MAELEZO YA YOUTUBE: MAFUNDISHO YA NABII HEBRON – (HABARI NJEMA)

[ad_1]

Haleluya, karibuni sana katika kipindi tena siku njema ya leo ambayo siku ya leo ninakuletea habari njema, habari njema kutoka kwa YESU, habari njema kwa mataifa yote, habari njema kwa anayemjua na asiyemjua. Lengo langu na lengo la MUNGU ni habari mjema ifike kwako. Amenituma habari njema ifike kwako. Amenituma niwaeleze habari njema kuhusu habari za ufalme wa mbinguni. Hajanituma nieleze habari mbaya.
BWANA YESU asifiwe. Haleluya; Baba ninawaombea watoto wako tayari kwa kusikiliza habari njema kwa siku ya leo, ninafuta ndani ya mioyo yao wale wote waliopokea habari mbaya wakajulishwa kama ni Injili kumbe sio Injili wakapokea habari mbaya. Na ndio maana wanateseka, ndio maana wanahangaika, ndio maana wamechanganyikiwa, ndio maana hawana mbele,ndio maana wanajuta na wanahangaika, hii yote ni kwa sababu hawakupokea habari njema, walipokea habari mbaya. BABA ninakutukuza, ninakuinua, ni kwa utukufu wako, Amen.
Watoto wa MUNGU, siku ya leo nitakwenda kufundisha habari njema aliyoileta YESU alipotumwa kutoka mbinguni. Yeye hakuleta habari mbaya, alileta habari njema. Ni habari njema kwa sababu pasipo hiyo habari njema hauwezi ukamwona MUNGU hauwezi ukafika alipo yeye, hauwezi ukafanikiwa. BWANA YESU asifiwe. Haleluya, utafungua na mimi katika kitabu cha WAGALATIA 1 : 6-9. Neno la MUNGU linasema hivi; nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi ili yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kuigeukia Injili yanamna nyingine, wala si nyingine lakini wapo watu wataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubirie ninyi injili nyingine isipokuwa hiyo tuliyohubiri na alaaniwe. BWANA YESU asifiwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena mtu awaye yote akiwahubi ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. Tutafungua nawe kitabu cha WARUMI 1 : 16, nitaendelea kuisoma, neno la MUNGU linasema hivi; kwa maana siionei haya injili kwa sababu ni uweza wa MUNGU uletao wokovu kwa kila aaminiye kwa Myahudi wa kwanza na kwa Myunani pia. Haleluya; BWANA YESU asifiwe. Umesoma katika kitabu cha WAGALATIA neno la MUNGU linasema ambaye atakayeleta habari tofauti na neno la MUNGU na alaaniwe. BWANA YESU asifiwe. Alaaniwe kwa sababu MUNGU anasema hivyo kwa sababu sio habari njema. Kwa hiyo Biblia ikibadilishwa ikaenda kinyume au anayefundisha, tayari amelaaniwa. BWANA YESU asifiwe. MUNGU alipokuwa akinifunulia somo hili ili kuwafunulia watoto wa MUNGU na kuwafundisha, kwanza alinifundisha mimi kwa faida yangu kwa miaka mika mingi japo yalikuwa yamekaa ndani ya moyo wangu ila wakati wake ukifika nitafundisha kama sasa ilivyo. Haleluya. Sasa watu wengi wanajua kwamba wanapokea habari njema ila wanapokea habari mbaya. Nitakufundisha tofauti ya habari mbaya na habari njema. Habari njema zinatoka mbinguni. Habari njema ni habari ya ufalme wa MUNGU, kusimamia neno la MUNGU kama lilivyo bila kulibadilisha kunyooka straight kama MUNGU anavyotaka yeye. Ikiwa ni tofauti tu, ni habari mbaya. Mfano imeandikwa, usiabudu sanamu. Sasa kanisani wanahubiri Biblia kidogo ukweli halafu wanaabudu sanamu. Hizo zote ni habari mbaya ninawaeleza watoto wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Unapovunja amri za MUNGU tayari umepokea habari mbaya, na unapopokea habari mbaya inakaa ndani yako inakujengea mabaya unazidi kulaaniwa na kulaaniwa. Lakini nitazungumza katika kipengele cha watumishi. Maana watumishi wengi nimekuta katika maombi na MUNGU alivyokuwa ananifundisha wameshalaaniwa. Yamkini hata ni wewe unayeangalia hapo umelaaniwa kama ulikuwa hujui. Kama unachangisha pesa kanisani, MUNGU amesema hivi, atakayefundisha tofauti na MUNGU anavyopanga na alaaniwe. Sasa wewe utabisha wapi hujalaaniwa? unaabudu sanamu umelaaniwa, unachangisha watu pesa kanisani umeshalaaniwa. Ni freemason halafu unajifanya mtumishi umelaaniwa. Umejiamkia tu kwa kutafuta pesa kwa kudanganya watu kwa kujifanya wewe ni mtumishi kumbe