DELILA ALIYEMSALITI SAMSONI, AKAMATWA RASMI KUZIMU TAREHE 15.12.2012

DELILA ALIYEMSALITI SAMSONI, AKAMATWA RASMI KUZIMU TAREHE 15.12.2012

[ad_1]

DELILA ALIYEMSALITI SAMSONI, AKAMATWA RASMI KUZIMU TAREHE 15.12.2012.
WAAMUZI 16:1-30
Ndugu msomaji na mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU na hata kufanana na yeye kwa sura na mfano wake, napenda kukuelezea kwanza kuhusu Samsoni. Samsoni ni mnadhiri wa MUNGU, ambaye MUNGU alimwandaa kwa ajili ya kazi yake kama mpiganaji au jemadari aliyetumika kimwili nyakati hizo, ila hakuweza kufikia lengo alilopangiwa na MUNGU afanye, na sababu kuu alikuwa na tamaa na alikosa utii, akatoa siri ya asili ya nguvu zake, hata akaangamia ila na yeye mwishowe alipata nguvu tena baada ya nywele kuota na akalipiza kisasi, japo na yeye alikufa na haikujulikana mwili wake ni upi. Napenda ujue pia huyu Samsoni ni mmoja wa wazee 24 waliopo mbinguni pamoja na MUNGU. Nilipata bahati ya kuongea naye,  na mimi pia alinifundisha mambo mengi na pia ni rafiki yangu sana. Kazi yake anatumika kwenye ulimwengu wa roho kuwapiga maadui wa YESU na maadui wanaopinga kazi kazi ya YESU.  Kwa sasa, yale mamlaka aliyokuwa anatumika kimwili katika vita hapa ulimwenguni, anatumika katika ulimwengu wa roho na mnavyofikiria Samsoni, kuzimu yote, wachawi wote, kwa viwango tofauti kwa sasa hivi ni yeye anapigana nao. Anao uweza, hauelezeki. Shetani kwa sasa hana nafasi, ni kibano, hata wanavyojiunganisha mfano manabii wa uongo, wachawi, mizimu, wote hao anawalipua kila muda. Anampenda sana MUNGU. Siku moja niilipigana katika ulimwengu wa roho, mwishowe alikuja kwa hasira sana; alitamani ashuke kimwili abakie hapa ulimwenguni aanze kuwacharaza watu wanaotumia jina la BABA yake vibaya, wengine kewatesa wana wa MUNGU.
Kwa sasa nakufunuliwa mambo ya uchawi na nguvu za giza, hazina nguvu, serikali ya mbinguni wakiwamo wazee 24, wapo kazini kufanya maandalizi ya ujio wa YESU KRISTO wa Nazarethi, na ndio ninaoshirikiana nao, pia akiwamo na YESU mwenyewe. Uwezo wao hauelezeke, mitandao ya shetani imeangamizwa sasa hivi. Haya ni mabaki tu na kila siku yanazidi kuangamizwa kwenye ulimwengu wa roho. Kwa sasa ni vita vikali sana na wanaotumia nguvu za giza wanalitambua hili, hawana amani. Mengine hata nikieleza hutaelewa, ni mambo ya sirini na MUNGU.
Delila:
Huyu ni mwanamke aliyemsaliti Samsoni kwa Wafilisti, alitumiwa na shetani kumuangusha Samsoni na kuharibu kusudi la MUNGU. Huyu Delila alikuwa kuzimu na alipewa cheo kikubwa sana katika ufalme wa shetani. Nilishangaa sana, shetani na yeye, mtu akimtumikia duniani, anapokufa humpa cheo, ila mwisho lazima ni jehanamu. Shetani ameiga kwa MUNGU, mfano wale waliomtumikia kikamilifu MUNGU, na wao makao yao ni ya kifalme hawatahukumiwa milele tofauti na malipo ya shetani ambayo ni jehanamu. Malipo ya MUNGU ni uzima wa milele.
Kazi za Delila alikuwa anamwaga roho za kuangusha watumishi wale walioitwa na MUNGU, kuharibu maono yao na wasifanikiwe kusonga mbele, kama ilivyo leo hii watumishi 98% wamemsaliti YESU na kukata tamaa, na wengine kuirudia dunia.
Kitengo hicho ni Delila na baraza lake, na anafanya hizi kazi kama mzimu. Amekamatwa tarehe 15.12.2012 saa saba mchana nilivyokuwa kwenye maombi, ilikuwa ni tendo la dakika 17. Hivi vyote nimemnyang’anya kila kitu, mwishowe Malaika Mkuu Mikael akamfungia, pia na wale waliomuua Samsoni (Wafilisti) wote wameshakamatwa, wapo kifungoni. Na sasa, kanisa na wale watumishi walioitwa mtaona hawaanguki tena, wanasonga mbele, na kazi itakuwa siyo ngumu tena. Ila wale waliojiita, wenyewe au kujifanya, mtazidi kuaibika na kuporomoka. Kazi hiyo anaifanya YESU peke yake. Nimekuambia