JE, NI SAHIHI KUFANYA MAOMBI KATIKA KABURI LA YESU AU KATIKA MAKABURI YA MITUME?

[ad_1]

BWANA YESU asifiwe, watu wote wa mataifa yote, au kwa jina lingine huyu YESU anaitwa
Nabii Issa.
Katika makala hii ya Nabii Hebron, nitaelezea na kuweka kweli kwa watu wote, ili hii kweli iwaweke watu huru na siku moja mfike mbinguni sababu hata mimi sikuujua ukweli hadi YESU mwenyewe alivyonifundisha kama Mtume wake kwa ajili ya kazi yake atakavyo yeye na siyo mapokeo ya watu. Mambo hayo alinifundisha miaka minne iliyopita (2011) kuhusu watu wavyopokea na  kufundishwa uongo japo hawajui na wengine wanajua. Aliniambia hivi Hebron, hivi mimi nipo kaburini au mbinguni? Nikajibu upo mbinguni. Akaniuliza swali lingine, hivi mimi jina langu ni kaburi au ni nani? Nikamjibu wewe ni YESU. Akaniambia, Hebron, mimi sipo pale kaburini, na siishi pale, wala hakuna kitu changu chochote, hivyo itafika wakati utaenda, ila usisujudu pale, nenda katembee kama vile mtalii na
ukajifunze. Usifanye ibada wala kuabudu kaburini kabisa, akaniambia na mimi kwenda kutembea Israel, ila usivisujudie vitu hivyo iwe ni makaburi ya mitume, na maeneo yote, ukienda tofauti na hivi utakuwa umepotea na utakuwa umevunja moja ya amri ya MUNGU; usiabudu chochote, wala kukisujudia chochote kwa mfano wa kitu.
Akanieleza, huku Israel ni mahali pa historia na kumbukumbu za mitume na hata mimi katika
maisha tuliyopitia, mimi nipo mbinguni, ila sipo kaburini sasa watu wanafanya sala pale kaburini; maombi yale yanabadilishwa katika ulimwengu wa roho, yanachukuliwa na yesu wa uongo na kuunganishwa na mpinga kristo na shetani anakuwa anao uhalali sababu imeandikwa katika amri zile kumi “usisujudie”. Sasa pale kaburini ni kama sanamu. Au nikuulize wewe, je, unaposali pale kaburini; je,  shetani akikuuliza hilo swali, utamjibuje? Ni nani unamsujudia hapa kaburini? Je, anaishi hapa? Jibu ni hapana, na kama haishi hapa, sasa unamsujudu usiyemjua pasipo kujua au kwa kujua. Hivyo basi, kama kwamba YESU katika eneo ambalo hayupo uelewe umemwabudu shetani na watu wengi  wanafikiria eti walienda katika kaburi la YESU na hata katika makaburi yote ya mitume na manabii, elewa pia, nataka uelewe kuwa hata shetani na yeye anao mitume  wake hivyo hivyo na MUNGU anao wa kwake na wapo hapa duniani wanaendeleza kazi walizotumwa. Nataka muelewe ukuu wa YESU hata kimwili, kwani YESU katika kaburi lake angekuwapo au baraka zake au nguvu zake, nawaeleza hivi, aliyefika pale angebadilika kiroho na kimwili. Cha ajabu walevi, wachawi, watumishi wa uongo wanaenda kila siku, cha ajabu  hawabadiliki na zaidi hata waabudu sanamu wanaenda hakuna mabadiliko ya utakatifu. Hiyo ni ishara YESU hayupo kaburini hivyo  msifanye maombi katika kaburi la YESU. Utakayesikia elewa ili upone, utakayekaza shingo, ujumbe umeupata na YESU anajua umeujua ukweli hivyo utubu na uwache. Wewe nenda katembee tu na kujifunza.  Yeye yupo mbinguni na atarudi kulinyakua kanisa ambalo ni mtu aliyeokoka na asiyefanya matambiko, YESU hana matambiko. Niliogopa sana maana na mimi sikuyajua haya. Mimi YESU nipo mbinguni, natafutwa katika roho na kweli, njia nilishaionyesha ifuatwe; na hata katika Biblia haijaruhusu watu wakaabudu katika kaburi langu mimi YESU.  Katika kaburi kuna mizimu, hivyo ukifanya sala kaburini unakuwa unaungana na mizimu, na mizimu inakuwa kwa shetani. Jitengeni na mizimu.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Sitarudia wala kujaribu kusujudu katika kaburi lako kwa sababu  wewe haupo pale.

Nabii Hebron.

[ad_2]