Close

PEPO IMANI


Pepo imani linaitwa pepo imani sababu imani hii ni yeye ndiye muasisi, pepo huyu hutoka kuzimu katika serikali ya joka kuu. Kama vile MUNGU mbinguni alivyo na utatu mtakatifu, hivyo hivyo na shetani anao utatu mchafu. Nitaelezea katika kipengele cha pepo imani, pepo imani ndiye roho mchafu ambaye ni moja kati ya  nafsi tatu za shetani. Kazi ya pepo huyu ni kuwaingizia wanadamu roho wake ili ROHO MTAKATIFU asipate nafasi, haijalishi  mkristo anasema ana ROHO MTAKATIFU au anamtaja ROHO MTAKATIFU kimwili ila katika ulimwengu wa roho ni pepo mchafu. Watu wamepigwa upofu na ni baada ya imani zao kutekwa na pepo huyu hapo utashangaa mtu anasema anamuamini YESU lakini hataki kuokoka na kumkiri, au mtu atasema yeye ni mkristo safi ;alini anatenda ukristo mchafu kwa kuabudu sanamu, au utakuta mtu anajiita mhubiri au mtumishi wa MUNGU lakini ni mlevi, mzinzi, mchawi, na hata ni freemason, hii yote ni kazi ya pepo imani.
Pepo huyu wa imani yeye jinsi amuingiavyo ni kwa kupitia kwenda kinyume na biblia, au kwa kupitia elimu inayoongezwa na wanadamu katika kulipunguza neno la MUNGU au kuugeuza mafundisho tofauti na kuwapiga upofu watu wajione wapo na ROHO MTAKATIFU ila kumbe wapo na pepo imani. Aliponituma YESU WA NAZARETI hapo mwanzoni nilikuwa nashikwa na butwaa sababu nilirudisha ufahamu katika ulimwengu wote na nikifanya uchunguzi kimwili niliogopa sana mimi Hebron, niliona wasi wasi kama vile ilivyo wewe utakavyoona wazi wazi imani za watu wanasema wapo na ROHO MTAKATIFU kumbe tayari ni pepo imani mfano kanisa linabariki pombe na kusema imehalalishwa na MUNGU wakati ukija katika neno la MUNGU linasema ole wake yeye ampaye mwenzake kilevi (hili ni onyo la ROHO MTAKATIFU ambaye yeye yupo  kulishuhudia neno la MUNGU kwetu).
Ila roho mchafu yeye kazi yake ni kuleta na kupindua na kujiingiza katika neno la MUNGU kama vile malaika wa nuru pasipo watu kuelewa. Pepo imani huyu hukaa kwa watumishi ambao YESU hajawaita au waliojiita au walioasi kasha hukaa ndani yao na kuua imani za watu kwa kuwafundisha tofauti mfano andika sadaka majina, kuweka kikapu cha sadaka ya mchungaji na mke wake, kulazimisha watu kutoa ahadi, kanisa kuwa na benki na kuchaji riba, wakati neno kupitia imani ya MUNGU inasema usimchaji mtu riba, sasa kama kanisa linalo benki ujiulize je ndiyo imani takatifu hiyo? Jibu ni imani ya pepo huyo na kazi zote ni za mapepo na shetani na watu wanaoshiriki, wanafikiri wanaujenga ufalme wa MUNGU kumbe wanaujenga ufalme wa shetani na majina ya watu yanawekwa katika kitabu cha mauti ya shetani.
Mtumishi mwenye pepo imani siku zote yeye na kanisa lake ni michango tu ili hilo kanisa liendelee na unyang’anyi zaidi, soma kitabu cha Nabii Hebron JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI, utamjua zaidi jinsi huyu pepo imani alivyo na alivyoteka kanisa akishirikiana na mpinga kristo. Ukibatizwa ubatizo wa maji ya kisima, ubatizo wa maji ya kikombe, ubarikio wa watu wazima, kubatizwa kwa jina la mchungaji, na kushiriki katika kanisa ambalo lina sanamu, au mtumishi ni mtu wa mshahara au ni mchawi au amemsaliti YESU, hapo utaipokea hiyo imani ya pepo imani hata pasipo wewe kujua. Pia pepo imani hilo ndilo kiongozi wa wachawi, manabii wa uongo, watumishi walioasi, wanaotafuta pesa, biashara, waizi wa nyota, wafufua misukule au mazingaumbwe.
TUBU:
BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uitoe imani ya pepo ndani yangu, uiweke imani ya ROHO MTAKATIFU ndani yangu. Unitoe jina langu katika kitabu cha mauti ya shetani, na mapango yake. Najitenga nao kiroho na kimwili, niongoze ROHO MTAKATIFU siku zote za maisha yangu. Amen.
Nawakaribisha nchi zote na watu wote katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWKOZI WA MATAIFA YOTE, hili ni kanisa alilolipa jina YESU peke yake kwa kinywa chake ikiwa ni kwa ajili ya nchi zote ili awakomboe na awafungue na awapeleke peke yake mbinguni. Sababu aliwatuma wachache na wamemsaliti sasa anafanya kazi peke yake na ndipo lile neno limetimia utukufu wa kanisa la mwisho ni mkuu kuliko ule wa kwanza. Hii ina maana yeye sasa atafanya hayo na ndivyo ilivyo.

NABII HEBRON.