MAKANISA MENGI YAMEKUWA NI BAR ZA POMBE NA WAHUDUMU WAKE NI BAR MAID TENA WANATUMIA BIBLIA NA JINA LA YESU KUHALALISHA KUMCHAFUA YESU KUWA YEYE NI MTENGENEZAJI WA POMBE!!!

[ad_1]

JE YESU ALITENGENEZA POMBE? SOMA UJUE UKWELI SASA.

Watu wote mataifa yote nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye ndiye mwana wa pekee wa MUNGU aliye hai na aliyempendeza MUNGU kuliko watoto wake wote aliowaumba MUNGU, na pia ndiye aliyemtuma aje aukomboe ulimwengu huu na hata ile siku ya mwisho ni yeye ndiye aliyepewa mamlaka ya kuja kuhukumu katika ile siku ya kiama. YESU huyu huyu amenituma kwa mataifa yote niwaeleze habari njema ili iwaponye, kwa mtu yule ambaye ataipokea katika moyo wake pamoja na habari zake za ufalme wa MUNGU. Amenituma niwaeleze kuhusu fadhili zake, upendo wake na neema yake kwa ajili ya ulimwengu huu na kwa watu ambao watamkubali yeye 100% na siyo nusu nusu au robo robo.
Leo nitaelezea jambo ambalo linasikitisha ndani yangu na pia hata linamsikitisha YESU pamoja na serikali ya mbinguni pamoja na malaika zake, kwa ajili ya uongo anaosingiziwa YESU na wanadamu ya kuwa yeye alitengeneza pombe wakati yeye hakutengeneza pombe na watu wakapigwa upofu wakaamini huo uongo na makanisa kupitia biblia na watumishi wakasema ni kweli na wakati ni uongo na watumishi na wao wakaanza kuwapa na waumini pombe kanisani wakisema ndiyo damu ya YESU wakati ni kilevi. Ukisoma Yohana 2: 1-11 utaona jinsi YESU alivyokuwa katika harusi na katika harusi hiyo walitindikiwa na divai, ikafika wakati mama yake YESU akamueleza mtoto wake tazama wametindikiwa na divai, baadaye YESU akawaambia waweke maji katika mabalasi na walipoweka wanafunzi wake yeye aliyabadilisha yale maji yakawa divai, kisha akawaambia mmoja wapo chota mpelekee mkuu wa meza, na alipopelekewa aliionja hata akastaajabu akasema mwenye sherehe aliandaa divai mbaya kwanza na kisha mwishoni ndio akaitoa divai njema zaidi.
Hii ilikuwa ina maana ile divai ya kwanza ilikuwa siyo nzuri, ina uchahu, imechanganywa na vitu vinginevyo. Na aliyoitengeneza YESU kwa miujiza wake ilikuwa kama juice fresh ya matunda ya mzabibu. Divai hii aliyoitengeneza YESU iitwa njema sababu ilikuwa ni tamu haina uchachu kama vile unapokunywa kitu unapokitaste katika ulimi wako na pia haikuwa na mchanganyiko wa kitu chochote kile ilikuwa ni direct from mbinguni. Sasa swali jiulize je mbinguni wanatengeneza pombe? Jibu siyo na pia jiulize je pombe inatengenezwa wapi, jibu kuzimu, na pia jiulize mwenyewe je YESU alitenda miujiza ya kuzimu au mbinguni? Jibu ni ya mbinguni, sasa kwa nini watu wanasema YESU alitengeneza pombe na hata sasa baadhi ya makanisa ulimwengu yanapitisha pombe katika nyumba za ibada zao kuwa ni kitu halali na wakitumia kulitaja jina la YESU hata wakati wakinywa katika nyumba za ibada. Jibu, huyo ni shetani ndiye amewateka na kuwapiga upofu. Sasa leo ufunguke akili yako kama ulikuwa hauelewi na ukaona ni sahihi.
Jambo lingine la kukuhakikishia kuwa YESU hakutengeneza pombe ni kupitia neno lake MUNGU.
1.     MUNGU ameonya akasema ole wake ampaye ndugu yake kileo, je itawezekana YESU ajisaliti yeye peke yake na kumkufuru MUNGU? Jibu unalo sasa.
2.     Mithali 9:4-6 inasema hivi “Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, njoo ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganya. Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, mkaenda katika njia ya ufahamu.”
Hapa unaona neno linasema kuhusu divai, ilivyochanganywa ndiyo wajinga wamechanganya na mkate. Neno linasema acheni ujinga mkaishi mkaende katika njia ya ufahamu ina maana kuwa watu ambao wanakunywa divai iliyochanganywa imekuwa pombe hao hawana akili (Mithali 9:6). Sasa ukiangalia hapo katika nyumba za ibada za leo hii nyingi sana wanashiriki divai iliyochanganywa na mkate na biblia inasema hao ni wajinga, hawana akili wala hawajui walitendalo. Sasa fahamu ziwarudie leo hii na kama biblia inasema ni wajinga basi divai iliyochanganywa ni pombe na kama ni pombe katika ulimwengu huu ni kilevi kinachopatikana bar tu ndiyo sehemu yake maarufu, na wale wanaowahudumia watu vileo katika bar huitwa BARMAID. Sasa cha ajabu kilevi sasa hivi limetolewa bar na kuletwa katika nyumba inayoitwa kwa jina la kanisa na watumishi ndio wagawaji wa kilevi hicho na MUNGU ukisoma katika neno lake yeye anakataa kuhusu pombe na kama ni mtumishi wake yeye hawawezi kugawa pombe kanisani sababu atakuwa anayo akili timamu na siyo mjinga, na kama anagawa divai iliyochanganyika hiyo ni pombe au kilevi na sasa atabisha yeye siyo BARMAID?
