MAELEZO YA YOUTUBE: MAFUNDISHO YA NABII HEBRON – (WATAMBUE WANYANG’ANYI MAKANISANI)

[ad_1]

BWANA YESU asifiwe ndugu mtazamaji na msikilizaji, karibu tena kwenye kipindi cha Mtume na Nabii Hebron. Siku ya leo nitakwenda kufundisha somo kuhusu”mtumishi ni nani na mnyang’anyi ni nani “. Kwanini YESU alisema watokeao nje ni wanyang’anyi na alisema ni wezi? Alikuwa anmaanisha ni nani na ni akina nani.
“Baba ninawaombea na kuwatakasa mioyo yao maana YESU wewe ulivyoleta ujumbe huu uliuleta ili kwamba na kuacha iwe kumbukumbu yetu na sisi tukapate kujifunza tusikutane na wanyang’anyi na wala tukikutana na wanyang’anyi wasitunyang’anye.”
BWANA YESU asifiwe.Tutafungua neno la MUNGU kutoka kitabu cha Yohana 10:1-2, 7-10.BWANA YESU asifiwe. Neno la MUNGU lina sema hivi,”YESU akawaambia Amin amin nawaambieniyeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo lakini akwea penginepo ,huyo ni mwivi nae ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. ” ”Basi YESU aliwaambia tena amin amin nawaambieni mimi ndimi mlango wa kondoo wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi ,lakini kondoo hawakusikia .Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi ataokoka ;ataingia na kutoka nae atapata malisho. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu na mimi nilikuja ili wawe na uzima ,kisha wawe nao tele. Amen”
BWANA YESU asifiwe ,nitawaeleza maana ya mnyang’anyi na kwanini YESU alielezea wanyang’anyi.YESU alikwisha kujua kuwa atakapoondoka watakuja wanyang’anyi na watafanya kutumia jina lake kujiita, kufundisha na kujiita wachungaji lakini kumbe ni wanyang’anyi.BWANA YESU asifiwe.
YESU alikwisha kuona mbali  BWANA YESU asifiwe, kwamba kupitia jina lake shetani amekwisha kuandaa watu waje kutumia jina lake ili kuja kuwanyang’anya na sio kuchunga kondoo. Mnyang’anyi siku zote kazi yake ni kufilisi na kunyang’anya bali mchungaji sio kunyang’anya wala mchungaji hata siku moja halipwi mshahara yeye amejitolea. BWANA YESU asifiwe.
Nitakuja sasa tuongee katika kifungu tulichosoma, BWANA YESU asifiwe kuhusu unyang’anyi na utumishi. Kwanza kabisa naeleza katika kanisa maana uko unyang’anyi wa aina nyingi lakini mimi naeleza katika kanisa kazi aliyonituma YESU. BWANA YESU asifiwe uko unyang’anyi katika kanisa sasa hivi lakini watu wanaona ni utumishi, jambo la kwanza wamemnyang’anya MUNGU neno lake halafu nitakuja ya pili wananyang’anya kondoo kivipi. BWANA YESU asifiwe. Wamemnyang’anya MUNGU neno lake kwanza wameondoa ubatizo wa maji mengi wameweka ubatizo wa maji ya kikombe. Hao wanaitwa wanyang’anyi wa neno la MUNGU . wanyang’anyi wamemnyang’anya YESU haki yake hawataki ile haki ya YESU ikapate kusimama ndio maana wameweka ubatizo wa maji ya kikombe. Nikuulize swali ndugu mtazamaji na msikilizaji yamkini unajua na wewe unajiita mchungaji kumbe umeshakuwa mnyang’anyi na hupendi maana hukujua. Achana na hiyo kazi maana na wewe umeshakuwa ni mnyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe . Unyang’anyi kupitia neno la MUNGU, imeandikwa kwamba watu wasiabudu sanamu lakini leo hii mchungaji