JE UNAJUA KUWA 98% YA WATUMISHI WA KWELI AU WAUMINI ALL OVER THE WORLD BADO HAWAJAZALIWA MARA YA PILI, NA HAWATAENDA MBINGUNI!!

[ad_1]

YOHANA 3:1-6 JE NI WEWE?

“Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2Huyo alimjia usiku, akamwambia Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa MUNGU; kwa maana hakuna mtu awzaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa MUNGU yu pamoja naye. 3YESU akajibu akamwambia, Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa MUNGU. 4Nikodemo akamwambia, awezaje mtu kuzaliwa, akiwa ni mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5YESU akajibu, amin, amin nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa ROHO, hawezi kuingia ufalme wa MUNGU. 6Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa ROHO ni ROHO. 7Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
BWANA YESU ASIFIWE, nawasalimu watu wote wa mataifa yote, ambao mmeumbwa na MUNGU na pia unafanana nay eye kwa sura na mfano wake. Amenituma mwanae wa pekee kwenu nyie niwaeleze ukweli na kuwaonyesha njia ya kweli ili kila atakayeifuata ataurithi ufalme wa MUNGU na kila atakaye kaza shingo kukataa kumrejea MUNGU aokoke ataurithi ufalme wa shetani ambapo mahali peke ni jehanamu alipoandaliwa yeye na malaika zake na wanadamu waliomkataa YESU WA NAZARETI. Amenituma mengi ni kwa ajili yako wewe unayetafuta njia ya ukweli ya mbinguni ili siku moja na wewe ukakae na YESU mahali alipo na yeye . Ameniambia niwaeleze mbatizwe watu wote yaani mzaliwe mara ya pili kama alivyozaliwa yeye mara ya pili ili mfike mbinguni, kinyume cha hapo, kama haujazaliwa mara ya pili hakika hautaenda mbinguni huo ndio ukweli. Wengi wakristo mnadanganyika mpaka sasa mnajiita wakristo lakini hamjazaliwa mara ya pili. Nitaelezea jinsi inavyotakiwa ili uzaliwe mara ya pili.
Kwanza mwanadamu anazaliwa kimwili na baadaye anaonekana mwili halisi (huku ndiko kuzaliwa mara ya kwanza) na kuzaliwa mara ya pili lazima uwe mtu mzima na una akili zako hapa unazaliwa kiroho hivyo hauhitaji kurudi tena tumboni mwa mama yako na pia haiwezekani urudi tena kwenye tumbo la mama yako. Jinsi ya kuzaliwa mara ya pili ni unabatizwa katika maji mengi yanayotembea kama vile YESU alivyobatizwa katika mto Yordani. Na unapozaliwa mara ya pili ni tendo la imani, ukubali peke yako wewe mhusika na uamue kutoka moyoni mwako ukiwa unayo akili timamu kama vile YESU alivyokuwa na akili timamu na akaonyesha njia ifuatwe ambayo ndiyo sahihi. Tazama Nikodemo yeye alikuwa ni mtumishi katika masinagogi (leo hii ndio wanaitwa watumishi, wachungaji, waalimu, mtume, nabii, wazee wa kanisa, shemasi, maaskofu).
Nikodemo alimuamini YESU kuwa ni mwana wa MUNGU lakini alikuwa hajazaliwa mara ya pili na hakujua ukweli, mpaka pale alipoelezwa na YESU ya kuwa mpaka uzaliwe mara ya pili ndio utaurithi ufalme wa MUNGU. Nikodemo alishangaa, hivi ndivyo ilivyo hata sasa manikodemo ni wengi hawajazaliwa mara ya pili na wanahubiri makanisani katika ulimwengu wote wakati hata wao hawaendi mbinguni. Na kama mtu anakuhubiria habari za ufalme wa mbinguni wakati yeye mwenyewe haendi, sababu hajazaliwa mara ya pili je hauoni huku ni kuwapotosha watu  waangamie roho zao na hauoni hawa ni viongozi vipofu? Na hata waumini wao wamekuwa vipofu? Rudi katika neno, linasemaje? Je ni biblia gani wanayoitumia? Jibu ni ya shetani ndio watu hawazaliwi mara ya pili ili wasiurithi ufalme wa MUNGU na kama hawajazaliwa mara ya pili basi ni wazi na ni kweli bila kubisha makanisa hayo ni ya miungu na yesu wa uongo na mpinga kristo. Na je kama ni mtumishi na unahubiri kanisani halafu wewe peke yako hauendi mbinguni je hauoni utadaiwa hizo roho na MUNGU? Na kama ulikuwa haujui sasa amua ukazaliwe mara ya pili na utoke huko sababu huko ni mahali feki na ni mahali pa gereza la kuwahifadhi wanadamu wasimjue YESU ili akija katika unaykuo watu wabakie hapo hapo sababu hawajazaliwa mara ya pili, kama ulikuwa hauelewi sasa elewa na utapona roho yako. Makanisa mengi zaidi siyo ya MUNGU WA KWELI bali ni ya miungu.
