MAKANISA YA KAINI YAMEJAA KATIKA ULIMWENGU WOTE

[ad_1]

1.      WANAO WAUMINI WENGI (ALL OVER THE WORLD)

                                      2.     WANAO MAJENGO MENGI

MWANZO 4: 3-7
“ Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. BWANA akamwambia Kaini, kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”
Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron na wa mataifa yote, kazi yangu aliyoniagiza YESU WA NAZARETI niwaeleze ukweli kuhusu yeye ili watu wote mumjue yeye alivyo na siyo baadhi yenu. Mmeona mpo sawa katika kumjua yeye na kumbe tayari mmeshapotezwa na viongozi wa makanisa na madhehebu wakitumia jina lake tofauti na kanuni za MUNGU alivyopanga. Ukienda tofauti tu haijalishi unamtaja MUNGU aliye hai tayari wewe umeshapotea na umelaaniwa.
Mfano halisi; ukitazama Habili na Kaini wote hawa walimtolea MUNGU aliye hai sadaka na siyo MUNGU tofauti ni wa kweli. Sasa jiulize kwa nini ni sadaka ya Abeli tu ndiyo ilipokelewa tu na ya Kaini ikakataliwa? Jibu, ni sababu Kaini hakufwata fomula ya kumtolea MUNGU na madhara yake mpaka leo hii Kaini akalaaniwa na anazunguka tu katika dunia hii akiwa hana Baraka na kuzunguka mahali pasipojulikana.
Kaini ni mtoto wa Adamu wa kwanza aliyelaaniwa na MUNGU sababu hakutenda vyema kwa ajili ya kutomtolea MUNGU kwa moyo safi na biblia inasema usipotenda vyema ujue dhambi inakuvizia, sasa yakupasa uishinde. Ila makanisa ya leo na pia watumishi idadi kubwa isiyohesabika, hawatendi vyema kama Abeli, bali wanatenda vibaya katika swala la sadaka. Kivipi? Kwa sababu wao wameacha kufuata haya yafuatayo nitakavyo yaorodhesha baadhi kama wameacha kutenda vyema na wao wote alichokipata Kaini  na wao hiyo roho ndio ipo ndani yao inafanya kazi ndani yao na katika ulimwengu wa roho, na roho hiyo imeambukiza hata waumini na majengo yao na kila kitu, hii sababu ya kwenda kinyume na atakavyo MUNGU. Na watumishi wanafikiri MUNGU anadanganyika au hana akili au hawaoni kama vile Kaini alivyomtolea MUNGU kwa udanganyifu na kukataliwa sadaka yake.
Imeandikwa utoapo sadaka yako hata mkono wako wa kushoto usijue, ila makanisa yameacha kutenda vyema. Waumini wameambiwa andika jina na pia hupewa risiti. Ndugu msomaji wa makala ya Nabii Hebron, nakujulisha rasmi sadaka zote hizo hazipokelewi na MUNGU sababu tayari siyo vyema sadaka yako ijulikane na mtu, na MUNGU anataka aijue yeye peke yake. Sasa funguka hapa embu ona huu utahira ulivyolishikilia kanisa na waumini? Na ona jinsi wanadamu wanavyotupa pesa zao chini wakijua wanamtolea MUNGU na MUNGU amezipokea. Na kama unafanya hivyo ujue roho ile ile iliyokuwa ndani ya Kaini ndiyo ipo ndani ya sadaka hizo na hayo makanisa. Na sababu ipo ndani yao basi hayo ni makanisa ya Kaini, na watumishi wake katika ulimwengu wa roho wao ni Kaini na waumini waliopo hapo nao ni watoto wa Kaini, na kama hawa wote ni (Kaini family) inamaana yaliyompata Kaini muasisi na wao yapo kwao.
