UBATIZO WA FREEMASON UNATUMIKA SASA MAKANISANI ALL OVER THE WORLD 90%.

[ad_1]

Katika ulimwengu huu tunao ubatizo wa kweli ambao uliletwa na Yohana ambaye ndiye aliyetumwa na MUNGU kuanzisha huduma ya ubatizo kutoka kwa MUNGU. Na ubatizo huu ni ubatizo pia aliobatizwa YESU WA NAZARETI, ukisoma katika kitabu cha Mathayo 3: 13-17 inaelezea vizuri kabisa. Neno ubatizo ina maana kuzamishwa katika maji tena mwili wote na ubatizwe kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU. Ukisoma biblia yote utaona ni ubatizo wa maji mengi peke yake tu ndio ubatizo uliotokea kwa MUNGU na  unaelezea maelezo yake jinsi ipasavyo watu wabatizwe na hata katika injili ya Mathayo 28: 18-20 YESU anawaeleza wanafunzi wake na ukisoma katika injili ya Ufunuo wa Yohana 22: 18-20 ole wake atakayeongeza maneno ya unabii wa kitabu hiki au kupunguza hakika sehemu yake ya uzima itaondolewa na MUNGU.
Watumishi wengi na makanisa, madhehebu mengi katika ulimwengu wote wameongeza maneno yao katika injili na wengine wanayapunguza ili kuficha maana ya Neno la MUNGU. Hawa wote hii ni picha halisi tokea hapa ulimwenguni tayari sehemu yao ya uzima haipo wala safari yao siyo ya mbinguni bali ni safari ya jehanamu. MUNGU anaangalia Neno lake, haijalishi sehemu nyingine wanafuata biblia na sehemu nyingine wanabadilisha. MUNGU siyo wa michanganyo, yeye ni MUNGU mkuu (ALPHA NA OMEGA). Wewe mwanadamu ni nani hata umchanganye MUNGU? TUBU, kuchanganya Neno la MUNGU na uongo ni kumtukana MUNGU na kumdharau. Nawaeleza wazi watu wote mnaolibadili Neno la MUNGU au kulipunguza wote mmemtukana MUNGU, na yeye MUNGU 2013 alisema na mimi akaniambia mimi ni MUNGU wala zaidi hayupo na hatakuwepo. Kama mimi sina mwanzo wala mwisho, je Hebron kwa nini wanadamu wananitukana? Nikanyamaza kimya maana nilijua wametumia lugha chafu kama vile watu katika ulimwengu huu wakitukanana wenyewe kwa wenyewe, akaniambia siyo maana alijua ninawaza nini, kutokana na alivyoniuliza. Akaniambia hata wewe Hebron, ukienda kinyume na Neno langu utakuwa umenitukana, niliogopa, akaniambia waeleze watu warejee kwangu na njia ya YESU WA NAZARETI atakayewafikisha kwangu. Watu wote wanaobatiza ubatizo ambao sijaagiza mimi hao wananitukana au kuvunja sheria zangu.
Nitaelezea kwa kifupi mpaka katika makala nyingine. Hayo yote ni MUNGU ndiye anayenifundisha ili niukomboe ulimwengu, yeye yupo ndani yangu. Sasa enyi watu wote huu ni wakati wa kujua kweli yake maana wapo watu wa matabaka mawili. Wapo wanaompenda MUNGU na wapo wanaomchukia kabisa, ila wanampenda lusifa. Na lusifa na yeye anao ubatizo wake (Namba 666) ile unaingia katika paji la uso katika roho na ubatizo wa lusifa (freemason) au mpinga kristo ni huu. Unabatizwa ubatizo wa maji ya kikombe kichwani tu na ubatizo mwingine wa freemason ni ubatizo wa maji mengi ila ni ya kisima, hayatembei, na ubatizo mwingine wa freemason ni ubatizo wa kubatizwa kwa jina la mchungaji haijalishi ni ubatizo wa maji mengi huo ni ubatizo wa freemason. Ili uwe mkristo ni lazima uokoke na ubatizwe ubatizo wa maji mengi (SOMA KITABU CHA UBATIZO WA KWELI KWA ULIMENGU WOTE CHA NABII HEBRON) inaelezea kwa undani na utaelewa na hakuna cha kubisha kitakuweka huru. Sasa shetani anazo trick nyingi na amelipiga kanisa upofu kabisa sababu watumishi wamemsaliti wakayapokea ya shetani badala ya kutenda maneno ya MUNGU. Wewe mwenyewe kibinadamu unajua ubatizo wa kweli ni wa Yohana wa maji mengi. Sasa huu ubatizo wa maji ya kikombe nikuulize upo katika Neno la MUNGU? Jibu haupo (haya ndiye maneno ya shetani sasa).
