MAHUBIRI LEO HII KATIKA ULIMWENGU WOTE NI MAHUBIRI YANAYOTOKANA NA SAUTI ZA WATU NA SIYO SAUTI YA MUNGU!!!

[ad_1]

Mathayo 15: 8-9
Neno la MUNGU linasema “watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami, nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”
Watu wengi katika ulimwengu wote mahali hapa wanashindwa kupaelewa na kupambanua, ila sasa  ufunguke ufahamu wako na ROHO MTAKATIFU wakati unasoma mafundisho haya ya Nabii Hebron atakufunulia zaidi uelewe ili upone roho yako na wewe utoke katika mfumo wa kusikiliza mahubiri ambayo unasikiliza sauti ya mtu badala ya sauti ya MUNGU. Ukisoma katika injili ya Mathayo 15:8-9 inaelezea vizuri kabisa na maneno haya ni YESU mwenyewe ndiye aliyeyatamka, na sababu ya kuyatamka ni hivi, katika kipindi kile pia walikuwepo watumishi wanaohubiri habari za MUNGU ila walikuwa ni wanafiki (Mafarisayo na Masadukayo) katika midomo yao huonyesha wanampenda MUNGU ila ndani ya mioyo yao hakuna kitu na kama hakuna kitu ina maana wanaabudu bure na hata hao wanaosikiliza hawatapokea kitu katika mioyo yao bali yataishia katika midomo ya wasikilizaji tu na mafundisho hayo hayatendi lolote katika mioyo ya watu na ndiyo maana watu maisha yao katika makanisa ni mabaya na ni ya vifungo tupu vya shetani wala hakuna mpenyo.
Japo asubuhi, mchana na hata usiku kila mahali ni mahubiri tu na mikutano mingi lakini utashangaa watu hawabadiliki kiroho wala kimwili, hii ni sababu hao wanaohubiri kwanza hawampendi MUNGU katika mioyo yao na katika mioyo yao YESU hayupo na kama hayupo mafundisho yote wanayoyahubiri sehemu mbali mbali yote ni feki na ndiyo mbegu zilizomwagwa katika mwamba barabarani, na siyo katika udongo mzuri. Watumishi wengi 95% all over the world ni wapigaji wa makelele tupu kupitia sauti za vinywa vyao na siyo sauti ya MUNGU itokayo katika kinywa au ROHO MTAKATIFU. Ingekuwa kweli ni sauti ya MUNGU ndiyo itokayo katika vinywa vyao basi hakika katika ulimwengu huu maovu yangekuwa hakuna, na shetani angekuwa hajawapata watu wengi kama alivyowateka sasa.
Ukiangalia Television mbali mbali au hata Radio nyingi za injili tena ni 24 hours zinahubiri na kufanya maombezi, ingekuwa kweli hao wanaohubiria katika hivi vyombo ndani yao ni YESU kweli yupo ndiye anayeongea kupitia hicho kinywa hakika kila mtu angepona hapo hapo roho yake na kupokea uponyaji halisi kutoka kwa MUNGU. Lakini cha ajabu watu wanalala hata na radio ikihubiri usiku kucha wakitegemea ile sauti inayoongea ni ya MUNGU na itawafungua na kuwaponya, cha ajabu ndiyo mapepo yanawanyonga kisawa sawa, sasa jiulize wewe peke yako kwa ufahamu wako inawezekanaje wewe unafungua TV na Radio usiku kucha au unalala karibu na TV ili upate maombi, lakini shida ipo pale pale? Jibu hayo ni makelele tu mbele za MUNGU na pia wewe mwenyewe, na hii ni sababu wamejiita au wanatafuta pesa  kwa kutumia jina la YESU na kumbe hao ndio wasaliti wakubwa wa YESU na kwa kutumia midomo yao watu waliwaamini pasipokujua kupitia sauti za maneno ya vinywa vyao wakijua ni sauti ya MUNGU.
NOTE:
Ø Nitakueleza kwa ufupi ufunguke kuhusu kujua sauti ya MUNGU na sauti ya midomo ya watu wakati wakihubiri. Kwanza kabisa ukiona kinywa cha mtumishi kinataja michango tu, harambee, mapatina uelewe hiyo siyo sauti ya MUNGU ni sauti yake peke yake.