MUNGU hajakuita, umelaaniwa. Utabisha hujalaaniwa? Na kama umelaaniwa, tayari mbinguni huendi. Sasa madhara yake na wale wote ambao mnasikiliza mmeshalaaniwa kwa sababu mwenye laana hana baraka, anatoa laana, na laana, na laana. Mfano YESU alipokuja, alileta habari njema ya ubatizo wake wa maji mengi akasema kila mtu afuate njia yake. Sasa watu watu wanabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe nikuulize swali, hiyo ni habari njema au mbaya? Kama ni ni habari njema ina maana ubatizo huo umetoka mbinguni. Kama ni habari mbaya hauko mbinguni, hauko kwnye Biblia. Anakubatiza kwa jina lake mtumishi. Hiyo ni habari mbaya. Imeandikwa ubatizwe kwa jina la YESU tu basi. Sasa haya yametoka wapi? Amenituma niwaeleze habari njema. Utakaposikiliza utapona na utabadilika, maana watu wanafikiri mtumishi akishasoma Biblia hivi tu basi, huyo ndie anayeeleza habari njema. Soma Zaburi ya 23 Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu lakini anakunywa pombe; anakueleza habari njema gani? Watoto wa MUNGU ni wakati wa kufunguka. Sasa hivi kuna mikuno mingi sana, utaambiwa semina, injili inapelekwa lakini sio habari njema. Hata kama wanasema habari ya wokovu, wanayoyatenda ni biashara, kutafuta pesa, wamechanganya na uchawi na wana wa MUNGU ndio maana matatizo hayaishi yamejaa kwenye nchi mbalimbali wala hayaishi kila siku asubuhi mchana na jioni kwa sababu wamekuja wajamaa sasa hivi, badala ya kuendeleza habari njema wanaleta habari mbaya. Unataka kumwona mtumishi, utapita kwa sekretari, utaandika jina, utatoa hela, utapewa kuponi ili upewe appointment hiyo habari njema au mbaya? Hiyo ni mbaya. Imeandikwa utoapo sadaka yako mtu yeyote asijue. Leo makanisa yanakuambia andika namba ya simu na kiasi, unapewa risiti. Hiyo ni habari njema au mbaya? Jibu ni mbaya. Sasa kama wanafanya hivyo, wamelaaniwa, na wewe unayeshiriki laana imekuhusu ndio maana hakuna baraka. Unafilisika. Ni mahali pa kukimbia wala usishiriki. Hizo ibada ni makelele mbele za MUNGU, na MUNGU siku moja nilikuwa naongea naye, akaniambia Hebron sipendi mtu mwenye dhambi hata kusikia sauti yake, hata kuona mahali anapolala. Sasa pata fahamu, kama watu wanakuwa na roho ngumu, wanaenda kinyume na MUNGU, ukienda kinyume na MUNGU ni laana unaitafuta. Ukiabudu sanamu umefuata laana. Ukiabudu Mathayo, sijiu Eliza umefuata laana. Wewe mwabudu MUNGU peke yake. Ukiabudu haya maua, ukiniabudu mimi umeshalaaniwa. Umeabudu ng’ombe, umeabudu miti umeshalaaniwa. Ninawasihi mfunguke. Ndio maana maisha hayaendi. Mje kwa YESU siku ya leo.
Haleluya. Na msidanganywe kwa sababu MUNGU kama amewatuma watumishi waeneze neno lake, ni habari njema, sasa hivi habari ni michango, michango, michango mitupu, support redio, support TV. Hizo ni habari mbaya. Kama MUNGU amemtuma huyo mtumishi habari njema amesema asifikiri nini wala nini, yeye aende atafungua milango mambo yaanyooka. Lakini hayanyooki kwa sababu ni habari mbaya. Hivi kanisa lina benki. YESU amesema hivi; msichaji riba, lakini mtumishi ana benki. Amesema msiwe na mabwana wawili. Sasa hizo ni habari njema au ni habari mbaya? Sasa msingi tayari umekwisha haribika, na mti ukishaharibika, na matawi yameharibika yote. Watu wanamsubiri YESU, atarudi, mnatazamia wengine wanakwenda kumbe hamuendi. Hizo ni habari mbaya. Sababu iliyopo ni hawa wajamaa wamelaaniwa. Kwanza mimi siwawaiti watumishi niwaite wajamaa. Tena bora ni bora nisiseme wajamaa, maana jamaa wengine ni watu wazuri tu, mfano jamaa yako jamaa yangu, jamaa yule, lakini watumishi wameoza. Ndio wauza madawa ya kulevya, wauza bangi, wauza pombe, ni washirikina, wanatoa makafara. Sasa atakuleteaje habari njema mtu kama huyu? Mtu kama huyu ambaye anakuambia ili ubarikiwe au akuombee lete pesa, hiyo ni habari njema au ni habari mbaya? Amenituma niwaombee bure, hiyo ndio habari njema. Amenituma niwafundishe, niwaongoze ili mumwone yeye. Hiyo ndio habari njema. Lakini mambo ya sheria sheria ili iwe hivi, fanya hivi, kuangalia vitu vyako, ni wezi hao.
