JINSI SHETANI ALIVYOWATEKA VIJANA WA DUNIA HII. JIBU JINSI YA KUPONA, SOMA HAPA.

[ad_1]

Ndugu msomaji, ninakusalimu katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI ambaye ni mwokozi wa maisha yangu na ulimwengu wote. Mimi naitwa Nancy Hebron na kwa neema yake amenichagua kueneza injili yake kupitia Huduma yake; HUDUMA YA YESU NI BWANA na MWOKOZI WA MATAIFA YOTE INTERNATIONAL MINISTRYchini ya uongozi wa Mtume na Nabii Hebron.

YESU aliponiita kufanya kazi yake, sikuamini, niliona ni utani. Nilijiangalia jinsi nilivyo; mchafu, muovu, nimejaa dhambi na Je? YESU angetaka kunitumia mimi kwa kusudi gani, kwa sababu gani, nani angenisikiliza mimi hata ningemhubiria kuhusu YESU?! Na kwa nini mimi na sio mwingine? Nilijiuliza maswali mengi sana. Lakini kama neno lake kwenye Isaya 55:8 inavyosema “Mawazo yetu sio mawazo yake na njia zetu sio njia zake.”
YESU alinijua jinsi nilivyo na akaniambia nisiogope kwa kuwa yeye ndiye alinichagua na angenibadilisha na kunitumia kuwa mfano kwa vijana na wanawake dunia nzima. Aliniambia nisiangalie umri wangu kwa kuwa angenitumia kama vile alivyomtumia Yeremia.

Mwanzo ilikuwa ngumu sana kukubali kile alichoniambia kwa kuwa nilijidharau na kuona isingewezekana, na hapo ndipo nilikosea kwa kuwa kazi yake haifanyiki kwa nguvu zetu bali kwa nguvu zake ndani yetu. Na madhara ya kujidharau kwangu ilichukua muda kufanya maamuzi. Nilijiambia nitaomba nimalizane na dunia ndipo nimtumikie. 

Ndugu msomaji, usidanganyike, hakuna kitu kama kumalizana na dunia, muda na wakati ni sasa, YESU anarudi na Je? Atakukuta wapi? Duniani au Ulimwenguni?
Basi, alishaniita mtumishi wake lakini bado nilikua mbishi. Nilitaka kuishi kote kote. Niwe kwa YESU na pia duniani. Huo ulikuwa ni upumbavu, na wale ambao hawamjui au hawamkubali YESU ndio wanaisha katika upumbavu na mimi nilikuwa bado nimejaa upumbavu. Nikawa nasua sua kwa muda, nilikuwa vuguvugu. Niliishi maisha mawili tofauti kwa kuwa ujana wangu na matamanio yangu yalikuwa yananipumbaza sana. 

Ndipo siku moja nikafungua neno la Ufunuo 3: 15-16
“Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi au moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto nitakutapika utoke katika kinywa changu.”
Niliogopa sana, na ndipo ubishi wote uliisha, japo nilikuwa na kasoro zangu nilikuwa na hofu ya MUNGU na sikutaka kumkosea.

Japo ilikuwa ngumu YESU alinisaidia kufanya maamuzi, kuacha dunia na mambo yake na kuishi ulimwenguni kwa  YESU. YESU KRISTO WA NAZARETI ni mweza yote, na ukijiachia kwake yote yanawezekana, hata kutoka duniani. Na kupitia makala hii ninapenda kusema zaidi na vijana, ili wajue kuwa dunia haina lolote, kwa YESU ndio mambo yote, na ninamwomba MUNGU ukimaliza kusoma makala hii utafanya maamuzi kuja kwa YESU full.

DUNIA NI NINI, NA ULIMWENGU NI NINI?
Dunia na Ulimwengu zipo mahali pamoja lakini ni vitu viwili tofauti au ni sehemu moja lakini ni tofauti, Kivipi basi?

Dunia ni pahali ambapo shetani anatawala na yeye ndiye kiongozi, na wale ambao hawajamkubali YESU ndio wako chini yake, na yeye ndiye mungu wao, haijalishi kama wewe ni mkristo, kama haujaokoka shetani ndio kiongozi wako, na dunia ni muunganiko moja kwa moja na kuzimu.
Unaweza kujiuliza inakuaje shetani ndio kiongozi wa dunia na MUNGU aliumba vyote. MUNGU aliumba ulimwengu na sio dunia. Wale ambao wameokoka na kumwamini YESU, wanafwata na kuishi katika sheria na amri zake ndiyo wanaishi ulimwenguni.