kwa sababu ninajua kinachoendelea na anachokifanya kwa ajili ya maandalizi ya ujio wake. Asilimia 45% ya watumishi ulimwenguni ni wachawi kiwango cha juu, 53% hawajielewi na wengine wamerudi nyuma, na wengine wanaongozwa na mizimu; hawa pia wamepotea. Funguka, fuata Biblia inavyosema. Soma vitabu utajua mkao unaotakiwa ukae, ndio utapona. Ni aibu 2% tu ulimwenguni; hawa ndio YESU anawatumia. Wengine wote siyo YESU anawaongoza, ni hatari sana (Yohana 14:6) kama hawaongozwi na YESU wanaongozwa na shetani, haijalishi wanamtaja YESU, ni kwa unafiki tu, kwa midomo yao ila mioyoni mwao ni mbwa mwitu.
Nikuulize swali, je, kwa hali hii ulimwengu ungepona? Hapana. Sasa hivi kanisa limekuwa ni sehemu ya kutafuta pesa na kuwanyang’anya mali wana wa MUNGU. YESU amesema mnaibiwa. Yeye hahusiki; nyumba yake ni nyumba ya sala, alishayakataa hayo na sasa yamerudishwa na yeye hashiriki vitu hivyo, ni vya shetani. Kanisa sasa hivi – (baadhi), yana nyumba za bar, bank, na kufanya minada na harambee. Yeye (YESU) sio masikini, YESU hauzi pombe, YESU hachaji mtu riba, kama kanisa lina bank, ina maana YESU anachaji mtu riba? Neno linasema, usimchaji mtu riba, hizi bank ni za shetani ndani ya kanisa. Hata kanisa halipaswi kukopa pesa bank ndio lijenge jengo, hilo jengo hamtakaa mumwone YESU milele mahali hapo.  Kama huyo mtumishi amemwita YESU, yeye atalijenga mwenyewe. Tena hata siyo kwa njia ya michango, acheni mnaibiwa na hamtabarikiwa milele na hamtarithi mbingu (Ufunuo wa yohana 22:18-20).
NENO linasema, utoapo sadaka, hata kushoto isijue, ajue MUNGU tu. Leo hii, sheria ya MUNGU imepuuzwa, unaandika jina, kiasi, na namba ya simu na wengine wanakupa risiti. Sadaka hizo hazipokei, mnaibiwa na shetani. YESU kaniambia, Biblia ndio katiba au muongozo wa kumjua yeye. Je, nikuulize, haya yametoka wapi? Tafuta, hamna kwenye biblia, yametoka kwa shetani. Nikuulize swali, soma kitabu chote cha Mwanzo mpaka Ufunuo, tafuta ubatizo wa kikombe kama utauona; jibu haupo. Na hata kwenye mafaili ya mbinguni haupo. Ubatizo wa kweli ni wa maji mengi tu aliobatizwa YESU (Yohana 14:6). Kama hujabatizwa kama YESU, ameniambia hujabatizwa, na mbinguni huendi, haijalishi unaongoza dini kubwa au cheo, au degree za Biblia; hata hiyo elimu ni bure, chunguza kama ubatizo wa kikombe upo? Jibu haupo, umetokea kwa shetani. Ubatizo wa kweli ni wa Yohana aliotumwa na MUNGU kubatiza, ndio wa MUNGU huo wa kikombe sio wa MUNGU. YESU alinieleza mfunguke, mpone na mtii yale aliyoagiza MUNGU, msifanye ubatizo ambao hajaagiza (Ufunuo 22 18-20). Na usikubali kubatizwa kwa jina la mchungaji, MUNGU ameagiza mbatizwe kwa jina la BABA, na MWANA na ROHO MTAKATIFU. Huyo anayewabatiza kwa jina lake, haijalishi ni ubatizo wa maji mengi, ndugu, bado hujabatizwa. Hapo unakuwa umewekwa wakfu, wewe ni wa huyo mtumishi tu, na siyo wa YESU. Na mtumishi wa jinsi hiyo, hatumiwi na YESU 100% huyo ni msaliti wa YESU au ni muuaji wa kiroho kwa wana wa MUNGU, na mbinguni hauendi. Ndugu, uzidi kufunguliwa na uzidi kumjua YESU wa Nazarethi aliye hai. Ole wenu nyie mnaowaongoza wana wa MUNGU vibaya. Alichoniambia YESU, mmesha hukumiwa wala majina yenu hayapo katika kitabu cha uzima wa milele. Badilika, na ole wao wanaozika au kufukia Biblia, hukumu inawasubiri, na mmeshalaaniwa na MUNGU mwenyewe. Msifukie Biblia; ina maana mnazika NENO la MUNGU lisiendelee. Na usikubali picha yako au jina lako au pesa yako ifukiwe kanisani, kwa mtumishi anayefanya hivyo, huyo ni mchawi, na anaongozwa na shetani ili kukuangamiza wewe. Hii ni kwa ulimwengu wote. Ujumbe huu ninaokuletea wewe, nimeamriwa na YESU niutoe kwa ulimwengu wote.
YESU ANAWAPENDA, MRUDIENI YEYE. 