BWANA YESU asifiwe. Alisema watakuja makristo wengi, hata sasa ni wengi, na wamejaa; Tanzania na dunia nzima. 99% watumishi wamelaaniwa, wana laana, hawana baraka.  BWANA YESU asifiwe. Huo ndio ukweli. Ukitafuta mtu wa kukubariki sasa hivi ni shida, humpati. Atakuambia tu BWANA atafakunyia, haleluya, haleluya, lakini mchunguze; ana laana kuanzia mguuni. Sasa watu walionaga MUNGU yeye haoni, wanamdanganya. Ni sawasawa na mtoto mdogo analamba sukari halafu imebaki mdomoni, baba yake au mama yake anamuuliza kwa nini umelamba sukari? Yeye anajibu “mimi sijalamba mimi”. Ndio watumishi wa sasa hivi, lakini MUNGU anaiona na MUNGU anaona mnataka baraka lakini mna laana. Sasa mtapata wapi? Mtamwonaje MUNGU? BWANA YESU asifiwe. Kanisa limeacha njia ya MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Limekwenda kinyume kabisa, badala ya habari njema sasa hivi ni habari za laana, habari mbaya. Sasa hivi habari kanisani ni pesa, michango michango michango. Hayo majengo ni mapango ya laana. Na ndio maana hata mliojenga hambarikiwi kwa sababu mmedanganywa hamkutoa kitu ambacho kinajenga ufalme wa MUNGU, bali kimejenga ufalme wa laana. Ndio maana unadaiwa sana kanisani. Hizo ni habari njema? Makanisani sasa hivi habari ni madeni tu. Watu wengi mna madeni. YESU hakutuma habari za kuchukua pesa zenu bwana. Na kama unatoa pesa ujue hizo ni habari mbaya. Pesa inauma, ukitaka kumtolea MUNGU, toa ukiamua, kwa moyo wako, tena usitake ujulikane. Iwe ni siri yako, maana kuna watu wengine wanasema nikitoa nikionekana ndio MUNGU ataniona; rudi kwenye neno la MUNGU; ficha mtu asijue. MUNGU anaona kama unamtolea bwana. Sasa hawa jamaa wamekuja na saikolojia ya kukuchezea chezea, andika jina, sasa mtu akiandika jina anaona aibu kutoa mia mbili, masikini ya MUNGU atatoa elfu, kumbe elfu ndio bajeti yake ya kula siku nzima. Sasa huyu MUNGU akunyang’anye mpaka uishiwe ni mungu gani huyu? Na zaidi wakiona hivi kuna kitabu askofu anatakiwa aje akisome hapa, ni saikolojia tu ili udanganywe askofu ataona nimetoa ngapi ataiona vizuri kweli. Taka MUNGU akuone, usitake mwanadamu akuone wala mchungaji akuone, hao wamelaaniwa. Ukweli ndio huo; katika nchi utasikia kuna semina nyingi sana. Hivi kweli wangekuwa wanapeleka baraka kuna watu wangekuwa na shida? Sasa hivi ukipita katika Tanzania ukipita kwenye kijiji kimoja makanisa labda mia mbili au mia tatu. Yote yanaeleza eti habari njema. Habari gani watu wana shida? Habari gani nchi haifunguliwi? Habari gani mpaka nchi ikafilisika? Kama kweli serikali inatoa vibali, ili hao jamaa waiombee nchi, na MUNGU aibariki nchi. Miaka yote nchi hainyanyuki, wachawi nfio wanaitesa, shetani ndio anaitesa mnabaki kulaumu viongozi; siri iko wapi? Hawa jamaa wana laana. Kwa sababu mahali palipo na nabii au mtumishi wa MUNGU wa kweli lazima baraka zishuke, lazima kuwe kuna njia, lazima kuwe kuna upenyo, upenyo uko wapi? Watu sasa hivi wanatafuta majibu baharini; baharini ni kwa waganga wa kienyeji. Na siwacheki kwa sababu watumishi wenyewe nimekuwa nikifungua watu wengi sana wemeniambia mimi nimekwenda kwa mganga zamani hizo nashangaa namkuta mchungaji naye amepaki na suti, mganga ananiambia namtengeneza na huyu jamaa bwana, si anaenda kuhubiri huko? Sasa mganga atakupa nguvu gani wewe ya kwenda kupeleka habari njema? Zaidi unaenda kumwaga makufuru, makafara. MUNGU awaaibishe, MUNGU awashushe wote mnaotumia uchawi. Nimetamka neno hili halirudi kama vile mvua inavyonyesha inagonga chini, mazao yanatokea. Ndivyo ilivyo, watu wamechoka, watu wanakata tama, watu wanalala njaa sababu pesa zao mnavyozichukua mnaenda kupeleka kwa mashetani, wanalaaniwa, watoto wa MUNGU linda sana ulicho nacho, pesa yako mtu asiizoee. Wengine mpaka watumishi wanajua akaunti ya mtu Fulani ina shilingi Fulani. Yeye ametumwa huko wewe? Kama MUNGU amekutuma, kahubiri, nenda mbele. Fungua mtu aende zake. Acha kuangalia ana suti, acha kuangalia ana gari, acha kuangalia ana nyumba. Mwenye ghorofa ndio unafuatwa mpaka nyumbani. Wewe mwenye kinyumba cha majani hawakufuati, kwenda huko huna kitu. Sasa hiyo ndio habari njema? Ni wakati sasa hivi injili ifanyike kama vile YESU alivyofanya. Hiyo ndiyo injili. YESU alilala kwenye mapango, YESU alilala chini, YESU alilala barabarani, yaani mahali popote. Kwenye shida yupo; leo hii YESU alichukua pesa za watu? YESU alinyang’anya? Sasa wanachukua jina la YESU wamebadilisha injili ya namna nyingine, Na Biblia inasema mtu wa namna hiyo au nyingine na alaaniwe. Sasa