JE UNAMJUA MUSA WA UONGO?

[ad_1]


Yamkini ni jambo jipya kwako ila mimi Nabii Hebron nakufunulia siri hii ujue kuwa yupo Musa wa uongo na makao yake yapo kuzimu, japo Musa wa kweli aliyewaongoza wana wa Israeli kutoka Misri na kuwatoa kwa Farao, huyu yupo mbinguni na yeye ni mmoja wa wazee 24 wanaomsujudu MUNGU mbinguni.
Nitaelezea kuhusu huyu Musa wa uongo, huyu yupo kuzimu na anacho kitengo chake alichopewa na shetani cha kuwarudisha watu Misri yaani kwa Farao na kuhakikisha watu hawaendi katika nchi ya ahadi, yaani mbinguni. Na kazi yake kubwa yeye alikuwa anawaongoza watumishi wanaotumia nguvu za giza ili kuharibu wanadamu waangamie, pia nataka uelewe ipo pia bahari ya Red Sea katika ulimwengu wa kiroho ambayo ni ya kuangamizia watu roho zao ili wasivuke kwenda nchi ya ahadi. Na anayeyafanya hayo ni Musa wa kuzimu, Musa huyu wa kuzimu kazi yake kubwa ni kuvunja sheria za MUNGU na kusambaza hiyo roho katika makanisa na kwa watumishi wavunje sheria za MUNGU na wawafundishe watu mafudisho ya kuzimu na kuyaingiza katika makanisa mbali mbali katika ulimwengu wote. Hivyo usishangae ndiyo maana kuna watumishi freemason, wachawi, wakujiita, kujifanya, wasaliti na watumishi wa mishahara.
Nitaeleza kwa kifupi japo watu mfunguke na mpone, ukisoma katika nyaraka za Musa wa kweli aliamriwa asiabudu sanamu na alizivunja alipokuta wana wa Israeli wamejenga Ndama, na hata sasa watumishi ndiyo Musa wa uongo, ukikuta mtumishi anayekwenda kinyume na Neno la MUNGU huyo ndiye Musa wa uongo anayewapeleka watu kwa Farao (shetani). Mfano wa Musa wa uongo- watumishi wanaobatiza ubatizo wa kikombe, kuabudu sanamu, kutoa huduma ya kiroho kwa pesa, kubatiza kwa majina yao. ZAIDI SOMA KITABU CHA JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI, NA MJUE KRISTO WA UONGO, nilivyoviandika mimi Nabii Hebron.
Watu wengi all over the world 98% wanaongozwa na Musa wa uongo ambao ndiyo watumishi waliomsaliti YESU, wanatumia jina lake ila ndani yao ni MBWA MWITU. Jichunguze, je wewe mtumishi anayekuongoza ameitwa na MUNGU kama alivyoitwa Musa wa kweli? Utamjuaje, mtazame mafundisho, matendo yake, na je amebadilisha Neno la MUNGU? Akiwa ameitwa na MUNGU kama Musa alivyoitwa hataweza kuzivunja Torati maana anamjua yeye aliyemuita. Na akienda kinyume ujue ndani yake ipo roho ya Musa wa kuzimu ya kuwarudisha watu kwa Farao badala ya kuwapeleka katika nchi ya ahadi ambayo ndiyo mbinguni.

NABII HEBRON.

[ad_2]