JINSI SHETANI AMEWADANGANYA VIJANA NA KUWASHIKILIA DUNIANI?

2 YOHANA 1:7
“Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa YESU KRISTO yuaja katika mwili. Huyo ndiye Yule mdanganyifu na mpinga KRISTO.”

Mdanganyifu ni nani basi?
Mdanganyifu ni mzinzi, mlevi, mvuta sigara na bangi, muongo, msengenyaji, mwenye tamaa, muaji, mwabudu sanamu, mwizi, anapenda pesa na vyeo, mshirikina, wasio na heshima, wana kiburi na kujua na mmenginevyo, kwa kifupi wadanganyifu ni wale wenye tabia za shetani.

Dunia ni mahali pa giza, mahali ambapo vijana wengi wanakaa kwa kuwa wanaogopa kuitwa washamba. Shetani amewaekea ugumu kwenye mioyo yao ili waone kuwa wokovu ni ushamba na wazee tu ndiyo wanaokokaga. Siwalaumu vijana kwa kuwa hata mimi kabla ya kumjua YESU nilikuwa na waza hivyo.

Kwa nini lakini? ni kwa sababu makanisa yapo duniani na sio ulimwenguni. Na makanisa hayo yanagandamiza na kudanganya wana wa MUNGU, kuwanyag’anya mali zao na pesa zao, na kuwaacha na nuksi, balaa na mikosi. Nilikuwa nikimwangalia mwana wa MUNGU nilikuwa sioni udhihirisho wa YESU ndani yake au mabadiliko. Mtu aliyeokoka ndiyo alikuwa amechakaa, hajipendi tena na ukimwangalia unawaza tu kuwa nikiokoka nitafanana kama huyu na nitakuwa maskini, na ndicho kinachowakimbiza vijana wasije kwa YESU. Lakini haya yote ni kwa sababu kanisa lipo duniani kwa shetani na siyo ulimwenguni kwa YESU.

Njia nyingine shetani amehakikisha anavijana wengi duniani ni kupitia nyumba za starehe; disko, casino. Disko na casino ni muunganiko moja kwa moja na kuzimu. Ukiwa kwenye hizo nyumba unashiriki kila kitu na shetani na watoto wake, na malaika zake (majini na mapepo). Na kila ukiwa humo, majini na mapepo yanakuvaa na wewe unakuwa na tabia kama zao, uovu, uchafu na mara nyingi unajikuta unafanya mambo ya uchafu hata kama haupendi kwa kuwa wameshakuvaa na wanakuendesha jinsi wanavyotaka. Kwa hivyo unazidi kuwa mlevi, mzinzi, mvuta sigara na bangi hata kuwa mshiriki wa madawa ya kulevya. Shetani anakugaragaza kwa kuwa wewe ni wa kwake na anauhalali na wewe. 

Ukisikiliza miziki wanaopiga disko, kupitia hizo nyimbo shetani anakamata ufahamu wako na kukuendesha jinsi anavyotaka, akisema lolote au akitaka ufanye lolote utafanya kwa kuwa yeye ndiye kiongozi wako na hauna nguvu ya kukataa.

Kwenye casino, jinsi shetani anahakikisha amekukamata. Unapeleka pesa zako, na ukishaanza kucheza michezo yao, uthamani wa pesa zako zinapelekwa kuzimu na kupitia hizo pesa shetani anakumiliki na kukuwekea jini chuma ulete. Unajikuta kila wakati unataka kurudi huko hata kama unamaliza pesa zako zote huko, bado unarudi tu, hata ukiishiwa unakopa, ili tu urudi kucheza kamari. Na jinsi unavyo zidi kurudi na shetani anazidi kukushikilia.