Ø Ukifundishwa kuabudu sanamu, na ufundishwe ubarikiwe ukiwa mtu mzima na ubatizwe ubatizo wa maji ya kikombe au ubatizwe katika maji ya kisima au ubatizwe kwa maji mengi halafu kwa jina la mchungaji, Mtume au Nabii (elewa hicho kinywa chake na hata mafundisho yake yote hayatoki katika kinywa cha MUNGU na hamtapona roho zenu zaidi mtaangamia roho zenu na kutumikishwa kiroho na kimwili), sababu mtatumaini hayo maneno ya uongo na wewe ukijua kuwa upo sahihi kumbe umeshatekwa na shetani na katika ulimwengu wa roho na kupigwa upofu usijielewe, leo funguka.
Ø Ingekuwa mahubiri yanayohubiriwa na watumishi mbali mbali kwa Television au radio ni sauti ya MUNGU ndiyo itokayo katika vinywa hivyo kila anayeangalia au kusikiliza angepona pale pale na kubadilika na sababu ni maneno ya wanadamu ambayo ni sauti za watu, hivyo sauti hizo na zenyewe zinabakia katika midomo ya wasikilizaji tu na haziingii katika mioyo. Mpaka sasa umepata jibu, uwe makini sana katika makanisa na Television na Radio hao wanaohubiri ndani yao hakuna sauti ya MUNGU bali ni sauti zao, na wewe umeumbwa ili usikilize sauti ya MUNGU na iingie ndani ya moyo wako. Na kama unafundishwa sana na hauelewi au hayaingii katika moyo wako uelewe hayo ni maneno yenye sauti ya mtu na siyo maneno yenye sauti ya MUNGU, na hii inaonyesha kuwa hata watu ambao wameongozwa sala za toba na watumishi wa jinsi hii ina maana hata hizo toba ni toba za maneno ya midomo na hata mnaoongozwa hizo toba wokovu unakuwa ni feki tu au dini tu pale pale na huu ndio wokovu wa mazoea umetokana na sala za toba za sauti za watu na siyo sauti ya MUNGU.
Ø Maombezi mengi yanayoongozwa sehemu mbali mbali ni watu wanapiga tu makelele wenyewe sababu msingi ni sauti za watu katika midomo siyo ROHO MTAKATIFU ni kuchaji watu pesa tu. Kila hitaji mtu analotaka aombewe leta pesa kwanza, ukiona haya uelewe hapo ni ZERO, ni maombi ya shetani. Au ukute mtumishi au Nabii anachaji watu pesa ndio akuone wewe PRIVATE elewa huyo na hicho kinywa chake sicho kinywa ambacho sauti ya MUNGU inakitumia bali ni nguvu za giza au mizimu au freemason.
Ø Katika ibada mbali mbali ule mwisho utasikia waumini wanaelezwa neema na iwe na wewe, sasa ufunguke mbona unatamkiwa neema iende na wewe siku zote lakini matokeo yake hambarikiwi ni nuksi, balaa na mikosi na kuteseka tu. Elewa kuwa hayatokei hayo sababu umesikia sauti ya mtu na siyo sauti ya MUNGU ndiyo uliyoisikiliza kutoka katika kinywa chake, ulisikiliza na kupokea maneno na wewe ukayapokea katika mdomo wako.
NOTE:
YESU anarudi wakati wowote, amenieleza niwaeleze mtubu, mumrejee yeye, anajua wengi mnampenda ila sala za toba mlizoongozwa hazikuwa za sauti ya MUNGU bali ni za sauti za watu. Hivyo sala za toba zikawa ni bure na ndiyo sababu wokovu umekuwa kama dini, na dini siyo wokovu.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE DHAMBI ZANGU, NAKUREJEA WEWE UWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA WA MILELE NA UNITENGE NA MAHUBIRI YALIYO NA SAUTI ZA WATU, MIMI NATAKA KUSIKIA INJILI YENYE SAUTI YAKO TU, NA AKILI ZANGU UZISHIKE WEWE PEKE YAKO NISISHIKILIWE POPOTE. NAMKATAA SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE NA MAFUNDISHO YA UONGO.
AMEN.

NABII HEBRON.

[ad_2]