wengi wana laana. Ukishakuwa na laana mbinguni huendi, ni kitanzi. Watumishi jiangalieni, ni wangapi mna laana nyie? Mnasema baba wa kiroho au mama wa kiroho. Unakuta mama wa kiroho ambaye ni mchungaji yeye ndio anazini na watoto wake, ameshalaaniwa. Ni mama gani huyo? Baba wa kiroho yeye kazi yake ni kuzini na waumini tu. Baba wa kiroho ni baba wa kimwili. Wewe utazinije na mtoto wako wewe? Mnawajua na mnawaelewa. Wana laana. Biblia inasema na alaaniwe anayefundisha injili ya namna nyingine. Na tena zaidi wengine nimekuta ni maaskofu kabisa, watu wananiletea mashitaka, wanawaingizia vidole kwenye viungo vyao vya siri watoto wa kike. Na ni wamama wenye heshima wakijua wamekuja kwa BWANA YESU, Bwana atawatendea. Ficha watoto wa MUNGU viungo vyako vya siri usimuonyeshe mtu huko. Ficha. Ukiona hivyo ana pepo huyo. Na wanajiita maaskofu ni wengi sana. Kesi hizi ziejaa, waumini wamekuja kushtaki, matokeo yake wanakuwekea mapepo na kukuharibia maisha yako. Hivi mmekuwa madaktari nyie au manesi? Huko kwenye viungo vya siri mnafuata nini? Shika mikono, mwombee mtu. Huko unafuata nini? Mnayajua. Msione kwamba watoto wa MUNGU wanashitaki kwa baba yao. Wanalia, wananung’unika, wao wakiamini wanaongea na MUNGU kumbe wanaongea na pepo. Nafungua na serikali kweli iwakamate watu wa namna hiyo, iwaadhibu kabisa, maana huku ni kumtukana YESU. Kabisa kabisa, kutumia jina la YESU na wanawake wakisikia habari ya YESU wanaamini kweli. Vua nguo nikuombee wanakubali. Serikali MUNGU awafungue macho muwaone watu wa namna hii. Najua hata serikali, viongozi wanampenda MUNGU, lakini kwa namna haikubaliki wala hairuhusiki, hata mimi mwenyewe siikubali, sijui kama yuko ambaye anayekubali. Ninamwomba MUNGU mtakamatwa, mtakutwa. Mnamwona MUNGU ni mjinga, lakini nawaeleza ukweli. Ndugu msikilizaji yawezekana ni ndugu yako, au ni baba yako au ni mama yako amefanyiwa vitu kama hivyo, wanajijua hawasemi lakini wanapokuja kwa mtumishi kamili anafungua moyo anakuambia. Ni mambo mazito, lakini wanafanyiwa makanisani. Kama imefika mahali mtu anamwambia mwanamke (mtumishi), kaibe pesa za mume wako leta hapa. Ni mafundisho gani hayo unayomfundisha? Ni waizi na wengi wameibiwa na kunyang’anywa mali. Lakini njiani na suti na VX kumbe ni waizi wakubwa hawa. Wanachafua jina la Mwenyezi MUNGU. Ni wakati wa kila mtu sasa hivi kuamua kumtetea MUNGU, wewe unayempenda MUNGU, lakini kama humpendi wewe acha. Sikulazimishi, mimi nakufundisha. Iko faida kwa MUNGU, iko hasara kwa shetani. Uzima wa milele ni mbinguni, uzima wa mauti ni kwa shetani. Chagua leo njia utakayoiendea.
BWANA YESU asifiwe. Wengi wamekaa katika makanisa ya wokovu wanaomba, wanaomba wanajua wanaenda mbinguni wako sawa, lakini wamejazwa mapepo, wameibiwa nyota hukohuko kanisani. Sasa ni habari gani hizi zinaletwa? Hizo sio habari njema, hizo ni habari mbaya. BWANA YESU asifiwe. YESU alituma wale mitume wake wa kwanza waeleze habari njema waieneze. Sasa imekuwa kinyume sasa hivi inaelekezwa habari mbaya. Haitaitwa mbaya, mimi ninachokufungua ujue ni mbaya utaona iko tofauti na Biblia. Kwanza ubatizo wa maji ya kikombe, hiyo ni habari mbaya. BWANA YESU asifiwe. Habari YESU aliyoileta, kwanza alikuja Yohana akatengeneza njia, ubatizo wa maji mengi. Akaja YESU na yeye akasema fuateni njia yangu. Sasa hiyo ndiyo habari njema ya mbinguni. Hii ubatizo wa kikombe sio habari njema, ni habari mbaya na wengi mmeipokea na mmeikubali. Hata mimi niliipokeaga, nimeikataa na kuitupa huko. Kila uliyewekwa alama hiyo, wewe maisha yako ni habari mbaya tu. Sasa hawa watumishi ndio YESU amewatuma kazi hiyo? Haipo. Soma Bblia, tafuta, haipo. Anasema atakayehubiri injili ya namna nyingine na alaaniwe. Soma Wagalatia 1 : 6-9. Inaeleza wazi wazi. Utabisha huna laana? Utabisha wewe unayesoma majina ya wana wa MUNGU waliotoa sadaka na kuandika majina? Utabisha wewe unayetumia mizimu? Utabisha wewe ambaye ni freemason? Utabisha? Utamjibuje BWANA? Madhara yake, kila aliye katika kanisa hilo, laana iko nay eye. Kwani ndiyo chanzo cha laana. Hakuna baraka, uondoke umfuate YESU, umuombe MUNGU kama siku ya leo akuongoze pa kwenda, na usiogope, usiweke urafiki katika mambo ya imani. Wewe angalia MUNGU amekuongoza wapi ndio uenende. Ulikuja peke yako, utarudi peke yako, BWANA YESU asifiwe. Wengi hawajarudi. Idadi kubwa wanaenda kwa shetani sasa, hawaendi mbinguni. Ulitoka kwenye raha mbinguni, ukazaliwa, uje ushinde ulimwengu na urudi, YESU alionyesha njia hiyo hiyo, lakini wewe wapi?