anawaambia watu waabudu sanamu makanisani,hao ni wanyang’anyi, kwanza wamemnyang’anya MUNGU, MWENYEZI MUNGU wanamdhulumu.BWANA YESU asifiwe. Ninakuja kwa upande wa MUNGU halafu nitakuja tena kwa upande wa wanadamu wapate kuelewa namna gani wanyang’anyi walivyo maana mnyang’anyi akijiita mnyang’anyi watu hawatakwenda, akijiita mchungaji, mwalimu, mtume, na nabii watakwenda.Sasa YESU alikwisha kujua iko siri inayofanyika hapo watajificha kwa ndani kwa mlango wa nje.Mlango wa nje ina maana ya kwamba maneno ya nje ya Biblia ndiyo yameingizwa na ndio yamejaa makanisani. BWANA YESU asifiwe, ukisoma neno la MUNGU linasema ‘nimekupa bure toa bure’ huo ni mlango wa kondoo. Lakini mlango wa nje ‘leta pesa yako ndio ufunguliwe’.Hao ni wanyang’anyi; sio watumishi hao si wachungaji, hao ndio wanyang’anyi. BWANA YESU asifiwe. Wanyang’anyi kama vile watu wanavyokwenda sokoni wanataifishwa mali zao,sasa watu ambao wanaenda kusali kwa wanyang’anyi wanakwenda kusali katika masoko. Alisema hivi YESU, wanapita na manguo yao marefu wakisalimia watu masokoni wakijifanya wako na mimi kumbe ni wanyang’anyi au ni mbwa mwitu. Huu mfano wa sokoni ilikua ni jingo ambalo linaitwa kanisa sasa. Mahali kuna michangomichango popote hapo ni sokoni. Sasa nikuulize wewe unavyokwenda sokoni si unakwenda kunyang’anywa? Utapata kitu? Utapata matango bila kutoa hela? Jibu hupati. Sasa kanisani unapata baraka zako bure mahali alipo  Mchungaji YESU wa Nazareti. Haleluya lakini usiogope MUNGU anakwenda kuwafungua amenituma habari njema yeye ambaye si mnyang’anyi BWANA YESU mpate kuuelewa ukweli wake maana wengi wametekwa na shetani kwa kutokujua.
BWANA YESU asifiwe. Wengine sasa wameanza kumnyang’anya mpaka MUNGU  wanawabatiza watu kwa majina yao, hoa wanaitwa wanyang’anyi.BWANA YESU asifiwe, sasa suala la wanyang’anyi watu wanatakiwa walielewe, sio kwamba atakuja kuwanyang’anya nguo mikononi hapana. Unyang’anyi wa kutumia jina la YESU makanisani, unatengenezewa mistari unatoa mwenyewe kwa nia yako. Unajua watu wamezoea kuita majangili ni wanyang’anyi , hao ni wa kimwili sasa kuna wanyang’anyi wa kiroho. Wa kiroho anakumaliza kila kitu ni bora hata jangili anaweza kukuonea huruma, lakini wa kiroho anakunyang’anya kila kitu. Maana jangili au mwizi vile ana hofu ya MUNGU anavokutana na MUNGU anaacha, lakini hawa wanaitwa wanyang’anyi kwasababu wameshamkufuru MUNGU. Wanamnyang’anya MUNGU haki yake yeye na kunyang’anya watu wasipokee neno la MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Mfano imeandikwa niabudu mimi peke yangu lakini leo utaambiwa abudu nyota, abudu mwezi, abudu jua BWANA YESU asifiwe abudu Yohana,Mathayo watoto wa MUNGU wale waliokufa, tayari hapo mmeshamnyang’anya MUNGU kwahiyo nyie mnaofanyo hivyo  ni wanyang’anyi. BWANA YESU asifiwe. Sasa kama unaongozwa na mtumishi wa namna hiyomnyang’anyi na wewe maisha yako kwamba huyo anakupeleka katika shimo uangamie. Uelewe kwamba haupo katika kuongozwa na mchungaji mwema bali unaongozwa na mchungaji mnyang’anyi aliyevaa ngozi ya kondoo kwa nje kumbe na mwizi ni jangili na wamejaa kila mahali.
