Close

JE UNAJUA KUSUDI LA SHETANI AMBALO MCHUNGAJI ANABATIZA KWA JINA LAKE?

[ad_1]

Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na aliye ndiye kweli milele, leo nawafundisha na kuifichua uovu wa wachungaji ambao wanawabatiza watu kwa majina yao. Swali la kwanza ndugu msomaji soma biblia yote, haijaruhusu watu wabatizwe kwa jina la mchungaji. YESU aliyenituma kwa mataifa yote aliniambia mwanangu Hebron watoto wangu wanateswa na shetani na wengi wametekwa na wanaotumika kuwateka ni watumishi waliomsaliti na kumkufuru MUNGU na kulibadilisha neno la MUNGU na pia na wale waliojiita ambao mimi siwajui wala BABA yangu hawajui na wale walio wachawi. Sasa nenda uwafungue watu na uwaeleze habari zangu za kweli, na kila atakayeipokea na kuokoka na kuishi maisha matakatifu huyo ataokoka.
Sasa nakuja katika mada yak wa nini mchungaji anakubatiza kwa jina lake au anawabatiza watu katika kanisa lake kwa jina lake? Jambo la kwanza huo ni ufunuo aliopewa katika biblia ya shetani ndio anaoutumia.
Jambo la pili ndani yake hana ROHO MTAKATIFU bali anayo roho mchasu na hana MUNGU wa kweli ndio sababu hayatendi kama ilivyoamriwa na MUNGU katika ubatizo na pia hana ROHO MTAKATIFU ndiyo sababu hashuhudii kweli ya MUNGU.
Jambo la tatu, anakuwa ni mwili mmoja na wewe badala ya wewe kuwa ni mwili mmoja na YESU, hivyo atakutawala na kukumiliki siku zote na YESU hatakumiliki kabisa na hata ule mwisho hauendi mbinguni na zaidi unakuwa ni mfuasi wa serikali ya shetani na mpinga kristo pasipokujua wewe muumini hii ni siri ya pastor.
Jambo la nne, uelewe mtumishi huyo anatumia nguvu za giza 100% haijalishi analitaja jina la YESU au hapo awali alikuwa ni mtumishi wa MUNGU wa kweli. Ukiona hayo uelewe ameacha njia ya mbinguni anaelekea jehanamu pamoja na waumini wake.
Jambo la tano, ni agano la shetani ambalo anapewa na shetani kama kiapo cha kukuteka wewe uwe ni mali ya shetani kama alivyo yeye mchungaji na kukufanya uwe na uhusiano mbaya na YESU.
NOTE:
Rudi katika biblia angalia mifano yote hautakuta mwanadamu anatakiwa abatizwe kwa jina la mchungaji. Ni YESU peke yake ili awe mwili mmoja na mtu ili awe mkristo yaani mwili mmoja na YESU ni lazima aamini na akubali akiwa na akili yake na aokoke. Ikiwa ni tofauti uelewe hajabatizwa na ni ubatizo wa maji mengi peke yake, zaidi soma blog ya Nabii Hebron www.prophethebron.blogsot.com, tafuta masomo ya ubatizo na vitabu vitakuweka huru. Na kama ndugu msomaji umebatizwa kwa jina la mchungaji yeyote Yule nakueleza haujabatizwa na pili wewe siyo mkristo, na tatu wewe siyo mwili mmoja na YESU sababu umekubali na ukaamini kubatizwa kwa jina la mchungaji (Soma Marko 16:15-16) wewe umemuamini mtu badala ya YESU hapa ni kinyume, sasa amua ukabatizwe upya hata hapo katika kanisa hilo umeshapata jibu hapo ni kaburi la kiroho za kuua roho za wana wa MUNGU. Amenituma YESU niwaeleze ulimwengu wote, anayesikia sikia, atakayekaza shingo jehanamu inamsubiri.
BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu unitoe katika kifungo hichi nilichobatizwa kwa jina la pastor ambaye ni saliti wako, niokoe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima, uniongoze mahali sahihi nikabatizwe upya niwe na ushirika wa kweli na wewe. Amen.

NABII HEBRON.

[ad_2]