JINSI YA KUIMALIZA CORONA (COVID-19) ULIMWENGUNI POTE.

JINSI YA KUIMALIZA CORONA (COVID-19) ULIMWENGUNI POTE.

BWANA YESU ASIFIWE watu wa MUNGU nawasalimu kwa jina la MUNGU aliye hai aliyeumba mbingu na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Katika jambo hili linalotikisa dunia kwa sasa kupitia huu ugonjwa wa Corona napenda mjue na kuelewa kwa wale ambao hawajui chanzo cha ugonjwa kuwa ugonjwa huu haujaletwa na MUNG, bali umeletwa na shetani ili aangamize watu wote na shetani amepata nafasi sababu watu wamefanya dhambi sana mpaka shetani akawashtaki wanadamu na ndipo akapata kibali cha kuleta pigo hili, MUNGU yeye ni wa haki na shetani anajua kabisa MUNGU anafuata haki, na ndipo aliposhtaki na akapata nafasi ya kuipiga dunia.

Nimekuwa nikieleza kwenye YouTube sana na pia kwa njia ya makala ni jinsi gani tufuate maelekezo ya MUNGU ili tuweze kuliondoa hili pepo Corona. Hapa cha kufanya ni kuomba rehema na toba watu wote wa ulimwengu na kumaanisha kuacha dhambi kabisa, tena iwe ni toba na rehema ya kudumu siku zote za maisha yetu ili huyu adui asije akapata tena nafasi ya kuipiga dunia. Tumemwomba MUNGU na ameturehemu na sasa Corona itaisha sababu MUNGU anasikia maombi ya watakatifu wake anaopendezwa nao katika dunia hii. Ila bado litakuja pigo lingine kwa wale wanaoabudu miungu, majini, mapepo, mizimu na vitu vyote ambavyo siyo MUNGU wa mbinguni, hivyo nawasihi mataifa kwa wale wasiojua kuwa ni dhambi kuabudu miungu waache maana kazi ya Nabii ni kutoa taarifa kwa ajili ya yatakayokuja na ndiyo niliyoambiwa na MUNGU, hawatakuwa na amani kabisa wamrejee MUNGU watubu sasa, hili jambo la miungu litakuwa ni pigo kubwa zaidi ya Corona (Covid-19), ila litawahusu tuu hao wasiomuabudu MUNGU aliyewaumba, muiache, haiongei, hajibu, haijakuumba.

Read More

Live a Reply

Live Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *