WAJUE WATUMISHI WANAOONGOZWA NA MIUNGU BADALA YA MUNGU ALIYE HAI, NA NI WAKRISTO!!!

[ad_1]


Ukisoma katika kitabu cha injili ya Mathayo ambayo maneno yake yametoka kwa MUNGU aliye hai na siyo maneno ya miungu Mathayo 10: 7-9 “Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema: Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo. Mmepata bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha, wala mapesa mshipini mwenu.” Ndugu msomaji na binadamu uliyeumbwa na MUNGU aliye hai na watu wote  wa mataifa yote, nyie mmeumbwa na MUNGU aliye hai bali miungu haiumbi lolote bali miungu ni roho wa shetani.
Sasa nitafundisha kuhusu watumishi wanaoongoza makanisa na watu wanaamini na kupokea mafundisho yao pasipokujua kuwa wao hawaongozwi na MUNGU aliye hai bali wanaongozwa na miungu na ndani yao ni miungu ndiyo inayofanya kazi ya injili hizo za kipepo, maana hata siku moja usitegemee miungu kuwa itakuhubiria habari njema ya MUNGU aliye hai bali siku zote ni mtumishi kwenda kinyume na biblia tu. Ukiona hivyo ujue anaongozwa na miungu na hata wewe unayemfuata au kuabudu katika kanisa hilo ujue unaabudu kwa miungu na umetekwa na wewe. Zaidi fuatilia makala ya Nabii Hebron utafunguka zaidi na giza litatoka utaona nuru, katika injili ya Mathayo 10: 7-9 MUNGU anasema wewe mtumishi wangu nimekupa uwezo wa kuhubiri na kuwaponya watu bure sijakuchaji kitu chochote na wewe usimchaji mtu yeyote pesa, sawa sawa na neno langu, ukiona mtumishi anaombea watu bure na hachaji mtu yeyote pesa au kutoa kiingilio cha pesa ndio uonane na yeye kwa private issue ujue huyo ni mtumishi wa MUNGU, na ukiona anachaji pesa na anachaji kiingilio ujue ule uwezo alionao hajapewa na MUNGU aliye hai bali amepewa na miungu. Maana kama ni nguvu za kweli za MUNGU hazitatenda kazi maana ROHO MTAKATIFU hawezi kumsaliti MUNGU na neno lake.
Hivyo watu wengi katika ulimwengu huu wanashindwa kutofautisha kati ya mtumishi anayetumiwa na MUNGU wa kweli na mtumishi anayetumiwa na miungu. Ila utapata picha kidogo na mengine ROHO MTAKATIFU atakufunulia haijalishi upo katika nchi yeyote ile, alichonituma YESU WA NAZARETI niwaeleze ukweli watu wote wa mataifa yote na usipotezwe na watumishi waliomsaliti MUNGU na bado wanajiita manabii, mitume, wachungaji, wainjilisti, waalimu.
WATUMISHI WANAOONGOZWA NA MIUNGU
Kwanza huduma yeyote lazima utoe pesa hata kuwaona kwa private issue na pia kiwango cha kuwaona ukiwa wewe peke yako ni kikubwa tofauti na kiwango cha kuombewa mkiwa group. Sasa mtumishi wa jinsi hii huyu anaongozwa na nguvu za miungu (na shetani) ila kwa nje watu wamepigwa upofu, wanaona wanaenda kukutana na MUNGU aliye hai kumbe unaenda kujipeleka kwa miungu na unanajisika hata kama ulikuwa na MUNGU wa kweli yeye huondoka kwako sababu umenajisika na MUNGU ni mtakatifu bali miungu ni michafu. Nawaeleza watu wote wa mataifa yote na muelewe ya kuwa sasa hivi kanisa 98% unaongozwa na miungu pasipo watu kuelewa, ila amenituma YESU WA NAZARETI niwafungue macho, fahamu na mpone roho zenu na mtengwe na miungu.
