KUFUFUA MISIKULE NI MAZINGAUMBWE 100% NA NI KIINI MACHO

[ad_1]

Ndugu msomaji wa makala ya nabii Hebron, leo napenda kukufundisha na kumuabisha shetani na watumishi wake wanaotumia nguvu za giza wakidai ni YESU ndiye anaye fufua hiyo misukule. Soma katika kitabu cha Yohana 11:40 -44, YESU akamwambia mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa MUNGU? Basi wakaliondoa lile jiwe . YESU akainua macho yake juu akasema , Baba nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa unanisikia siku zote, lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kuwa ndiwe uliyenituma. 

Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro njoo huku nje. Akatoka nje yule aliye kufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake umefungwa leso . Naye YESU akawaambia mfungueni, mkamwache aende zake. Huu ni mfano halisi ambao YESU alimfufua Lazaro. Katika ufufuo wa kweli ambao YESU anautumia katika kufufua, jambo la kwanza yule aliyekufa ambaye ndiye maiti lazima kila mtu amuone kwa macho yake, na hii inadhibitisha ya kuwa ni kweli na kitakachotokea kila mtu alikiona kabla ya ufufuo. Yaani macho kwa macho na siyo kiini macho. 

Nitazungumzia kuhusu hizi ibada za kufufua misukule tena watumishi hao hulitumia jina la yesu wa uongo ili kuwapoteza watu na kuwaibia vitu vyao. Hiyo siyo ufufuo wa YESU. Hizo ni kiini macho, watu mnafungwa macho na hao mnaoambiwa ni misukule wamefufuliwa na hata mara nyingine mtaelezwa wameanguka kutoka angani huo ni uongo hakuna kitu. 

Tazama YESU kila aliyemfufua kila mtu alimuona kwa macho yake ya nyama na damu. Je hii misukule wewe uliiyona kabla haijafufuliwa? Jibu ni hapana hamjaiona, je YESU alifufua maiti ambayo watu hawakuiona kwa macho yao? Jibu ni hapana, zidi kuelewa uwajue hawa manabii wa uongo waliotabiriwa na YESU mwenyewe katika Biblia . Nitaeleza kuhusu mazingaumbwe au kiini macho. 

Hapa Tanzania miaka ya nyuma ya 1980 kulikuwa na mwana mazingaumbwe aliye jiita jina la “PAMA BULA” , na wengineo ambao kwa sasa hii huduma ya mazingaumbwe imepotea siku hizi hata mashuleni hazipo tena, je umeshajiuliza mazingaumbwe yameishia wapi siku hizi hayapo tena hata mashuleni katika shule za misingi? Jibu hayo mazingaumbwe siku hizi yameibiwa na watumishi Wanaotumia nguvu za giza kupitia katika makanisa na hata mikutano ya injili ya kipepo ambayo YESU wa Nazareti hayupo. Mazingaumbwe ni kupofushwa macho msione kile anachotaka kukifanya na baadaye kinatokea, mfano hiyo siyo misukule ni watu ambao tayari ameshawaandaa na anakuwa nao hapo ila anawapofusha macho na akitaka kuwaonyesha anawafungua macho yenu na nyie mnashangaa eti kweli. 

Nitatoa mfano kwa wale waliobahatika kuona mazingaumbwe, utashangaa mfano unaambiwa angalia kwenye boksi kuna karatasi tuu, zile atazibadilisha ziwe biscut, ndugu msomaji hizo ni kiini macho akitaka mzione anawarudishia macho yenu mnashangaa mnaziona biscuit . na mwengine anaweza akawaonyesha watu ndani ya kikapu mkaona hakuna kitu ila badaye akasema ataita nyoka na mtaiona ndani ya kikapu. Hapa anachokifanya mnapigwa upofu, nyoka anakuwa naye pale pale kwenye kikapu, utashangaa kuiita uongo na baadaye nyoka anaonekana. Huo ni upofu ( KIINI MACHO ) Jambo lingine ili ujue kama jamaa ni waongo na ni watoto wa shetani ambaye ndiye mfanya mazingaumbwe ( yaani kiini macho). 

Kama huyo mtumishi ni wa YESU wa kweli kwa nini asingeenda mochuari kuwafufua wale maiti kama YESU alivyo fufua? Au kwa nini asiende makaburini akiwa na makutano yani watu waone macho kwa macho makaburini watu wakifufuliwa na makaburi kupasuka na wale waliokufaga wafufuke kama Lazaro na wafunguliwe sanda zao wawe huru wakaishi tena ? Wangefanya kama alivyofanya YESU wa Nazareti hapo ndipo muamini lakini kinyume na hivyo ni mazingaumbwe, na kama ni mazingaumbwe je hufikiria hawa watumishi ni salama kwa ajili ya roho za wana wa MUNGU? Jibu siyo salama, na hata hao wanaoongozwa nao wajijue tayari wametekwa na shetani, YESU wa Nazareti alisema msiziamini kila roho bali zichunguzeni kama zinatokana na mimi, usidanganyike tena. 

Natumaini umeelewa hawa ni wachawi. Jiulize kwa nini wasiende mochuwari kufufua? Au kwenye misiba? Jibu hawawezi maana ufufuo wa YESU lazima muone aliyekufa na siyo kiini macho. Ila ufufuo wowote wa misukule siyo ufufuo hayo ni mazingaumbwe. Hata kutolewa vitu kwenye mwili mfano mawe, chuma, ndulele na watumishi , hayo yote ni mazingaumbwe tupu. 

NOTE: 
1. Na wengine watumishi hutafuta hata jeneza na kuweka mtu aonekane amekufa au hata anaweza huonekana katika familia mtu amekufa na kumbe hajafa, wanachofanya yule mtu mnapigwa upofu mnaona amekufa kabisa, halafu huyo mtumishi anakuwa ameshajipanga maana ni yeye ndiye ameandaa hayo mazingaumbwe, mtashangaa ameletwa kanisani , akifika pale anawafungua macho yenu nyie mnaona mtu amefufuka kumbe mazingaumbwe. 

2. Ili uamini anayefufua watu aende mochuwari akafufue watu, au wale wanaokwenda kuzikwa aende kimwili kufufua. Si anasema anafufua watu kwa jina la YESU? Nakuambia hawasubutu maana ni wanamazingaumbwe hao. Usidanganyike ewe mwana wa MUNGU. 3. Madhara ya kushiriki au kuabudu kwa kanisa linalofanya mazingaumbwe, mfano kufufua misukule, kubadili maji kuwa mafuta ya taa na mengineyo, hata Apple kulibadilisha kuwa embe au chungwa wote hamtaenda mbinguni, pili mnaibiwa nyota zenu na Baraka za maisha yenu. Maana adui kazi yake ni kuharibu tu. Na nyie mkifikiria munamfuata YESU au kumpokea YESU, kumbe mnampokea Ibilisi (Mazingaumbwe ni miujiza ya shetani.) Na hao wanayoyafanya hayo siyo watumishi wa YESU wa kweli ni WAONGO. 

NABII HEBRON

[ad_2]