MATUKIO MBALIMBALI YA IBADA SIKU KUU YA KRISMAS 25-12-2012.
Mtume na Nabii Hebron akiongoza umati wa waumini waliofurika kwa wingi katika ibada maalum ya kumbukumbu ya siku aliyozaliwa mwokozi wa ulimwengu YESU KRISTO wa Nazarethi wimbo wa kuabudu.
Waumini wa Kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE wakisifu na kuabudu katika ibada maalum ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO wa Nazarethi, ambaye ndiye mwokozi wa ulimwengu wote.

Mtume na Nabii Hebron akiwaombea wagonjwa na wenye vifungo mbalimbali, kwa ishara ya wagonjwa kushika vazi lake, kama YESU alivyofanya akiwa ulimwenguni, nao wagonjwa na wenye vifungo walipokea uponyaji papo hapo.
Baba huyu pia alipokea uponyaji wake papo hapo baada ya kugusa vazi la Mtume na Nabii Hebron katika ibada ya leo ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa MASIHI wa ulimwengu, yaani YESU KRISTO wa Nazarethi.

Waumini wakimtukuza YESU KRISTO wa Nazarethi, baada ya kupokea ile nuru ya mwanga wa nyota iliyowaongoza mamajusi kumlaki YESU KRISTO wakishangilia kuunganishwa na baraka za siku kuu ya Krismasi.

 Kwa mawasiliano;
+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149

Email:
Imeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,
KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]