MAHUBIRI KWA NJIA YA REDIO KUHUSU JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI

[ad_1]

Nashukuru sana MUNGU akubariki. Napenda kuomba kumshukuru MUNGU kwanza kwa ajili ya muda huu.
“BABA yangu na MUNGU wangu uketiye mahali pa juu asante kwaajili ya watangazaji wa redio hii ,asante kwaajili ya kila mmoja anayesikiliza muda huu maana wewe MUNGU umempa kibali hicho. Baba nitumie upendavyo kwaajili ya ujumbe ule ulionipa kwaajili ya kanisa la ulimwengu mzima. Baba ninafungua masikio ya kila mmoja akapate kusikia.  Ninatuma Malaika wako wakawakusanye watu wako wakapate kukusikiliza wewe wala wasisikilize kama kuniangalia mimi bali MUNGU nitumie upendavyo. Ni kwa utukufu wako sifa nakurudishia wewe  AMEN.”
BWANA YESU asifiwe ndugu msikilizaji mahali popote  nchi yote, mkoa wote, wilaya yote uliyopo wa kanisa lolote, mpagani mwislamu leo hii niko mbele yako kukuletea ujumbe ambao YESU ameniagiza kuwaeleza kanisa lake na kuwaeleza watu wake wote wa ulimwengu mzimaa. Aliniita nilivyokuwa Serengeti katika kazi yangu ya u’DRIVER GUIDE akanirudisha Arusha akaniambia nakutuma nahitaji mwili wako uende ukaeleze haya yote ninayokueleza maana moyo wangu unauma na MUNGU amehuzunika kwasababu ya mambo mabaya yanayofanyika kwenye makanisa, mambo mabaya yanayofanyika na watumishi wamemsaliti wakaenda kunyume nay eye alivyowaagiza. Nikamwambia “Baba nitumie lakini mimi siwezi.” Akaniambia nahitaji mwili wako tu wala usiogope nimekushika mkono hata Paulo nilimuita hivyohivyo na wewe ndivyo hivyohivyo na zaidi na zaidi nitakutumia. Sasaivi ni wakati wa wa kuupindua ulimwengu wote ubadilike uniridie mimi YESU maana sasa nakaribia kuja wakati wowote na kanisa limetekwa na shetani. Akaniambia 2% ya kanisa ulimwengu mzima ndio iko na yeye,98% hayupo watu wanapiga kelele tu wakijua wanamwimbia YESU na kumwabudu YESU lakini YESU haonekani makanisani.
Ndugu msikilizaji kwa siku ya leo penda embu chukua kitabu chako utafungua Injili ya Marko mtakatifu 11:15-17 nami nasoma;Wakafika Yerusalemu nae akaingia ndani ya hekalu akaanza kuwafukuza wale waliokua wakiuza na kununua ndani ya hekalu akazipindua meza za wabadili fedha na viti vyao wauzao njiwa wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya kati ya hekalu akafundisha akisema, je; haikuandikwa nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe. YESU alinipa na ujumbe huu wakati akiwa ananifundisha na kunieleza hili jambo alikwisha kulifanya enzi hizo akiwa katika ulimwengu huu kabla hajapaa kwenda kwa baba yake. Akaniambia, nyumba yangu ni nyumba ya sala, sasa hivi imekuwa sio nyumba ya sala, imebadilishwa kama vilevile nilivyokataa na ndio maana sionekani makanisani. Watu wanalia, wanakata tama, wanazunguka na kutoa machozi wakifikiri kwamba mimi YESU nimewaacha. Mimi YESU ninawapenda, tatizo wamekuwepo mafarisayo na masadukayo, tena wameibadilisha injili yangu na kufuata yale ambayo ni ya adui.
BWANA YESU asifiwe. Ndugu msikilizaji ninakutia moyo usiogope, maana unakwenda kufunguliwa siku ya leo hata kama ni mtumishi uliyepo katika madhabahu nyingine yoyote, yawezekana mwingine umerithi kutoka kwa baba wa kiroho, ambao walikwisha kutekwa na shetani. Watu wamekuwa wakijiona kwamba wamesimama na YESU, kumbe wamekwisha kutekwa na shetani. Shetani ameingiza tekniki (technique) ndani ya makanisa, amewaingizia roho ya kupenda fedha, amewaingizia roho ya kufanya kanisa la MUNGU kuwa nyumba ya biashara, sasa hivi YESU  haonekani makanisani. Tukija katika Injili ya Neno la MUNGU tulilosoma hapa katika kitabu cha Marko, YESU alivyoingia hekaluni, aliwakuta wafanyabiashara akawafukuza lakini leo hii wameyarudisha. Na baada ya kufukuza ukiendelea kusoma mistari ya chini unaona watu walimfuata wakaenda kupokea uponyaji. Leo hii YESU hayupo kabisa maeneo hayo, na ameniambia niwaeleze ulimwengu mzima, atakayesikia asikie, atakayekasirika akasirike, lakini ni BWANA amesema. Imechosha, imechosha jina lake kutukanwa. Watumishi wamekuwa wakitumia jina lake kunyang’anya magari, kunyang’anya fedha, watu wa MUNGU wamekuwa wakiteseka, wanafunga na kuomba na kulia; majibu hakuna. YESU anasema leo hii, anakufungua mahali hapo hapo ulipo katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI maana wamekuwa na mioyo migumu, wamekataa kuacha kupenda fedha, wamebadililika, japo fedha ni nzuri; sio zenyewe zikumiliki katika jina la YESU. Wamefanya kazi ya MUNGU kuwa ni mradi na wewe hata kondoo zake BWANA YESU ameniambia wamekuwa wakinyang’anywa mali, wkainyang’anywa fedha wakijua wanamtolea MUNGU. Watumishi wamekuwa wakitumia jina lake kusema, BWANA amesema toa, akaniambia, mimi ndiye director wa kanisa. Je; mimi ni masikini? Nimekwesha kusema, nimewapa bure, mtoe bure. Kwa nini mnawaambia wanangu watoe pesa ndio muwaombee? Akaniambia MUNGU hutoa bure, shetani lazima ulipe.
BWANA YESU asifiwe. Najua wako wengi wamekwisha kuumia sana, lakini umefika wakati sasa ni mwisho. Ameniambia YESU ulimwengu mzima, mlioko Canada, mlioko China, mlioko Malaysia, wote na nchi zote lazima mnasikia. Huko ni mnaenda kufunguliwa. Iwe ni mtumishi yeyote unayetaka kuponywa, siku ya leo unaenda kuponywa na ubadilike. YESU amekataa, mwisho wake unakuja, mtachomwa kama moto. Mmefanya YESU amebaki asilimia mbili (2%), asilimia tisini na nane (98%) shetani ndiye amekamata kanisa.
BWANA YESU asifiwe. Ni mambo ya kutisha, ni mambo ya kutia aibu. MUNGU anasema watumishi wanamdharau, ameanza nao vizuri, na amewaita wamefika mbele wamekengeuka. Akaniambia sema kila ninachokuambia. Ole wake atakayekugusa, mimi niko na wewe katika jina la YESU KRISTO wa Nazareti. BWANA YESU asifiwe. Akanifunulia tena, akaniambia; Paulo nilivyomuita, nilimtuma na yeye hivi hivi. Alikuta wameenda kubadilisha injili, injili ambayo niliwaambia wameenda kuipindisha pindisha yale niliyoyaagiza wamekataa. Ukisoma katika kitabu cha Wagalatia 1:6-8, Injili imebadilishwa kabisa kabisa na mpango wa YESU aliouacha maana yeye ndiye kiongozi wa kanisa. Kanisa limevamiwa, na shetani amewaingizia watumishi, watumishi wamekuwa kama taahira, hawajui wengine wanafanya nini, japo kuna wengine wanakwenda kuzimu. Ila wanaokwenda kuzimu, BWANA YESU mwezi uliopita aliniambia kwa kuomba nifunge njia zote za kuzimu kule wanakokwenda kuchukua maana baba yao lusifa alikwishakufungwa na mtumishi ambaye MUNGU alikwisha kumuandaa wakati wa nyuma ila na yeye alikataa kumsikiliza, MUNGU akamuweka pembeni. Sasa hivi MUNGU anakwenda na wanaokwenda, maana YESU anarudi kulichukua kanisa lake, na shetani amechukua wengi hata hii asilimia mbili (2%) iliyobakia anataka izidi kupungua, azidi kuichukua ili achukue ulimwengu wote. YESU amesema, hapana, hapana. Mawe yatazungumza, anga litazungumza, ardhi itazungumza, miti itazungumza, viumbe vyote vitazungumza kwa ajili ya yeye.
 BWANA YESU asifiwe. Ujumbe huu YESU alionipa, alivyonieleza nililia sana, maana na mimi nilikuwa sijui wala kuelewa. Ni vitu vya kutisha. Kimwili binadamu ukitembea nje, utafikiri watu kweli wanamwabudu YESU, lakini mioyoni mwao hamna. Viongozi wametekwa asilimia kubwa ulimwengu mzima, na wengine hawajijui wala hawajielewi. Mambo aliyoniambia ni mengi sana zaidi ya elfu moja na hata hapa sasaivi kuna kitabu ambacho amenipa maagizo nikiandike kwa ujumbe ule alionieleza. Kitabu chenyewe kiko madukani sasaivi kikotayari. Ujumbe wake juu ya kichwa cha habari ‘JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI.’ Sasa YESU analitaka kanisa lake. Nyie aliowatuma mmemsaliti. Kumsaliti mnalitaja jina lake lakini  hamtendi yale ambayo anayataka yeye YESU. Sasa kama hamyatendi yale ambayo ameyaagiza  YESU ,hayo mnayoyatenda ni ya nani? Jibu ni ya shetani. Unamtumikia shetani kwasababu unafanya ya shetani.
Kitu cha kwanza watu na wanaoamini kanisani, wamekamatwa katika sadaka sasaivi ni habari ya sadaka tu. Toa toa tu, toa toa tu, sawa kutoa ni kuzuri ; akaniambia mwanangu  sadaka ni ibada ya mtu mwenyewe na mimi peke yangu. Lakini sasaivi sadaka mtu anaambiwa aandike jina lake kwenye sadaka ya fungu la kumi na aandike mpaka namba ya simu na kiasi.  Kwani mimi MUNGU ninahitaji simu ya kuangalia na kumpigia simu aminitolea kiasi gani? Akaniambia huyu ni shetani. BWANA YESU asifiwe. Akaniambia katika maandiko imeandikwa kwamba wakati unanitolea sadaka yako ficha hata kulia na kushoto isijue. Je;nyie watumishi haya yametoka wapi? Akaniambia waeleze,waeleze. Mimi ndio mtumishi mkuu(ndio YESU) na mimi ninakaa ndani ya mtumishi ambaye namuongoza mimi. Nikiwa ndani yake yale niliyoyakataa  na aliyoyakataa baba yangu MUNGU  hayawezi kufanywa kanisani.