BWANA YESU asifiwe. Sasa wengine nitakufundisha ndugu msikilizaji na mtazamaji, nikufundishe; hivi sadaka siku zote kanisani inatolewa wapi? Si inatolewa kwenye kikapu cha sadaka? Sasa iweje leo mchungaji (ndio mnyang’anyi hao nawaita) wanasema usaini hapa juu ya nguo milioni, elfu hamsini, na mguu elfu tano tano, mia tano; sasa niwaulize swali ndugu watazamaji na wasikilizaji, je, ule mwili wake ndio kapu la sadaka? Jibu sio. Je, MUNGU aliamuru sadaka watu wasaini kwenye nguo ya huyo mnyang’anyi? Hajaruhusu hivyo. YESU mwenyewe katika nguo yake haijawahi kusainiwa hivyo. Sadaka ni kitu cha shukurani kati yako wewe na mwenyezi MUNGU. Lakini iweja sasa leo hii wanaibuka wanyang’anyi na wanawanyang’anya wana wa MUNGU na wanaona kweli nikisaini kwenye mabega maisha yangu yatazidi kunyanyuliwa. Nikisaini hapa kwenye miguu, katikati, maisha yangu na mimi yatazidi kunyanyuliwa. Watu wanajikakamua kumbe wananyang’anywa mali zao na pesa zao. Hao ninasema ni wanyang’anyi, ndio YESU anasema wako hapa. Wanyang’anyi ni watumishi wanaosoma majina ya watu kanisani wametoa shilingi ngapi, wakupa risiti, wanataka email, box namba na tarehe uliyotolea. Kwa YESU hakuna mambo kama hayo, hizo ni saikolojia za wanyang’anyi. Wamesema hivi, wanapita mlango wa nje. Huo ndio mlango wa nje mwana wa MUNGU uliyopita kwako na maisha yako vile ili na wewe upate kuelewa kwamba yameshaangamia, umeibiwa kila kitu kwa hiyo hufanikiwi. Mikosi, balaa, unafikiri unaenda mbinguni kumbe umeshanyang’anywa pia haki yako ya kwenda mbinguni. Hata unabaki na haki ya kupelekwa kwa shetani, leo upate kufunguka.
BWANA YESU asifiwe. Ndugu mtazamaji na msikilizaji, nimefundisha kwa ufupi unyang’anyi, watumishi wanavyomnyang’anya MUNGU haki yake kwa ufupi. Na sasa nitaingia kwa jinsi mnyang’anyi anavyokunyang’anya wewe kanisani. BWANA YESU asifiwe. Wewe ukiona ni mtumishi wa MUNGU anakuambia kasomeshe watoto wangu MUNGU anakuambia, huyo ni mnyang’anyi. Muulize swali; wakati unazaa watoto wako wewe, hukujua kuwa unatakiwa kuwasomesha? Muulize swali; wakati unazaa watoto wako hukujua wanatakiwa kula? Wewe mtazamaji nikuulize; wewe unavyowazaa watoto wako hujapanga maisha yao uweze kufikiria watasomaje, utawasaidia, yeye anakuja kukupangia? Hao ni wanyang’anyi. Wanakuibia mpaka haki ya watoto wako na Baraka zako wewe unaona unapeleka kwa mwenyezi MUNGU, kumbe unailaani familia yako wewe mwenyewe, inabaki na mateso. Na siku ile ya mwisho mwenyezi MUNGU atakuuliza.
