BILA KUOKOKA WEWE SIYO MKRISTO!! KUJIITA MKRISTO NA HAUJAOKOKA HAUNA TOFAUTI NA MPAGANI!!

[ad_1]


BWANA YESU ASIFIWE! Nawasalimia kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na ndiye aliye Kristo wa kweli, leo ninafundisha kuhusu ukristo ni nini? Na wokovu ni nini? Maana watu wengi katika ulimwengu wote wanapigwa upofu na shetani wakajiita wao ni wakritso bila kuokoka. Amenituma niwaeleze ukweli wake maana anajua wengi mnampenda na pia wapo wasiompenda yeye, amenituma niwaeleze ukweli kuhusu yeye YESU WA NAZARETI na jinsi ipasavyo mtu akamilike ili awe mkristo kamili na siyo mkristo mpagani. Ameniambia yeye alipokuja hapa ulimwenguni yaani yeye Kristo alitumwa na BABA yake awaletee wanadamu wokovu na wokovu mtaingia tu pale kwa yule atakayemkubali kwa kumkiri kwa kinywa chake kama ndiye BWANA NA MWOKOZI kwa kufuata yale aliyoyaleta katika ulimwengu huu.
Ukisoma katika kitabu cha Yohana 3:16 inasema kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu hata akamtuma mwana wa pekee ili kila mtu amuaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Na ukisoma katika kitabu cha Warumi 10: 9-10 bila kumkiri YESU hakuna wokovu, bila kumkiri YESU hakuna ukristo. Sasa shetani na yeye anajua wokovu ndio nini na sababu anajua wokovu ndio ukristo wa kweli. Yeye akayateka makanisa na kuwanyima wasiokoke bali wajiite tu wao ni wakristo. Unatakiwa ujiulize katika akili yako je YESU alileta jina lake tu au MUNGU alimtuma aulete wokovu? Na atakayemkiri ndiye atakaye okoka.
Makanisa yametekwa na shetani 98% katika ulimwengu wote yamekuwa siyo makanisa ya YESU KRISTO wa kweli. Sababu hayana wokovu na hata viongozi wao hawajaokoka. Sasa kama makanisa yaliyopo katika ulimwengu huu yaliyo mengi hayakiri wokovu bali yanatumia jina la YESU kujiita wakristo. Nawaeleza mfunguke makanisa yote katika ulimwengu huu ambayo watu hawaokoki hayo siyo makanisa ya Kristo wa kweli, sababu kama yangekuwa ni ya kristo wa kweli lazima yangekuwa na wokovu na siyo litrugia au sheria. Ila uelewe yapo makanisa yanayoona yapo sahihi mbele za MUNGU kumbe yapo sahihi kwa kristo wa uongo. Kristo wa kweli yeye alileta wokovu na uzima, ila kristo wa uongo yeye alileta jina lake tu na hana wokovu, sasa embu fungukeni mataifa yote. Je mfano anarudi leo hii je wanaojiita wao ni wakristo na hawajaokoka wataenda mbinguni? Jibu ni hapana, na je jiulize hivi hao wote waliofariki na wakajiita wao ni wakristo na hawajaokoka je wanaenda paradiso? Jibu unalo sasa hao wote wapo kuzimu sababu hawakuokoka bali waliongozwa vibaya kwa kufuata mapokeo yaliyo elimu ya wanadamu na ndivyo ilivyo leo hii YESU anao wakristo waliokoka 2% katika ulimwengu wote hiyo 98% ipo chini ya kristo wa uongo na inawezekana na wewe ni mmoja wapo na haujielewi na unaona wewe ni mkristo safi na unahaki ya kuwa mkristo, fungukeni enyi wanadamu mimi Hebron nilipotumwa na YESU na alionieleza ni mengi ila aliponieleza watumishi wamemsaliti sikuelewa vizuri ila aliendelea kunifundisha mpaka nikamuelewa maana katika ulimwengu huu hata mimi sijawahi kuona mwalimu anayefundisha kama YESU na unaelewa vizuri.