BWANA YESU asifiwe. Ni mapenzi ya MUNGU tumwabudu yeye peke yake, si kuabudu wachawi, si mizimu, sio vibao vya waganga mabarabarani kila mahali, yote hayo wanayoyafanya wamelaaniwa na MUNGU. Na wewe unayekwenda kwa mganga umelaaniwa kama ulikuwa hujui, na unashiriki umelaaniwa. BWANA YESU asifiwe. Wengine wanakwenda mpaka kwa waganga wanachanjwa miguu ili wapendwe, hivi, upendo unatoka kwa waganga au unatoka kwa MUNGU? Lakini siwalaumu, nawafundisha mpate kuelewa ukweli kwa sababu mambo yalikwisha kuharibika na injili ikabadilishwa badilishwa, sasa imekuwa ni habari mbaya. Na mimi siionei haya injili, ni uweza kutoka kwa MUNGU ambayo ninakueleza, wala sipindishi, nakuambia vile vile ili usalama wako upone, ili ubadilike, ili uwe safi. BWANA YESU ASIFIWE. Mimi sitaki hata shilingi kumi yako. Mimi ninamjua yeye aliyenituma, nafuata injili yake “habari njema” usiulize watu wala usifanye nini, wewe songa mbele kama alivyonituma. Anarudi, lakini sasa wengi wako kwenye laana, wameshikiliwa, ni kudanganywa, makanisa yamekuwa kama ni makampuni, ni masoko, ni biashara, ni pesa pesa pesa tu, kunyang’anya mali za wana wa MUNGU na hata wewe mwana wa MUNGU mnaona kama mnamtegemea MUNGU. Mmelaaniwa, hiyo ni habari mbaya, amenituma niwaeleze habari njema, mumrejee yeye. Amenituma niwaeleze habari njema ya uzima wa mbinguni, anarudi, makao yako tayari. Wale wanafunzi wa YESU waliokuwepo hapa ulimwenguni, wao walikuwa na makao yao tayari mbinguni, na hata sasa wapo katika miji yao. Walishinda, na wewe je, unategemea kwenda wapi? Kinachokupeleka mbinguni ni habari njema. BWANA YESU asifiwe. Unajua watu wanaona kwamba injili au habari za neno la MUNGU ni stori stori tu zisizotimia. Lazima litimie, neno la MUNGU halirudi bure. Makao yapo mbinguni na kila mtu ana makao. Lakini yule aliyeshinda, mwenye dhambi hatakwenda, aliyelaaniwa hatakwenda, ambaye amefundisha habari ya injili ya namna nyingine hatakwenda. Kwa nini MUNGU anasema alaaniwe, kwa sababu ile injili anayofundisha ni kwamba anafanya kazi ya shetani, sasa yaliyompata shetani unakuwa umefungiwa na mapigo hayo hayo ya shetani, haijalishi unasali sala ya Baba yetu, unasoma Biblia, mara neema, hiyo injili itakurudi. Imani tuliyofundishwa ni kumwamini BWANA YESU, hakuna imani ya nikea au imani ya mitume. Unatakiwa umwamini BWANA YESU peke yake. Hata mimi ni mtume, unkisema imani ya mitume mimi imani gani itakusaidia wewe? Wewe  mwamini YESU peke yake. BWANA YESU asifiwe. Achana na injili ya imani za nikea, achana na injili za kuabudu watoto wa MUNGU. Achana nao hata akina Petro, hao sio MUNGU, hao hawana nafasi, habari njema ninayowaeleza mwamini MUNGU BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU peke yake. Wao wana umoja. BWANA YESU asifiwe. Na ndio tumeongozwa, sasa hizi injili nyingine au kanisa lina Biblia yenye vitabu vingine na wanavipa majina mengine, hizo injili ni habari mbaya. Amua leo kuachana na habari mbaya. Amua leo kuachana na tabia za kidunia, amua leo kuachana na uzinzi na uchawi na umrejee BWANA YESU. Amua leo kuachana na masanamu na utoke huko, usiabudu, usibusu, leo uje kwa YESU ambaye amenituma habari njema. Tazama nikueleze mfano YESU mwenyewe angekuwepo ulimwenguni nikuulize wakati anafundisha; rudi kwenye ufahamu wako, je, ungeabudu sanamu mbele yake? Jibu usingeabudu. Ungeabudu watoto wake (wanafunzi wake)? Jibu usingeabudu. Kwa nini usifanye hivi hivi wakati ameamuru kwamba msiabudu? Hii ni kumdharau. Na anayemdharau, laana inamhusu. Soma neno, sio mimi nalaani, ninawafunulia muelewe.