BWANA YESU asifiwe. Wanyang’anyi wanaonyang’anya wana wa MUNGU wanajiita watumishi. Hao sio watumishi bali kila anayekula kondoo, anazini na kondoo, huyo ni mnyang’anyi. Ni ajabu sana ukiangalia simu za watumishi utakuba wanaita kondoo zao bebi (baby) na hani (honey) na ana mke. BWANA YESU asifiwe. Na ukisoma meseji wakizituma ni maajabu watoto wa shule yaani wanavyowaharibia maisha yao. Hawa ni wanyang’anyi. Wanawalaani wanawajaza mimba, wanawapa ukimwi. BWANA YESU asifiwe. Ni wanyang’anyi, wanatumia jina la YESU. Ninawaambia leo hao sio watumishi wa MUNGU. Ukikuta mtumishi anachangisha pesa kwenye redio, mwambie huyo ni mnyang’anyi. Biblia inasema, asisumbuke atafanya nini; MUNGU atafungua milango. Kwa sababu yeye ni mnyang’anyi anaendeleza kazi ya unyang’anyi kupitia jasho lako wewe na ukitegemea kwamba MUNGU atakubariki lakini hakubariki. BWANA YESU asifiwe. Jambo lingine ujue ni mnyang’anyi, Biblia inasemama hivi, sadaka yako utoapo, kushoto wala kulia isijue, mtu yeyote asijue. Wao wanakuambia andika jina. Ile kuandika jina, tayari wamemnyang’anya MUNGU Neno lake. Unaona wanavyomnyang’anya MUNGU? Na wewe sasa ukitoa vile waziwazi, umenyang’anywa na zaidi nawatangazia leo kila sadaka yako inapojulikana na kiasi, ina maana umemtukana mwenyezi MUNGU, umemwambia shetani wewe uko juu MUNGU si kitu. Ninakueleza kama ulikuwa hujui, ndio maana ninapiga kelele kutetea Injili, watu mfunguke MUNGU asitukanwe tena, Neno lake lifuatwe. Vile vile hata katika mahakama, sheria na katiba mtu anapovunja tayari ameenda kinyume na mpango wa MUNGU. Sasa sadaka leo hii majina, risiti, ni tayari katiba ya mwnyezi MUNGU imevunjwa. Sasa malipo ni ule mwisho utayapata na wengine wataanza kupigwa sasa hivi, na tayari wamekwisha kuanza.
BWANA YESU asifiwe. Watoto wa MUNGU, mtumishi sio mnyang’anyi sasa jina la mtumishi linaharibika kwa sababu ya nini? Sababu ya utapeli. Nyie wenyewe ni mashahidi mmechoka, sasa hivi kila kitu ni habari ya pesa, kama ni habari ya pesa ndio njia ya unyang’anyi. Anasema mlango wa nje; wewe ulifikiri mlango wa nje utafunguliwa uone wapi? YESU akasema ni wanyang’aniyi hao. Sasa na wewe uwe makini, siku ya leo ukapate kufunguka, usiitwe mnyang’anyi. Kama unampenda MUNGU, achana na hayo. BWANA YESU asifiwe. Wanyang’anyi wanakuwa na mabenki ya kanisa, kanisa halitakiwi kuchaji riba. Mwenyezi MUNGU hachaji riba; amekwisha kukataa riba. Sasa kama wamemwibia jina la MUNGU wakaingiza kuchaji riba, wamemsaliti MUNGU, wamemchukia MUNGU, lakini wanasema BWANA akae na wewe; wapi? Chunguza matendo yao ni namna gani wanavyokwenda. Hapo ndipo utaelewa tofauti ya mtumishi na mnyang’anyi. Nimekuja nikufundishe; wanyang’anyi siku zote wanavunja katiba ya Neno la MUNGU lakini kwa kivuli cha utumishi; wanabatiza ubatizo wa maji ya kikombe, wanabariki watu wazima, wanabatiza watoto wadogo, wameongeza huduma ya sita ya Uaskofu. MUNGU alianzisha huduma tano, zimekuwa sita. Unaona unyang’anyi huo? Hao ndio wanyang’anyi. Jambo lingine wanavaa kofia wakati biblia inasema mwanaume asivae kofia wakati anapohubiri. BWANA YESU asifiwe. Sasa hao ndio wanyang’anyi lakini wanajiona mtumishi wa MUNGU.
