UJUMBE WA YESU KWA MWAKA 2013 KWA ULIMWENGU WOTE NA WATU WOTE.

UJUMBE WA YESU KWA MWAKA 2013 KWA ULIMWENGU WOTE NA WATU WOTE.

[ad_1]

UJUMBE WA YESU KWA MWAKA 2013 KWA ULIMWENGU WOTE NA WATU WOTE.
Ndugu msomaji na mwanadamu uliyeumbwa kwa mfano wa sura ya MUNGU, nakusalimu katika jina la YESU KRISTO wa Nazarethi, nakutakia heri njema ya mwaka 2013, uwe ni mwaka wa wewe kumjua YESU wa kweli na usidanganyike tena na manabii wa uongo au watumishi waliomsaliti YESU kama Yuda Iskarioti, wanaofanya kanisa kama nyumba ya biashara, au mradi na wengine 45% ni wachawi kiwango cha juu wakifanya miujiza ya kipepo na kuwaibia wana wa MUNGU nyota zao, maisha yao na zaidi, kuwaangamiza kiroho na kimwili. Ujumbe huu mimi nakuandikia wewe au kukufikishia wewe kwa niaba ya YESU wa Nazarethi. Haya yote ni yeye kaniambia niueleze ulimwengu na atakayetii na kuyafanyia kazi atapona maisha yake, na asiyetii ataangamia. Kwa sasa 98% ya kanisa ulimwenguni limetekwa na shetani, limekataa kufuata amri za MUNGU na limeamua kuzivunja amri hizo na kufuata yale aliyoyakataa mungu na kama limekataa kuyafuata ya MUNGU jibu ni ya shetani na lipo chini ya shetani, haijalishi wanamtaja ROHO MTAKATIFU, na dhambi hii haisameheki kamwe. Mfano tunajua kwamba YESU ndiye njia ya uzima (Yohana 14:6) na (Ufunuo wa Yohana 22:18-20) inasema ole wake aongezaye maneno ya unabii wa kitabu hiki (yaani Biblia), sehemu yake ni hukumu.
YESU ameniambia, watu wote  ulimwenguni wabatizwe  ubatizo wa maji mengi kama alivyobatizwa yeye na kama Yohana alivyotumwa kuja kubatiza, alitumwa na NUNGU na akatii, sasa leo hii watu wametekwa na shetani, wamepofushwa, hawabatizwi kama mimi YESU, nawaambia ubatizo huo wa kikombe siyo wa MUNGU wa Ibrahimu na Isaka,  ni ubatizo kutoka kwa shetani, kwani hata kwenye mafaili ya baba yangu mbinguni haupo, na kama haupo hata kwenye Bibli, Je umetoka wapi? Nikuulize wewe, Je, hivyo ndivyo alivyoagiza MUNGU? Jibu sivyo,  na je, huoni hapo tayari ubatizo wa kikombe umeongezwa nje ya Biblia (Ufunuo wa Yohana 22:18-20)? Ole wenu, ndivyo alivyoniambia, na mimi sipunguzi lolote, nanukuu alivyonieleza, “ubatizo wa kikombe ni ubatizo uliotoka kwa shetani ili kuwaangamiza wanadamu wasinifikie mimi YESU wa Nazarethi”. Ubatizo ni kiapo kati ya mtu na MUNGU aliye hai, na MUNGU aliye hai aliandaa anavyotaka yeye ili akupate, ila na mwanadamu amekataa kufuata fomula aliyoitoa MUNGU katika ubatizo wa maji mengi, mwanadamu akafuata fomula tofauti na ya MUNGU, na hakika bila kufuata fomula hiyo huwezi kupata jibu la kweli; unapata jibu la uongo na unafeli. Nakupa mfano 1+0=1 na 1+1=2, ubatizo wa kweli ni 1+0=1 huu haujaongezwa lolote nje ya alivyopanga MUNGU, na ubatizo wa kikombe 1+1=2) ndio huu tayari haufai ni feki, umeongezewa mapando ya shetani. Je wewe unapenda ubatizo alioagiza MUNGU ufuatwe au unapenda ubatizo ulioongezewa mambo ya shetani? Funguka ufahamu wako hata kama unazo degree za elimu ya Biblia, tafuta mahali popote, hutaona huu ubatizo wa kikombe, ni ubatizo wa maji mengi.  Haijalishi unao umaarufu gani au cheo gani, MUNGU atabaki kuwa MUNGU tu. Kwa yeyote ambaye hajabatizwa ubatizo wa majii mengi, nakujulisha hujabatizwa na huendi mbinguni. Hata kama unaifanya hiyo kazi ya kanisa na umebatizwa ubatizo wa kikombe, wewe hujawa mwanafunzi wa YESU KRISTO wa Nazarethi, na yeye hakujui. Haya ndiyo aliyoniambia, na mimi nayasema kama alivyoniamuru. Mmepotea, rudini kusoma NENO upya, acheni mapokeo ya shetani (Mathayo 28:19-20 mkifundisha kuyashika yote niliyoyaamuru. Je, ubatizo huo wa kikombe ndio aliamuru tufuate? Jibu ni hapana, na kama umefuata ya hapana na wewe umekuwa hapana kwa YESU, umekataliwa. Usiongozwe na kiongozi kipofu, atakupotosha maana yeye anayebatiza kinyume na YESU, yeye hamjui YESU, wala NENO halijui; kama angejua, angetii kubatiza kama YESU, wote waliobatizwa ubatizo huo (wa kikombe), hamjabatizwa wala hamjawa wanafunzi wa YESU wa Nazarethi, maana ili uwe mwanafunzi wake, lazima utimize (Yohana 14:6).
