Close

JE UNAJUA NI JINSI GANI AU NI NJIA ZIPI ALIZOZITUMIA SHETANI KUINGIZA MAFUNDISHO YA UONGO MAKANISANI KATIKA ULIMWENGU WOTE? PATA KUJUA SASA (NI KWA NJIA YA NDOTO)


BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, namshukuru sana na kumtukuza sana pamoja na serikali yake ya mbinguni kwa ajili ya kunifundisha  mengi na niwafundishe mataifa yote ili wapone roho zao, sababu hata wewe unayesoma ukipiga picha katika ufahamu wako uangalie muenendo wa makanisa ya leo utaona yapo kinyume haijalishi wanalitaja jina la YESU. Leo nitaelezea kuhusu ambavyo neno la MUNGU lilivyochanganywa na uongo, ilikuwaje, na ni njia zipi itakusaidia upone na wewe roho yako.
Kwanza kabisa katika historia ya vitabu vya biblia kwa kiwango kikubwa walioandika walioteshwa ndoto, mfano ukisoma hata katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana utaona, ukisoma Ayubu 7:14, Daniel 2:1, Daniel 7:1, Mwanzo 37: 5-9 (hii mistari utaisoma katika biblia yako, itakupa picha ya ndoto, na katika ndoto zipo za MUNGU wa kweli na za shetani hivyo hivyo, ila nitaelezea kwa upande wa kanisa na jinsi gani neno lilivyobadilishwa na kanisa kuifuata elimu dunia. Kila mtu anajua biblia ni kitabu cha MUNGU na ni kitakatifu na amekihakikisha yeye peke yake na ndio iwe katiba yake katika imani ifuatwe, lakini sasa shetani na yeye  akatumia ndoto hivyo hivyo akawaotesha watumishi ambao hawajaitwa na YESU, wanatafuta pesa, wachawi, au wa upande wa mpinga kristo, wakawaotesha wale waasisi baadhi ya makanisa mbali mbaliwakaanzishe makanisa ambayo yana maono ya kipepo au yenye ndoto za shetani halafu wakabadilisha biblia baadhi ya vipengele na kuwapiga watu upofu waone wanatumia biblia ya kweli kimwili ila katika ulimwengu wa roho wanatumia biblia ya shetani na ndiyo sababu hapa ulimwengu wanayafanya hayo. Unajua kila jambo alifanyalo mtu ndilo lililomjaa katika moyo wake.
Nitaelezea baadhi ya vipengele ila vingine nakuombea ufunguke macho na ubongo uliogandishwa sasa vifanya kazi vizuri ili watu wamjue MUNGU wa kweli. Shetani aliwaotesha waasisi wa dini mbali mbali ya kuwa ubatizo wa kikombe ndio wa MUNGU wakati ukisoma biblia hakuna ubatizo wa kikombe kabisa, lingine kanisa liabudu sanamu, lingine kanisa lifungishe ndoa ya jinsia moja, linguine kanisa libariki pombe, kubatiza watoto wadogo, kanisa lifanye biashara, lichangishe harambee, litoe makafara, watumishi wawe freemason na wachawi, wafufue misukule waseme ni YESU kafufua kumbe ni mazingaumbwe. Watumie biblia halafu yeye ataingia ndani yao atende miujiza (huyu ni shetani). Walipotii na shetani akaingia ndani yake afanye kazi. Pia lazima muelewe mwanadamu hana uwezo wa kutenda miujiza au kuponya ila linachofanyika ni uungu unaingia ndani yake unafanya hiyo kazi na kwa upande wao hao wanaotumia uchawi ni shetani ndie anayeingia kwa Yule ambaye alikubaliwa na shetani au ameitwa na shetani, au aliyemsaliti YESU sasa anabadilishwa anatumika katika upande wa shetani, YESU hundoka anabakia yesu wa uongo.
Sasa ili ujue ndani yake ni YESU yupi? Chunguza msingi wa neno, miujiza, ubatizo, habari za michango, kuandika sadaka majina, ufisadi, unyang’anyi wa mali za watu. Angalia anaweka bendera kanisani au kwenye gari lake, bendera yake binafsi. Kuabudu sanamu, kuvaa misalaba, kuabudu watoto wa MUNGU badala ya MUNGU, YESU na ROHO MTAKATIFU peke yake, haijalishi wanachanganya hi ni kukupiga upofu wewe uone upo sawa ila kumbe tayari umetekwa na shetani. Watu wanafikiri kutekwa na shetani, shetani atakuja na kamba na pingu kimwili, sasa uelewe pingu anazozitumia shetani au kamba au mtego wa kukukamata wewe ni neno lililoongezwa katika biblia na linatumika makanisani. Na hapa ulimwenguni watu wanaona wapo makanisani ila katika ulimwengu wa roho yanaitwa ni magereza ya kiroho, sasa ukiwa katika gereza la kiroho nikuulize swali je roho yako itapona? Jibu unalo ni mateso sana mpaka ule mwisho. Ila sasa uamue na uipende roho yako, ile siku ya unyakuo utabakia hapo kama usipotngeneza na utoke huko kiroho na kimwili ili pingu hizo zisikupate tena.
