TOBA YA KWELI NA TOBA YA UONGO

[ad_1]


Ndugu msomaji nakusalimu katika Jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai, BWANA  wa MABWANA na MUNGU wa MIUNGU.
Namshukuru MUNGU kwa kunipa kibali cha kutoa Ujumbe ambao yeye mwenyewe anataka ujue ukweli jinsi shetani alivyogeuza na kulidanganya kanisa.
Toba impendezayo MUNGU ni ipi?
Ndugu msomaji toba impendezayo MUNGU ni ile ya kumkubali MUNGU, kumkiri na kufuata neno lake na kufanya toba ya kweli ya kutubu mabaya yote ulioyafanya kwa kujua au kutokujua, kwa kukiri kwa kinywa chako mbele za MUNGU wako aliye kuumba kwa sura na mfano wake; kumkubali yeye MUNGU akutoe huko na kukubali kuacha yale ambayo ni mabaya na ni dhambi mbele za MUNGU wako aliyekuumba. Kufuata neno lake yaani kufuata maisha ambayo aliyoyaishi YESU KRISTO wa Nazareti. Kufanya toba ya kweli kwa njia ya ubatizo wa maji mengi. Kufuata ubatizo wa Yohana  ulikuwa ni Ubatizo wa toba ambao hata YESU KRISTO WA NAZARETI aliupitia kwa kuzamishwa ndani ya maji ya mto yanayotiririka.
MATENDO YA MITUME 19: 4
Paulo akasema Yohana alibatiza ubatizo wa toba akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani YESU.
Ndugu msomaji pata kufunguka sasa juu ya toba ya kweli mbele za MUNGU wako lazima upitie ubatizo ambao YESU alibatizwa, ndio toba ya kweli na ndiyo toba ya kumkubali MUNGU na kumrudia MUNGU. Kama wewe ndugu msomaji haujabatizwa ubatizo wa maji mengi jua wewe bado haujafanya toba ya kweli mbele za MUNGU aliye hai.
Mambo yamebadilishwa ndugu msomaji kanisa limekosa muelekeo yale ambayo yalio kuwa yanafanywa na YESU KRISTO wa Nazareti hayafuatwi tena,  toba ya kweli kwa njia ya ubatizo wa maji mengi haipo. Neno la MUNGU limegeuzwa watu wazima wanabarikiwa na watoto wadogo wanabatizwa tena ubatizo wa kumwagiwa maji kwenye paji la uso. Je mtoto mdogo ana ufahamu na uelewa wa kutambua kinachofanyika kwa wakati huo? Jibu ni kwamba hatambui chochote kwa wakati ule.
Ndugu msomaji wapi kwenye biblia imeandikwa juu ya ubatizo
wa watoto wa changa kuwa ni toba ya kweli? Je ubatizo wa wafu ni ubatizo wa toba ya kweli? Je kubatizwa katika kisima huu ni ubatizo wa toba ya kweli? Ubatizo wa kumwagiwa maji kwenye paji la uso ni ubatizo wa toba ya kweli? Aina zote hizo za ubatizo nilizozitaja  sio ubatizo wa toba ni machukizo mbele za MUNGU.
Toba ni njia inayompendeza MUNGU na ndio maana mwanadamu amewekewa njia mbili: Njia yenye Nuru (uzima wa milele) na njia ya giza (kuzimu kwa shetani). Unapochagua njia  ya nuru utafuata yale ambayo YESU anataka na yeye mwenyewe alifanya na alionyesha njia itupasayo kuiendea.
Ndugu msomaji kanisa halijafundishwa ile toba ya kweli inayompendeza MUNGU, viongozi na watumishi wa kanisa wametekwa na wameacha muongozo yaani Biblia wameongeza na kupunguza neno la MUNGU makanisani hakuna toba ya kweli.
Neno la Mungu MATENDO YA MITUME  5:31  “ Mtu huyo MUNGU amemtukuza kwa mkono wake wa kuume awe mkuu na mwokozi awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.”
 Ndugu msomaji wa makala hii neno linaelezea juu ya YESU KRISTO WA NAZARETI mwana wa MUNGU ambaye alishuka duniani ili kupitia yeye tupate toba ya kweli na msamaha wa dhambi zetu.
Pata kujua mwana wa MUNGU unayesoma makala hii; nataka ufunguke na uelewe toba ambayo ni chukizo mbele za MUNGU aliye hai.
Hakuna mwanadamu chini ya hili jua hata aseme yeye ni Mtakatifu,  hakuna aliye mkamilifu wote wanapaswa kupitia njia ya toba, aliyemkamilifu ni YESU KRISTO wa Nazareti tu peke yake aliyezaliwa kwa uwezo wa ROHO MTAKATIFU.
