JE UNAJUA NI KWA NINI SHETANI AMEWATEKA WAKRISTO FAHAMU ZAO NA WAKABATIZA WATOTO WADOGO AU WACHANGA? SOMA…..

[ad_1]

Kila mtu anampenda MUNGU na watu waliosikia habari za YESU na kila anachokitaka kifuatwe ili uwe wakristo watu hupenda. Ila shetani amewateka watu akishirikiana na mpinga kristo, sababu anajua ubatizo ni point muhimu sana ya kufanya mtu awe kiungo kimoja na YESU wa kweli. Sasa ili avuruge kusudi hili alichokifanya akabadili ufunuo huu kama ninavyoelezea. Kwanza biblia inasema hivi Marko 16:16 “aaminiye na kubatizwa ataokoka na asiyeamini, atahukumiwa.” Huu ni mfano halisi sasa tuje katika swali? Je mtoto mdogo na mchanga je anaamini lolote au anajijua? Jibu haamini lolote. Je kama haamini je atakuwa ameokoka? Jibu hajaokoka! Je hayo maji ya kumwagiwa kichwani ndiyo kuzamishwa mwili wote? Jibu, siyo na kama siyo je hawa watoto wadogo wamebatizwa au hawajabatizwa mpaka sasa jibu hawajabatizwa mpaka sasa, na kama hawajabatizwa mpaka sasa basi siyo wakristo kabisa bali ni wakristo wa kujiita kimajina wala YESU hawajui, na kama ulikuwa haujui sasa elewa na ubatizwe upya sababu mpaka sasa wewe siyo mkristo na hata katika kanisa linalofanya haya kinyume na biblia, hayo siyo makanisa ya YESU ni makanisa ya yesu wa uongo na mpinga kristo yapo hapa ulimwenguni ili kuwazuia watu wasiwe mwili mmoja na YESU ili wawe wakristo, haijalishi hata mtu atajiita yeye ni pastor, mtume, mwinjilisti, mwalimu, nabii, kama hajabatizwa ubatizo wa maji mengi yeye siyo mkristo.
Na pia wakati akibatiza ni lazima aokoke (huko ndipo kuamini) na cha ajabu hata watu wazima wanabatizwa ubatizo wa kumwagiwa maji ya kikombe, tena hata sala ya toba hakuna, haya yote ni njia ya shetani. Na kazi zote za jinsi hii ya ubatizo nawaeleza MUNGU haujui, iwe ni maombi, injili, hata kujenga haya makanisa, siyo ya YESU WA NAZARETI ni mapango ya mpinga kristo, ni magereza ya kiroho. Hivyo kama ulibatizwa ubatizo huu na ukiwa mtoto mdogo, nakueleza ukweli, wewe haujabatizwa na pia wewe siyo mkristo haijalishi unajiita hivyo, fuata ukweli.
Amenituma YESU niwaeleze ukweli, karibu anarudi, na akija kama haujaokoka na kubatizwa ubatizo wa maji mengi yanayotembea na kuishi maisha matakatifu hautaenda mbinguni sababu wewe siyo mwili mmoja na yeye kiroho na kimwili, hizo injili zote unazozifuata ni za uongo, point kubwa okoka, uamini, ubatizwe kinyume na hapo utabakia kuwa mwanafunzi wa mpinga kristo sababu moja ya kimwili ipo wazi haina ubishi. Je biblia inaruhusu ubatizo wa watoto wadogo? Na je si mpaka uokoke umkiri kwanza YESU ndio tendo la ubatizo lifuatwe, je umeokoka? Haiwezekani kupata ubatizo kama haujaokoka! tazama wengi mmedanganywa haujaokoka halafu mnasema nyie ni wakristo, ipo neema yake. Tubu sasa hivi; sema YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniokoe na uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele niwe mwanafunzi wako na uniongoze nikabatizwe kwa ubatizo wa kweli ili niwe ninaoushirika na wewe na nipate kibali cha kuwa mkristo. Amen.

NABII HEBRON.

[ad_2]