MAELEZO YA YOUTUBE: AGENT WA KUZIMU AKAMATWA

MAELEZO YA YOUTUBE: AGENT WA KUZIMU AKAMATWA

[ad_1]



Nabii Hebron: Kaaa.
Nabii Hebron: Hii inatoka kuzimu kabisa hii
Nabii Hebron: Tena ametumwa kumuua Hebron
Nabii Hebron: Kaeni chini msiogope
Nabii Hebron: Umefuata nini hapa?
Agent wa kuzimu: Tumekuja
Nabii Hebron: Mmekuja kufanya nini
Agent wa kuzimu: Tumemfuata Hebron
Nabii Hebron: Mmemfuata nani?
Agent wa kuzimu: Hebron
Nabii Hebron: Hebron mnataka mumpeleke wapi?
Agent wa kuzimu: Tumeleta bomu.
Nabii Hebron: Bomu iko wapi?
Agent wa kuzimu: Ya kuchoma hii kanisa
Nabii Hebron: Hyo bomu iko wapi?
Agent wa kuzimu: Kuna mganga mmoja anayo huko nje.
Nabii Hebron: Huyo mganga yuko wapi?
Agent wa kuzimu: Yuko kule nje.
Nabii Hebron: Haya twende ukamkamate.
Nabii Hebron: Wewe mganga kuja hapa.
Nabii Hebron: Mnaogopa nini?
Agent wa kuzimu: (Anawika kama kuku)
Nabii Hebron: Waite wenzako wote
Nabii Hebron: Mbona mnaogopa!
Nabii Hebron: Mbona mnaogopa?
Waumini: Hatuogopiii…
Nabii Hebron: Weeee
Agent wa kuzimu: Niache
Agent wa kuzimu: Nikubomoe?
Agent wa kuzimu: Nikubomoe?
Agent wa kuzimu: Unanifahamu?
Agent wa kuzimu: Eeh, unanifahamu?
Nabii Hebron: Lete annointing oil
Nabii Hebron: Na wanaowatuma ni watumishi sasa, na lusifa
Nabii Hebron: Kunywa hiyo. Huyu ndio Hebron mwenyewe sasa
Agent wa kuzimu: eeee!
Nabii Hebron: Nakuvunja.
Agent wa kuzimu: Eeeeeh (Anapiga makelele ya kuita msaada)
Nabii Hebron: Na wewe nimekuambia hivi, usiogope sijui kuchoma, hapa hailipuliwi kitu.
Nabii Hebron: MUNGU anawaruhusu wapigwe upofu waje ili niwakung’ute.
Agent wa kuzimu: Aahhhhhhhhhhhhhh
Nabii Hebron: Hivi MUNGU anachezewa? Amejaa kwenye moyo wangu,hata dunia nzima hawaniwezi. Hata kinyamkera cha aina gani hakiwezi. Wewe unaogopa nini bwana?
Agent wa kuzimu: Niache..
Nabii Hebron: Hebu niwekeeni vizuri..
Agent wa kuzimu: Nitakumaliza..
Nabii Hebron: Njoooo sasa…
Agent wa kuzimu: Nitakumaliza…
Nabii Hebron: Utammaliza nani?
Agent wa kuzimu: Nitakumaliza
Nabii Hebron: Nimalize sasa…
Agent wa kuzimu: Nisamehe.
Nabii Hebron: Nikusamehe nini?
Agent wa kuzimu: Nisamehe basi..
Nabii Hebron: Nikusamehe nini?
Agent wa kuzimu: Sirudii tena.
Agent wa kuzimu: Si hii kijana inajiita Hebron
Nabii Hebron: Nani kakutuma? sema.
Nabii Hebron: Nafutagano la kusema siri zote, sema…. Sema.
Agent wa kuzimu: Tusamehe.
Nabii Hebron: Nikusamehe nini?
Nabii Hebron: Wamekutuma ufanye nini? sema.
Nabii Hebron: Wamekutuma ufanye nini?
Agent wa kuzimu: Tunaliswha.
Nabii Hebron: Upanga nilio nao nakata kichwa.