BWANA YESU  asifiwe. Ni mambo ya kutia aibu. akaniambia waambie huu ujumbe ni kwaajili ya watu wote mimi YESU sitafuti pesa ya mtu wala mimi sio masikini ninyang’anye watu mali zao. Maana jina langu linatukanwa na mimi sasaivi kanisani nimeitwa mnyang’anyi. Jina langu linatukanwa. Lakini YESU ananiambia yeye hahusiki huko ni hao na mambo yao wameyapata hukohuko. Nimewaonya, nimewakataza wamekataa. Akaniambia na ujumbe huu ninaokupa wapo ambao niliwapa wapeleke, nimesema nao lakini wamekataa; wamekuwa kichwa ngumu, wamekataa kabisa kusema, wamekataa kusema wameukalia. Watu  wanazidi kuteseka shetani anazidi kulipiga kanisakama anavyolipiga sasahivi;amelipiga mpaka kanisa limechoka, direction hakuna, watu wameanza mpaka kutafuta majini muhubiri,jinni maono ndio wamekuwa nayo, mwisho wao umefika. YESU amesema watubu kinyume cha hapo wataangamia. MUNGU amekasirika kabisa amechukia;ni ulimwengu mzima mabara yote. Na akaniambia Tanzania ndio EDEN,anaanzia Tanzania. Mwanangu usifikirie pesa utatoa wapi,mimi baba yako nitaleta pesa na kila kitu cha kukuongoza,nahitaji mwili wako tu. Hata sasaivi usione ni Hebron anazungumza ni MUNGU mwenyewe anapita kwenye kinywa kukueleza ujumbe wake. Wewe uliyeumia na majeraha leo MUNGU anakwenda kuyatengeneza, majibu ambayo ulikua huyapati leo unakwenda kuyapata live, live na ni bure.
BWANA YESU asifiwe. Oh! Inatia huruma sana. Leo nilivyokua nyumbani kwangu akaniambia katika watumishi mia moja(100), wawili  tu ndio wasafi. Sasa tunakwenda wapi? Kanisa lirudi sasa lijipange upya. Upendo umeondoka makanisani wenye pesa ndio wanapendwa wasio na pesa hawaangaliwi. Akasema yeye ni MUNGU anawapenda wote. Mahali penye madhabahu kama hiyo amesema hiyo madhabahu imekufa na ambayo inachangisha watu ela kanisani hayupo;amesema watumishi wamuulize yeye pesa. Amesema wapige magoti yeye atazileta, si kuwakamat akondoo zake. Kondoo wamekamatwa na kukamatwa matokea yake hawabarikiwi wala hawainuliwi. Umaskini unazidi shida zinazidi na mimi katika neno langu  katika Malaki 4 “ukininyooshea na kunitolea nitakuinua” Kwanini hunyanyuliwi? Mimi MUNGU ni muongo? Tatizo liko kwenye kanisa; wana wa MUNGU tuombe kanisa liko kwenye tatizo. Kweli imeondoka kabisa, watu wanapakana mafuta BWANA atafanya. Unaambiwa nenda na neema ya MUNGU ikuongoze  matokeo yake ni nuksi balaa na mikosi. Sasa YESU analikamata kanisa , analibadilisha ukubali usikubali. Wewe un ayeenda chini nakwambia sasaiva malaika wanakuteketeza. Kazi zote zimefungwa katika jina  la YESU. Hakuna amani kwa wabaya ,wabaya ni washirikina wote , wabaya wanaongozwa na shetani. MUNGU amekuumba wewe kwa sura ili umtumikie, ili umwabudu  yeye lakini leo unamwabudu shetani . je; hujapotea? Ziko namna nyingi sana ndugu msikilizaji ninitaendelea kukuelezea na vitabu nitaendelea kuvitoa anavyonielekeza MUNGU ili nikufikishie ujumbe wewe. Hata ukusema kuandika siwezi inabida sasa niseme vile vinavyoshuka  maana ni vingi na ni mazito  na ni makubwa. Shetani ameukamata ulimwengu, YESU anawahitaji, YESU  anakuhitaji. Wewe uliyekuwa umekata tama, na kuona kwamba YESU hayupo, YESU yupo nakuambia. Ameniambia watumishi wamemsaliti. Mtu yeyote anayefanya kazi ya MUNGU kwenda kinyume na YESU, huyo anamsaliti. YESU alisema kwanza, nyumba yake ni nyumba ya sala lakini angalia leo nii nyumba yake ni sehemu ya kukusanyia hela tu. Nyumba yake leo hii ni mahali pa michango, nyumba yake leo hii ili uambiwe neno ubarikiwe unaambiwa utoe hela. Je, YESU anahitaji hela yako ili akubariki? YESU hubariki bure bure. Ukipenda kumtolea MUNGU mtolee bure, usiogope mtu. Nimekuambia muangalie MUNGU wewe ni wa wa thamani sana, wala pesa yako usimruhusu aizoee zoee mmefanywa ATM machines. MUNGU amekasirika, umasikini umezidi, umasikini unaingia mpaka kwenye vitanda. Leo ni mwisho wewe unaesikiliza ufunguke ufahamu maana hata wengine mnasikiliza mpo mia saba ishirini (720) sasa hivi nyie watumishi mnanisikiliza na mnaniona, mnaumwa matumbo, omba toba maana unaijua kweli MUNGU hakutuma kazi hiyo. MUNGU anabaki kuwa wa rehema pale pale.