Na je umeshajiuliza ni kwa nini lazima mtu azaliwe mara ya pili ndio uende mbinguni? Soma masomo haya na ubishi utakwisha 1 Wakorintho 15:50…, Yohana 3:6, Mathayo1: 18-25. Watu ni lazima wazaliwe mara ya pili sababu kila mwanadamu anayezaliwa lazima azaliwe na dhambi ya asili ambayo unarithi kutoka kwa wazazi wetu, na pia mwili imetokana na udongo na hivyo itarudi kwa udongo, sasa ili uzaliwe mara ya pili ni ubatizwe ubatizo wa maji mengi ukiwa mtu mzima, unapozaliwa mara ya pili unaondolewa ile dhambi ya asili na unavuliwa sura ya asili, unavalishwa sura ya mbinguni ambayo ni sura ya YESU (Adamu wa pili) na tendo hili ni la roho yako na mbinguni hauwezi kwenda kama bado haujazaliwa mara ya pili. Zaidi soma kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA WATU WOTE (Nabii Hebron Kisamo) utaelewa vizuri na utaona jinsi mamilioni ya watu mpaka sasa hawajijui ya kuwa hawaendi mbinguni. Sababu ya kina Nikodemo wa siku hizi (watumishi wasiomjua MUNGU wa kweli).
Tendo tu la kutozaliwa mara ya pili katika makanisa pamoja na watumishi hii ni dalili tosha wanamtumikia mungu wasiomjua (mungu wa uongo) haijalishi wanalitaja jina la YESU (YESU alishasema watawadanganya wengi wakitumia jina langu) hata sasa angalia je maneno ya YESU hayajatimia? Watu wote ambao hawajazaliwa mara ya pili bado wanayo dhambi ya asili na hakuna mwenye dhambi ambaye atakayeingia mbinguni. Jichunguze je hauna hiyo dhambi? Zaidi shetani akabadilisha formula ya kuzalisha watu kiroho mara ya pili, wakristo wengi badala ya kubatizwa wakiwa watu wazima na akili zao, sasa wakizaliwa tu wanamwagiwa maji kichwani wanaambiwa wameshazaliwa mara ya pili. Nawaeleza watu wote unapobatizwa kwa maji ya kichwani, maji ya kisima, au kwa jina la mchungaji, nawaeleza mnakuwa mmebatizwa au kuzaliwa mara ya pili ili muurithi ufalme wa shetani na hili limefanyika ili kuwapiga upofu watu waridhike tayari tendo hilo la kuzaliwa mara ya pili limefanyika kwao. Swali je ulipobatizwa uliona, ulikubali, uliamini, ulishaokoka? Jibu ulilonalo ni taarifa tu uliopewa ulivyokuwa mtu mzima. Na ukifuatilia kitabu kitakatifu biblia utaona utaratibu wa mtu kuzaliwa mara ya pili, lazima aamini, akubali, aone kwa macho yake. Ikiwa ni kinyume ujue mpaka sasa haujazaliwa mara ya pili na mbinguni hauendi (hivyo ndivyo kanisa lilivyotekwa na shetani unapokea mafundisho ya uongo na uongo ukapokewa na watumishi na waumini na wanaposhiriki tu wanakuwa wanaongozwa na miungu na siyo MUNGU mtakatifu na kibinadamu nitaelezea mfano wa mkunga anayezalisha hospitalini au nyumbani, siku zote wanafuata formula ya kuzalisha , wanajua mtoto anatokea katika eneo Fulani na kudeal nalo mpaka mtoto azaliwe na aonekane. Hata kiroho formula ni hivyo hivyo tu ambazo zimeonyeshwa na MUNGU zifuatwe ndipo mtu atazaliwa mara ya pili kiroho.