Waumini: Kwa jina la YESU….
Agent wa kuzimu: Aaaaahhhhhh.. Nisameheee..
Nabii Hebron: Mnaogopa nini? Kaeni kwenye viti baba yenu nipo fit bwana
Waumini: Ameeen
Agent wa kuzimu: Huyo mganga anataka aondoke
Nabii Hebron: Asiondoke. Mikaeli shika hapohapo. Hata angekuwa kaskazini anga la tatu si wanaletwa?
Waumini: Ameeen
Nabii Hebron: Na ninakuambia leo ndio unaingia kaburini wewe.
Waumini: Ameeen
Nabii Hebron: Hautaishi tena.
Waumini: Ameeen.
Agent wa kuzimu: Nisamehe
Nabii Hebron: Enhe, umetumwa ukafanye nini na kuzimu. Sema hapa
Nabii Hebron: Sema haraka
Nabii Hebron: Moja, mbili, tatu, ninakuvunja kichwa chako..
Nabii Hebron: Vua mavazi yote
Nabii Hebron: Huyu yani ametoka kwa yule anaitwa shetani kabisa. Kisa kumfuata Hebron anasema ukwe….
Waumini: ukweliiiii.
Nabii Hebron: Kanisa la wajanja hili. Au siyo???
Waumini: Ameen..
Agent wa kuzimu: Tumekuja sasa
Agent wa kuzimu: Niko relini, niko relini ninafufua watu.
Nabii Hebron: Mnasikia manabii wa uwongo?
Nabii Hebron: Sema wewe mchawi una fanya nini?
Agent wa kuzimu: Tumefufua watu 10. kutoka kuzimu
Agent wa kuzimu: Tumetuma huyo mtu aje kufufua watu
Nabii Hebron: Mmetuma kuja kufufua watu huko kuzimu?
Nabii Hebron: Mnasikia ninayowaambia
Agent wa kuzimu: Watu wengi wameondoka na yule dada amekufa juzi juzi, ni sisi tumemuua.
Nabii Hebron: Mmesikia? Mikutano mnaenda mnauliwa.
Nabii Hebron: Na mmeua wangapi?
Agent wa kuzimu: eeehhhh
Nabii Hebron: Nakukata kiuno..
Nabii Hebron: Hao wenzako wote nawaua.
Nabii Hebron: Sogea hapo. Anakung’utwa…Hebu mwachieni, sogeeni. Malaika zunguka hapo. Acheni awekwe katikati. Hakuna kusimama. Haendi popote. Ni bakora, haendi ati si mnaona?
Nabii Hebron: Bakora.Nikisema nimesema mimi. Bakora. Rudisha hicho kichwa huku kisije kikaumia, ni
bakora.Na anayekusumbua wewe ni bakora tu. Bakoraaaaaaaa. Hakuna kusitasita, kwa nini utoke jasho bwana? Niko vizuri mimi wewe. Nakukanyaga kichwaaaaa..
Nabii Hebron: Mnaogopa nini?
Nabii Hebron: Yesu anabipiwa? Lakini usije ukasema YESU, YESU wakati huna YESU, ohooooo…
Nabii Hebron: Mnaona anaita? Ita.. Nawapiga bara zima, dunia nzima…Si mnaona mkono anafanya hivi?
Nabii Hebron: Si mnaona? Waite! YESU amenituma, niko full msiogope. Niko full….Na nyie ninawaangalia mko full…
Waumini: Ameen.
Nabii Hebron: Unaogopa nini wewe? Aa tulia.Haguswi mtu hapa. Yaani ole wake agese hata mtoto wangu  hapa…Wewe…..Usiogope. Hata kiti cha kanisa hili uguseguse tu…ole wako. Kikupige.
Nabii Hebron: Sema vyote ulivyotumwa kutoka kuzimu.
Nabii Hebron: Leta annointing oil.
Nabii Hebron: Halafu wanakuja wanataka kuombewa? (Anammiminia annointing oil ghafla anajigaragaza sakafuni)
Nabii Hebron: BWANA YESU asifiwe. Sasa wanakujaga wanataka waombewe, ili mtumishi anaponyosha mkonounashikwa. Sasa mimi sishikwi…Umesikia?