Mtumishi wa MUNGU; ndugu msikilizaji anaposimama kuhubiri uwe makini sana. Manabii wa uwongo wamejaa. Mtu yeyote anayesema kinyume cha neno la MUNGU kanisani ni nabii wa uwongo. Sio mpaka aende kuzimu, ile kufundisha tu kinyume na mapenzi ya MUNGU . Oooh MUNGU tusaidie, saidia ulimwengu wote, ufungue BWANA YESU, fungua kila mmoja, fungua wanaosikiliza, ondoa majeraha kwa kila mmoja, ondoa BABA yangu. Hata wale waliopotea wamekata tamaa sasa hivi ni watumishi wako wanaonyanyaswa, wamenyang’anywa na huduma zao kwa kutumia nguvu za kipepo. Malaika wafanye kazi akiwepo malaika Mikaeli wafyekefyeke na kuwarejeshea vitu vyao. Wasio na nyota warudishiwe maana wengine ni misukule, hawana nyota, wanazurura tu na kanisani asubuhi, mchana na jioni ni kuomba, kuomba, suruali zimetoboka, mapigo kila mahali. MUNGU aonekane, MUNGU yupo kuanzia siku ya leo. Wewe uliyemsikiliza ninakuambia mwana wa MUNGU utaona mabadiliko. Usiangalie jina kubwa la mtu anayehubiri wa siku nyingi. Kama ana MUNGU sikiliza. Kama hana MUNGU achana naye. Macho ya rohoni watu mmevunjwa vunjwa, YESU anawarejeshea macho yenu.
YESU akaniambia, mtumishi wangu ninakupenda, sio kwamba ninawachukia hao, ninawapenda. Upendo wangu uko pale pale, ila mpaka atakayetubu kwa sababu wamefanyika kuwa geti la kuziba wengine wasinione mimi, lakini ninakutumia kama chombo, napeleka ujumbe wangu mwenyewe. Lazima wafunguliwe na akaniambia sasa hivi watu idadi kubwa ndio nahitaji iingie Kaanani. Na anakwenda kutumia watumishi wale waliodharauliwa na kukataliwa. Ndio anakwenda kuwatumia kwa kiwango kikubwa sana na atawatumia kwa namna isiyo ya kawaida. Ambao hawajawahi kuonekana hapa ulimwenguni akaniambia, sasa hivi najua mnasubiri ujio wangu, na neno langu linasema utukufu wa kanisa la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza; lakini je; angalia utukufu wangu ni mkubwa au kanisa ndio limeangamia? Akaniambia kanisa limeangamia, nashindwa kushuka; nitashukia wapi? Watu wanafikiri niko kwenye mavinanda tu. Wako watumishi waliojificha mpaka kwenye migombani. Nasema nao hawasikilizi, wanapigwa lakini sasa yatosha wanakwenda kuaibika. Na MUNGU anakwenda kuwanyang’anya. Ananyanyua watumishi wengine ili kazi yake iende. Mmekuwa sugu, ni wizi tu kanisani, akaniambia; mimi YESU enzi zangu nikiwa ninahubiri hapa ulimwenguni, nilishaanza kuwaambia watu nipe gari lako, nipe nyumba yako, mimi ni masikini? Akasema, wanangu wananipenda sana, wakisikia jina langu wanatetemeka  wakijua wananitetea mimi kumbe hawanitetei mimi. Akaniambia, wengine wameongeza ‘toa mpaka ikuume’watu wanatoa mpaka wanauza vitu vya nyumba, mpaka wanalala chini. Matokeo yake hawapati kitu. Siletewi mimi, wala mimi siagizi vitu vya namna hiyo. Kaini na Abeli waliponitolea, Abeli alinitolea kwa roho ya upendo na furaha sana na amani, bila kuuma. Lakini Kaini moyo wake ulikuwa unauma. Mimi sipokei sadaka za moyo kuuma. Akaniambia, mafungu ya kumi watu wanaambiwa andika namba ya simu halafu anawekwa kwenye attendance, mwisho wa mwezi usipotoa shetani anaingia ndani ya mtumishi anakupigia simu anakuambia, “we mbona huonekani wewe, unajua umerudi nyuma sana kiroho?”. Mimi YESU siangalii pesa. Sadaka yako wewe mwana wa MUNGU ni siri yako kati yako wewe na MUNGU na ndio maana haineni unapoandika jina au upapowapa hao inanena kwao, thawabu yako imebaki hapohapo. Usiandike jina tena, ni mapinduzi YESU ameanza ulimwengu mzima ili wewe unyanyuliwe na uwe makini pia unapotoa. Kama hiyo madhabahu ni ya kuzimu, asilimia Fulani inaenda kuzimu ungine inabaki kwa huyo mtumishi, matokeo yake Baraka unazozipata ni za shetani; nuksi, balaa, mikosi na kufilisika. Lakini ukitoa mahali ambapo yeye yupo utainuliwa,  utabarikiwa na utaurithi uzima wa milele. Kataa kabisa hata nyie mnaokataa tena mshindwe kabisa katika jina la YESU. Ninawaona na kuwasikia. Mlizoea, kuzime imesikia, bab yenu amesikia na anakula bakora sasa hivi kuzimu na mtandao mzima wa watumishi wanaokwenda kuzimu ulimwengu mzima, malaika Mikael kamata teketeza. MUNGU amekasirika. Imefika mahali mnamchezea MUNGU ni wakati sasa wa BWANA YESU kudhihirika ulimwengu mzima.
