SISI SOTE WAKRISTO SIYO KIUNGO CHA KRISTO

[ad_1]

Imeandikwa sisi sote tu viungo vya Kristo, yaani wakristo wote., Ndugu msomaji pata shule hii usipotee, kwa sasa usemi huu,wa Neno la MUNGU umebadilika siyo mwili mmoja tena sisi sote.
Nitakufundisha uelewe vizuri na utapata jibu kamili 100%. Watu katika ulimwengu huu wamebakia kujipa moyo na kusema sisi sote tu viongo vya KRISTO, hii siyo kweli, nitaelezea kumuhusu YESU huyu wa Nazareti jinsi alivyo na jinsi alivyo na ushirika na MUNGU BABA na ROHO MTAKATIFU, hawa tu ndio wanao umoja na umoja wao upo milele. Isipokuwa wanaadamu ambao tunamwamini YESU 98% imebakia YESU jina tu wala siyo viungo vya Kristo tena ila utaujua ukweli endelea kusoma ujumbe huu nikupatiayo mimi Nabii Hebron.
Jambo la kwanza ili ujue sasa hivi kweli hili Neno la MUNGU la ya kuwa sisi sote tu viungo vya Kristo imekuwa kinyume siyo wote tena ni mwili au katika viungo vyake angalia haya yafuatayo halafu uyalinganishe utaona tofauti kabisa na siyo tena wote ni viungo vya Kristo.
Ø Wakristo wengine wanaabudu sanamu ( Siyo kiungo cha YESU)
Ø Wakristo wengine hawabatizwi ubatizo aliouagiza MUNGU ubatizo wa Yohana  (siyo kiungo cha YESU)
Ø Kubatizwa kwa jina la chungaji (Siyo kiungo cha Kristo)
Ø Kanisa kufungisha ndoa za ushoga(siyo kiungo cha Kristo)
Ø Makanisa kuwa na mabenki na kudai riba  (siyo kiungo cha Kristo), madhara ya riba ni mfilisi au kunyang’anya YESU alisema usidai riba kwa kanisa maana anajua madhara ya riba mtu akishindwa kulipa anafilisiwa na kamaBenki ni ya kanisa inamaana YESU ataitwa mfilisi wakati yeye siyo mfilisi. Aliyajua haya mambo hayo yafanywe na taasisi zisizo za kanisa tu. Kwenye riba kuna kudhulumiwa.
Ø Wakristo wengine wanaacha kumuomba MUNGU aliye hai wanarudi kuwaomba wanadamu kama yeye ambao waliumbwa na MUNGU wakati imeandikwa umuabudu MUNGU peke yake tu,(siyo kiungo cha Kristo)
Ø Watumishi wote ambao ni freemason (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Wakristo wanaopinga wokovu (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Makanisa yanayokopa benki halafu waumini wanalipa riba (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Watumishi wanaofanya zinaa hao wote (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Ibada za kushiriki ibada za wakfu (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Wakristo wanaofanya mitambiko (Mila) (siyo kiungo cha Kristo)
Ø Makanisa yote yanayowaambia watu waandike majina katika sadaka zao na namba za simu, wakati imeandikwa utoapo sadaka yako ni siri yako kati yako wewe na MUNGU tu. Hapa utaona tayari Neno la YESUwa nazareti limekufuriwa na kupuuziwa. (tayari siyo kiungo cha Kristo)
Ø Wakristo walio wachawi au washirikina,au walevi au watendao maovu na wanajiita ni wakristo na ni mwili mmoja huu ni uongo mtupu. Watu wa namna hii siyo kiungo kimoja na YESU maana YESU siyo mlevi, mchawi, na siyo muovu. Ili uwekiungo kimoja na YESU fuata ya YESU wa Nazareti kiimani na kimatendo. ( walio kinyume siyo kiungo cha YESU haijalishi unalitaja jina lake.
NOTE:
Mpaka sasa kwa mifano michache umezidi kuelewa, embu nikuulize swali sasa je kwa mfumo huu sisi sote ni viungo vya Kristo? Jibu  ni siyo kweli.
Na wengi hushiriki tu tukijua sisi sote tu pamoja  mwili wake, ndugu msomaji, mwili wa YESU siyo huo na hii yote ni sababu ya kukataa kulishika Neno la MUNGU na kwenda kinyume na kimatendo, na watu wakijijua kweli wapo katika umoja wa mwili wa Kristo na kumbe wameshaachwa, funguka ufahamu wako hii yote imetokana na mapokeo ya elimu  ya wanadamu wakaacha kufuata  ya MUNGU.
Na wanadamu kujikuta ni wapumbavu mbele za MUNGU. Na shetani ili amwangamize mtu yeyote mlango mkubwa anaoutumia ni kumfanya awe mpumbavu halafu ndipo hummiliki  na MUNGU huondoka, matokeo yake ni kuishi katika mapigo na zaidi kwa picha hii kanisa limegawanyika na kuwa siyo makanisa yote ni mwili wa Kristo tena.
Jichunguze utapata jibu lako upo wapi wewe?

NABII HEBRON

[ad_2]