Nabii Hebron: Sema vitu vyote walivyokutuma kuzimu haraka. Moja, mbili, tatu. Nakunywesha damu ya YESU.
Nabii Hebron: Nabii hawa, toa vitu sijui chungwa liwe nini. Mnaona? Halafu nchi yetu itabadilika kweli?
Waumini: Hapana.
Nabii Hebron: Hapana
Nabii Hebron: Ndio wanategemewa waombee rais, waombee mawaziri, waombee bunge. Si wauaji hawa?
Waumini: Ndio.
Nabii Hebron: Nchi itanyanyuka, ole wake anayewaloga viongozi wa Tanzania.Mimi ninatamka wazi,niko
nimesimama mimi. Ole wake, kichwa kule..
Waumini: Amen
Nabii Hebron: Wala siogopi, watu wote mmeumbwa na MUNGU. Sawa sawa? Sasa ndio maana wananifuata maana Tanzania inabadilika.
Waumini: Amen
Nabii Hebron: Na Kanisa la mwisho ni Tanzania hapa YESU NI BWANA NA MWOKOZI. Watasema kila kitu
wanachotumwa hawa.
Nabii Hebron: Leta anointing oil. Nimekwisha omnbea wewe usiogope.(Nabii Hebron anammiminia agent wa  kuzimu annointing oil mdomoni, mara agent anageuka haraka na kuanza kufutia mdomo kwenye sakafu).
Nabii Hebron: Piga mkuki wa hapa. Piga hapa. Hapo chini napabadilisha kuwa moto!!! Huko unakosogea
upigwe mkuki. Nakupiga mkuki wa hapa…. Haya ongea haraka.                              
 Nabii Hebron: Haraka. Sema haraka umekuja kufanya nini hapa. Usitupotezee muda, sisi tunataka baraka bwana. Sema Haraka. Simama mwenyewe unieleze mwenyewe, mbele ya mahakama ya BWANA YESU. Simama haraka.
Nabii Hebron: Mikaeli shusha jiwe juu yake.
Agent wa kuzimu: Nisamehe
Nabii Hebron: Simama mwenyewe
Agent wa kuzimu: Nisamehe
Nabii Hebron: Simama haraka.
Agent wa kuzimu: Nisamehe
Nabii Hebron: Simama ueleze kila kitu nitakusamehe. Simama.
Agent wa kuzimu: Tumetumwa
Nabii Hebron: Enhe, mmetumwa nini?
Agent wa kuzimu: Tumekuja kukujaribu wewe
Nabii Hebron: Kunijaribu nini?
Agent wa kuzimu: Hebron
Nabii Hebron: Enhe. Hebron kumjaribu nini?
Agent wa kuzimu: Tumepita kila kanisa, tumekosa mtu aliyesimama kama Hebron
Nabii Hebron: Kwani mnatafuta nini?
Agent wa kuzimu: Si watu wengi wanasema Hebron ni freemason?
Nabii Hebron: Enhe, kwa nini sasa wanakuja kwangu?
Agent wa kuzimu: wanasema ni freemason wengine wanasema ni mchungaji, kwa hiyo tumekuja tuangalie kama ni mchungaji wa kweli.
Nabii Hebron: Mmekuta nini?
Agent wa kuzimu: Tumekuja na kijana mmoja, ana bomu tatu ya kulipua hii kanisa, halafu mimi nikatangulia nikakaa nikasikia tu Hebron anaongea kuzimu, kuzimu.
Nabii Hebron: Enhe.. Sasa mimi ni freemason au ni mtumishi wa MUNGU? Mimi ni nani mmekuta?
Agent wa kuzimu: Hebron.
Nabii Hebron: Mmekuta nini hapa? Si mmejaribu?
Agent wa kuzimu: Ee,. Tumeshindwa.
Nabii Hebron: Kwa nini mmeshindwa?
Agent wa kuzimu: Ana mwanga, sisi tunaishi na giza.
Waumini: Ameeen.
Nabii Hebron: Arusha mmechezea makanisa mangapi?