Jambo linguine, MUNGU amekwisha kuonya, usiabudu sanamu wala kubusu, wala kusujudia kitu chochote alichokiumba yeye. Leo hii, baadhi wamempuuza MUNGU na kumdharau, wanaabudu sanamu na hata kutaja majina ya watakatifu waliopo mbinguni wawaombee, MUNGU amechukia, mnaofanya hivyo ni hukumu inawasubiri. Ni makosa na ni dhambi. YESU alitutumia msaidizi ambaye ndiye ROHO MTAKATIFU na imeandikwa, amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa. Hawa watakatifu waliopita ni wanadamu tu kama wewe na wanawashangaa sana mnapowaomba wao! Niliongea nao, na mmojawapo  anayechukia sana ni mama yake YESU, akasema, mimi mwenyewe namwabudu MUNGU wangu aliyeniumba, wao wananiabudu mimi. Waambie ulimwengu wote sisi hatuna ushirika nao, wamwabudu MUNGU tu, wala hatuwaombei lolote, zaidi tunachukia  wanavyomdharau MUNGU na kukataa sheria zake. Yakobo, Yusufu na Musa, Ibrahimu na Sara mke wake Ibrahimu mama wa mataifa, walinieleza kwa uchungu sana kwa niaba pia ya watoto wa Ibrahimu, Ibrahimu akasema, wanangu wanalia, wapo kifuani mwangu wanachukia kuabudiwa. Ninachokueleza ni hatari  na mnaoabudu sanamu mkifa nyama zenu zinaliwa na shetani na wakuu wa giza huko kuzimu, huu ndio ukweli na hata waliokufa wote nyama zao au miili yao ni chakula cha majeshi ya shetani na hamna aliyeenda paradiso hata mmoja na nimewaona, ni mabilioni ya watu wanateseka. Yawezekana ilikuwa hujui, sasa ufunguke na uache, uokoke na ubatizwe kama YESU kwa maji mengi katika kijito cha utakaso maji yanayotembea, kama umebatizwa katika maji mengi katika kisima, bado hujabatizwa, kwani hicho kisima sio kijito (yaani mto) – tayari ni feki, na aliyebatiza hajatii yale aliyoamriwa yafuatwe yalivyofundiswa (Mathayo 28:19). Ukiwa pia umebatizwa kwa maji mengi halafu ukabatizwa kwa jina la mtumishi, huo sio ubatizo, amekumiliki yeye akutawale na mbinguni  huendi, unakuwa wa huyo mtumishi. Watumishi wengi wanafanya kazi ya kanisa kama ni mahali pa kutafutia pesa wakitumia jina la YESU vibaya, na hao wote ndio manabii wa freemason na anahubiri au kuponya  watu! Huyo anatumia nguvu za shetani na ni mtoto wa shetani, na ndio manabii wa uongo! Mwisho umefika, watakuwa vichaa, watajinyonga na kuporomoka; kazi hiyo anaifanya YESU peke yake na yupo kazini, anarudi sasa, ngome zote za shetani zimebomolewa na vita vinaendelea. Utukufu wa kanisa la mwisho ni mkuu kuliko wa kwanza, na sasa umetimia. Wanaotumia nguvu za giza, mambo hayaendi tena, ulimwengu umeshikwa na YESU na Serikali ya Mbinguni, na ufalme wake tayari umejengeka ulimwenguni na nchi aliyoichagua ni Tanzania na mataifa yote yataponea hapa.
Muda siyo mrefu mtayaona kimwili, japo kwenye ulimwengu wa roho tayari imeshakuwa, na Tanzania ndiyo Edeni. Uzidi kumjua YESU anavyotaka wewe ufuate na usifuate mambo ambayo hayapo katika kitabu cha muongozo (Biblia) au katiba isiyobadilika, ni ya MUNGU tu.
Pia kwa sasa kanisa halina umoja ulimwenguni mwote. Watu wanakutana, wanapanga mikakati ya kanisa madhehebu mbalimbali, cha ajabu kila dhehebu lina sheria zake nje na Biblia, na mengine yanapinga wokovu, mengine yanaabudu sanamu, hayafuati ubatizo wa kweli, mengine yapo kibiashara na kimiradi kutafuta faida.