BWANA YESU asifiwe. Watu wamekukuwa ni wachawi, sasa hivi wakihubiri wanavaa hirizi kwanza, wanaangusha misukule, wanamazingaombwe hao. Waliotumwa wanaojifanya kupeleka  habari njema hawapeleki habari njema, ni habari mbaya. Ndio mbwa mwitu. Leo utoke katikati ya mbwa mwitu. Usikubali ukasikia mtu anatuma habari kwenye televisheni m-pesa saidia kipindi sijui nini, hiyo ni habari mbaya. Kwa nini ni mbaya? Rudi kwenye injili usisumbuke utafanya nini wala nini, ina maana kama ni MUNGU amemtuma atafanya mwenyewe, kama hajamtuma ndio anakuja na habari mbaya. Sasa habari mbaya yoyote ndio unaanza kuchangishwa pesa, kuvutwa, watu wanajenga nyumba za watumishi wanaambiwa MUNGU ameniambia mnijengee nyumba, mnalala njaa nyie mnanyang’anywa, habari mbaya hizo. Angalia, MUNGU amemwita,amwambie amjengee; MUNGU atanyanyua mtu amjengee lakini sio kwa namna ya kukuambia wewe leta, wewe fanya hivi, wewe kataa. Ndio maana mmefilisika, wengine mpaka mjenga makanisa, mkijua kwamba mnaeneza habari njema,na mioyo yenu inajua inaeneza habari njema lakini ni habari mbaya. Ndio maana unaumwa, umekaa hapo mpaka sasa hivi, unaangalia, haunyanyuki, hakuna msaada. Unasema MUNGU kumbuka sadaka zangu kama za Cornelio; wapi? Hazikutenda habari njema, zilitenda habari mbaya. Haleluya. Hata mafundisho yote unayofundishwa sijui ya imani, sijui ya heshima, sijui ya ndoa, lakini baba wa kiroho akishakuwa tayari ana laana, laana haitakaa iondoke pale. Sasa wewe ninachokuambia, ni ondoka maana wako wengene wamekataa na wamemwasi MUNGU, wako wengine wanapaa, sasa hivi ni kuruka nchi ya Zimbabwe ndio wanakimbilia sana na Austalia. Naendelea kuvunja na kubomoa kwenye ulimwengu wa roho makao yao yote kwa jina la YESU. BWANA YESU asifiwe. Habari njema inakuja bure. Ni ajabu sana hata serikali inatoa kibali kwa kanisa, ikisikia kanisa au huduma ya mungu, hawachaji kodi. Serikali yenyewe inaeneza habari njema, lakini hawa jamaa huku wanaeneza habari mbaya. Serikali chunguzeni hata mimi jamani. Kataeni, waulizeni hata kwenye Biblia wapi imeandikwa jamani kwa nini mnamdhulumu MUNGU namna hii, kwa nini mnachukua pesa za watu, kwa nini mnanyang’anya watu pesa. Kwa nini mnatumia jina la Mwnyezi MUNGU, hata wewe uliyeko kwenye serikali MUNGU atakuuliza ulikuwa wapi wewe watu wakatumia jina langu kunichezea chezea? Lakini kama mlikuwa hamjui muelewe.
BWANA YESU asifiwe. Makanisa sasa hivi ni uchawi, uchafu mtupu. Lakini mnampenda MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Unampenda MUNGU njia ni ipi? Wahuni wameingia huku jamani makanisani, kama vile duniani unasikia mtu fulani ni mhuni, na watumishi wamekuwa wahuni. Ni pesa tu. Atakuja mwingine anakuambia leta dhahabu zako zote anazichukua, anakuambia MUNGU hataki uvae, dhahabu ni mashetani. Nikuulize swali mwana wa MUNGU. Nani kaumba dhahabu? Nani kaumba tanzanite? Sasa MUNGU ameumba najisi hivyo? Wengine wanakatazwa hata kuvaa dhahabu, vaeni mpendeze. Hizo sio habari njema, ni wivu. BWANA YESU asifiwe. Mmenielewa watoto wa MUNGU? Amenituma niwaeleze mumrejee yeye, yeye sio mnyang’anyi, yeye injili yake si ya kuwafilisi watu. Yeye injili yake si ya kuwanyang’anya watu mali zao. Yeye injili yake anaipeleka mwenyewe, na hata watu wakimtumikia atawabariki atawainua, hawatabki kama walivyo. BWANA YESU asifiwe. Lakini sasa hawa mbwa mwitu, wanaitwa kwenye Biblia mbwa mwitu kwa sababu wamebadilisha neno la MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Watajiita majina mengi; daktari, mtume, nabii, askofu, mchungaji, lakini YESU mwenyewe hawajui. Sasa watumishi wote walio hivyo MUNGU hata hawajui majina yao. Sasa wewe unaenda kwa mtumishi ambaye MUNGU hamjui unategemea nini? Lakini ni vigumu kumuelewa mtumishi mwenye MUNGU na asiye na MUNGU mimi nakufundisha. Zaidi fuatilia masomo yangu katika redio mbali mbali za Tanzania kila wiki na katika website www.prophethebron.org na vitabu vingi nilivyovitoa na DVD zitakusaidia. Na zaidi ukaribie upate mafundisho ili uwe imara usonge mbele. Mimi ninachotaka ni roho yako ipone, nataka roho yako ibadilike umjue MUNGU, mapenzi ya MUNGU yatimie. Kila mtu aishi kwa raha, amfurahie, taifa lifurahi. Mnaambiwa maombi, maombi, maombi yanafanyika sana lakini watu wana laana sana hata MUNGU hawajui. Sasa maombi yamekuwa ni ya kichawi. Wachawi wanawanga usiku. Wengine wanaenda mlimani unasikia wanaenda kwenye kuomba. Lakini