NDOA ZA MAKANISA YA KIKRISTO ZATEKWA NA YEZEBELI. (MAMA WA MAKAHABA)

[ad_1]

Ndugu msomaji wa makala ya mtume na nabii Hebron, siku ya leo napenda kukufundisha tena kuhusu ndoa zinazofungwa na makanisa jinsi zilivyotekwa na Yezebeli au Malkia wa kuzimu ambaye ndiye mama wa makahaba wote katika ulimwengu huu, au kwa maana nyingine ili uelewe zaidi, nitakupatia mfano katika ulimwengu huu, unajua nini maana ya kahaba na mpaka mtu kufikia kuitwa kahaba.?

(Mfanya uzinzi wa kujiuza mwili wake, au kuvaa nguo na kuonyesha maumbile yako badala ya kuyasitiri.)
Sasa anayesababisha wanadamu  wawe hivyo ni huyu malkia wa kuzimu au kwa jina jingine anaitwa mama wa makahaba.

Anachokifanya anamwaga roho yake kwa wanawake ili wamkosee MUNGU na wawe wafauasi wake hata pasipo kujua na wengine wanajijua.

Ukiona mtu mwanamke anavaa mavazi ya kuonyesha uchi wake mfano mapaja, tumbo(kitovu), matiti yake anavaa (transparent clothes) Hilo utambue moja kwa moja  ndani yake ipo roho ya huyo mama  wa makahaba aliyepo kuzimu na unapovaa hivyo tu tayari na wewe unaunganishwa katika mtandao wa makahaba wa kipepo.

Utakuta mwingine hazini kimwili ila anaolewa na majini, yanakuwa ndiyo mume wake na watu waliolewa na majini, huota ndoto za zinaa sana na pia  huota wananyonyesha watoto na hawawaoni , ukiona hivyo ujijue umeshikiliwa na malkia wa kuzimu (YESEBELI) soma Ufunuo 2:20-24 ,
Lakini nina neno juu yako ya kwamba wamridhia yule mwanamke  YESABELI, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha  watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa  sadaka kwa sanamu.
Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama nitamtupa juu ya kitanda na hao wanaozini pamoja nae, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo  yake.
Nami nitawauwa  watoto wake na makanisa yote yatajua ya kuwa mimi ndiye nichunguzaye  viuno na mioyo , nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasiyo na mafundisho hayo wasiyo zijua fumbo za shetani  kama vile wasemavyo, sitaweka juu yenu mzigo mwingine.

Na ukisoma tena 2Wafalme 9:22, ikiwa Yoramu alipo muona Yehu, akasema  je ni amani  Yehu ?  Yehu akajibu ni amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yesebeli na uchawi wake ni mwingi?  Hesabu 25:1 Basi  Israeli akakaa Shitimu kisha watu wakaanza kuzini pamoja  na wanawake  wa Moabu.

Katika vitabu nilivyo vinakili hapa na mistari  yake inaonyesha waziwazi ya kuwa  Yesebeli  hutumika  kwa wanawake ili kuwaangusha wanawake / watumishi katika uzinzi  hiyo ndiyo kazi yake kubwa.

Ila nitaelezea  kwa kifupi hasa katika ponti; Ndoa  zanazofungwa makanisani na makanisa  kupitisha hayo mavazi ya ajabu na aibu huko ndiko watumishi kuzini na huyo Yesabeli (kitendo cha kuruhusu hayo mavazi ya uchi tayari hata aliyevaa hilo gauni , tayari ameshakuwa  mama wa kahaba katika ulimwengu wa roho na kama ameshakuwa kahaba katika ulimwengu wa roho, hata  ndoa hiyo MUNGU  haiungani na yeye sababu tayari yale mavazi aliyoyavaa ya kipepo yasiyo na heshima na watumishi hawasemi lolote mnaendelea kuangamia.

Hii ni sababu wameshazini na Yesebeli na amewashika fahamu zao wakapigwa upofu na kuruhusu binti bibi harusi uvae mavazi ya uchi, mbele ya BABA yako MUNGU.

Nitaelezea mavazi ya bibi harusi ambayo ni ya mitindo iliyo dizainiwa na malkia  huyu Yesebeli. Shela au gauni ambalo bibi harusi  huvaa huku mabega yake na mgongo vikiwa havijafunikwa , pia matiti yake yanaonekana kifua, gauni la transparent, na nyingine yeyote ambayo siyo ya heshima inayoonyesha maumbile ya bibi harusi hizo zote ni za kahaba na bibi harusi anapozivaa hizo ina maana  na yeye amekuwa mama wa makahaba, kutokana na mavazi yasiyo ya  heshima, japo wengine wanasema ndiyo mtindo wa kisasa siku hizi.

