ALIYONIAMBIA YESU WA NAZARETI…………..

[ad_1]

Bwana YESU WA NAZARETI amenituma niwaeleze ukweli kuhusu yeye usidanganyike tena. Amesema watumishi wamemsaliti 98% katika ulimwengu wote na kumgeukia shetani na kufanya kanisa litekwe na shetani. Watumishi wamekua wachawi, freemason, wanatenda miujiza kwa kutumia nguvu za giza, wanawatoa waumini makafara kwa shetani, wamebadilisha kanisa linaloitwa kwa jina lake kuwa pango la wanyang’anyi wakitumia jina lake, watumishi wanakula kondoo (yaani kuzini na waumini na wake za waumini na wengine kunyang’anya waumini wake zao).
Amenituma niwaeleze ya kuwa hiyo michango mnayochangishwa makanisani, niwaeleze yeye hausiki na ni uwizi wa pesa zenu, kama ni mimi YESU nimemuita mtumishi tayari humuandalia njia ya kazi hiyo, mimi YESU siyo maskini wala BABA yangu MUNGU aliye hai. Huo ni ujanja wa shetani na watumishi wenye tamaa ya pesa kuwaibia wana wa MUNGU pesa zenu, akasema kwa sauti ya hasira. Tazama na wengine wanatoa mpaka akaunti namba kwenye TV kuomba pesa za kipindi, waambie mimi sipo naye huyo na wote mnaotoa pesa hizo mnaibiwa na hautaziona baraka zangu. Akasema watoto wangu wakisikia kitu chochote kinatajwa  kwa jina langu hufurahia, ila na adui hulitumia jina hili pia.
Nilikwisha sema muwe makini watatokea wakristo wa uongo, ndio hawa sasa utawajua kwa matendo yao. Akasema, Hebron, leo hii watu wanatumia jina langu kuingiza madawa ya kulevya katika nchi zao na kufanya biashara haramu. Je? Mimi YESU ninauza madawa ya kulevya? Niliogopa! Akaniambia OLE WAO shoka lake lipo shingoni na mda siyo mrefu hawataonekana tena katika ulimwengu huu. Na kazi hiyo anaifanya yeye peke yake, na atawafichua na watajisema wenyewe. Walizoea kuziloga hata nchi zao ila ni mwisho na hii itaanzia Tanzania, nchi ambayo ameniambia hii ndiyo Edeni ya sasa na ataibadilisha na mataifa yote watakuja kuponea hapa Tanzania. Ni yeye mwenyewe atakaye yafanya hayo wala siyo mwanadamu. Na mengi aliniambia utayakuta ndani ya website hii na blog na kwenye vitabu.
Makao ni mengi na nimeyaona ila hakuna watu wa kwenda, idadi kubwa 98% ni ya shetani na watumishi tena wale maarufu cha ajabu majina yao sijayaona katika kitabu cha uzima, niliogopa sana, akaniambia kama hawa viongozi wapo kuzimu na hao wanaowaongoza wapo kuzimu pia. Mfunguke akili zenu sasa hivi watumishi 98% ni matapeli, ni wachawi wa kiwango cha juu sana. Ila nimeshafunga njia zao za kwenda kuzimu kama alivyoniagiza jemedari YESU WA NAZARETI. Akasema, imefika mahali hata watumishi wanajiita wao ni YESU. Je? Waulize wao ndiyo mwana wa pekee? Wao wapo mbinguni? Au walikufa na kufufuka? Jibu, hapana. Na wengine wamejiita majina ya watoto wa MUNGU walioushinda ulimwengu, mfano Eliya. Akaniambia waambie hao ni waongo na ndani yao ni shetani anaongea na ndiyo maana hata wana wabatiza watu kwa majina yao. Hawa tayari wamemkufuru ROHO MTAKATIFU pia.
Amenituma niwaambie sadaka ya kweli ni fungu la kumi tu na shukurani hizo nyingine zote ni uwizi mtupu na pia uangalie mahali pa kumtolea MUNGU. Ukikosa; tulia muombe atakuongoza yeye, watumishi wamekuwa wana mazingaumbwe. Akaniambia waumini hawana shida wao ndivyo wanavyofundishwa mafundisho ya kuibiwa mali zao tuu, kila siku ni baraka  tuu. Hiyo ni laana tupu na mmekuwa KAINI wa pili maana dhambi imewashinda mmetenda vibaya (Mwanzo 4:7) SOMA UTAONA.
Ameniambia mbatizwe ubatizo wa maji mengi kama alivyobatizwa yeye. Huo ubatizo wa kikombe ni chapa ya mpinga kristo namba 666 na watu wote ambao hawajabatizwa ubatizo huo wa maji mengi hao siyo wafuasi wake. Yeye hakuonyesha ubatizo huo na hata katika biblia utafute haupo! Hayo ni mapokeo ya shetani, hata kama unajiita wewe ni mchungaji na haujabatizwa ubatizo aliobatizwa YESU WA NAZARETI, wewe siyo mwanafunzi wake kabisa, na wala siongezi lolote wala kupunguza namheshimu YESU na MUNGU aliye hai, na hakuna chochote kitakacho jaribu kunizuia kusema kweli yake milele, MUNGU hazuiliwi ila shetani ndiye huzuiliwa.
Amenituma niwaeleze yeye huponya bure na hataki  pesa za mtu yeyote, hao wanaowaambia leta pesa  wanatumia nguvu za kipepo maana shetani hatoi bure lazima ulipe kama vile wanaoendaga kwa waganga lazima walipe pesa.
Amenituma niwaeleze mda wowote na wakati wowote anarudi kuja kuwachukua wale walio wake, mrudieni YESU enyi wanadamu hakuna mtu yeyote atakaye kwenda mbinguni ambaye hajaokoka tena kikweli 100%.
Amenituma niwaeleze sasa hivi utapendwa kanisani sababu unayo pesa.
Amenituma niwafundishe habari njema na kuwafungua na kuwaponya na kuwaelekeza njia ya kwenda mbinguni, maana 98% hawapo katika njia ya uzima wapo katika njia ya mauti. Na watumishi wanajijua kabisa kuwa hawapo sawa na wana Agano na shetani la kuangamiza roho hizo. Ila lazima mfunguliwe na mpone. Zaidi endelea kusoma vitabu au fika katika Kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Utajua ukweli zaidi na utakuwa huru, wala msidanganyike tena na kutumikishwa kama punda. MUNGU amekasirika sana jinsi watumishi wanavyowatesa wanadamu, wamekuwa wachawi kupita waganga wa kienyeji. Na kwa nje hutaja jina la YESU ila ndani ya mioyo yao ni mbwa mwitu.
Mwenye ufahamu afahamu Asema BWANA WA MAJESHI.

NABII HEBRON.

[ad_2]