Kivipi? Maisha ya watu wanatoa sadaka hawana Baraka za MUNGU, na maisha ya kusumbuka hayataisha milele na mwisho ni jehanamu kwa sababu kama MUNGU alivyomlaani Kaini atazunguka siku zote za maisha yake hapa ulimwenguni ndivyo na kwa watu wote wanaomtolea sadaka tofauti na mpango mwema wa MUNGU, na pia ujiulize je MUNGU hajaelezea jinsi ya kumtolea sadaka? Jibu, ameeleza. Sasa jiulize hii elimu ya kuandika sadaka majina imetoka wapi? Jibu, inatoka kwa Kaini na shetani ili Kaini apate wafuasi wengi. Hivyo kama umefanya hivyo ujijue wewe ni Kaini, na mchungaji na yeye ni Kaini, na makanisa yaliyo hivyo na madhehebu yote ni ya Kaini, haijalishi jina la MUNGU linatajwa. Kaini alitaja jina la MUNGU huyu huyu akiwa na Abeli, na Abeli wa leo hii ni makanisa yanayotenda vyema atakavyo MUNGU. Hapo hakuna ubishi 100%. Nawajulisha wazi pesa zenu mmepoteza kama Kaini alivyovichoma yale mazao yake akabakia na majivu tuu na ndivyo ilivyo, ni wengi mmechoma pesa zenu na mali zenu mmebakia na majivu tupu.
Partiners wote ambao mnaitwa na watumishi nyie wote ni Kaini kama alivyo huyo mtumishi (siyo mpango wa MUNGU kuwachagua) na ujiulize kwa nini partiners lazima awe na pesa? Je, hao wakristo wasiyo na pesa MUNGU hawathamini? Funguka akili, mnaibiwa na mnapotezwa. YESU WA NAZARETI ameniambia ni machukizo tupu. Mmedanganywa na watumishi wamemuasi YESU, ni wala rushwa na wanyang’anyi. Kama ni yeye amewaita amewatengenezea njia. Ila ukiona hayo ya partiners mmh amejiita au KUACT kama vile cinema, na wengi ni wachawi.
Mwanzo 4:7- “ kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” Je hawa wanaoandika sadaka wametenda vyema? Na kama ni siyo vyema je watapata kibali? Jibu, hakuna kibali na ndivyo ilivyo, funguka ufahamu.
Mambo mengine, ubatizo wa kweli ni wa maji mengi sasa hawa wanaobatiza ubatizo wa kikombe wanatenda kama alivyoagiza MUNGU? Jibu, siyo vyema. (Haya huu ni mfano halisi) ujijue na ujue kuwa hawana kibali, dhambi imewaotea na ikawashinda badala ya wao waishinde dhambi, dhambi imewashinda au kwa lugha nyingine au maana nyingine shetani amewashinda! Ni mali yake, na kilichompata Kaini ndicho kinachofanya kazi ndani yao na hawatamuona MUNGU. Na MUNGU ameniambia mkitaka kumuona yeye mtende vyema 100% siyo nusu au robo au kiasi au kuchanganya. Yeye hachanganywi na dhambi hata kidogo au vyeo vya shetani kama vile ubatizo wa  maji ya kikombe, au kubatizwa kwa jina la mtumishi. Hivyo ni vyeo vya shetani na kama unavyo ujielewe hivyo na uchukue hatua ubatizwe ubatizo mwema na siyo ubatizo mchafu (Soma kitabu cha UBATIZO WA KWELI KWA ULIMWENGU WOTE cha Nabii Hebron) utapona na uchukue hatua. Ukaondolewe roho ya Kaini, ndiyo maana usumbufu na mateso hayakuishi.
Watumishi wanaokopa pesa benki za ujenzi wa makanisa (hao ni Kaini)
Watumishi wanaochangisha pesa za harambee na michango na kusoma majina ya waumini wale wanaotoa sadaka na kuwapa vyeti vya hongera (hao ni kaini FULL), maana siyo vyema mbele za MUNGU.