kule wanachoenda kufanya wanaenda kukutana na miungu. Hivi wewe, mtu anazini na waumini kanisani; ana baraka gani huyo? Hivi wewe mtuanachangisha pesa, hivi wewe, mtu anahubiri injili tofauti na MUNGU; amechanganya mahali pengine ukweli, pengine uwongo halafu anakuambia hili ndilo neno la MUNGU. Ninakuambia hilo sio neno la MUNGU. Ninakueleza injili kutoka mbinguni ambayo ni uwezo wake halisi kutoka mbinguni ambayo ni uwezo wake halisi uingie ndani yako, uujue ufalme wa MUNGU na ukubali ubadilike. Usitishwe wala usiogope; mambo yameharibika. Sasa hivi na wachawi, wananyang’anya watu pesa, makanisa ni mengi, miujiza ikafanyika ya shetani lakini haitatoka tena nimeibomoa nazidi kuiharibu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti. Msiogope, mrejeeni MUNGU, yeye anawapenda  njia iko wazi. BWANA YESU asifiwe. Usiogope cheo cha mtu, wewe muangalie. Kama ana MUNGU sawa, kama hana MUNGU ondoka. Sasa wengi wanatumia jina la MUNGU. Hivi unajua hata ng’ombe ni mungu? Hivi unajua hata shetani ni aina ya mungu? Si ndio miungu hao? Si ndio mabaali? Sasa hivi imekuwa kama kipindi kile cha Eliya. Mabaali walikuwa mia nne hamsini,yaani watumishi hao, Eliya alikuwa peke yake. Wote walikuwa wanasema tunamwomba MUNGU. Eliya akajijua akakaa pembeni, akasema ombeni nyie na mimi niombe. Akawaambia nyie mpo wengi, ombeni mungu wenu atajibu, hakujibu. Eliya MUNGU akajibu. Ndivyo na picha ya makanisa ya sasa hivi yalivyo. BWANA YESU asifiwe. Hizi Biblia watu wanazibeba siku hizi ni kusanii watu, kuibia watu, watoto wao. Sasa hivi hata imekuwa mtu akienda kwenye maombi nakusihi iwe mwanamke au mwanamke, hakikisha kama ni mke wako nenda naye. Na mwanaume kama anaenda kumwona mtumishi wa kike kwa appointment, sindikiza, kaa hapo. Akimwambia toka uje siku nyingine hapana, nyie ni mwili mmoja. Mambo yameharibika, vijana wanalia, wamama wanalia, mambo yameharibika, serikali ikaone jambo hili. Hata wakachunguze huko makanisani, watayakuta. Najua mnajua, MUNGU azidi kuwafungua, na azidi kuibariki serikali ya Tanzania na kuiinua juu sana, hao wanaotuchafulia nchi yetu MUNGU ninaomba uwaondoe maana wanapofundisha vibaya tofauti na MUNGU alivyoagiza, tayari nchi inalaaniwa, nchi haisongi mbele, BWANA YESU asifiwe. Laana inabaki pale pale, na MUNGU yeye anaangalia haki siku zote, BWANA YESU asifiwe. Haleluya. MUNGU ninakupenda, MUNGU ninakuinua.
Nakwenda kuwaombea wote ambao hawajaokoka, ninawasihi mrejee habari njema aliyonituma YESU ya wokovu, na iingie ndani yako. Yamkini yawezekana umeongozwa sala ya toba lakini aliyekuongoza hiyo sala haijaingia ndani maana yeye mwenyewe hana habari njema ndani yake, ana habari mbaya ila amejificha. BWANA YESU asifiwe.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe dhambi zangu zote, nilizozitenda kwa kujua au kwa kutokujua. Niondolee habari mbaya, mafundisho mabaya kwenye fahamu zangu na akili yangu. Uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele. ROHO MTAKATIFU niongoze wewe mahali pa kwenda katika jina la YESU. Nisidanganyike tena, nisifungwe na nguvu yoyote kwa jina la YESU. Ninawafunika kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti. Ninawaombea wagonjwa, ninawafungua. Msio na nyota narejesha. Mlio na kesi ninafuta, mabalaa, mikosi nafuta kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti, mnaologwa kwenye nyumba zenu kila uliyewasha TV au radio, naachilia moto mchawi hatakanyaga tena, na wewe ambaye ni mchawi naunguza uchawi wote, nakuvua mavazi ya kichawi yote kwa damu ya YESU. Ninakuvua mapete ya kishetani nayachoma, ya ki-freemason nayachoma, mazindiko yote ninayachoma ninayapindua ninakamata ninachoma ninatupa gerezani kwa jina la YESU. BABA ninainua serikali ya Tanzania juu, rais, mawaziri, makatibu, nainua madini, BABA ninaondoa mabaya yote katika nchi ya Tanzania. Ninaombea bunge, BABA ninaombea na katiba. Ninaomba kusudi lako likatimie, la adui hakuna. BABA, wanaochezea wabunge fahamu zao kwa kuwaloga wasiwe kitu kimoja au kukubaliana jambo ambalo ni jema kwa ajili ya maslahi ya nchi ninaliondoa kwa kwa damu ya YESU KRISTO wa Nazareti. BABA, kusudi lako litimie. Tanzania ni yako, umeiumba wewe, na watu wote ni wa kwako. MUNGU, kilichoingia au kuharibu kiondoe. Ninakuomba kwa sababu wewe unajibu. Wewe ni MUNGU na hata siku moja hujaniambia uwongo wala husemi uwongo. Asante kwa sababu yamekuwa.