Wanaibuka watumishi wanabatiza ubatizo kwa kutumia majina yao na wenigne kubatiza ubatizo wa maji mengi lakini ubatizo unabatizwa katika kisima badala ya maji mengi ya mtoni, na wengine waumini wanawasujudia eti wao ndio MUNGU na wengine wanajiita wao ni YESU kabisa na hata majina, (nawaeleza muelewe ukweli hayo unayotenda siyo ya MUNGU wa kweli, na zaidi hata katika biblia (katiba) hayapo. Sasa utatafuta jibu usipate wanayatoa wapi? Sasa nakujulisha uelewe na ujitenge nao ili roho yako ipone, mafundisho hayo walioteshwa na shetani, na shetani akajifanya yeye ndie MUNGU, na kumbe yeye ni pepo mchafu na watumishi wanapoyatumia mafundisho hayo hiyo ndio njia ya kuwafunga watu pingu, na kamba, na kuwaweka katika gereza la shetani katika ulimwengu wa roho, ila hapa ulimwenguni watu wanajipa moyo wao ni wakristo na wataenda mbinguni. Leo funguka kama upo mahali pa jinsi hiyo uelewe umetekwa na shetani na upo katika gereza la kiroho unasubiri kuhumu pasipo wewe kujua.
Amenituma YESU WA NAZARETI niwafungue akili zenu na fahamu sababu shetani alizigandisha hata watu pamoja na kuwa na akili bado hawaoni hili ni mbaya na hili halipo katika biblia. Nitaelezea mfano halisi na uwaulize watumishi je imeandikwa wapi mtumishi uvae kofia ukihubiri? Jibu hana, soma 1 Wakorintho 11:3-7 utaona MUNGU amekataa mwanaume asivae kofia yaani mtumishi akihubiri ni marufuku, ila shetani akawaotesha ndoto wavae kofia na sasa wanavaa kofia (hii ni picha halisi ndani yake siyo YESU anayehubiri bali ni pepo shetani sababu kofia anayoivaa madhabahuni ukisoma biblia imekataa. Sasa utashangaa wanavaa na je kama wanavaa je huku si ndio kumsaliti YESU? Uelewe kama ulikuwa haujui, hivyo na msingi wa makanisa ya jinsi hiyo ambayo yamechanganya neno la MUNGU na uongo, sasa uelewe hayo walioteshwa na shetani wakayakubali na wameamua kufanya kazi ya shetani. Ila siku ya mwisho watalia wengi wakisema mimi niliongoza kanisa, YESU atasema sikujui sikujui, sehemu yako wewe ni katika ziwa la moto, hii sababu walikubali ndoto za shetani na wakayaacha ya MUNGU aliye hai (Ufunuo 22: 18-19).
Na zaidi maana ya hizo kofia yeye ni mkuu wa hilo gereza hivyo ataliongoza na kulilinda mpaka mwisho wake, na ndio sababu haukuti ni watumishi wote katika hilo kanisa ndio wanaovaa hizo kofia, kofia hizo ni maalum tu kwa kiongozi wa gereza na atapewa cheo tofauti na huduma zile tano, mfano Askofu, hii siyo huduma alioianzisha YESU ni huduma namba sita. Hivi swali je YESU yeye alikuwa hana akili aone kuwa cheo cha Askofu ndio liwe cheo kikubwa? Niwaulize haya yametoka wapi? Yametoka katika ndoto za shetani ili watu waingie katika mateso wamkufuru YESU kama ilivyo sasa, acheni, tubuni. Mtu akienda tofauti na biblia tayari njia yake ni Jehanamu. Sasa je kama watu wanaongozwa na watu wanaoenda jehanamu je watawapeleka watu mbinguni kweli? Jibu unalo. Akisema watakuja wakristo wengi nao watawateka hata wateule, sasa chunguza neno, na wengine wanapewa cheo cha uaskofu bila kujua kuwa Askofu hapaswi kusimamia kanisa, yeye ni mhudumu kanisani kama vile mfagiaji, mlinzi. Mimi kanisani kwangu ninao Maaskofu wengi na nimewaweka wakfu ni haki yao ndio wanakaribisha watu kanisani, kuangalia wakati ibada inaendelea. Hata ubishe soma biblia jibu hautaona huduma hiyo kama YESU alianzisha ili iongoze kanisa, haipo, hii ni huduma iliyoletwa kwa njia ya ndoto, na kila aliyeikubali kwa makusudi shetani akawaotesha waasisi wake wavae kofia kanisani, hili ni kosa na ni dhambi.
Amenituma YESU WA NAZARETI niwaeleze ukweli mfunguke ili mpone, ile siku ya mwisho hakutakuwa na kujitetea, mimi Hebron nimeufikisha ujumbe wa MUNGU kama ulivyo, kataa elimu dunia, hii ni elimu dunia ya mungu wa dunia hii (shetani).
TUBU:
BWANA YESU naomba unisamehe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima, najivua hii huduma ya sita siitaki, nakurejea wewe, uniongoze niponye roho yangu, amen.
Mataifa yote karibuni katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, karibuni katika ibada zote.
NABII HEBRON.