Nakurudisha katika habari aliyoniambia. Akaniambia wako watumishi wanavaa nguo, zile nguo wanapozivaa anakupangia wewe utakayesaini kwenye mikono au kichwa utatoa milioni. Nyie ambao wa elfu kumi kumi mtasaini miguuni. Mwana wa MUNGU, akaniambia BWANA YESU, mimi YESU niliwahi kufanya kitu kama hicho? Hicho kimetoka wapi? Wengine wanamtupia hela hata mpaka miguuni wanamwambia hizo ndio za kwake za kula. Mimi niliwaambia; wasisumbukie watakula nini, watavaa nini. Je, mimi ni masikini? Maua ninayanyeshea maji, ndege wa angani wanakula. Je, niliyemuumba kwa sura yangu si zaidi? Funguka mwana wa MUNGU, funguka watumishi hao wametekwa, n wengine sio kwamba wametekwa, wanajijua kabisa. Sadaka ya kweli ni funfu la kumi nay a shukrani na kumtolea MUNGU mtu asikupangie, mambo ya sadaka sijui za majengo amekataa. Sijui za Injili amekataa. Amesema pesa zote zipangiwe kazi yake. Haya matabaka-tabaka hizo nyingine zinakwenda wapi?
BWANA YESU asifiwe. Sikiliza mwana wa MUNGU, YESU amekataa ili akunyanyue, ili akuinue. Endelea  kukaa kwenye redio yako. Chochote kilichopungua ndani yako, leo utarudishiwa, balaa zote na mikosi zinaenda kufutwa juu yako na utakuwa huru sasa. Akaniambia, leo hii mimi nimesema kwamba mimi ndio kiongozi wa kanisa, director. Nawaambia msikope, si kanisa lisikope? Akaniambia ni machukizo matupu. Leo hii kanisa linakwenda benki. Likipelekwa jina langu kanisa si inajulikana ni mimi YESU? Wanapeleka proposal wanakopa hela kwa ajili ya kunijengea eti mimi jengo. Mimi MUNGU masikini? Wakati nimekwisha kusema msikope, wala msilipe riba kanisani. Mnaambiwa mchange hela kwa ajili ya kulipa deni la kanisa, eti mimi nikalipe riba? Ina maana nyie mnapoenda kutoa mimi YESU ninakwenda kulipa riba. Mimi sipo hapo, sipo uliyekuwa unafanya hivyo umeliwa. Ulimwengu mzima hata mliopo Japan, badilikeni. MUNGU amekasirika. Mambo yote hayo mikopo kazi aliyoituma YESU kwa watumishi wake ni kuponya roho watu sasa hivi kanisa lina-deal na mahoteli, lina-deal na ma-saccos, ndio kazi YESU ametuma hiyo? YESU amewapa watu muwaombee wakafanye kazi hizo na wataleta kanisani.
BWANA YESU asifiwe. Kingine alichoniambia, sasa hivi kuna watumishi wanaenda kwenye hizo nchi wanazozijua wao. Wanajua ubatizo ni kiapo changu mimi na mtu, lakini wao nanabatiza kwa majina yao. Mfano labda mtumishi anaitwa Ndoo, anakuita, anakubatiza kuanzia leo ninakuita  ninakubatiza kwa jina la Ndoo. Wewe ni wa kwangu. Watu wamenyang’anywa, YESU hakupati wewe uliyebatizwa kwa jina la mtu mtafute mtumishi anayeongozwa na ROHO wa MUNGU akubatize tena na kufuta hilo agano. Ikishindikana, njoo Moshono, nitakufungua. BWANA YESU asifiwe. Akaniambia, waeleze wanangu, watumishi wengine wamebadilika, wanachukua picha na pesa za waumini wanachimba pale madhabahuni wanafukia. Akaniambia, waambie wanazikwa hapo. Hawatakaa wanione wala kufanikiwa kiroho, ni kurudi nyuma, wanakuwa watumwa wa yule yule mtumishi. Sasa YESU anasema, mtu wake ndio yuko namna hiyo? YESU aliyafanya hayo? Alichukua picha zenu akafukia chini? YESU aliwafungia mashida na balaa na mikosi? Watu wengine wamekata tamaa, wameingia mpaka kwenye wokovu wanataka kuacha wokovu maana tangu wameingia ndio mambo yamebadilika kuwa mabaya zaidi. Watumishi 45% ni washirikina ulimwngu mzima lakini wanalitaja jina la YESU. YEU akasema, siku ile ya mwisho nitakuambia sikujui, sikujui. Oooh! Tulitoa pepo kwa jina lako,… sikujui. Iko siri kubwa sana hapo mwana wa MUNGU. Akaniambia, hapa Tanzania nina watumishi wangu nilianza nao, tena alikuwa anawatumia mpaka akina malaika Mikael anakaa nao, wengine alianza nao hata katika biashara zao za kuuza maandazi na wengine katika hali Fulani mpaka amewanyanyua. Ilikuwa ni jambo la kutisha maana ukisikia YESU, YESU kweli yupo. YESU anaongea na watu na YESU anashuka. Akaniambia, hasira yangu nikishuka mimi kama mimi, nchi yote, milima itasambaa, hakuna kitakachobaki lakini ninatumia mwili wako mimi nitashuka kwa mwili wangu ule mwisho. Nenda niandalie kanisa. Usijidharau ulivyo, niangalie mimi.