Kama huu ubatizo ni tofauti na ule ubatizo wa Yohana tayari umekwenda kinyume na Neno la MUNGU, unalifuata neno la shetani na ukalikubali hivyo na wewe unafanyika kuwa mwana wa shetani au unakuwa na wewe ni freemason bila kujua na matokeo yake katika ule mwisho na wewe unaingia jehanamu, maana akija YESU katika ule mwisho anakuja kuwachukua wale walio wake, ni alama yake atakayoiangalia, ni ubatizo wake yaani chapa yake ambayo ndiyo Yohana alimbatizia pia YESU. Kama ukiwa na ubatizo tofauti na wa Yohana hatakuchukua na pia hata waliokufa kama hawajabatizwa ubatizo wa maji mengi habari ya mbinguni na hiyo waisahau. Na katika ulimwengu huu na mataifa yote wakristo wengi wanapinga jambo la freemason na hawataki kabisa ila pia wapo wanaoitaka na kuupenda ufreemason.
Naelezea kwa hawa wanaompenda YESU na hawajijui kumbe na wao tayari ni freemason bila kujua. Kama unabatizwa ubatizo tofauti na YESU, tayari na wewe unayochapa ya freemason (666). 98% all over the world shetani ameliteka kanisa, na YESU amenitoa katika kazi yangu ya professional driver     nikiwa Serengeti, akaniambia nautaka mwili wako niupeleke ujumbe wangu na niukomboe ulimwengu maana watu wanaona wapo sawa na kumbe tayari shetani amewateka, sasa jichunguze kama na wewe siyo freemason, tena bila kupenda, ukawekewa chapa ya 666, ukijua ndiyo ubatizo wa kweli na ndiyo alama ya YESU WA NAZARETI na ndiyo alama ya mkristo. Freemason wameliteka kanisa na wamejiekea mizizi na kuwafunga watu akili zao wasielewe hata Neno lilivyo wazi la ubatizo, badala ya YESU kuwawekea watu chapa zake sasa freemason ndiyo anayewekea chapa zake kwa wingi na wakristo idadi 90% wanapigwa chapa ya freemason na namba 666, bila kujua na hao watumishi wanaobatiza na kupiga chapa 666 ubatizo wa maji ya kichwa hawa ni watenda kazi wa shetani japo wapo wanaofanya bila kujua sababu ya mapokeo. Ila ili upone utoke huko na ukabatizwe kwa maji mengi ufutwe chapa ya freemason ili uwe mkristo wa kweli.
NOTE:
Ø Chunguza hata wewe mwenyewe na ujiulize ni kwa jinsi gani wakristo wengi wanabatizwa tofauti na YESU. Hii ni sababu shetani ameliteka kanisa alishirikiana na roho za watenda kazi wake freemason.
Ø Na kama umebatizwa ubatizo tofauti ujitambue wewe ni freemason sio mkristo wa kweli.
Ø Freemason wao wanamuamini shetani na wanamuona YESU ni mbaya na wanaamini eti YESU ndiye aliyemfitini lusifa akafukuzwa mbinguni na MUNGU, wakati ukweli ni huu; Lusifa alitaka ampindue MUNGU ndipo akatupwa na kutolewa mbinguni. Joka kuu ambaye ndiye baba yake shetani. Sasa lengo la freemason ni kupinga Neno la MUNGU na kulibadilisha ili wale wote watakaoamini au kuyafuata katika kanisa na wao wanaunganishwa na freemason. Sababu wana uhalali maana umebatizwa tofauti na Neno la MUNGU. Ila amua usiwe tena mfuasi wa freemason, ubatizwe ubatizo wa kweli, na kama mpaka sasa haujabatizwa ubatizo wa maji mengi akija YESU au ukifa hauendi mbinguni.
Jichunguze, jibu unalo. Elimu hii siyo kutoka katika akili yangu nimeelezwa na YESU WA NAZARETI. Anawapenda watu msipotee, yatunze maneno haya ni uzima na uwaeleze na wengine. Soma zaidi blog yangu na zaidi karibu katika KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Ipo shule ya mbinguni.
NABII HEBRON.

[ad_2]