Waabudu sanamu (ni wana wa Kaini) hawana kibali mbele za MUNGU huo ndio ukweli, toka huko. Soma kitabu cha Nabii Hebron JINSI KANISA LILIVYOMKUFURU ROHO MTAKATIFU, utayakuta mengi na utapona ukiamua.
NOTE
Hivyo basi yeyote yasiyo mema au kutenda kinyume cha MUNGU katika kanisa au waumini ni dhambi na shetani amewashinda. Hivyo hata ibada mnazoenda na nyimbo mnazoimba ujue ni bora ungekaa nyumbani tuu unajichosha kupiga makelele tuu hakuna kibali cha MUNGU na giza tupu limetanda juu yenu. Cha kufanya soma kitabu cha Nabii Hebron LIJUE KANISA ALILOLIJENGA YESU WA NAZARETI ALIVYOKUWEPO HAPA ULIMWENGUNI na MJUE YESU WA UONGO, hakika utapona roho yako, vipo katika blog ya Nabii Hebron na vinginevyo vingi tuu.
Pia najua wengi hampendi kuwa Kaini japo hata mimi nilishakuwa Kaini huko nyuma sababu nilipewa na kufundishwa mafunzo yasiyo mema mbele za MUNGU na nikamtii mchungaji kumbe ndio kuangamia. Hakuna kitu nilichofanya kikasimama vizuri ni mpaka nilipoigundua siri hii. Na wewe funguka kataa ukaini. Na unaweza ukasema huandiki jina katika sadaka yako, lakini sadaka yako unatoa katika madhabahu ya Kaini, hapo bado umepotea tuu. Huwezi kujitoa wewe katika moto halafu ukarudisha vitu vyako katika moto ule, jibu utaangamia tena.
Watumishi wanao omba omba pesa katika TV au Redio au MPESA hao hawatendi vyema, wanamuaibisha YESU na MUNGU ya kuwa wao ni omba omba, ni masikini. Na hii ni dhambi iliyowaotea na imewakamata na kama imewakamata inamaana ni wana wa shetani sasa au wajukuu na vitukuu vya Kaini vya leo hii, maana Kaini yupo hai mpaka leo na hayo ndiyo mazao ya ile roho ya Kaini. Na unavyotoa na wewe unaunganishwa na mapigo ya Kaini. (hao ni Kaini). Soma kitabu changu JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI.
Kanisa la YESU wa kweli haliwezi kutekwa ila kanisa linalotekwa ni lile ambalo halitendi vyema, dhambi inashikilia kanisa na kuhani, na inawashikilia na waumini.  Hata mkiombaje hakuna majibu maana wote mmekuwa Kaini, sasa Kaini yupi atamtoa Kaini mwenzake? Tafuta mahali alipo YESU wa kweli na mtumishi umechunguza tabia zake na kama anatenda sawa sawa na biblia, akiwa tofauti huyu ni KAINI TUU hakuna lolote.
Mpaka sasa umepata picha ya Kaini alivyojiingiza na kulimiliki kanisa ili na ile laana yake na mapigo wamsaidie kuibeba ambayo ndiyo dhambi ya sanamu, majina kwa sadaka, ubatizo wa kikombe, ubatizo wa watoto wadogo; sasa jiulize utabisha wewe siyo Kaini wa leo na endapo unayafanya kama yeye?  Wacha upone. Uokoke na umtegemee YESU WA NAZARETI, mambo yameshaharibika katika ulimwengu wote. Imefika hata mtu anajiita yeye ni YESU? Hivi, muulize yeye ndiye MWANA WA MUNGU WA PEKEE? Au  yeye aliushinda ulimwengu? Na je kwa kuwa anaishi hapa ulimwenguni sasa hivi wakati neno linasema YESU atarudi siku ya mwisho yaani kimwili. Pia muulize mama yake ni Mariamu? Halafu alitabiriwa wapi huyo YESU anayejiita sasa hivi katika ulimwengu huu? Huyo ni SHETANI, msidanganyike.

NABII HEBRON.

[ad_2]