WAKRISTO WA ULIMWENGU WOTE, MSIKUBALI KUFANANISHWA AU KUWA WAPUMBAVU MBELE ZA MUNGU.

[ad_1]

WAKRISTO WA ULIMWENGU WOTE, MSIKUBALI KUFANANISHWA AU KUWA WAPUMBAVU MBELE ZA MUNGU.
MATHAYO 7:26
Neno la MUNGU linasema hivi; Na kila asikiaye hayo maneno yangu na siyafanye atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba  yake juu ya mchanga.
Ndugu msomaji wa makala hii ya Nabii Hebron, pokea huu ujumbe wa YESU wa Nazareti ili uzidi kumjua yeye na kama humjui endelea kusoma katika blog yangu prophethebron.blogspot.com kuna masomo mengi yatakayo kufungua zaidi na hayo yote ni YESU ndiye kanipa nikufikishie na wewe mahali ulipo nchi yeyote, bara lolote, kisiwa chochote.
Ujumbe huu ni kwa ulimwengu mzima,  MUNGU anasema kila Neno lake  lililoandikwa katika kitabu chake kitakatifu ambapo ndani yake , limeandikwa Neno lake , ambapo Neno hilo ndiyo yeye. ( Ufunuo wa Yohana 19:13,  Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu na jina lake aitwa, Neno la MUNGU.
Natumaini unazidi kuelewa  ya  kuwa  Neno hili ndilo MUNGU, na kama  ndilo MUNGU ukalijua au kusoma ilivyoandikwa halafu ukafanya kinyume na Neno linavyosema, YESU anasema ni mtu asiye na akili  maana mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya jambo tofauti  na maagizo ya MUNGU,ila mpumbavu ni mtu asiye na akili   au yupo ovyo ovyo tu.
Neno la MUNGU  linasema walio au aliye kinyume na Neno lake huyo ni mpumbavu, haijalishi ni mtumishi,au mtu wa tabaka lolote asiyetenda  sawa sawa na Neno lake  MUNGU, huyo ni mpumbavu, na hata kibinadamu  kila mtu anachukia  kuitwa mpumbavu au kufanya upumbavu na hata watu wakijua wewe ni mpumbavu hawakusikilizi wala kukujali.
Na MUNGU fomula yake  ndivyo hivyo hivyo, hawasikilizi wapumbavu au wenye dhambi na ili akusikilize ni mpaka uache upumbavu au wenye dhambi na ili akusikilize ni mpaka uache upumbavu au dhambi.  Ila nitakuonyesha kwa kidogo tu, ujue wakristo hawapendi kujiingiza katika upumbavu wa kumdharau MUNGU ila 98% wanaingizwa pasipo kujua au kuelewa na wanaosababisha na hata na wao wawe wapumbavu mbele za MUNGU ni viongozi wa dini zao, huwafundisha kuyatenda yale ambayo  MUNGU ameyakataa na waumini huyafuata kumbe kiongozi ameshakuwa kipofu na ndivyo watu wanavyoangamia kwa sababu ya elimu ya ujinga ambayo siyo MUNGU amepanga muijue ila shetani amewapa mafunuo ya kuzimu ya kumpinga MUNGU na silabasi ya masomo iliyopangwa  ukasoma nyingine wakati wa mtihani lazima yale mawili utafeli yote na kupata (zero) 0. huu ni mfano nimekupa tu, ili uelewe vizuri, kuhusu kufananishwa na mpumbavu na inawezekana na wewe ulisha kuwa mpumbavu au hadi sasa unafananishwa na mpumbavu mbele za MUNGU. Ila utapona kama ukitaka na kupenda kubadilika, kinyume na hapo ni  hukumu inawasubiri.

Na sababu ya wanadamu kukataa neno la MUNGU na kulifanya ilivyo, ni shetani ndiye hulifanya maana anajua ukiwa mpumbavu yeye  atakumiliki, maana yeye pia shetani ni mpumbavu mkuu. 

Na ukiyafanya na kutii neno lake MUNGUwewe  utafananishwa na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, hata majaribu yakija na mafuriko hayataweza kuibomoa au kuiharibu.