Njia nyingine ni kupitia mavazi ya Yezebeli na mapambo yake pia, shetani amehakikisha anawaunganisha vijana na kuzimu na kuwashikilia duniani.
Dunia imejaa mashindano, majivuno. Ni mahali ambapo vijana wengi hawapo, wanatembea na kuishi lakini nafsi zao zimeshikiliwa na kutumikishwa na shetani na ni mpaka neema ya MUNGU iwafikie na kuwatoa huko.

JINSI YA KUTOKA DUNIANI NA KUISHI ULIMWENGUNI?

WAFILIPI 4:13
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”
Ndugu msomaji, kwanza ni vyema kujua hatuwezi jambo lolote bila uweza kutoka kwa MUNGU. Kwake kuna vyote, kuna amani, furaha, kicheko, baraka, uponyaji, ufufuo na WOKOVU.

Ndugu msomaji, wokovu ni kwa neema yake, na ukisha mkiri YESU  kama mwokozi na mchungaji wako, mwachie maisha yako na moyo wako na yeye ndiye atakubadilisha. Maisha ya utakatifu sio kitu cha siku moja bali siku hadi siku YESU ndiye anakutengeneza na kukuimarisha kwa ajili ya utukufu wake. Anachukua kisichofaa na kukitengeneza kwa ajili ya utukufu wake.

Basi, kutoka duniani ni kwa njia ya kumkiri YESU, kuamini anaweza yote na kutii sheria na amri zake. Kuishi maisha matakatifu. Kuabudu kanisa ambalo lipo ulimwenguni na sio duniani; kanisa ambapo yeye yupo na wanafwata yale anayotaka yeye. Mahali ambapo wanabatiza ubatizo wa Yohana, mahali ambapo wanamwabudu yeye tu na siyo masanamu, mahali ambapo hawanyang’anyi pesa au mali zako, mahali ambapo hawana sadaka zaidi ya fungu la kumi na sadaka ya shukurani, mahali ambapo hawafanyi harambee, mahali ambapo kuna neno ambaye ni MUNGU, na hilo neno likijaa ndani yako linakubadilisha siku hadi siku. Mahali ambapo kuna nuru na udhihirisho wa YESU KRISTO WA NAZARETI.

YESU ANAWAPENDA VIJANA

1 YOHANA 2: 14
“……. Nimewaandikia ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la MUNGU linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda Yule mwovu.”

YESU anawapenda vijana na anajua kuwa wakiamua kuja kwake wanaamua kabisa, na ndiyo maana shetani na yeye anafanya juhudi zote kuwapoteza ili wasimjue YESU.
Kumpenda YESU sio ushamba, bali ni ukombozi. Na heri uitwe mshamba wa YESU na kuurithi ufalme wake, kuliko kumkataa na kuchomwa jehanamu.

Kama YESU anajua kuwa unauwezo wa kumshinda shetani, wewe ni nani kutokuamini unaweza kumshinda shetani?

YESU anakuita leo, anakupenda na anataka uwe mtoto wake kwa kumkiri yeye kama mwokozi wa maisha yako. Kama uko tayari, sema maneno haya;

“BWANA YESU NIKO MBELE ZAKO, MIMI NI MWENYE DHAMBI. NINAOMBA REHEMA KWA KUWA NIMEENDA KINYUME NA MAPENZI YAKO SIKU NYINGI. LEO NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE NA MAMBO YAKE YOTE. NINAOMBA UNITOE DUNIANI ILI NIWEZE KUISHI ULIMWENGUNI. NINAKUKARIBISHA MAISHANI MWANGU NA MOYONI MWANGU. ANDIKA JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA, NA UKIRUDI NIWEZE KUONDOKA NA WEWE NA KUURIITHI UFALME WAKO. AMEN

Kuokoka kwako ni agano kati yako na MUNGU wako, siyo lazima watu wengine wajue. YESU atakubadilisha kwa muda na wakati unayompendeza yeye na watu watauona wokovu wake kupitia matendo yako. Dunia haina starehe kama ulimwenguni kwa MUNGU BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU, na siku ya leo umefanya maamuzi sahihi ya kumkiri YESU. Usiogope mwana wa MUNGU, yeye sasa ni mchungaji wako na hautapungukiwa na kitu.

MUNGU WA IBRAHIM, ISAKA NA YAKOBO AKUBARIKI NA AKUHIFADHI.

MWALIMU NANCY HEBRON KISAMO.


[ad_2]