Ndugu msomaji,haya yote yanayofanywa sio ya umoja wa YESU KRISTO wa Nazarethi, kanisa la YESU ni moja tu, haligawanyiki, hembu angalia lilivyogawanyika. Je ni YESU kaligawanya kanisa? Jibu hapana. Imeandikwa, siku za mwisho YESU atakuja kulichukua kanisa lake. Kanisa ni mtu anayemfuata YESU, na kutii amri zake, msiotii hamchukuliwi, mtaangamia. YESU haji kuchukua majengo, jengo ni wewe, na kama siyo hekalu lake hakuchukui.
Kanisa haliruhusu ndoa za jinsia moja, leo hii baadhi ya makanisa yanaruhusu kufunga ndoa za jisia moja, je YESU anaruhusu? Jibu Haruhusu. Kanisa linaabudu sanamu, lingine halina Krismasi, lingine halibatizi ubatizo wa maji mengi, ligine linafanya biashara lina benki linachaji riba. Haya yanayofanya haya siyo makanisa ya YESU, sababu yanafanywa ni kinyume na YESU, hata alivyokuwa ulimwenguni (Marko 11:15-18) aliyakuta yanafanywa katika nyumba ya sala, aliyatupa nje ndio akaingia na sasa yamerudishwa yale aliyoyakataa na kama yamerudishwa na yeye hahusikina makanisa hayo na huduma zote hambarikiwi na YESU, imekuwa ni makampuni. Ole wenu! Ole ya MUNGU ipo juu ya hao wanofanya hayo na hamna makao yenu mbinguni. Mataifa yote kwa rangi zote na jinsi zote, YESU anawapenda, mrudieni yeye, fuateni sheria zake nanyi mtapona. Muwe makini sana, 98% kanisa halina YESU wa Nazarethi ulimwengu mzima, kila mtu ajichunge nafsi yake.
Okoka, dini ya kweli ni wokovu tu kwa watu wote, umkiri yeye ya kuwa ni BWANA na mwokozi wa maisha yako. Usikubali kuchaguliwa partners wa huduma yoyote ile, partners ni watu wote wanaomwamini YESU na YESU hana ubaguzi wa tajiri wala masikini. Mliochaguliwa partners kwa sababu ya pesa zenu siyo mimi YESU nimewachagua, wala sibagui mtu. Watu wote ni partners wangu, wote mnaoitwa au mmeambiwa mimi YESU nimewachagua siyo kweli, ni uwongo, hamtabarikiwa na mtazidi kufilisika kama mnavyoendelea kufilisika. Jiulize swali, kwa nini partner lazima awe na pesa? Jibu ni mfumo wa shetani aliowawekea watumishi baadhi roho ya kupenda pesa kama Yuda Iskarioti aliyekuwa mwanafunzi wangu, na mwisho wake aliangamia. Usikubali kuitwa partners ukaambiwa mimi YESU nimekuchagua, mimi nawapenda wote. Ina maana mimi YESU nawapenda matajiri tu na masikini siwapendi? Mimi YESU sipo hivyo, wala siyo mnyang’anyi wa mali zenu. Ni hao na mambo yao wamenisaliti mimi YESU na baba yangu. Ole wao, hata michango makanisani, mimi YESU na baba yangu siyo masikini, msitoe, mnaibiwa. Hii ni kwa ulimwengu mzima. Kama kazi ni yangu, mtumishi aniombe, mimi mwenye kanisa nitaleta, ila walio sio wangu na walioingiwa na tamaa ya pesa, hao ndio wamejijengea mbinu za kutumia jina langu YESU kukusanya na kuwaibia. Niliwaambia, nimewapa bure toeni bure, msisumbuke mtakula nini, mtavaa nini, nanyi mmekataa kutii, hukumu imo juu yenu na ninyi wanyang’anyi, kazi niliyoifanya ni kuponya watu na kueleza habari njema za ufalme wa MUNGU. Leo hii habari ya pesa na miradi siyo nilivyotaka, mmenisaliti. Nitawaambia siwajui siku ile, mtalia na kusaga meno.
SALA YA TOBA KWA UNAYETAKA KUMPA YESU MAISHA YAKO.
Sema; BWANA YESU, YESU wa Nazarethi, naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele. Shetani sikutaki tena, mimi ni mali ya YESU wa Nazarethi kuanzia sasa. BWANA YESU, nishike mkono, nisitoke mkononi mwako milele. Amen.
Mpaka hapo umeokoka, na mimi ninaendelea kukuombea. Ukitaka msaada zaidi, niandikie kwa email ya maombi ([email protected]), utajibiwa na kuombewa zaidi.
Huu ndio ujumbe wa YESU wa Nazarethi kwa ulimwengu wote.
Nabii Hebron.