Japo utasemwa sana, usijali hata mimi nilisemwa, utazushiwa maneno, tena furahi sana kama mimi nilivyofurahi maana ndio unanyanyuliwa. Kama huna kitu cha MUNGU hufuatwi na na wanaokufuata ni shetani yupo ndani yao. Hata mimi mafarisayo si walinifuata japo walikuwa wanamuomba MUNGU? Ni MUNGU yupi anipinge mimi. Ndugu msikilizaji, ninakuomba na ninakusihi rejea kwa BWANA YESU, uliyekata tama, wengine mmepigwa na watumishi, wengine BWANA YESU akaniambia mnaenda makanisani wanawake, wachungaji au wale viongozi wanawaangusha kiuzinzi wanawaambia bwana amesema. Akaniambia, mimi ninakaa ndani ya mtumishi. Je, mimi nafanya uzinzi? Mengine akaniambia mwenye pesa sasa hata akifanya uzinzi hagombezwi, lakini asiye na pesa hafanyi kitu, atatangazwa kila mahali. Je, mimi ni MUNGU wa namna hiyo? Mimi ni MUNGU wa haki. Rudi kanitumikie. Nikamuuliza, nitapata wapi pesa, akaniambia, habari ya pesa achana nayo. Usifikiri, niulize mimi ndiyo director wa pesa. Nitakuletea watu, na watu nawaleta mwenyewe. Kusi na kasi italeta, niangalie mimi. Anza Tanzania, utaingia Rwanda, utaingia Uganda. Akaniambia, na wanafunzi nitakaokuwa nao atawatumia kwa kiwango kikubwa sana; usiende shule ya aina yoyote. Nilizuia hata elimu yako ulivyokuwa mdogo kupelekwa Marekani, nilizuia mimi. Nilikuwa nikimkasirikia baba yangu kwa nini hanipeleki chuo, au shule; nilirudi na kuomba rehema, kumbe ni YESU aliniambia mwenyewe alizuia maana wangesema nimesoma mahali fulani. Utukufu wangu sishirikiani na mtu.
Ndugu msikilizaji, ni mengi sana na katika vipindi vingine kutakuwa na na vipindi kwa ajili ya kuwaombea laivu (live) kwa simu na unafunguliwa hapohapo. Haijalishi umekaa wapi, hata kwenye msitu, utatolewa, YESU anashuka sasa kuwatoa watoto wake. Umekuwa ukizurura, huna makao, YESU atakulisha kama kunguru anavyodondosha mkate. Ni wakati wa kweli.
Ndugu msikilizaji, mrudie YESU umwangalie BWANA YESU. Na wewe unayempenda YESU,  endelea kumpenda BWANA YESU. Nina kitabu ambacho tayari nimeshaki-register, kiko sawasawa, utakipata madukani. Kichwa cha habari cha kitabu hicho “JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI”. Utayakuta mengi, mengi japo kuna mengine mengi mengi. Ni wewe meletewa ujumbe na YESU upate kuelewa. Injili yangu sio ya kibinadamu, mimi sikuitwa na mwanadamu. Paulo aliitwa na MUNGU alileta ya ki-MUNGU vile vile. Haya ninayokueleza unaweza ukashangaa, aliniambia, wewe ndio mtu wa pili kwenda kupeleka habari hizi laivu (live) sasa baada ya mimi kuzisema wakati huo. Niliowatuma wamekataa, wameogopa lakini mimi niko na wewe milele na milele. Wasaidie watu wote, wapende, wafungue, wasaidie, japo wapo ambao watakuja kwa ajili ya kunisanifu, ameniambia atanionyesha. Kwa hiyo ukija kwa ajili ya kunisanifu sikuhudumii.
BWANA YESU asifiwe. BWANA YESU atusaidie. Akaniambia, watumishi wengi wameenda kuharibikia kwenye mabara ya  ulaya. Wameanza vizuri, hapo wakienda ulaya wanavalishwa majoho ya vyama fulani vya freemason wanapewa pesa nyingi sana kwenye account zao zinatisha na mpaka nchi ya Tanzania imeingia kwenye mateso; kanisa halijakaa mahali pake. Nchi itaponywaje sasa? lakini sasa hivi YESU ameikamata Tanzania, mtaona mabadiliko yasiyo ya kawaida sasa kuanzia serikali kila mahali. Elimu ya Watanzania iliibiwa, wanyama wa Tanzania waliibiwa uthamani wao hata watu, wageni wanakuja wanaiba vitu. Uchawi mtupu….  Airport zote hakuna tena madawa ya kulevya yatakayopita. Uchawi sasa hivi haufanyi haufanyi kazi. Hayo ni baadhi ya mambo tu YESU aliniambia.
