DALILI ZA KUMJUA MCHUNGAJI AU MTUMISHI ALIYETEKWA NA YUPO KUZIMU

[ad_1]

                              

 Ndugu msomaji na mwanadamu uliyeumbwa kwa mfano wa sura ya MUNGU na siyo ya shetani, MUNGU huyu aliye hai anawapenda watu wake, na hapendi wapotee anataka muwe salama ili siku moja mfike na muwe mbinguni na siyo kuzimu alipo shetani, na ndipo penye  makao yake.

Nitakufundisha kidogo ili ufunguke fahamu zako maana watu wengi katika nchi zote wanampenda MUNGU aliye hai ambaye ndiye BABA yake YESU KRISTO WA NAZARETI ila madereva, au viongozi wanao waongoza katika Imani ya Kikristo hawapo tena katika ufalme wa MUNGU ila wapo katika ufalme wa shetani (kuzimu) japo mnawaona kwa macho ya nyama na damu katika ulimwengu huu .

Na kama hawapo katika ufalme wa MUNGU japo wanamtaja huyu YESU, ujue hata hizo injili  na makanisa hayo yote yapo kuzimu na hao waumini wanapelekwa  kuzimu wote na watumishi,  na siyo lazima mtumishi awe mshirikina ndiyo atatekwa na shetani, ila hata akienda kinyume na NENO la MUNGU tu, hiyo ndiyo tiketi ya yeye kutekwa na shetani (free ticket)  ila zaidi  nitaelekeza ili uweze kumjua mchungaji au mtumishi ambaye yupo duniani na anafanya kazi ya kanisa kimwili na kumbe huyupo katika channel ya YESU WA NAZARETI. Soma Mathayo (7:15-19) Jihadharini na Manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa undani ni mbwa mwitu wakali, mtawatambua kwa matendo yao.

Je watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti? Hivyo ndivyo kila mti  mwema huzaa matunda mazuri, na mti mwovu huzaa matunda mabaya wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.

Kwa kifupi, nitakuelezea tunda baya na tunda jema, anasema mtawajua hawa  watumishi kwa matunda  yaoya kuwa ni wema au ni mbwa mwitu.

Mchungaji mwema ni YESU  na YESU  kwa sababu ni mwema yeye huzaa mema. Na yeye hukaa ndani ya mtumishi aliye mwema na kutenda mema na hufanya mema na kulitenda  Neno lake. Huyo  ndiye salama na yeye hayupo kuzimu.

Ila akitenda tofauti na Biblia na Neno la MUNGU kuwa tofauti , tayari ujue huyo mtumishi ndani yake ni mfalme wa kuzimu ndio anakaa na kwanza  ili atende  kinyume na Biblia au Neno la MUNGU ufahamu wake na roho yake  tayari vinakuwepo kuzimu vina elekezwa  kuharibu kazi ya MUNGU na matokeo yake utayaona kwa huyo mtumishi anafanya mambo tofauti  na ya mbinguni na tofauti na  Neno la MUNGU.

Nitakuelezea baadhi ya mambo yafuatayo ili utakapo yaona  wewe muumini ujuwe na wewe mtumishi utakapojikuta unayafanya haya yafuatayo, ujijue upo kuzimu katika ufalme wa shetani, umeshakamatwa au kutekwa nyara tena bila kujijua na wapo wengine wanaojijua ila hufanya siri wasijulikane, maana wanapapenda kuzimu sanana 98% katika ulimwengu wote wapo huko. Na kamawapo huko je, unategemea hayo ufundishwayo yatakuwa mema kwako au unapandiwa mazuri?

Jibu ni unapandikiziwa mapando ya roho za kuzimu ili na wewe usije ukaenda mbinguni , ubaki kuwa mtoto wa shetani bila kujijua, ila sasa utajijua na ukiujua ukweli ndio uponyaji  wako kazi inabaki kwako kusuka au kunyoa.


MATENDO HAYA YAFUATAYO UKIONA MTUMISHI ANAYAFANYA KIMWILI UJUE YUPO KUZIMU TAYARI.

  1. Mwanachama wa chama cha freemason ( Angalia kwenye mtandao)

  1. Akiwa mshirikina na anaenda kwa waganga wa kienyeji

  1. Anafanya mitambiko na desturi za Mila

  1. Hajaokoka halafu anaongoza kanisa au waumini

  1. Anabatiza ubatizo wa maji ya kikombe (Ubatizo tofauti na Biblia)

  1. Kuabudu sanamu , na kufanya ibada za wakfu

  1. Kuzika Biblia na kufukia majina ya waumini kanisani  na vitu vyao

  1. Mtumishi anayebatiza watu kwa jina lake, haijalishi ni ubatizo wa maji mengi.

  1. Mlevi, mzinzi, anachangisha pesa kanisani, kufanya kazi ya MUNGU ni mradi au biashara

  1. Anayefufua misukule, kutoa watu vitu vinavyoonekana kwa macho mfano nywele, chuma, mawe, chupa, nyoka na vinginevyo .

  1. Kufungisha ndoa kwa agano la shida, kusoma majina ya waumini wanaotoa sadaka ya  fungu la kumi na kuwapa vyeti vya hongera(congratulation certificates) na kuwapa risiti mara watoapo sadaka, na huwaambia watu waandike sadaka zao majina katika bahasha, wakati MUNGU aliyepo mbinguni anasema mnitoleapo sadaka asijue hata mtu yeyote,ila kwa sababu ufahamu na roho yake vipo kuzimu(Nafsi) ndiyo mana anatenda hayo ya kuzimu anavyoelekezwa na kuzimu.
  2. Mtumishi anayezini na waumini, kwa watumishi wa jinsia ya kiume hupenda kuzini na wasichana wenye umri mdogo tena ni waumini na watumishi wa kike huzini na wa umri yeyote.

  1. Huomba pesa za kufanyia hiyo kazi kwa wanadamu, maana shetani hana pesa hivyo hukuomba wewe uwasaidie, na wewe hufanya bila kujua. Mfano hata pesa za (Partinership),kusapoti TV, au Redio.
Hii ni sababu MUNGU hajawatuma, akikutuma  yeye hukuandalia njia pasipo mtumishi kuomba omba na kumfanya MUNGU ni masikini.
            Jibu siyo ila shetani na yeye ni aina ya mungu ambaye ni masikini ndiyo  
             maana fomula yake yeye nikuomba omba,kila kitu katika ulimwengu huu.
            
     14.  Kuwachapa waumini bakora wanapolipuka mapepo, kuwalisha waumini  
             udongo wa kaburi au kutengeneza kaburi eneo lolote na  kupaita golgota  
             mwende mlilie  shida zenu zote hapo,ukila tu, umeila mauti ya kuzimu, na
             umejiingiza katika kaburi lako la mauti. ( Huyu ni muuaji)
     
    15.   Zaidi soma kitabu cha Nabii Hebron (a) JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA  
      SHETANI,  (b) MKRISTO USIKUBALI KUWA MPUMBAVU (c) MPINGA KRISTO     
       NI NANI?  Natumaini utapata picha halisi au utamjua YESU vizuri na roho   
       yako itapona na hautakubali kuongozwa na mtumishi ambaye ndani yake  
       kuna ufalme wa shetani na siyo ufalme wa MUNGU aliye hai



     NABII HEBRON.

[ad_2]