Akaniambia  hivyo ndivyo watu wanafarijiwa kwa uongo kwa maneno ya kukataliwa kuokoka na wakiambiwa mimi ndivyo nilivyo. Akaniambia waeleze watu wote wanaotaka kuja mbinguni mahali nilipo mimi, wapokee kile nilichokileta yaani wokovu peke yake ndio uzima wa milele na mtu ili anipokee mimi cha kwanza apokee wokovu aokoke, anapookoka ndipo mimi naingia ndani yake na yeye anaitwa mwanafunzi wa Kristo aliye hai, na pia akisha okoka aishi maisha matakatifu, na atimize misingi ya wokovu, ubatizo wa maji mengi na siyo ya kikombe au ya maji ya kisima. Ifanywe kama nilivyofanya mimi nilipoonyesha njia na pia ubatizwe kwa jina langu tu na siyo la mchungaji au mtu yeyote yule. Hapo utakuwa mkristo maana aliye mkristo lazima afanane na mimi kiimani na kimatendo. Sasa watu wengi wanajiita wakristo lakini hawafanani na mimi kiimani wala kimatendo.
Sasa mpaka sasa umepata picha ili uwe mkristo ni lazima uokoke na kama haujaokoka wewe siyo mkristo. Nina nukuu maneno alionieleza YESU kwa kinywa chake, nilirudisha fahamu zangu katika picha halisi ya ulimwengu huu nilisikia kulia sababu mabilioni ya watu wanajiita ni wakristo wanadanganywa kwa kupewa mafundisho ya mpinga kristo ili waangamie wasiende mbinguni na ndivyo ilivyo sasa leo uokoke ili uwe mkristo kamili, na zaidi hayo makanisa yote ambayo hayakubali watu waokoke hayo yote siyo matawi ya YESU wa kweli haijalishi wanalitaja jina lake. Alisema YESU msiziamini kila roho bali zijaribuni, utazijaribu kwa matendo. Sasa kwanza kwa nini hawataki tendo la wokovu, na pia hata makanisa yao why yanaitwa ya dini? Je YESU alileta makanisa ya dini? Jibu siyo, YESU alileta wokovu ambalo ndilo kanisa la wokovu sasa watu wanang’ang’ania makanisa yale ambayo YESU aliyakutaga enzi zile na wakakataa kutoka huko na kulifuata kanisa la wokovu, ambapo pasipo wokovu hauna haki ya kwenda mbinguni na huo ndio ukweli 100%. Na shetani bado hakuchoka akajua watu wanajua wokovu ni kitu cha thamani sana na wokovu ndio ukristo, akayateka makanisa baadhi ya wokovu na akawaita watumishi ambao ndio watumishi wanaofundisha uongo katika makanisa yanayojiita makanisa ya wokovu na watu wapo pale wakijua wanakutana na YESU wa kweli kumbe wanaenda tena kukutana na shetani pasipo kujua alichokifanya.