Sasa YESU aliingia hekaluni akaykuta, leo wameyarudisha  na kama wameyarudisha ndugu msikilizaji, ninakuuliza, je, ni ya YESU au ni ya shetani? Jibu ni ya shetani. Haya wanayoyafanya ni ya YESU? Jibu sio ya YESU. BWANA YESU amekataa katu katu, na ili aonekane makanisani mambo hayo yaachwe majibu mtayaona na majibu ya YESU sio mpaka utoe hela ndio ujibiwe. Hao wanokuambia alikuja mtumishi mmoja akaniambia, sio mmoja, hata zaidi ya wane. Unataka umuoe yule? Haya ngoja nitaomba, halafu unipe kiwanja basi. Jamani, YESU yuko hivyo? Mwingine una madeni yako, anakuambia, ninaomba halafu ukisamehewa utanipa shilingi ngapi? YESU yuko hivyo? Ndio kanisa sasa limekuwa hivyo. Sasa sio kanisa, YESU amekaa pembeni na wako wengine watumishi ambao amewaandaa MUNGU anaenda kuwafungua ambao wanataka kusema kweli yake. Wamekuwa wakifungwa na kubaniwa na kukataliwa tena wanaitwa wana mapepo ya kuzimu na utambuzi. Nawaambia, wewe ni bora zaidi. MUNGU akuinue huko uliko, MUNGU akubariki. Mwangalie YESU. Mwangalie BWANA YESU. Mtegemee yeye peke yake. Mambo ya kuambiwa toa toa tu, YESU hakufanya hivyo, amekataa; kanisa limepoteza ramani, direction, ni dunia nzima manaosema Tanazania kwanini unasema hivi, ni dunia nzima mpaka wameona kanisa halina nguvu, wameona ni shetani tu ana nguvu. Kila kitu ni Nigeria tu, ni Nigeria tu. Mmeenda kuzimu. Manaona YESU hana hata pesa. YESU utukufu wake umerejea sasa. Na kanisa la mwisho ndio hili limerejea. Jina la huduma hii aliniambia kanisa langu liitwe YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, na ndivyo nimelifanya. Sibadilishi, sipunguzi, ninamheshimu YESU. Wewe unayemdharau, shauri yako. Moto unakusubiri.  Tafuta ushirika na YESU. Usiwe mnafiki, hata kama unakaa kanisani unanena, unanena unanena nini? Watu wana majini yananena. Kipindi kijacho nitaendelea kuelezea. Naomba niombe. Wewe ambaye hujaokoka nitakuongoza sala hii. Utengeneze maisha yako na YESU. Hata na wewe mtumishi.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe makosa yangu yote, niliyoyatenda kwa kujua au kwa kutokujua, nishike mkono BWANA YESU. Nitengeneze, nifungue fahamu zangu nikujue wewe YESU wa kweli. Nikujue wewe YESU wa kweli. Nimekutafuta sana, na sijakuona. Nishike mkono sasa.
BABA, asante kwa majina ya watoto wako, upige mhuri duniani na mbinguni, roho hizi zote zilizokusikiliza, watengeneze, wakumbatie. Usimwache hata mmoja aliyekusikiliza, nakuomba aurithi ufalme wa mbinguni. Napiga muhuri duniani na mbinguni, BABA yangu na MUNGU wangu, nakuomba, nakurudishia sifa na utukufu. Kwa nyie wagonjwa, ninatuma malaika, mahali popote unapoumwa ninatuma malaika waende wakarejeshe wengi wamekuwa makaburini, nyota zenu, fahamu zenu. Mliofichwa kwenye makanisa ya kipepo nawachomoa, akili zenu, fahamu zenu, baraka zenu, uthamani wenu, ndoa zilizofungiwa kwa waganga, kwa wachawi mpaka kwa lusifa mliowekwa malaika Mikael nenda na kikosi chako kila mahali kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Mabara yote waliowekwa makaburini, baharini watolewe wote. Nyota zao kwenye maduka, kwenye maviwanda, dunia nzima kwenye milima kule upareni Same mtolewe wote kwa jina la YESU. Mliochukua nyota za watu, vyeo vya watu dunia nzima, serikali ya aina yoyote mnaotumia uchawi ninauharibu kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Ninaharibu mipango yenu yote. Ninawateketeza na YESU amekwishawashikilia wote mnaoteswa; mwisho wa kuteswa. Yeyote anayekupeleka kwa mganga malaika kamata, teketeza na hakuna uganga utakaofanyika na uchawi juu ya mtu yeyote. Maisha yaliyokwama, kukata tama na wewe unayetaka kujiua hakuna kujiua katika jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Roho za mauti, pepo la ukimwi, cancer, asthma toka katika jina la YESU. Nyie mliowapata waume na wanawake kwa kwenda kwa waganga ninafuta hizo ndoa katika jina la YESU. Na makanisa yaliyopitisha hizo ndoa, YESU hahusiki kupitisha ndoa za kipepo katika jina la YESU. Kanisa limepigwa upofu, lishindwe katika jina la YESU. Ndio maana ndoa ni shida, balaa na mikosi na watumishi wanasema BWANA amefanya. BWANA hajafanya. YESU hashirikiani na kanisa la kipepo. YESU hashirikiani na mtu anayenda kwa waganga, ninafuta katika jina la YESU. Na nyie wanawake mnaowaloga waume zenu, kuwakamata waume wa watu waachilieni mara moja dunia nzima. Hakuna lolote litafanyika katika jina la YESU. Mnaopanga kuua watu  na kufukia ndani ndani mpate madini watu wote wale natuma malaika wakatolewe waogeshwe kwa damu ya YESU waongozwe sala ya toba na malaika wa Injili, pelekwa Paradiso. Misukule mnaowekwa kwenye magari mtolewe wote kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Akili zenu zilizofukiwa ardhini umekuwa taahira hujielewi nakufungua kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Na wewe uliyepewa cheti cha ‘congratulation’ unatoa fungu la kumi, hilo kanisa limekuga katika jina la YESU na ndio maana matokeo yake haufanikiwi. Ati hongera unatoa fungu la kumi vizuri. YESU ametoka wapi kusema mambo hayo. YESU hakusifu. Hiyo ni saikolojia kutoka kwa shetani baba yao lusifa. Eti hongera; na wewe mtumishi unayechukua majina majina ya watu unasema unasoma, hawa wametoa fungu la kumi unawataja pale mbele wewe MUNGU amesema kulia wala kushoto isijue. Hayo unayoyazungumza yametoka wapi? Wacha, wacha katika jina la YESU. Utapeli mtupu kila mahali, wacha. Na usitishwe mtu yeyote unayesikiliza, usiogope tai, usiogope joho. Mwangalie YESU, kama hana YESU ndani yake ni mshanii chapa mwendo katika jina la YESU. Usiwe mtumwa, wewe ni mtumwa wa BWANA YESU.