Agent wa kuzimu: ee?
Nabii Hebron: Arusha mmechezea makanisa mangapi?                                                       
Agent wa kuzimu: Tumeenda mpaka Dar, mpaka Kenya.
Nabii Hebron: Enhe,
Agent wa kuzimu: Yani hamna kanisa ambalo sijaenda, kila kanisa kila mkoa. Tukaenda kuangalia watumishi. yani tukikuta mtumishi ambaye hajasimama, tunateka nyara.
Nabii Hebron: Nyara?
Agent wa kuzimu: Eee.. tunapeleka kuzimu
Nabii Hebron: Enhe,
Agent wa kuzimu: Kwa hiyo yule mchungaji ambaye yuko relini ametoka juzi juzi kulekuzimu.                  
 Nabii Hebron:  Ameenda wapi?
Agent wa kuzimu: Ametoka kuzimu.
Nabii Hebron: Ametoka kuzimu?
Agent wa kuzimu: Eee yuko relini.
Nabii Hebron: Ametoka kufanyaje huko?
Agent wa kuzimu: Anakuja kufufua watu. Ila watu hawajajua njia ambayo anaitumia.
Nabii Hebron: Anatumia njia gani?
Agent wa kuzimu: eee?
Nabii Hebron: Anatumia njia gani?
Agent wa kuzimu: Anatumia njia ya mapepo.
Nabii Hebron: Ya mapepo? Kwa nini atumie jina la YESU?
Agent wa kuzimu: Si anawaambia watu tu njoo njoo (agent akifanya ishara ya kuita).
Nabii Hebron: Anawaitaje waje?
Agent wa kuzimu: Si anaita watu wa kutoka kuzimu?
Agent wa kuzimu: Dada juzi niliruhusu afufuliwe. maana mimi ndio kiongozi pale.
Nabii Hebron: Wewe ndio kiongozi pale?
Agent wa kuzimu: eee. ndio mimi naandika.
Nabii Hebron: Wewe ndio unaandika? Unaandika nini?
Agent wa kuzimu: Naandika majina yao
Nabii Hebron: Ya watu gani?
Agent wa kuzimu: Tunakula nyama ya watoto wachanga.
Nabii Hebron: Mmesikia? mmesikia? Sasa wewe wamekutuma kufanya nini kwangu? Kwa nini usiende kwingine?
Agent wa kuzimu: Tumejaribu makanisa zote, yani kanisa ambayo sijawahi kuja ni hapa. Ndio nimekuja leo.
Nabii Hebron: Hizo nyingine mmefanyaje?
Agent wa kuzimu: Tumepitia tumeona hamna hata mmoja aliyesimama. Yote ni ya kutanga tanga tu.
Nabii Hebron: Kwa nini sasa? Wapi na wapi mmepita. Rudia upya.
Agent wa kuzimu: Tumeenda mpaka Dar, Kenya, Uganda, tumeenda kila mkoa, hakuna mtumishi aliyesimama.
Nabii Hebron: Sasa mbona wanafanya miujiza?
Agent wa kuzimu: Tumekuja kwa vile watu wanasema MUNGU yuko Moshono, ya Hebron.
Agent wa kuzimu: Sasa nimekuja kuangalia leo kama Hebron amesimama. Nilipofiga getini, nikaona Hebron. Yaani ana mwanga.
Waumini: Ameeen (wakipiga vigele gele na makofi).
Nabii Hebron: Sasa hao ambao hawajasimama wanapeleka watu wapi?
Agent wa kuzimu: Yule mganga ametoroka.
Nabii Hebron: Atakufa huko huko.
Agent wa kuzimu: Bado hata dawa zake.
Nabii Hebron: Hata hizo dawa agalia nazichoma hapo hapo. angalia kwa macho yako nazichoma..
Nabii Hebron: Si mabomu ya kulipua nyumba, ni ya kichawi.
Nabii Hebron: Mnaona anavyocheki?
Nabii Hebron: Nini kinatokea huko sasa? Nini kinatokea?
Agent wa kuzimu: Eee?
Nabii Hebron: Hiyo mabomu iko wapi?