PICHA ZA IBADA NA MAOMBEZI KATIKA IBADA YA LEO TAREHE 01/01/2013
Mtume na Nabii Hebron akimwombea muumini na kumtoa katika kifungo alichokuwa akitumikishwa. Tukio hili lilitokea katika ibada ya leo 01/01/2013.

Bibi huyu alikuwa akiombewa na Mtume na Nabii Hebron katika ibada ya leo tarehe 01/01/2013 iliyofanyika katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Moshono – Arusha.

Aliyebebwa pichani, ni muumini aliyekuwa akisumbuliwa na nguvu za giza, alipokea uponyaji wake kwa kuombewa, kuvuliwa nguvu za giza na kuvishwa nguvu za MUNGU.

Waumini wakiwa katika ibada ya leo 01/0102013, wakiimba, kusifu na kuabudu.

PICHA MBALI MBALI ZIKIONYESHA WAUMINI WAKIPATA HUDUMA KATIKA KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

Mchungaji Kiongozi Dorcas, akihubiri Injili katika ibada iliyofanyika katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, huku waumini wakimsikiliza kwa makini.

Baadhi ya magari ya waumini wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE yakiwa yameegeshwa nje ya kanisa wakati wa ibada.
Baadhi ya magari ya waumini yakiwa yameegeshwa nje ya kanisa wakati wa ibada.

 Kwa mawasiliano;

+ 255 759 610 820
+ 255 718 154 433
+ 255 718 916 864
+ 255 764 042 149



Email:

[email protected]


Imeandaliwa na Priscus & Dorcas Macrine,

KANISA LA YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.

[ad_2]