Watumishi ambao ni viongozi wa kanisa wamebadilisha ile toba ya kweli, wameiongezea wameiita kitubio, namna inavyofanyika ni kinyume na neno la MUNGU, kitubio hiki ni unakwenda mbele za  mtumishi na kukiri dhambi zako ambazo umefanya kama umezini unasema na ni mara ngapi, umeiba unasema ni mara ngapi umefanya kila uovu ulioufanya unasema mbele ya huyo mtumishi. Ukishamaliza kusema hayo yote uliyoyafanya huyo Mtumishi atakwambia usali sala fulani, tena urudie mara kadhaa atakwambia ni aina ya sala gani ukasali kama vile adhabu ya dhambi zako ili upate ondoleo la dhambi zako. Halafu atakwambia umesamehewa dhambi zako nenda na amani ya BWANA.
Hivi inakuingia akilini mwana wa MUNGU unayesoma makala hii?
Je MUNGU aliyaruhusu hayo mwanadamu kufanyiwa toba (kuungamiwa). Hii ni toba iliyo chukizo mbele za MUNGU;  halafu mtumishi ambaye unayeenda kutubu kwake maovu yako , kwanza yeye ni mtenda dhambi zaidi hata yako wewe ambaye umeenda kutubu, tena unakuta huyo mtumishi ni mlevi.
Hajabatizwa ubatizo wa toba, (yaani wa maji mengi) ana mke zaidi ya mmoja au mwanamume zaidi ya mmoja , ni mvuta sigara  na pia sio mtumishi wa MUNGU ni mwanachama wa freemason.
Hakuna toba kama hiyo ni chukizo mbele za MUNGU wala kwenye Biblia haijaandikwa.
Watumishi wanao fanya hivyo jua ni watumishi wa shetani na wanachukua taarifa za dhambi zako wanapeleka kwa baba yao lusifa kwake hakuna ondoleo la dhambi wala hakuna kufutiwa dhambi, matunda yake ni unachuma mateso, mzigo wa dhambi unaongezeka mara zile ulizofanya unajikuta unakua wewe ni mtumwa wa dhambi, funguka mwana wa MUNGU upate kupona.
Onyo: Ole ya watumishi wanao fanya hayo.
MUNGU alipomleta mwanae YESU KRISTO WA NAZARETI alikuja kwa ajili ya dhambi zetu aliteswa na kufa msalabani aliacha njia ili kila mmoja apate kwenda kwa BABA (yaani MUNGU)  kuomba toba na msamaha bila kupitia kwa mwanadamu.
Moyo wa kushuka na kunyenyekea na moyo wa toba ndio MUNGU anapendezwa nao, unapokiri makosa na dhambi ulizofanya na  ukatambua  kuwa umekosa mbele za MUNGU, hakika MUNGU atakusamehe.
YESU WA NAZARETI ndiye alifungua mlango wa kila mmoja aende mbele za BABA yake kuomba toba na kupata msamaha wa dhambi.
Mtumishi ambaye anachukua nafasi ya MUNGU tena huyo ni mwabudu sanamu ambaye ameifanya kuwa ni mungu wake ambaye ni lusifa shetani, na wewe mwana wa MUNGU unayeenda kuungama kwa mwanadamu ni sawa na anayeabudu sanamu na baba yako ni lusifa (shetani). Maana mwanadamu hawezi kutoa uhai kwa kitu chochote alichokiumba MUNGU, wala mwanadamu hawezi kutoa msamaha wa dhambi kwa mtu yeyote.
NENO LA MUNGU MARKO 1: 4-5
Yohana alitoka akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba iletayo ondoleo la dhambi.
wakamwendea nchi yote Uyahudi nao wa Yerusalemu wote wakabatizwa katika mto wa Yordani wakiziungama dhambi zao.
Ndugu msomaji neno la MUNGU lipo wazi kabisa linaelezea juu ya toba ya kweli, kama wewe mwana wa MUNGU ulishawahi kwenda kuungama  dhambi zako kwa mtumishi na wewe unaendelea kutubu kwa mwanadamu kuanzia leo mrejee MUNGU kwa kusema sala hii
BABA katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI niko mbele zako, naomba unisamehe mimi ni mwenye dhambi naomba unisamehe dhambi zangu zote, BABA naomba uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, naomba ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu namkataa shetani na kazi zake na mambo yake yote kuanzia leo BWANA YESU uwe Mwokozi wa maisha yangu. Amen

[ad_2]