JINSI TANZANIA MPYA ITAKAVYOKUWA MUDA WOWOTE KUANZIA APRIL 2012 UNABII WA NABII HEBRON!

[ad_1]

Nawasalimu kwa jina la mwenyezi MUNGU, MUNGU aliyeumba mbingu na ulimwengu na ndiye MUNGU aliumba watu kwa mfano wake, MUNGU asiye na dini, MUNGU wa watu wote. Napenda kuwajulisha kuwa nchi hii ya Tanzania imechaguliwa na MUNGU na ndio Edeni ya sasa, na nchi hii ameipenda yeye kwa makusudi yake kwa ajili ya kuandaa kanisa lake la mwisho ambalo linaloongozwa na mwana wa pekee YESU WA NAZARETI. Aliponiita nimtumikie, aliniambia hayo japo yapo mengi bado hajaniruhusu niyaseme, ila nitaelezea kwa ufupi katika baadhi ya maeneo tofauti.
Jambo la kwanza uchawi au viongozi watakaotumia uchawi hawatakaa katika madaraka ya kuongoza nchi hii, hii ni sababu sasa hivi ipo katika mkono wake nay eye hashirikiani na uchawi, na pia nchi hii ndiyo iliyochaguliwa ili mataifa yote waje wamjue YESU WA NAZARETI wa kweli na watu wafunguliwe fahamu zao wamjue YESU wa kweli na ni yeye MUNGU peke yake atawaleta na kuwaongoza ili waje wafunguliwe, sababu YESU WA NAZARETI amesalitiwa na watumishi 98% wote katika ulimwengu wote wauache njia ya MUNGU. Wengine ni wachawi, wengine wamejiita, wengine ni watumishi wa mishahara, wanabakia kuwadanganya watu, hao wanampenda YESU kwa kinywa bali ndani ya mioyo yao ni unafikii umejaa. Maneno hayo siyo yangu mimi Hebron, ni maneno ambaye aliniambia YESU WA NAZARETI  au jina lingine anaitwa Nabii Issa, mimi mwenyewe nilikuwa siyajui hayo aliponiambia peke yake.
Na zaidi 2012 alinipeleka mbinguni akanionyesha ulimwengu wote ulivyoharibika, ila nitaelezea kwa upande wa Tanzania, aliponionyesha niliogopa sana, sikuona sura yeyote ya mtumishi wa MUNGU zaidi ya marehemu Moses Kulola peke yake. Akaniambia katika Tanzania kwa upande wa watumishi wenye majina makubwa au kujulikana, akaniambia amebakia yeye peke yake hao wengine mimi sipo nao, na baadhi yao sijawaita hata siwajui bali wanawadanganya watu nimewaita na walifikaga mbinguni. Akanionyesha sura zao ila nitataja kazi zao tu kwa leo. Waliokuwa na benki, akaniambia huyo anajiita Nabii wangu, mimi hata simjui huyo ni mchawi, anawadanganya watanzania na wanaangamia. Akaniambia nenda ukaseme kweli yangu kama nilivyo na nitakavyo kuwa nakutuma, na usiogope mtu yeyote wala chochote, mimi nitakuwa na wewe siku zote, atakaye shindana na wewe anashindana na mimi MUNGU, je? Mwanadamu ataniweza? Akasema kwa sauti ya uchungu nenda uniandalie kanisa langu, watoto wangu wanateseka, wanapotezwa, na kupitia wewe mataifa yote nitawaongoza na kuwaleta kwako uwaongoze njia ya kweli.
Akaniambia kanisa linaloitwa kwa jina langu imebakia only 2% katika ulimwengu wote, hiyo ni 98% ni shetani ndie katawala na kuyamiliki pamoja na watu. Niliwatuma watumishi wachache na hao wamenisaliti wamegeukia upande wa adui. Ila sasa nitalikomboa kanisa langu na watoto wangu. Akaniambia nchi hii ni yangu na ni mali yangu mimi MUNGU, nitaibadilisha na itakuwa ndio taifa langu teule kwa ajili ya ukombozi wa mataifa yote, akaniambia mimi MUNGU ndiye nitakayefanya hayo kwa wakati wangu na tayari imeshaanza mengine kuyafanya, nitawatumia watu hao hao na nitawaongoza na viongozi watafanya vizuri, ila wale watu wenye nia mbaya na nchi hii atawatoa katika uongozi na hawatakaa katika serikali hii, yeye YESU atafanya ajuavyo yeye kuhusu uchawi.
Nimeelezea mara nyingi katika makala, Television na redio mbali mbali hata kabla hayajatokea na sasa yameshatokea mfano nilieleza kuhusu kuinuliwa mbuga ya Serengeti, mlima Kilimanjaro, kuinuliwa viwanja vya ndege Tanzania, gesi, mawaziri kutolewa kazini, ndege kutua kwa wingi katika nhi ya Tanzania na madini kurejeshwa kwa watanzania, mikataba mibovu kufutiwa na misamaha ya kodi itafutwa yote. Hayo ni baadhi ila yapo mengi zaidi soma makala ya Nabii Hebron kuhusu Tanzania.
·        Kuhusu mikataba ya madini bado tena hata hizo share za 50% katika serikali na wawekezaji wa nje, itafika wakati itafutwa na nchi kumiliki 100%.
·        Mikataba mibovu itafutwa yote, hata walogeje, this is the last time, YESU anaitengeneza nchi na ni yeye ndie atakaye yafichua yote ya uozo yaliyofanywa na watu kwa ajili ya ufisadi na kuwanyonya watanzania
·        Rais bora atatokea katika nchi ya Tanzania (atakuwa bora kuliko wote katika ulimwengu wote) ni MUNGU aliyeishikilia nchi atafanya hayo.
·        Tanzania itakuwa ndiyo headquarter ya airport katika bara la Afrika.
·        Nchi ya Tanzania jeshi lake limenyanyuliwa sana litatengeneza silaha ambao haijawahi tegenezwa ulimwengu wote. Na nchi hii haitakaa ivamiwe kivita na nchi yeyote (ni peke yake ipo mkononi wa MUNGU).
·        Tanzania ndiyo taifa tajiri kuliko nchi zote ulimwenguni, hayo yatatokea muda mchache ujao.
NOTE:
Na haya yote atafanya peke yake MUNGU ajuavyo yeye aliyeumba nchi hii, hakuna uchawi utakaofanya kazi tena, iwe katika viongozi wa siasa, na viongozi wowote wa serikali. Na pesa zilizoibiwa na nyingine kuwekwa nje ya Tanzania zitarejeshwa zote, myaonapo hayo msishangae. Ni YESU WA NAZARETI anayafanya hayo wala hasaidiwi na mtu yeyote (Nabii Issa). Na itafika muda  siyo mrefu iwe ni Rais, mawaziri, wabunge, madiwani watakaotumia uchawi ili wapate hivyo vyeo wataanguka (hawatapata) kama mnafikiri natania haya ng’ang’anieni hayo wale wanaopenda ushirikina majibu mtayaona (negative-).
Nimeyasema machche yale ambayo nimepata ruhusa kutoka katika serikali ya mbinguni. Mengine mimi sijaruhusiwa kuyasema. Watumishi ambao wanatumia nguvu za giza watakufa vifo vya aibu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA UZIDI KUINUA KUANZIA VIONGOZI, UCHUMI, BUNGE.

NABII HEBRON.

[ad_2]