BWANA YESU asifiwe. Jambo lingine mnyang’anyi hamjui MUNGU, wala MUNGU hajamuita, ila yeye amejiita, anatafuta maslahi yake. Mnyang’anyi anatoka kwa shetani, lakini hamtamjua akijisema hivyo utamjuaje? Chunguza matendo yake kuanzia sasa na ukishajua uondoke hapo. Haiwezekani mtumishi akubatize wewe kwa jina lake, amemnyang’anya BWANA YESU. Wewe ni wake. Sasa nikuulize; wewe ni wa mchungaji au ni wa mnyang’anyi? Na kama wewe ni wa mchungaji YESU, kwa nini umekubali kubatizwa kwa jina la mchungaji? Amenituma habari njema, kanisa sasa hivi limechakazwa. Hii ni dunia nzima, uwongo mtupu. Pamenuka, ni wizi. BWANA YESU asifiwe. Wanabaki kucheka serikali zina ufisadi, ufisadi uko kanisani ndio umeanza mizizi na ndio umestawi; na  yale matunda yakaingia kwa waumini, uovu unaendelea. Ninawaombea hata nchi mbalimbali muache ufisadi. Haya matawi ninayakata kwenye ulimwengu wa roho, kwa sababu ufisadi umeanza katika kanisa. Kanisa lingesema ukweli, watu wasingekuwa na ufisadi lakini ukiiba ndio unapendwa kanisani, ukiiba kwanza ndio unakumbatiwa kanisani kuleta pesa, na zaidi unakuta hata mchungaji na yeye anaingia huko. Sasa ni mchungaji wapi? Huyo ni mnyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe. Watoto wa MUNGU mpaka sasa mmepata picha na kuelewa mtumishi ni yupi na mnyang’ani ni yupi. Haleluya.. Anapokuwa anaeleza habari za watu huyo ni mnyang’anyi, hiyo ni dalili ya kwanza kwamba ni mnyang’anyi. BWANA YESU asifiwe. Ukikuta kanisa kuna kikapu cha mama mchungaji, baba mchungaji cha sadaka yake, hao ni wanyang’anyi. Wamemnyang’anya MUNGU. Kwanza biblia haijaruhusu kuwe na kikapu cha baba mchungaji au mama mchungaji. Kikapu ni kimoja tu peke yake cha sadaka. Na zaidi ukiona kanisani mtumishi (anajiita mtumishi huyo ni mnyang’anyi) anakasirika kabisa watu hawatoi mpaka anataka kulia, huyo ni mnyang’anyi amekikosa alichokuwa anakitafuta, sio mtumishi au ukikuta mtumishi anaangalia anachagua sadaka, anachukua noti, hizo za coin (sarafu) anazipiga kikapu huko, au anawaambia ndizo hizo mnamtolea MUNGU? Ninawaambia hivi, MUNGU kwake hakuna sadaka kubwa wala ndogo, ni ajabu sana hata ukisikia mtu anaombea sadaka, anasema MUNGU awabariki wale waliotoa kidogo na wale waliotoa nyingi; nawaeleza hao ni wanyang’anyi. Sadaka wewe unapotoa ndugu mtazamaji, unampa huyo mchungaji au unampa MUNGU? Nikuulize swali, MUNGU amesema ni ndogo au ni nyingi? MUNGU ndiye anayejua. Kwa MUNGU kila kitu; sadaka ni ya kwake lakini wanaanza kutengeneza mazingira aliyetoa ndogo na kubwa; ni wanyang’anyi.

BWANA YESU asifiwe, Haleluya; ni wakati wa kuelewa maana jina la utumishi limeoza. Sasa si utumishi, nimeamua kupasua katikati, kutenganisha utumishi na unyang’anyi. Na zaidi utaingia katika website www.prophethebro.orghalafu ingia katika blog pale, BWANA YESU asifiwe. Utakuta somo lililoelezea zaidi la unyang’anyi kwa hiyo utamjua mtumishi na mnyang’anyi. Na kwa kupitia somo hili ukirudisha picha yako katika maisha yako, utajiona mara nyingi umehudumiwa na wanyang’anyi. Na mnyang’anyi haji ili kubariki, anakuja ili kuiba anakufanya uwe kitegauchumi kampuni yake, kukutumikisha kama vile punda wako unavyompa kubeba mizigo ya maji akupelekee. BWANA YESU asifiwe, ndivyo unavyofanywa mwana wa MUNGU. Amenituma BWANA YESU niwaeleze habari yake kwamba msikubali kuongozwa na wanyang’anyi, wanapita mlango mwingine. Mlango mwingine ni maneno yanayotoka kwenye biblia mengine, BWANA YESU asifiwe, halafu wanatumia jina la YESU. Mtawajuaje? Kwa matendo.

[ad_2]