PEPO KANISA

[ad_1]

MATHAYO 24: 4-5, 22-28
BWANA YESU ASIFIWE, watoto wa MUNGU, YESU WA NAZARETI anawapenda sana na amenituma niwafundishe kuhusu ukweli wake na kuwaonyesha njia ipasavyo ambaye yeye peke yake ndio njia ya kweli na mtu akifuata njia nyingine zote katika kumfuata MUNGU wa kweli ni za uongo. Leo nitaelezea kuhusu kitu kinachoitwa  pepo kanisa wengine watashangaa labda nimechanganyikiwa kusema neno pepo kanisa, naita pepo kanisa kwa maana hii katika ulimwengu huu yapo makanisa ya aina mbili, makanisa matakatifu ya ukweli na makanisa ya roho mchafu au mashetani na bado yakaitwa kwa jina la kanisa la YESU hivyo hivyo, lengo langu mimi ni kukufundisha wewe uelewe na upone au usije ukaingia katika makanisa ya uongo (ya yesu wa uongo) ukadhania upo katika kanisa la kweli ambalo ndilo njia ya kweli na kumbe upo katika kanisa la njia ya uongo (mpinga kristo).
Nitaelezea kwa ufupi ila zaidi uendelee kusoma makala ya Nabii Hebron kwa faida yako na mengine utafunguka zaidi katika kweli. YESU aliposema watakuja makristo wa uongo, je wewe ulifikiri yataongozwa na nani? Jibu ni roho mchafu, roho huyo ndio anayeitwa pepo, pepo huyu kazi yake ni kuyashuhudia yale yaliopo katika biblia ya shetani katika makanisa ambayo yametekwa na shetani au ni ya mpinga kristo. Pepo huyu hauwezi ukamuona kwa macho ila utamuona kwa kuchunguza mafundisho ya kanisani ambayo unafundishwa au anayoyatenda kuhani, haijalishi anatumia biblia, ukikuta tu anajiita ni mkristo chunguza ukristo wake je unayashuhudia yale mbinguni na neno la MUNGU kama lilivyo? Zaidi angalia tu ubatizo je ni wa mbinguni ule aliobatizwa yeye aitwaye njia ya kweli na uzima! Maji ya mtoni yanayotembea? Na yasiwe ni ya kisima, na pia kisima kisiwepo popote hata ndani ya hekalu wala yasiwe ya baharini, wala ziwani, au kubatizwa kwa jina la mchungaji.
Ukiyaona hayo uelewe kanisa hilo linalojiita kanisa kwa jina la kanisa la YESU uelewe hilo ni kanisa la yesu wa uongo na hata wewe mkristo ujielewe na wewe siyo mkristo wa kweli. Haijalishi unampenda YESU sawa, lakini YESU uliye naye ni huyo ambaye yeye ndie njia ya uongo, na ndio sababu ukabatizwa tofauti na YESU WA NAZARETI. Swali sasa kama unabatizwa tofauti na ubatizo wa YESU wa kweli je hauoni kama unajipiga chapa ya yesu wa uongo? Kama unabisha tafuta katika kitabu cha biblia  hautaona hizo type za ubatizo na kama hakuna. Nikuulize je haujapelekwa wrong way? Na wrong way ni wapi? Jehanamu, na kupitia ubatizo huu watu wengi wasipobadilika na kuukataa hakika ile siku ya unyakuo kwanza hawatanyakuliwa na pili hawataurithi ufalme wa MUNGU sababu hiyo siyo alama yake. Enyi mataifa nawaandikieni wakala huu msicheze na kupigwa batizo za uongo na usione ni kitu kidogo hakina madhara, yapo madhara makubwa na ya majuto, na hata hao wanaobatiza hivyo wajielewe hawaongozwi na ROHO MTAKATIFU bali yupo roho mchafu ndani yao ayashuhudiayo njia ya uongo. Japo wengine hawaelewi na wanarithi mapokeo ya elimu ya wanadamu wakimuona MUNGU yeye hana akili, siyo msomi wao ndio wanajua wanamsahihisha MUNGU, nawaeleza mtubu na hata misingi ya makanisa huyo hayupo roho wa kweli yupo roho wa uongo na ndio sababu mafundisho ya uongo yanayokubalika na yameendelezwa katika makanisa hayo, sasa ndugu msomaji jiulize ndani yako je kanisa likifundisha kinyume na neno lilivyo je ni roho gani yupo hapo? Jibu ni pepo na kama pepo yupo basi kanisa hilo linaitwa kanisa la kipepo, na kama kanisa linafundisha ukweli hilo linaitwa kanisa takatifu.