BWANA YESU asifiwe. Nitaeleza tena mabo mengine yanayoenda kutokea Tanzania. Naendelea kurudia, Tanzania ndio Eden. Wote watakaotumia uchawi hawatarudi mimi nakuambia hurudi, iwe uenyekiti, iwe ubunge, iwe ukatibu, iwe urais, hupati. Ameniambia MUNGU, kama unabisha, endelea. Tuone kama shetani ataingiza kiongozi, au MUNGU na shetani tuone ni nani zaidi. Habari ndiy hiyo. Toka huko, okoka, uanza upya. Mpango wa kusamehewa uko pale pale, MUNGU ni wa rehema. Nchi hii niliwaambia, ndege zitakuja nyingi, niliwaambia mmeona sasa kiwanja cha Kilimanjaro kimenyanyuliwa, bado; hiyo nib ado. BWANA YESU asifiwe. Jeshi la Tanzania sio lile, na nchi ya Tanzania hitakaa ivamiwe, jambo lingine, majira kwa nchi ya Tanzania, sasa mvua zitakuwa zinanyesha kwa wakati wake na muda wake. Ameniambia MUNGU wakati nikimuomba, akaniambia Hebron, nimerejesha majira ya nchi ya Tanzania sasa. yalikuwa yamefungwa na wachawi na shetani, yameshafunguliwa. Mvua zitakuja kwa wakati wake, kiangazi kwa wakati wake, kila mahali. Sasa zinavyokuja kuna shida tena? Lakini ni hatua kwa hatua anaponiruhusu kusema. Ninayo mwngi sana kwa ajili ya nchi ya Tanzania, aliyoniambia, na anayafanya na ninayajua lakini ni yangu mwenyewe kwa utukufu wake, maana hawezi kutenda neno  lolote katika nchi bila kumwambia nabii wake, nami ameniambia tayari. Haleluya. Nchi hii ni taifa kubwa na tajiri kuliko zote. Iko mali hapa imehifadhiwa kwanza. Lakini wakati wake ukifika itakuwa. Hata mtafuteje hamtakaa muione. Narudia, uchawi Tanzania haufanyi kazi, viongozi mnaotaka kutumia uchawi, MUNGU hatawatumia nyie kwa sababu hawataki wachawi, kwa sababu MUNGU hashirikiani na mchawi. Wengi wana mapete, hayo mapete walipewa na mashetani, ni mameneja, wana vyeo mbalimbali, hiyo imetoka kwa shetana. Kwa hiyo inakuwa ngumu MUNGU kubariki nchi. Atapitia kwa mchawi? Atamtumia huyo? Sasa mmekaza shingo, anawaondoa, na anavyowaondoa mimi sijui, yeye mtanwona. BWANA YESU asifiwe. Madawa ya kulevya hakuna, pesa zilizoko nje ya nchi zitarejeshwa zote hapa. Zinavyorudishwa mimi siju, mimi nimekueleza. Utakapoyaona hayo usishangae. Haleluya, wala msiogope. BWANA YESU asifiwe. Elimu na matibabu kwa rais atakayepita na matibabu yatakuwa bure. Itafika mahali hii nchi hata Afrika kusini haioni ndani. Haina muda mrefu, na YSU atawatumia watu hawa hawa. BWANA YESU asifiwe. Ila msiogope kwa sababu MUNGU yeye ndiye atendaye kwa jina la YESU kwa damu ya YESU. Mtu yeyote una shida yoyote karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI, nitakuombea, wala usije na hela. Mimi ninakueleza habari njema. Unaumwa moyo, moyo ufunguke hapo hapo, kilema; simama uende; hiyo ndiyo habari njema. Mambo ya kufuata fuata hea yako wizi mtupu. Sio nguvu ya YESU, ni nguvu ya shetani inafanya kazi hapo, ndio maana unaambiwa leta. Sasa wamebadilisha ukienda kwa mganga utaambiwa mungu anasema leta kuku, leta bata. YESU hana hayo. Kwa baba yake kuna kila kitu. Makao yapo tayari. Rejeeni amesalitiwa vibaya sana BWANA YESU, injili imeharibiwa vibaya sana. Sasa hivi ni makelele, waimbaji, kila mahali ni makelele mbele za MUNGU. Watu wamemwacha MUNGU, wamemwasi MUNGU lakini wanatumia jina la YESU kufichia maovu lakini ni mbwa mwitu, ni wachawi, ni freemason, hawafai, ndio wanazidi kuwaangamiza wana wa MUNGU. MUNGU mtaonana naye mnaotesa watoto wa MUNGU. Lakini wewe uliyeteswa uliyenisikiliza hayo mateso hayatafanya kazi ndani yako tena. Na anayekuzuia kukufunga usije ukajua ukweli, nakuombea  hapo unaposikia sauti hii malaika wa injili watakuleta na utamwona MUNGU, utakkuwa huru. MUNGU akubariki sana, tutaonana muda mwingine, wala usiogope, mkae kwa amani, muishi kwa amani, anayekusogelea adui yeyote mkono wa MUNGU uwe juu yake. ninawainua juu sana. Amen.

[ad_2]