Natumaini unazidi kuelewa. Kataa upumbavu tii Neno la MUNGU usije ukafananishwa na upumbavu.
YAFUATAYO NI BAADHI TU YA MIFANO AMBAYO KAMA UNAFANYA KINYUME NA ILIVYOANDIKWA KATIKA BIBLIA TAYARI UMEKUWA MPUMBAVU:
Ø  Kuabudu  sanamu
Ø  Kuongozwa  na watumishi katika kanisa ambao ni wanachama wa freemason
Ø  Kubatizwa kwa jina la mchungaji
Ø  Kumuabudu jina la Nabii / mtume, mchungaji katika kanisa na kumuomba yeye kama ndiye MUNGU
Ø  Kubatizwa ubatizo ambao haujaandikwa katika Biblia, ubatizo wa kikombe.
Ø  Imeandikwa utoapo sadaka yako kulia wala kushoto isijue,ila unaambiwa andika jina lako, namba ya simu, na zaidi unapewa risiti. Huu ni upumbavu wa shetani.
Ø  Huduma inayofanya biashara ya mabenki kuchaji riba, wakati  kwenye Neno amekataa usimchaji riba. Madhara ya riba mtu akishindwa kulipa humfilisi na kumnyang’anya mali zake na benki hiyo iliyoitwa kwa jina la kanisa. Unamfanya YESU aonekane au kuitwa mnyang’anyi ( upumbavu )
Ø  Kanisa kufungisha ndoa za mashoga
Ø  Kutoa huduma ya kiroho kwa kulipisha pesa ( upumbavu)
Ø  Kufanya kanisa mahali pa kutapelia watu malizao.
Ø  Kuongozwa na watumishi wauzao madawa ya kulevya.
Ø  Kufungishwa ndoa kwa agano la shida la shida na raha
Ø  Wanaochoma au kufukiza ubani ndani ya ibada , huko ni kuzibariki sanamu zao. Soma Isaya 66:3b-4 na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu, naam, wamezichagua njia zao wenyewe, nafsi zao zafurahia machukizo yao.Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao kwa sababu nilipoita hawakuitika na nilipo nena hawakusikia bali walifanya maovu machoni pangu na kuyachagua nisiyofurahia. Kutenda tofauti na kukataa kusikia sauti ya MUNGU.
      Kamakwa mfano huu nilioutoa, umekuwa  mpumbavu na mapigo ya    
      MUNGU 
      siku zote huwapiga wapumbavu kama Neno lisemavyo.
Ø  Kubatiza watoto wakiwa wadogo hata hawamjui huyo YESU wala chochote na kuwekewa wasimamizi wa ubatizo huo, mwanamke na mwanaume, hii imetokea kwa shetani ili kuwafanya wanadamu wafananishwe na mpumbavu. Na zaidi huo sio ubatizo, Neno ubatizo maana yake ni kuzamishwa mwili wote.Hiyo kumwagia maji kichwani ni chapa ya namba 666 kwenye paji la uso na kamaulifanya hivyo batizwa kwa maji mengi ili hiyo chapa 666 ikutoke, Ufunuo wa Yohana 13:16 -18.
Ø  Kuongozwa na watumishi ambao hawajabatizwa ubatizo wa YESU wa Nazareti maana kwanza hao siyo wanafunzi wake soma mathayo 28:19-20 YESU anasema wabatizwa yani zamishwa hawa hawajazamishwa. Hawalishiki Neno la MUNGU kuanzia hapa ila hufuata wayatakayo ambayo ndio huu upumbavu YESU anaosema asiye lifuata neno lake nakulitenda. Huu n mfano halisi 100% unaoonekana na hawa wamebadilishwa wakawa ni watumishi wa shetani kwa chapa 666 kumfanya shetani awe na wanafunzi wengi badala ya YESU  kuwapata. Hawa ni wapinga Kristo. Utamjibu  Bwana. TUBU TOKA UTENGWE NAO ILI MUNGU AWE BABA YAKO! Isaya 33:1
Ø  Kitu chochote kinachofanywa na kanisa kinyume na Neno la MUNGU lilivyoandika haijalishi huko katikati jina la YESU linatajwa. Hao MUNGU huwafananisha na wapumbavu. Na wapumbavu hawatamuona MUNGU. Hao wanaoshiriki wote mnasababishwa muwe wapumbavu japo kibinadamu hata wewe hupendi unafanywa mjinga ila embu ona sasa jinsi kanisa linavyowafanya hata waumini kushiriki hayo japo hawataki au hawajui.
 NOTE:
  
   Usishiriki mahali ambapo MUNGU hudharauliwa, Neno lake halifuatwi ili upone 
   usishiriki kabisa jitenge nao na MUNGU atakuwa Baba yako wote walio watoto
   wa  kike na kiume.  Soma 2Wakorinthi 6:14-18
   
  
   NABII  HEBRON.
  

[ad_2]