Nabii Hebron: Hiyo mabomu iko wapi?
Agent wa kuzimu: Iko nje ya geti.
Nabii Hebron: Wapi? angalia.. iko tena?
Agent wa kuzimu: Si naona tumeingia nchi nyingine ambayo ni nyeupe!!
Nabii Hebron: Mnaenda wapi?
Agent wa kuzimu: Eee?
Agent wa kuzimu: Tunarudi zetu
Nabii Hebron: Mnarudi zenu?
Nabii Hebron: Mnarudi zenu wapi?
Agent wa kuzimu: Tunaenda nchi yetu.
Nabii Hebron: Nchi yenu wapi?
Agent wa kuzimu: Si kuzimu?
Nabii Hebron: Kuzimu wanasemaje sasa hivi?
Agent wa kuzimu: Bado nitakaa tu
Agent wa kuzimu: Bado nitafute watoto wachanga wawili nile niondoke.
Waumini: (Wumini wanamkemea….)
Nabii Hebron: Aisee watoto wote wana sura ya MUNGU halafu wamefanana na mimi. Sawa sawa? Hawaliwi!
Agent wa kuzimu: Nimemuona mmoja saa ile ambayo nimeangalia tu  akalia.
Waumini: Haaaaaaaaaaaaaaaahhhh shindwa pepo(waumini wanakemea)
Nabii Hebron: Mnasikia ninawaambiaga watoto wakiona wachawi wanali…
Waumini: Wanalia.
Nabii Hebron: Hamjaona hapo?
Waumini: Tumeona
Nabii Hebron: Mnaenda kuliwa masadaka kanisani. Wewe unaongozwa na mtumishi hajasimama?!. Umefikia nchi gani wewe? sema kila mahali umepita.
Agent wa kuzimu: Ile sadaka ambayo watumishi wanatoa makanisani kila siku kila siku, sisi tunapokea hiyo sadaka hamjui!
Nabii Hebron: Eee?
Agent wa kuzimu: Sisi tunapokeaga. Mtu akija kujiunga na freemason tutapatia hiyo mali. Yani tunaandikia miaka tano aishi. Halafu akifikisha miaka yake tano anakufa. Yani kama amerudia tena kuja kusaini tena unaongezea miaka mbili au tatu.
Nabii Hebron: Mmesikia?
Nabii Hebron: Tulieni hapa
Waumini: Amen
Nabii Hebron: Tulieni hapa. Mambo yameharibika.
Nabii Hebron: Nani aliyekutuma kuja hapa? Hiyo kuzimu. Sema, kwa nini wamekutuma kuja kwangu? Kwa nini?
Nabii Hebron: Madhumuni ni nini?
Agent wa kuzimu: Tumepita kila mkoa tukaona hatujawahi kuja Moshono.
Nabii Hebron: Enhe, huko kwenye mikoa mingine mmefanya nini?
Agent wa kuzimu: Tumeangalia kila kona, tukachagua watumishi, tumepeleka wachache ambao hawajasimama. Unakuta wengine wanahubiri wanawadanganya wengine, anatumia mapepo. Ukiona kama kina ….tumefika huko, anatumia mapepo. Ile maiki (mic) anayoongea nayo ni mapepo ni nyoka. 
Nabii Hebron: Tulieni hapa mambo imeharibika.
Nabii Hebron: Nani aliyekutuma kuja hapa? Hiyo kuzimu. Sema. Kwa nini wamekutuma kwangu?
Agent wa kuzimu: Eee?
Nabii Hebron: Kwa nini? Madhumuni ni nini?
Agent wa kuzimu: Si tumepita kila mkoa tukaona hatujawahi kuja Moshono.
Nabii Hebron: Enhe, huko kwenye mikoa mingine mmefanya nini?

Agent wa kuzimu: Tumeangalia kila kona tukachagua watumishi, tumepeleka wachache. Wale ambao hawajasimama. utakutawengine wanahubiri wanadanganya wengine, Wengine wanatumia mapepo, ukiona kama kina ….. tumefika huko ile maiki (mic) anayotumia ni mapepo. Ni nyoka.

[ad_2]