Sasa katika makanisa ya kipentekoste katika ulimwengu wote shetani akaingia ndani yao watumishi wakaanza kufungua makanisa wakisema ni ya wokovu kumbe siyo kweli ni mahali pa kuwatesea wanadamu na kuwapiga upofu waamini hapo ndipo wanafika salama, kumbe ndio njia ya jehanamu. Makanisa ya wokovu leo hii watumishi wengi ndio freemason, ndio waganga wa kienyeji, ndio wafanya mazingaumbwe, ndio wanaowabatiza watu kwa majina yao, ndio wanaobtiza ubatizo wa maji ya kisima, ndiyo yanayowafungia ndoa watu kwa agano la shida, ndiyo yanayofanya nyumba ya MUNGU kuwa sehemu ya biashara na ufisadi. Chunguza huko ulipo utapata picha ya kweli, sasa na makanisa ya jinsi hii pamoja  na watumishi ambao ndio viongozi hao pia siyo wakristo wa kweli, uchunguze Neno la MUNGU je kinaruhusu hayo? Na ukiona kanisa la wokovu pia lipo katika mambo ya kifisadi na kutoa huduma kwa pesa, uelewe hapo hayupo mwokozi YESU na siyo tawi lake bali ni tawi la shetani. Toka huko muombe MUNGU atakuongoza na kama hakuna pa kwenda wewe endelea kusoma makala ya Nabii Hebron na vitabu, MUNGU atakutunza na nitaendelea kukuombea maana hata sasa najua mpo maelfu katika uliwmengu mlio ujua ukweli wa YESU amewafungua fahamu zenu na hamtaki kurudia matapishi tena, bali mnataka wokovu safi siyo wokovu feki au wokovu wa kifafa. Na baada ya kuokoka hakikisha unailinda wokovu wako, maana shetani hapendi mtu aokoke, akiokoka tu anajua tayari huyo ni mkristo wa kweli wala simpati sasa kazi ni kwako wewe ambaye unaujua ukweli huu ya kuwa hauwezi ukajiita mkristo bila ya wewe kuokoka sasa chunguza ni wangapi wanaojiita ni wakristo na hawajaokoka? Ni mamilioni shetani anafurahia atakuwa nao jehanamu.
NOTE:
SALA YA TOBA
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU NA LEO HII UNIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE NAOMBA UNIOKOE NA KUNIOKOA KWAKO NI MIMI KUUPOKEA WOKOVU TU NA SIYO KINGINE, UNILINDE, UNIONGOZE, NIFUNGUE NIKUJUE WEWE KRISTO WA KWELI NA NIWE MFUASI WAKO. AMEN.
Baada ya kuokoka sasa wewe ni mkristo, na usiabudu mahali popote ambapo siyo kanisa la wokovu, na kanisa hata la wokovu ukikuta tu tayari ni michango na kutafuta pesa ondoka maana hakuna tena wokovu imekuwa ni dini, na hii ndio njia ya shetani aliyotumia pia kuyateka makanisa ya wokovu na kama yametekwa uelewe hayo tayari siyo tena makanisa ya wokovu haya yamekuwa makanisa ya dini tu. Na pia muwe makini katika makanisa yote ya wokovu, ukiona kuna bendera ya aina yeyote sasa ufunguke hizo bendera zinazo maana yake na ni maagano ya kuzimu hata ikiwekwa ya nchi. Mimi nakueleza uelewe, hizo bendera zinakuwa na majini na pia ni ishara ya ufalme wa giza unatawala hapo na ndio unaotenda kazi na siyo MUNGU sasa uelewe. Na unaweza ukadanganywa eti zinapokaa kanisani ni tunaziombea hizo nchi. Rudi katika neno imeandikwa hata katika nyumba ya MUNGU kisiwekwe kitu chochote kwa ishara yeyote, inapokuwa hivyo hiyo ni sanamu. Na pia imeandikwa katika nyumba ya MUNGU ni mahali pa sala tu, na pia imeandikwa ya Kaisari mpe Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU. Na zaidi endelea kusoma makala yangu utaendelea kujua mengi na kuponywa roho yako na pia karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ili uupokee wokovu wa kweli kutoka kwake mwenyewe. Na ukamilike uwe mkristo sasa wa kweli, ubadilike.
Wote nawasii sana muokoke leo hii na ndipo utakuwa mkristo na kama hujaokoka uelewe mpaka sasa wewe siyo mkristo, iwe ni askofu, mchungaji au mtumishi unayeona unafanya kazi ya kanisa elewa unamfanyia shetani ambaye ndiye kristo wa uongo. Soma Mathayo 23: 1-37, huu ndio ukweli.
SWALI: umeshajua wewe upo katika kundi gani la ukristo?
                Je ni ukristo wa kweli?
                Je ni ukristo wa kipagani?
                OKOKA SASA ILI UWE MKRISTO.

NABII HEBRON.

[ad_2]