KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE

KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE

[ad_1]

HUYU NDIYE ALIYEMZAA MTUME NA NABII HEBRON KIROHO – MOSES KULOLA.

PROPHET HEBRON ALONGSIDE HIS DAUGHTER REBECCA AND WIFE NANCY.

Ndugu msomaji wa blogu hii, nakusalimu katika jina la BWANA YESU, ambaye ndiye BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Katika blogu hii, tutakuwa tunatoa habari za mafundisho ya YESU kama alivyokuwa akifanya ulimwenguni. Kwa sasa, kanisa limetekwa na shetani 98% ulimwenguni mwote, na macho ya rohoni ya kanisa yamekufa kabisa, na ROHO MTAKATIFU hayupo katika kanisa, ndio maana kondoo hawapati tena malisho, wametawanyika, na wanateseka.

Mafundisho mengi yanapatikana katika vitabu, cd’s na dvd’s kama zinavyoonekana pichani, na pia katika tovuti ya Nabii Hebron www.prophethebron.org.  Pia, vipindi vya redio, Sunrise Radio 94.8FM kila Alhamisi saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku, na Radio 5 kila Alhamisi saa tatu kamili usiku hadi saa nne kamili usiku, kupata frequency kamili ya Radio 5 ingia katika website www.prophethebron.org.
Moses Kulola (Katikati), akiwa na Mtume na Nabii Hebron (kulia), mke wa Nabii Hebron (kushoto)

SHUHUDA NA MATUKIO YA WIKI HII – 25 November 2012

Shuhuda

Kijana huyu alikuwa na tatizo sugu la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka kumi na nne (14), aliombewa hapa katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, na leo tarehe 25 November 2012,  ameshuhudia kanisani katika ibada ya jumapili (siku ya BWANA) amepona kama anavyoonekana kwenye picha.
MATUKIO

Mtume na Nabii Hebron akisisitiza jambo wakati wa mahubiri katika ibada ya leo akifundisha tofauti kati ya nabii wa MUNGU Eliya (1WAFALME 18:21-40) na manabii wa Baali (wa uongo), jinsi nabii Eliya alivyojenga madhabahu ya MUNGU iliyovunjika, na akamuomba MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo ashushe moto kutoka mbinguni uteketeze dhabihu aliyomtengenezea MUNGU wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, ili kumdhihirisha MUNGU wa kweli ambaye yeye Eliya alimwabudu na kumtumikia baada ya manabii wa Baali kushindwa kushusha moto toka kwa mungu wao waliyemtumainia na kumtumikia. Na uwepo wa MUNGU ulidhihirishwa “live live” pale moto wa ELiya uliposhuka kanisani, watu wakapata uponyaji, waliokuwa na vifungo walifunguliwa kwa nguvu ya huo moto, na wenye mapepo yakawatoka. MUNGU wa Eliya akadhihirika pia kwetu siku ya leo. Hakika jina la BWANA lihimidiwe milele, Amen.
Mama huyu amefunguliwa kifungo alichokuwa akitumikishwa na nabii Baali, baada ya kumjua MUNGU wa kweli ambaye nabii Eliya alimwabudu na kumtumikia.  Na leo kupitia Mtume na nabii Hebron ambaye moto wa Eliya ulikuwa ndani yake kuwaponya na kuwafungua watu katika vifungo vyao, walivyotumikishwa na manabii wa Baali, hata mama huyu aliponywa. Wengi wameponywa na kufunguliwa.
Mtume na Nabii Hebron alifafanua NENO na kusema kuwa, kwa wakati huu watumishi wote waliokwenda kinyume na maagizo ya MUNGU ni manabii wa mungu Baali, mungu mfu. Nabii Hebron akaendelea kwa kusema, mungu Baali haoni, hazungumzi, hasikii, wala hana mikono inayosogea, ndiyo maana makanisani hakuna majibu.

Siku hizi, waumini makanisani wamezungukwa na kujawa na mateso, shida na kila taabu. Yote hayo yanatoka kwa mungu Baali. Pia nabii aliongeza kwa kusema “MUNGU ameniambia, katika bara lote la Afrika, tofauti na watoto wadogo, watu wazima wanaofariki dunia kila siku, kumi na tano tu (15) ndio wanaenda MBINGUNI.”
Ndugu msomaji wa blogu hii jiulize, unaishi kwa miaka themanini (80) ulimwenguni, halafu mwisho wako unaingia jehanam kwa lusifa. Haya makanisa na hizi dini zimekusaidiaje ili kuitengeneza njia yako ya kumwona MUNGU siku yako ikifika?

 Kwa mawasiliano;

+ 255 759 610 820

+ 255 759 253 593


+ 255 763 567 402


+ 255 764 042 149 


+ 255 765 955 677

[ad_2]