiza Yesu na kutoa mifano imepuuzwa, watu wote wanaoshwa  miguu kanisani je nikuulize swali kwa nini Yesu amesema ninyi kwa ninyi tu? Ina maana ni watumishi peke yao kwa ajili ya kazi yake. Na kama ingekuwa ni kwa watu wote, basi ingeandikwa kwa watu wote kama ilivyoandikwa mkawabatize watu wote.
Na ili uzidi kufunguka ufahamu wako je, ni mtumishi anayebatiza au ni muumini? Jibu ni mtumishi, hii ni sababu yeye ameshatofautishwa na kondoo. Ndiyo maana ni mtumishi tu ndiye anayetakiwa kuoshwa miguu tu, na sio waumini japo hata mimi niliwahi kuoshwa miguu, bila kujua ila nitakueleza hasara zake, kwa hiyo tayari hili ni kosa kubwa na kufanya kinyume na Yesu alivyoagiza. Na ukisoma  katika Yohana13: hakuna mahali Yesu amerudia  kuwaosha hawa mtume wake miguu ni mara moja  tu, hao wawafanyie wengine kwa kufuata kielelezo alichokifanya Yesu. Leo hii hakuna cha mtumishi wala muumini wote mnaoshwa miguu. Hebu someni Neno na kuelewa. Na utashangaa kila mara ibada  za kuoshwa miguu. Ni kuulize swali wewe unayeoshwa miguu wewe ni mtumishi? Jibu siyo na kamawewe ni mtumishi kwa nini na wewe kila mara unawanawisha miguu? Hauna jibu, umepotea.
Ndugu msomaji leo nakupatia siri kubwa na ufunguke kuhusu ibada  za kuoshwa miguu na hili ni kwa Dunia yote na mataifa yote,  Yesu kaniambia siyo mpango wake watu wote waoshwe miguu ni kwa watumishi tu, ila watumishi wengine wanaiga wenzao wafanyavyo ila 95% ya Ibada zote za “foot washing” kwa waumini, hutumia nguvu za giza na kuyanenea yale maji  wanapokuosha miguu wanakushika utayari wako unakuwa wewe ni wa hapo hapo tu hata kama mnamjua kabisa  mtumishi ni mchawi hauondoki hapo, hata kama mambo yako hayaendi  unaangamia hauwezi kutoka, maana miguu imeibiwa utayari na zaidi ule utayari unabakia katika  kitambaa na vile vitambaa huviweka kwenye kiti na begani,  kwenye kiti ni kukukalisha wewe hapo hapo tu, na begani anakubebesha mizigo ushindwe kuondoka. Funguka Yesu anawapenda mpone, unayesikia, sikia, unayekataa  utajuta. Na watumishi hao wakiona waumini wameanza kumshtukia mtumishi hayupo sawa na MUNGU haraka sana huitisha ibada ya kuoshwa miguu, na waumini wanafikiria ni jambo jema kumbe unaenda kumalizwa kiroho na kimwili, waulize swali, hawana jibu zaidi ya kukukimbia, na zaidi waulize wapi Yesu aliwarudia  kuwaosha mitume miguu wale aliowaosha? Jibu hawana. Huu ni mpango wa kwenda kinyume na Yesu. Amesema ninyi kwa ninyi tu, watumishi na kielelezo ni kama hao mitume na watumishi tu. Na zaidi ufunguke ukisoma katika Neno lake Yesu alifunga kitambaa kiunoni, akawafuta, sasa kwa nini hawa hawajifungi kiunoni kitambaa? Jibu umelijua.! na je, ndicho kielelezo alichokiacha YESU cha kuweka kitambaa  kwenye kiti na begani?  Huu  ni mfano halisi hiyo ni feki tu. Na waumini siyo watumishi waoshwe miguu ni mtumishi anaoshwa tu pale anapopakwa mafuta. Ufunguke ufahamu ili mtumishi akukamate kipepo, njia mojawapo ni hiyo na ujiulize swali kwa nini hurudia ibada ya footwashing kila mara? Na je wewe muumini ni mtumishi? Kataa na usishiriki na waulize swali na uangalie kwenye BIBLIA utaona ukweli mtupu, usishiriki dhambi na zaidi unaangamia, umeshiriki Neno la MUNGU kinyume na alivyopanga YESU.

[ad_2]