Wale walioshirikishwa pasipo kujua, na yeye alipo kuwa hapa ulimwenguni alisema msiziamini kila roho bali zichunguzeni kama kweli zinatokana na MUNGU. Kivipi? Utavichunguzaje? Kwanza njia rahisi ni kupitia neno lake, mfano nimekupa bure, toa bure, huyo ndiye MUNGU wa kweli bali formula ya miungu siku zote lazima utoe malipo, kwa sababu hata huyo au hao watumishi wanaongozwa na miungu hizo nguvu za shetani hawapewi bure lazima waingie maagano ya kutoa makafara ya damu, kuua, kuzini na kuenda kuzimu kipepo, na akitoka huko huanza kazi ya injili za kipepo sasa hawa ndio wale manabii wa uongo aliowataja YESU kuwa watakuja uliwenguni na sasa wapo tu wengi na watalitumia jina langu kuwateka wengi na ndivyo ilivyo katika ulimwengu wote. Watumishi maarufu idadi 99.9% wanaongozwa na miungu na hii ni katika Tanzania, Kenya, Uganda (Afrika yote, Europe yote, America Yote, Asia yote, Australia yote na mengineyo yote) na hii ndiyo njia aliyoitumia shetani kuliteka kanisa kupitia viongozi maana akishatekwa kiongozi basi amelipata kanisa lote maana dreva ni mchungaji na abiria wake ni waumini so anapolipeleka gari na abiria wake wapo ndani ndipo watakapoenda na yeye.
Sasa muelewe wana wa MUNGU injili sasa hivi imevurugwa na kugeuzwa na miungu kiimani na kimatendo. Hivyo muelewe na mjiepushe na huduma au watumishi wowote wanaochaji pesa, hao wanaongozwa na miungu na ukimfuata anakupeleka na wewe kwa miungu na kukutenga na MUNGU aliye hai pasipo kujua. Amenieleza YESU WA NAZARETI katika ulimwengu wote hata serikali zote mnaompenda MUNGU aliye hai na mnataka nchi zenu zipone msiruhusu huduma za pesa makanisani, mnazinajisi nchi, watu na mnalaaniwa. Na watumishi wa jinsi hiyo ndani yao ni lusifa ndio ameketi katika moyo wake ili awanyanganye watu pesa zenu alisingiziwa eti ni MUNGU ndiye amesema hivyo au amepanga hivyo, na ndani yake analo pepo mhubiri hivyo mnahubiriwa na pepo mhubiri badala ya ROHO MTAKATIFU chunguza mahubiri na matendo.
NOTE:
Cha ajabu muelewe MUNGU aliye hai ni MUNGU wa matajiri na masikini yeye hana ubaguzi, watu wote ni wake, ila mtumishi anayeongozwa na miungu yeye anaangalia pesa tu ndio akuone, na kwanza anakuwekea pepo lingine juu ya shida yako unajiona umepona ila baada ya muda shida ipo pale pale (belzebuli hawezi kumfitini belzebuli mwenzake. Nikuulize swali, je hawa watu wasio na pesa na wanataka msaada wa kiroho je MUNGU hawapendi? Jibu, anawapenda ila shetani hana upendo kwa watu anataka vitu vyao tu na aziangamize roho zao. Watumishi wote wanaochaji pesa ndio wakupe huduma au uonane nao hao wote wanaongozwa na miungu (mungu baali). Kataeni, wakimbieni mpone roho zenu, hata nchi zote wakataeni hao ni watoto wa shetani, ni wachawi, ni wauaji wa roho za watu na kuwavuna kuwapeleka kuzimu, tena hata watumishi wenye urafiki na watumishi wa jinsi hiyo jitengeni nao ina maana katika ulimwengu wa roho wao ni kitu kimoja.
SALA YA TOBA:
BWANA YESU WA NAZARETI, naomba unisamehe nimeabudu miungu pasipo kujua na kujua, naomba uniokoe katikati ya miungu na leo aliye BABA yako MUNGU aliye hai awe MUNGU wangu. Nilinde nisitekwe tena na miungu wala nisimtumikie tena. Niongoze siku zote mahali ulipo wewe na siyo kwa miungu tena.

NABII HEBRON.

[ad_2]