Sasa kiroho formula alizozileta MUNGU zimetupiliwa mbali watu wakachukua za shetani, sasa formula ya shetani je itakuzaa wewe kiroho na kukuondolea dhambi? Jibu unalo. Huu ni wakati wako sasa na ufanye maamuzi kama kweli unayo nia ya kweli ya kwenda mbinguni. Uzaliwe mara ya pili na uangalie pia anayekubatiza, sababu kama huyo mtu anayetumika kukuzalisha mara ya pili kama yeye amejiita, anajifanya, ni mtumishi wa mshahara na yeye hajazaliwa mara ya pili au ni mchawi, anafanya biashara; michango, benki, mlevi, mzinzi, muabudu sanamu, au amemsaliti MUNGU, au ni freemason au anaongozwa na mizimu, mfanya mazingaumbwe, au hata MUNGU hamjui ila yeye anajifanyia tu wala hajatumwa na MUNGU nakueleza ukweli bado utakuwa haujazaliwa mara ya pili sababu ROHO MTAKATIFU hayupo ndani yake ni roho myingie na hapa mabilioni ya watu wanapigwa upofu. Aliponionyesha YESU niliona watu ambao idadi yake sikuwa na hesabu ni umati ambao unawea ukajaa urefu wa kilomita 100 kwa urefu na upana, wakiwemo waliookoka na wamebatizwa kwa maji mengi lakini kumbe wamezaliwa feki na hawajui ukweli hii ni wan chi zote na mabara yote. Unayejiita mkristo haukamiliki kama haujaokoka, kuzaliwa mara ya pili ukiwa mtu mzima. Iwe ni waumini na watumishi. Mfano halisi nimeelezea habari za Nikodemo, tazama hata Paulo alibatizwa mara ya pili akabadilika, nawasihi mfunguke mkatae uongo MUNGU anawaoenda watu ndio sababu aliandaa njia njema ya watu wazaliwe mara ya pili na shetani hapendi kabisa watu wazaliwe mara ya pili sababu anajua pendo lake la dhambi litaondoka ndani yako na hata kupata. Haijalishi unaenda kanisani kila jumapili kama haujazaliwa mara ya pili mbinguni hauendi kabisa na kama unasali katika kanisa ambalo linabatiza ubatizo wa kikombe uelewe hapo ni pangoni au shimoni pa kuzika roho zenu, na hapo hakuna njia ya mbinguni ni jehanamu wala halipeleki mtu mbinguni sababu watu hawazaliwi mara ya pili kiroho. Haijalishi wewe ni tajiri namba moja wa ulimwengu wote, iwe ni mfalme, ni Rais wa dunia yote ni mtu maarufu wa aina yeyote au ni maskini au haujasoma, unajulikana, kama haujazaliwa mara ya pili nakueleza kwa mamlaka aliyonipa YESU WA NAZARETI ili watu waujue ukweli wapone roho zao, kama haujazaliwa mara ya pili mbinguni hautaenda na utajijua kabisa kuanzia sasa kama unaenda mbinguni au hauendi, chunguza ubatizo wako, na uishi maisha matakatifu ya kumpendeza MUNGU.
NOTE:
Hii ni story ya kweli kabisa mimi nilikuwa Driver guide katika nchi ya Tanzania, niliacha pale nilipokutana na YESU ana kwa ana Serengeti 2010. Nilikutana na kutembeza wageni karibu mataifa yote na mabara yote. Nitaelezea niliyokuwa naongea na baadhi ya wazungu (European, American, Indian, Chinese na wengineo wengi) walikuwa wananiambia hakuna MUNGU, wewe tumia akili yako usome, sisi hatuendi kanisani makanisa wanaenda wazee tu. Niliendelea kuwaombea sababu nilishangaa na wakati huo nilikua bado ni mchanga simjui YESU vizuri, lakini nilipokuja kuingia katika kazi yake nilikumbuka maneno waliyonieleza, kwa kweli sikuwalaamu kabisa niliona wapo sawa, sababu huko walipo walishachoka na kudanganywa na kupotosha na waligundua watumishi ni waongo na wakakata tamaa ni bora wawepo hivyo hivyo. Ila nawasihi nyie niliokuwa nawapeleka safari na wengine wote mlio kata tamaa sasa mrejeeni YESU, ni kweli mlidanganywa na YESU anawapenda. Amenituma kwenu mnaosema hakuna MUNGU, njooni kwake leo mtamuona MUNGU. Ni kweli mliondoka sababu YESU alikataliwa na watumishi na wao wakamleta yesu wa uongo wa miungu, na nyie mlishtuka, ni wajanja. Sasa leo nawakaribisha kwa YESU WA NAZARETI niliye naye ndani yangu. Useme BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, narejea kwako uniongoze wewe hadi kwa MUNGU WA KWELI, sababu tuliona hakuna MUNGU kumbe upo. Karibu ndani yangu, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, miungu siwataki tena na uniongoze ili niweze kuzaliwa mara ya pili, ili niweze kuurithi ufalme wako na mimi. Amen.
Ujumbe huu watumie na wengine kwa njia yeyote utainuliwa na utakuwa unamfurahisha YESU.
NABII HEBRON.

[ad_2]