BWANA YESU asifiwe. Kuna mtu mmoja, wewe ambaye umekaa mguu wako umepinda na mbele yako unaona sura ya mbwa hiyo sura ya mbwa ni pepo la uzinzi, ninaliondoa sasa hivi kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI na mguu wako ninaufungua unyooke moja kwa moja katika jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Wewe mwenye cancer ninaiondoa kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Ninakutamkia uzima, wewe mwenye uvimbe na utumbo ambao umeshonwa nyuzi zinaachia zinatoboa damu inatoka, ninakufunga kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Mliopangiwa kufa, wote mnaosikiliza ulimwengu mzima ninafuta hamna kufa kifo cha kipepo, utakufa kifo cha MUNGU tu peke yake, kifo anachotaka kwa wakati wake na kwa makusudi yake. Watu wengi wanateseka, kanisa limekosa mwelekeo. Mnaenda kwenye maombi, mnaomba Januari mpaka Desemba hakuna majibu; matokeo yake nguo zinatoboka, suruali zinatoboka BWANA hafanyi; hakuna, ni usanii tu. MUNGU ameniambia; MUNGU amekuambia nini? Wewe unayesema MUNGU amekuambia, wewe umejiona matawi ya juu eti una experience kwenye kazi ya MUNGU, Kazi ya MUNGU haina experience, anaifanya mwenyewe. Na nyie mnaotumia maandiko, maana akaniambia shetani anatumia Biblia. Nikamuuliza, sasa kwa nini anatumia Biblia? Akaniambia, shetani anaifahamu Biblia lakini anaitumia katika maandiko. Shetani hana NENO (udhihirisho). Neno linaponya, maandiko ni historia tu. Hata wengine wanaenda kwa waganga wanaambiwa ngoja nimuulize MUNGU nisome Biblia. Sasa jiulize, MUNGU anashirikiana na shetani? Hapana. Lakini shetani ni aina ya mungu na ndiye aliyeukamata ulimwengu lakini sasa mwisho wake. Unabaki kusema, Neno la MUNGU linasema mstari Fulani itakuwa hivi, nitabarikiwa, atatuponya. Hakuponyi, kwani kwanza hauna nafsi, hauna ufahamu au umezikwa.  Ni umasikini tu. Nyumba zenu zote malaika sasa hivi waingie fyeka fyeka mapepo katika jina la YESU. Na nyie mlioanguka hapo msiogope hapo wenzenu msiogope malaika wanawafungua wanawatoa kila kitu. Wenye upofu ambaye amesogeza jicho lake kwenye redio, ninalikomboa lile jicho, ninaondoa katika jina la YESU. Na umrudishie YESU sifa na utukufu. Usiniinue mimi, mimi ni mwanadamu, ni chombo tu.
Ndugu msikilizaji, mwangalie YESU, mwangalie YESU anarudi.

Maombi ni bure na lazima umuone MUNGU. Hakuna cha baadaye, hapo hapo kama alivyofanya YESU. Hakuna hela ya sadaka ya ukombozi. Wewe umewekwa gerezani huna hata shilingi kumi, unaambiwa ulete hela ndio uombewe; huyo sio MUNGU, cha shetani lazima ulipe. Wewe unakuta upo ICU, huwezi hata kupumua, unaambiwa MUNGU amesema ulete sadaka mara tatu. Uwongo. YESU ameniambia, wapende, waombee, wasaidie; nimekupa bure toa bure. Hao wanaosema pesa, ni nguvu ya shetani. Kwa maelekezo zaidi, ingia kwenye website yetu www.prophethebron.org, kuna blog kuna masomo mengi. Utafunuliwa sana. MUNGU akubariki, MUNGU akuinue sanana. Umetoka gerezani, wewe ni mshindi sasa. Pokea afya, pokea uzima, pokea amani, uishi salama, mwaka mzima uwe ni mwema kwako, umfurahie YESU. Amen. 

[ad_2]