WANAOJIITA WAO NI YESU HAO NI MASHETANI 100%

[ad_1]

WANAOJIITA WAO NI YESU HAO NI MASHETANI 100%
YOHANA 1:14


Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa mwana pekee atokeaye kwa Baba amejaa Neema na kweli.

Ewe mwanadamu uliyeumbwa na MUNGU aliyeumba dunia hii na sayari zote na vitu vyote ni mali yake. Tarehe 5.08.2013 muda wa saa nne za usiku kwa saa za Afrika Mashariki (Tanzania), Bwana YESU aliye mwana wa pekee wa MUNGU alikuja kusema na mimi kuhusu ulimwengu ulivyoharibika na utakavyoendelea, akaniambia Hebron usiogope kwa ajili ya machafuko yanayotokea sasa, na majanga katika nchi mbali mbali Neno la MUNGU lazima litimie na hizi ndizo dalili za ujio wangu. Ila machafuko haya hayatawaathiri wale waliopo na yeye, ila wale ambao hawapo na yeye yatawahusu; huo ni mpango wa MUNGU. Akanieleza na mengine ambayo hakuniruhusu niyaseme popote kama vile alivyomzuia Ezekiel kusema lolote.

Ila akaniambia waambie wanadamu wote mimi  YESU wa Nazareti nipo mbinguni kwa Baba yangu  na nitarudi hapo duniani siku ile ya mwisho (Nitarudi kimwili kama ilivyoandikwa). Akaniambia wameibuka watu wanajiita wao ni YESU akaniambia hao ni mashetani. Akaniambia je, huyo anayejiita yeye ni YESU alishinda mauti?  Nikamjibu hapana, akaniuliza je alisulubiwa msalabani? Nikamjibu hapana, je alikufa na kufufuka? nikamjibu hapana BABA, akaniuliza je yeye alipaa kurudi mbinguni? Akaniambia sasa angalia je anafanana na mimi sasa, nikamjibu hapana, akaniambia waambie watu ukweli wapone haijalishi  upo nchi gani, taifa lolote.

Ujumbe huu sio wangu mimi Hebron, ninanukuu kama alivyoniambia YESU wa Nazareti. Amesema msishiriki kumwita YESU, hivi mnajua uthamani wa jina la YESU? Niliogopa sana, maana aliongea kwa ukali. Wanadamu wanajifananisha na mimi na kushiriki utukufu wa MUNGU? Akaniambia ndani ya anayejiita  YESU mwanadamu, ndani yake ni shetani anakaa ili kuwapoteza watu, someni BIBLIA mtaona YESU anarudi ule mwisho wa dunia. Je, kama mtu anasema yeye ni YESU na yupo hapa duniani ina maana mwisho wa dunia ndiyo tayari? Jibu bado. Akaniambia  akishuka YESU kwa mwili wake yeye siku hiyo ya mwisho, hakuna kitu kitakacho salia hata milima itakuwa tambarare sababu ya nguvu zake na uweza wake.

Ndugu uzidi kufunguka anayejiita yeye ni YESU huyo ni muongo anawapoteza watu, na wote wanaomwamini huyo hawamwamini YESU, ni shetani amejipa jina hilo akamtumia huyo mwanadamu. Mnapo enda kwake mnaenda kujikabidhi kwa shetani 100%. Mrudieni YESU wa Nazareti na mtubu. Yeye anatafutwa kwa njia ya roho na kupitia msaidizi wake ambaye ni roho mtakatifu tu. Na zaidi uzidi kuelewa YESU hakuwahi kuoa, wala kuzaa watoto, na alizaliwa kwa njia ya ROHO MTAKATIFU, na alizaliwa kwa njia hiyo ili atuokoe kutoka katika dhambi ya asili.

Kila mwanadamu anadhambi ya asili isipokuwa YESU tu! Je huyo anayejiita YESU yeye hana dhambi ya asili? ( jibu anayo), na kama anayo je, huoni ni muongo huyo? YESU amesema ole wake shoka lipo tayari kwenye shingo yake na hukumu tayari. Imeandikwa wakati wa mwisho mkiambiwa yupo kule au kule msiamini, YESU alikuwa anayo maana. Yupo mbinguni tu  mkienda hamtamkuta, sasa angalia wengi walioenda je hawajaambulia patupu?
NOTE:
YESU YUPO MBINGUNI NA HAKUNA MTU MWINGINE ANAYEFANANA NA YESU. YESU MWANA WA MUNGU NA MWOKOZI WETU.

NABII HEBRON

[ad_2]