Na zaidi anayewapa watu vileo kanisani anawafanya watu wamkosee MUNGU kwa kunywa pombe na zaidi anapokunywa muumini na yeye anaingiziwa pepo mvinyo hivyo mtu anazidi kukomaa katika ulevi wa pombe na kupitia njia hii ya divai pombe, shetani hukamata fahamu za waumini na kuwapiga upofu wajione wapo sawa na mkirudi katika neno Mithali 9: 4-6 neno linakupa majibu ya kuwa wewe uko vipi? Na ukisoma katika Mithali 9: 4 kila anayeshiriki katika nyumba ya ibada yenye divai iliyochanganywa biblia inasema ni mjinga na hana akili. Sasa jichunguze je unayoakili au ni mjinga?
3.     Mithali 23: 29-30 “ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; waendao kutafuta divai iliyochanganyika.”
Hapa utaona biblia inasema unapokunywa divai iliyochanganyika lazima macho yawe mekundu, tazama mtu yeyote akilewa jicho  litakuwa lekundu pamoja na vurugu za ajabu, jiulize sasa ingekuwa ni divai njema jicho lingekuwa lekundu? Au unaleta vurugu au ugomvi je hicho ulichokunywa ni chema? Jibu siyo chema, unakunywa maroho ya kuzimu na yakishashiba au kukumiliki yanakuharibu ubongo uwe mjinga kama mashetani yalivyo majinga kataa kufananishwa na mashetani.
Ndugu wasomaji wa makala ya Nabii Hebron wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, YESU amenituma niwafungue akili na fahamu zenu sababu wapo wanaompenda YESU kikweli ila shetani amewapiga upofu hawaijui kweli, bali ni injili iliyopindishwa pindishwa na wakijua ya kuwa eti divai pombe ni mpango wa MUNGU. Divai iliyochanganywa ni mpango wa shetani yeye aliye haramu. Nawaeleza kuwa MUNGU yeye siyo haramu yeye ni mtakatifu na unapomsema YESU WA NAZARETI alitengeneza pombe unakuwa umemtukana, umemkufuru, umemchafua, umemdhihaki na umemuita yeye ni brewer TUBU, na uwe na akili na usiende katika nyumba ambazo ipo divai iliyochanganywa hapo ni bar na siyo kanisani, na hata hao wanaogawa divai iliyochanganywa yenye alcohol au chochote kile hao ni barmaid. Sasa swali je MUNGU alituma barmaid kuhubiri injili? Je barmaid ndiyo viongozi wa kanisa? Unatakiwa uelewe kile mtu akitendacho ndicho cheo chake, mfano ukinywa pombe unaitwa mlevi, ukizini unaitwa mzinzi, ukiwapa watu pombe unaitwa mhudumu wa kugawa pombe.
YESU WA NAZARETI nawaeleza ya kuwa katika sehemu zote zenye divai iliyochanganywa hapo siyo mahali pake, hata kama inafichwa au mnashiriki kwa mwaka mara moja hiyo ni dalili hapo ni bar. Ondoka ukatengwe nao uongozwe na MUNGU kama mwanadamu mwenye akili na asiye mjinga mahali hapo unaangamia roho yako na YESU ile siku ya mwisho akija kulichukua kanisa lake hatachukua mtu katika bar (makanisa yanayotoa divai iliyo alcohol) na pia hata kuna wengine utakuta wakati wanakata roho hawa wahudumu wanampelekea divai na mkate ambayo ni pombe, madhara yake divai hiyo inakufanya utengwe na ufalme wa MUNGU at the final time, sababu utakuwa umetenda dhambi na umelewa na ndani yako pepo pombe anakuwa ametimiza kazi yake aliyotumwa na shetani kuhakikisha kuwa kazi aliyotumwa na shetani ya kumvuna mtu huyo ameikamilisha. Na hata kama unayo akili timamu ukafikiria utaona kuwa pombe ni haramu, pombe ni kitu ambacho unapotumia akili zinavurugika na katika ulimwengu wa roho unakuwa kichaa sababu mapepo yamefunga ndoa na wewe na siyo ROHO MTAKATIFU.
Swali lingine unategemea kupewa Baraka za MUNGU ukiwa bar?
Unategemea uandikwe jina lako katika kitabu cha ufalme wa MUNGU ukiwa bar?
Je mgawa pombe ameitwa au ametumwa na MUNGU awape mtu vileo?
Leo utubu na ufuate sala hii na usishiriki tena kilevi na zaidi waulize kwa nini wanawapa watu vileo jibu hawana, fuata katiba ambayo ndiyo neno la MUNGU aliye hai na ambalo alimtuma YESU kuleta habari njema, na sasa imekuwa siyo habari njema bali ni habari mbaya. Hivi kanisa kugawa pombe, kubariki pombe hii ni habari njema au mbaya? Jibu ni mbaya na unapopokea habari mbaya na wewe utavunwa na mabaya na mwisho wake ni kwenda mahali pabaya peponi.
TUBU:
BWANA YESU NAOMBA UNISAMEHE, NIMEFUNGUKA AKILI NA UFAHAMU, SIENDI TENA KATIKA NYUMBA HIZO ZENYE DIVAI ILIYOCHANGANYWA SABABU NIMEJUA UKWELI. NIANDIKE JINA LANGU KATIKA UFALME WAKO, NIONDOLEE PEPO MVINYO NDANI YANGU, NIONGOZE WEWE PEKE YAKO USIACHE MILELE, ROHO WAKO MTAKATIFU ANIONGOZE KATIKA KANISA LAKO SAHIHI NA SIYO BAR TENA. AMEN.

NABII HEBRON.

[ad_2]