Ila pia uelewe katika uliwengu wote hautasikia kanisa linajiita siyo takatifu, hii ni sababu watu hawataenda, sababu hakuna anayetaka kanisa chafu ambaye yeye ni mkristo, ila upofu umeingizwa roho mchafu anayetengeneza mafundisho yake na yanapokelewa na kuaminiwa na watu, wao wanakuwa wana wa pepo mchafu au wana wa yesu wa uongo, na yesu huyo ni njia ya uongo, hivyo njia yake ili akupate ni wewe uskiriki neno tofauti basi uelewe umeshika njia ya pepo kanisa na siyo njia ya kanisa takatifu na hata ule mwisho YESU atalinyakua kanisa takatifu na siyo kanisa la kipepo. Na kanisa lazima uelewe ni wewe mtu siyo hayo majengo, sasa ndugu wasomaji kwa njia hii hauoni bado mamilioni ya wakristo wapo katika njia ya uongo na wala hawajui kama tayari wameshatekwa na mpinga kristo na tayari siyo watu wa YESU WA NAZARETI ambaye ndie njia ya kweli! Leo ufunguke utubu sababu neema yake ipo bado na usikaze shingo ukasema bado wakati. Watu wa jinsi hiyo MUNGU na yeye hawataki sababu wanamtaka pepo bado awamiliki badala ya ROHO WAKE MTAKATIFU. Na zaidi pepo huyu ndie kiongozi wa watumishi wa kipepo ambao wanajiita ni watumishi wa MUNGU. Sasa unatakiwa uelewe pia shetani ni aina ya mungu pia, jinsi kuhani alivyo ndivyo na yeye alivyofanana na aina ya mungu wake hapo utapata jibu je ni mungu wa kweli au ni mungu wa uongo. Angalia mafundisho yake hata kama anachanganya mengine kweli na mengine uongo, funguka akili, anaongozwa na pepo (roho mchafu).
MAMBO MACHACHE YA KUELEWA KANISA LINAONGOZWA NA PEPO AU MTUMISHI
Ufunuo 22:18
1.     Chunguza aina ya ubatizo.
2.     Kuabudu sanamu, ibada za wafu, kuabudu wanadamu.
3.     Kubariki pombe.
4.     Michango ya pesa na sadaka za ahadi, kuandika sadaka (bahasha) majina.
5.     Makanisa kufanya biashara mfano kuwa na benki, (haya ni mambo ya Kaisari tu siyo ya MUNGU WA KWELI). Huu ni unyang’anyi, wanachaji riba na MUNGU yeye hachaji riba watu.
6.     Kufufua misukule, kuombea watu kwa kuchaji pesa (uwizi) hawa ndio waizi wale ambao YESU aliwaita.
7.     Makanisa ambao ukisoma ndani yake yameandikwa majina ya miungu (haya makanisa yamejaa Afrika magharibi soma hata kusearch kwa google tafuta sura za makanisa ndani usome utaona maajabu, halafu wanakuja kuhubiri na watu wanawaamini, kumbe watu wanafanywa wamuamini yesu wa uongo na kutekwa pasipo kujua, hao ni watenda kazi wa shetani).
8.     Makanisa yanayoruhusu ndoa za jinsia moja.
9.     Makanisa ambayo watumishi wanavaa hereni wakihubiri (lile ni pepo lipo ndani yake, pepo linaloitwa malkia wa baharini na siyo MUNGU wa kweli).
10.                       Mtumishi anayevaa kofia akihubiri (mwanaume, 1 Wakorintho 11: 3, 4, 7)
NOTE:
Yapo mengi ya kuwafunulia wewe kimwili upate kuona na unapoona chukua hatua sasa utubu, sababu umeona mengi kupitia maneno haya uliyosoma au mahubiri ya Nabii Hebron ya njia ya ukweli.
TUBU:
BWANA YESU naomba unisamehe uniokoe sasa hivi nitoe katika kanisa pepo, niandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele ambao ndio njia ya kweli, roho wako mtakatifu aniongoze siku zote za maisha yangu na ni urithi ufalme wako. Amen.
Watu wote karibuni katika kanisa la YESU NI BWANA, Arusha Tanzania. Utaujua ukweli zaidi na utabarikiwa na yesu peke yake.

NABII HEBRON.

[ad_2]