Mmepotea ! hayo ni mavazi ya uzinzi mtupu. Cha ajabu utakuta binti anakuja kanisani manyonyo yapo nje na mgongo upo wazi, eti  anaenda apewe baraka za mchungaji na anapokwenda ni lazima mchungaji amwangalie usoni pia hata kifuani , macho huwa yanaangalia mahali pengi, hiyo tayari umemzinisha hata mtumishi kwa kukuchungulia matiti, na zaidi wengine  wanaovaa  mavazi ya kikahaba  unakuta wakati wa kusaini cheti cha ndoa mara nyingine titi linaweza likawa size kubwa  anapoinama titi linatoka nje ya nguo  inakuwa ni aibu kwa mtumishi huyo na pia kuichafua madhabahu na kuilaani.

Na ndiyo maana Neno linasema, Israeli amezini na Yesebeli. Ina kuwa siyo ndoa  tena hiyo ni laana tupu.  Na siyo kosa la bibi harusi ni kwa sababu, makanisa hayasemi ukweli na kuwafundisha  kipi kizuri na kipi ni kibaya.

Hivi ndivyo mama wa makahaba alivyoziteka ndoa  za wakristo kupitia mavazi. Na mwanamke huyo katika  maisha yake hiyo roho ya ukahaba  na uzinzi itamfuatilia kwa sababu alikubali kuyavaa mavazi yake na akavalishwa hiyo roho  bila kujua.

Shetani ametumia ujanja sana. na zaidi nitaelezea kidogo ili mabinti, na wanawake wapone kuhusu nguo za ndani zile zinazoitwa “Bikini” Zile  ni nguo ambazo amezibuni  Yesebeli  ili kuharibu nguvu za kike za wanawake na wanawake wapende kukutana kimwili  kinyume na maumbile. (yaani shoga), msivae nguo hizo, na madhara yake mnao zivaa nguo hizo huota ndoto za zinaa sana na hawadumu katika ndoa na pia ni shida  kupata mchumba kwa sababu anakuwa tayari  ameolewa na  majini na  anapokuja mchumba mwanadamu yanamvuruga akili au kuwafarakanisha mnaachana, na hata wanazuia usizae au kushika mimba.


NOTE:
Natumaini mmefunguka kataeni mavazi ya Yezabeli, na kama unapasali watumishi hawawaambii  ukweli ina maana tayari na wao wameshazini na Yesebeli au Yesebeli ndio anayezifungisha ndoa hizo na siyo YESU  wa NAZARETI.

Siyo heshima kuvaa mavazi ya uchi mbele za MUNGU hata kwa wazazi wako waliokuzaa kimwili, umeshavunja amri ya MUNGU.
 Mavazi ya uchi ya harusi ile kuyavaa tu, kanisani na watumishi kuruhusu ina maana hilosilo kanisa tena ni NIGHT CLUB, hayo ni ukahaba, na Yesebeli ndipo mahali pake.

Je nikuulize swali , je kanisa limekuwa ndiyo night club? Jibu siyo ila watumishi wanaoruhusu mavazi hayo kinyume na mpango wa MUNGU, hao ni wanachama wa Night club, au wamekamatwa na Yesebeli na kupendelea kuona uovu ukitendeka kanisani. (Marko 11:15-18) YESU alisema nyumba ya BABA yangu ni nyumba ya sala tu, ikiwa inamaana ni mahali pa heshima na patakatifu.

Mavazi ya night club ndilo kanisa linaruhusu watu waje nazo makanisani kufungia ndoa. Je, hilo ni kanisa la YESU wa NAZARETI? Au linakuwa pango la unyang’anyi?
Ni pango kama ilivyo mapango ya night club yalivyo.

Na ndoa hizo zimeshikiliwa na Yesebeli zote na hazipo katika kitabu cha ndoa mbinguni.
Inamaana ni kazi bure mnafanya na mtaendelea pia, mnakuwa mama wa makahaba.
Uzinzi upo juu yako. Uamue upone au uangamize ndoa yako.
Nawatumishi wanaoruhusu mavazi hayo hao ni viongozi vipofu.




 NABII HEBRON

[ad_2]